Dumelang
JF-Expert Member
- Aug 11, 2011
- 3,274
- 5,936
Tanzania tuna vijana wengi wenye mitaji na wanaojua kufanya biashara. Tatizo mara nyingi si mtaji, bali ni namna tunavyoutumia mitaji yetu.
Fikiria Kijana ana Sh milioni 10, 20, 50 au 100, mara nyingi anawaza kwenda China, ananunue nguo, viatu, vipodozi au vifaa vya simu, nk anarudi na kuuza.
Anaweza kupata faida nzuri. Lakini baada ya miaka 5 au 10, bado anafanya kitu kilekile: ananunua na kuuza. Ananunuq subaru ana pesa ya kukaa sehemu za starehe ila hajaongeza thamani ya kudumu vizazi na vizazi.
Kijana na mtaji wa mil 20 anafungua Mgahawa au bar
Uchuuzi si tatizo. Ni biashara halali na inaweza kuwa hatua nzuri sana ya kuanzia. Tatizo ni pale tunaposhindwa kupanda hatua inayofuata — kutoka “nunua na uza” kwenda “tengeneza na uza.”
Kwanini Matajiri wakubwa hawamiliki bar wanamiliki kiwanda cha kutengeneza pombe?
Fikiria mfano rahisi. Badala ya kutumia mitaji yetu chupa za vifungashio, cover za simu, protector za simu au bidhaa nyingine kutoka nje, kwa nini mitaji hii isiende kwenye kuanza kuzalisha bidhaa hizo hapa? Bidhaa za teknolojia nyepesi? Bidhaa mbazo production line yake complete inaringana na mitaji yetu ya mil 10 mpk 200? Au zaidi
Hapo ndipo thamani kubwa inaanza kubaki Tanzania: mashine, wafanyakazi, vifungashio, malighafi, usafirishaji na biashara nyingine zinazozunguka uzalishaji.
Na si lazima mtu aanze na kiwanda cha mabilioni. Unaweza kuanza na mashine moja, bidhaa moja na soko moja. Hata uchuuzi unaweza kuwa daraja la kuelekea huko. Uza kwanza, jifunze soko, tambua bidhaa inayotafutwa, halafu anza kuifungasha au kuizalisha mwenyewe.
Changamoto nyingine ni kwamba wafanyabiashara wengi wanaishia kwenye bidhaa zilezile. Wananunua kwa wauzaji wale wale na kuuza kwenye masoko yale yale. Mwisho wa siku ushindani unakuwa wa bei.
Lakini ukianza kuzalisha, unaweza kujenga brand yako, kudhibiti ubora, kuongeza uzalishaji na baadaye kuuza hata nje ya Tanzania.
Kwa hiyo kwasasa na dunia tunayoishi swali tunalopaswa kujiuliza watanzania si tu:
“Nitanunua nini China nikauze Tanzania?”
Bali:
“Ni kitu gani Watanzania wananunua kila siku ambacho naweza kuanza kukizalisha hapa?”
Hapo ndipo biashara inaweza kuanza kubadilika kutoka kujitengenezea kipato kwenda kujenga mali, ajira na uzalishaji wa ndani.
Hatuhitaji kila kijana awe na kiwanda kikubwa. Tunahitaji tu vijana wengi zaidi waanze kupanda ngazi kutoka mfanyabiashara → mfungashaji → mzalishaji → mwenye brand.
Kilimo ni backbone ya Tanzania tunaweza kubadiri mazao ya kilimo kwenda kuwa bidhaa kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo wakati mwingine kwa kuunganisha mitaji
Kuna watu wana pesa Tanzania. Mfano mtu anafungua bar maarufu 3 nchini zote zina thamani ya bilion 1 miaka mitatu bar imekufa. lakini hii bilioni moja angewekeza kwenye Kiwanda cha kubadili malighafi kuwa bidhaa kuna nafasi kubwa kukua na kujenga uchumi imara binafsi na wa nchi kuongeza mnyororo wa thamani na ajira nyingi kwa Watanzania wengine.
Ni muda wa kufikiri tofauti tupunguze uchuuzi na kuwekeza kwenye Uzalishaji