UTASHI
Senior Member
- Jan 19, 2013
- 135
- 56
Mrembo by Nature waswahili wanasema lisemwalo lipo huenda kuna ukweli hata kama mdogo ktk hayo uliyosikia. Nafikiri si wote na nataka kuamini kwamba si wote wenye majungu. Hata wanaoenda china husema haya haya kwamba watz ukiwakuta huko hata msaada hawakupi na ni wa kwanza kukukwepa. Sasa kama stori hizi tunazisikia tukiwa hapa bongo basi upo ukweli ktk hili kwa hao wanaoishi huko majuu. Najua umependa kuzungumzia watz na hukutaka kuongelea mataifa mengine ingawa na wao kwao majungu yapo.
Haha,.Ablessed,Nilifanikiwa kwenda China na nikaishi kule kama miezi 3,Ukweli ni kwamba Wa TZ ambao wapo China wanapiga vi dili vidogo vidogo,hasa vya kusaidia watu kununua vitu vya biashara na kusafirisha.Wa TZ wanaofanya kazi hizo wanaweza kuongea kichina vizuri tu.Wafanyabiashara wa Ki TZ wakienda China wanataka wasaidiwe kutembezwa kwenye makampuni na kupewa huduma ya kutafsiri kwa gharama ya Chini sana,Sasa wale vijana wanaona hailipi,maana kule kulivyo siku si kitu jioni utaona imefika na unachotafuta bao hujakipata,kijana hawezi kuhudumia wateja zaidi ya wawili kwa siku.
Wafanyabiashara wa K-TZ yasemekana wakiwaona Vijana wa K-TZ huko China basi wanasahau kua wapo kikazi,wao wanaingiza undugu na wanataka dezo/bei chini ndo maana wanakwepwa,.wanawapeleka wenye fuedha zao.{Hicho ndicho nilichokigundua mimi,Hasa Guangzhou}Wafanyabiashara K-TZ wawe wanajitahidi kuwalipa wale vijana ujira unaoridhisha,.