Ninayo maswali kuhusu mazingira ya uwekezaji nchini

kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
6,008
6,673
Naiuliza serikali LAKINI pia wadau woote wa maendeleo;

Iwapo tunamazingira mazuuuri ya uwekezaji Tanzania nikwavipi serikali inapata hasara kuuubwa tena ya aibu ya mabilioni katika uwekezaji wake?

Serikali imewekeza kwenye sekta muhimu saana kama mafuta(TANOIL), MAWASILIANO(TTCL), usafirishani (TRC, ATCL, UDART) iweje inapata hasara kuuubwa hivi?

Je, majibu nikwamba serikali yetu ni dhaifu saana katika kubuni,kusimamia/kuendesha miradi?

Kama biashara ningumu hivi nchini kwanini serikali inapambana kuchaji kodi na kujisifu kukusanya kodi nyingi kwa watu binafsi tunaofanya biashara huku ikijua biashara zina hasara kubwa?

Inakuwaje kampuni/taasisi inadumu miaka nenda rudi na mpaka leo inaitia nchi hasara na kupoteza kodi za wananchi?

Je,Haya sio matumizi mabaya ya kodi za wananchi? siyo uhujumu uchumi unaopewa kifua na serikali yenyewe?

Kunaugumu gani kuvunja kampuni na kuanza moja katika kubuni mradi na namna Bora ya kuuendesha?

Je, Serikali inaonesha mfano gani katika kuvuta uwekezaji NCHINI iwapo yenyewe inashindwa kuwekeza?

Alhamisi kuu njema kwenu wadau,akili ni nywele
 
Shida sio kuwekeza au kufanya biashara shid ya tanzania ni watu sahihi wa kusimamia hizo biashara na mashirika hayo..
 
Back
Top Bottom