Binti Magufuli
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 7,479
- 5,161
Krappppppp
Wakuu heshima mbele.
Nimefikia uamuzi wa kuuliza hili kutokana na tafiti zangu binafsi kupitia kusoma blog mbali mbali na kuongea na baadhi ya watanzania waishio majuu.
Je kwanini watanzania wengi walioko majuu wanaonekana kuwa na mtizamo mbaya kuhusiana na kujichanganya na watanzania wenzao wanaoishi nje kwamba wengi wao ni nuksi, majungu na majanga?? je ni kweli watanzania (walio wengi) ni nuksi, wambea na wajaa majungu wakiwa huko majuu? Ni juzi tu mke wa mzungu aliweka mada kuhusu wabongo majuu na watu walitiririka kwa kina kabisa kuonyesha kwamba Watz walio wengi huko majuu ni nuksi na si watu wazuri kujichanganya nao na kujenga urafiki.
Binafsi siishi huko hivyo sijabahatika kuishi nao wakiwa huko nje na kuona tabia zao. Je shida ni nini haswa?
Kibongo bongo (ki hapa hapa home) najua kweli wabongo ni nuksi, ila kwa majuu nilidhani kwa kujichanganya na wengine ule unuksi wa kibongo utapotea.
Nawasilisha.
CC Wabeba box na walea vibibi wote.
maisha ni kujichanganya bwana...maneno yapo hata kwenye kanga yapo...aani uogope kujichanganya kisa utasemwa..kwani ukisemwa wewe wa kwanza? huko ni kutojiamini na ushamba tu...Labda kwa wanawake ila kwa wanaume maisha huwa ya furaha na kusaidiana.
ndo maana sometimes nakupenda super mbabebs....labda wataje mataifa ambao hawana hizo tabia...Hiyo ni dhana potofu tu.
Ni potofu kwa sababu umbeya, upikaji majungu, na fitna ni tabia za kibinadamu.
Katika jamii nyingi kama siyo zote, watu wa aina hiyo wapo.
Sasa kudai hujichanganyi na wabongo walio majuu sababu eti wana tabia hizo ni kupotoka kwa sababu hata watu wa mataifa mengine wanazo hizo tabia.
Na mtu yeyote anayeamini kwa ujumla dhana kama hiyo basi huyo si 'observer' mzuri wa tabia za watu.
Kuna rafiki yangu anasemaga 'ukiwa huna hela kila utakachoambiwa utaona unadharauliwa ama kudolishiwa'
Hata kwetu wapo
........It begins with you.........
Naupenda sana huo msemo, na sijui kwa nini kila kunapotokea kitu katika maisha yangu kabla sijaona mwenzangu kakosea huwa naanza kujichunguza mimi, that is me!
kuna watu maisha yao ni drama tupu, sasa anaona akiwa nje bora ajichanganye na watu ambao hawamjui ili hata anapofanya drama zake hajali, maana anajua siyo wengi watajua, lakini sasa akijichanganya na wabongo halafu akafanya hayo mambo basi bongo yote watajua. Binadamu wote tunasema, ila sasa unaangalia je huyu atasema kwa population ipi? ina impact gani katika maisha yangu? hata wale wanaosema hawa-mind kusemwa lakini kitu kinaposema kuhusu wao wana-mind sana, hata kama ni kimya kimya
ushamba tu dear ..unakimbia ndugu zako kisa kusemwa? kwanza kwa nini uhisi utasemwa? ...kujiona kusipo na maana...........It begins with you.........