Watangazaji wa 360 Clouds tv kama hamtojali nitaomba mnijibu maswali yangu haya yafuatayo...

kwani kiingereza ni bora kuliko lugha yetu ya Kiswahili?,ningefurahi mno vyombo vyetu vya habari vitumie zaidi lugha yetu na kupiga zaidi nyimbo zetu
 
Wacha umbea.
Mbona hassan alishasemaga hawezi kingereza??? au hukuwepo sikuhiyo?

kingereza ni Lugha sio lazima kila mtua ajue, mwingine inashindikana kabisa kujua

Alisema lini na wapi? Je kwakuwa Wewe umeonyesha ' ushirikiano ' wako wa kuwa na ' Kiherehere ' kumjibia unaweza ukatuwekea hapa Jamvini hiyo Kauli yake ili nasi ambao hatukumsikia tuweze kuisikia na kuamini?
 
  1. Je ni kwanini kila mnapomualika ' Mgeni ' anayezungumza lugha ya Kiingereza ni Babie Kabae tu ndiyo anauliza maswali mengi ila mwenzake Hassan Ngoma anauliza machache?
  2. Je ni kwanini kila Mtangazaji Hassan Ngoma anapouliza ' swali ' la Kiingereza mara nyingi sana huwa anatetemeka?
  3. Je ni kwanini kila Mtangazaji Babie Kabae anapouliza swali la Kiingereza anakuwa ' comfortable ' kabisa na anauliza maswali ya maana?
  4. Je ni kwanini kila Mtangazaji Hassan Ngoma anapouliza ' swali ' la Kiingereza huwa ' anatupatupa ' mno mikono na hatulii ' Kitini ' kama ' Swala ' aliyekamatwa na Simba?
  5. Je ni kwanini kila Mtangazaji Babie Kabae akimwona Mtangazaji mwenzie Hassan Ngoma anauliza ' swali ' la Kiingereza huwa anaonekana ' anacheka ' kichinichini?
  6. Je ni kwanini kila Mtangazaji Hassan Ngoma anapokuwa ' anatafsiri ' kwa Kiswahili kile ambacho amekisia kwa Kiingereza huwa anachukuwa muda mwingi kukieleza huku akichanganya tena maneno ya Kiingereza tofauti na mwenzake Babie Kabae ambaye ' akitafsiri ' tu kwa Kiswahili huwa yuko ' brief ' na anaeleweka vizuri na kwa haraka?
  7. Je ni kwanini kila Mtangazaji Hassan Ngoma akimaliza tu kuuliza ' swali ' lake kwa lugha ya ' Kiingereza ' hupumua kwa nguvu na ni kama vile anaona ' ameutua ' mzigo fulani ' mzito ' sana?
Nitashukuru sana kama nikijibiwa hayo ' maswali ' yangu ' Kuntu ' kabisa na naamini na nina uhakika wa 100% kuwa ' Watajwa ' au ' Watangazaji ' wote hao wa Kipindi cha 360 wapo humu JF na ni ' Members ' wa ' Kutukuka ' kabisa hivyo watanipa ' ushirikiano ' wao katika kunijibu.

Nawasilisha.
Kwani Hassan Ngoma ni muingereza?!

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
ungekuwa straight hassan ngoma hajui english vzr. anatakiwa kurudi kwa ras simba...

babie yuko vizuri mnoo hata cnn akitangaza hutaona tofauti. nilikuwa namchukulia poa hadi siku nilipomuona anamuhoji kigogo mmoja wa world bank
 
Kwaio unataka kusema kuwa bwana Hassan ngoma hajui kuongea kizungu? ??

Sent using Jamii Forums mobile app

Siamini kama kweli hajui ' Kithungu ' hasa ukizingatia ni Msomi mzuri tu tena wa Masters Degree, Mchambuzi mahiri wa masuala ya Kiuchumi na Kijamii, amesoma Ulaya tena Uingereza, ana ' Exposure ' ya kutosha tu ya mambo / masuala mbalimbali, anajuana na Watu wakubwa wakubwa wengi tena wenye ' hadhi ' zao na wa ' Kimataifa ' zaidi, Mdau mkubwa wa Habari akiwa ni Mkurugenzi wa Chuo Kimoja cha Uandishi wa Habari pande za Mbezi ya Kimara na Mfanyabiashara mzuri tu.

Hivi unawezaje kuwa na ' Sifa ' zote hizo halafu usijue Kiingereza Mkuu? Binafsi napenda mno Kiingereza chake kwani ' kinavutia ' sana.
 
Maswali yote ni yakijinga tu! Na jibu ni jepesi kwamba jamaa hakijui kingereza vizuri ma labda nikuweke sawa kutoka kwenye ulimbukeni wa watanzania wengi kwamba kujua kingereza sio ujanja na kutokukijua sio ujinga pia lugha mama kwetu ni kiswahili sio kosa unaposhindwa kuongea lugha nyingine kwa ufasaha mbona wengine kiswahili kinawasumbua na tunaona sawa tu. Nachukia sana watu wanaotukuza kingereza, ni vizuri kukijua lakini kama nitaweza kuongea na wewe na tukaelewana inatosha ujinga ni pale tu unapoanza kumcheka mtu kwa sababu hiyo

Mkuu mbona umejibu kwa ' mhemko ' sana? au una Undugu wowote labda na hao Watajwa wa 360 Clouds tv? Halafu umejibu ' Kipumbavu ' sana hivi ni wapi labda katika thread content yangu nimesema kuwa Mtangazaji Hassan Ngoma hajui Kiingereza? Kuna Watu huwa ' mnanilazimisha ' niwadharau!
 
Kwani hujui kama Lugha hiyo ni ngeni kwetu?
Ikumbukwe hata Tz, uongeaji wa kiswahili hutofautiana mkoa hadi mkoa, mtu na mtu pia.
Hata comfortability wakati wa kuongea tunatofautiana Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
weka picha zao

Nenda YouTube kisha tafuta interview ya Kipindi chao cha Clouds 360 hasa cha leo Jumanne tarehe 18, July 2017 walipokuwa na ' Wageni ' wawili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mzee Ami Mpungwe na Balozi wa sasa wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania Thami Mseleku ujionee mwenyewe ndipo utaelewa kwanini nimeyauliza haya ' maswali ' yangu ' Kuntu ' saba ( 7 )
 
wa kiume ni wakujifunza kutokana na maendeleo.

Na hao Wanaume wenyewe unaowasema ni wa wapi Je ni Nyie ( Wewe ) wa Dar es Salaam au mnaojulikana kwa ' matatizo ' yenu ya ' Kutukuka ' na ya kutia ' aibu ' au Sisi wa Mikoani na Afrika ya Mashariki? Mkuu kumbe na Wewe pamoja na ' Ujanja ' wote huo ni Mwanaume wa Dar es Salaam?

Kazi ipo hakyanani!
 
Kwa hiyo kuongea kiingereza na yenyewe ni sifa jamani. Kikubwa anaeleweka anachotaka kumaanisha basi haina shida na ndo maana baada ya mda mreeefu we ndio wa kwanza kuhoji kiingereza cha huyo hassan
 
Na hao Wanaume wenyewe unaowasema ni wa wapi Je ni Nyie ( Wewe ) wa Dar es Salaam au mnaojulikana kwa ' matatizo ' yenu ya ' Kutukuka ' na ya kutia ' aibu ' au Sisi wa Mikoani na Afrika ya Mashariki? Mkuu kumbe na Wewe pamoja na ' Ujanja ' wote huo ni Mwanaume wa Dar es Salaam?

Kazi ipo hakyanani!

purely talented and charismatic Fella


hahahaha
 
Mkuu mbona umejibu kwa ' mhemko ' sana? au una Undugu wowote labda na hao Watajwa wa 360 Clouds tv? Halafu umejibu ' Kipumbavu ' sana hivi ni wapi labda katika thread content yangu nimesema kuwa Mtangazaji Hassan Ngoma hajui Kiingereza? Kuna Watu huwa ' mnanilazimisha ' niwadharau!
Mkuu Hujasema hajui kingereza ila hilo nijibu nililokupa mimi kwamba jamaa hajui kingereza vizuri na hilo sio kosa
 
kwani kiingereza ni bora kuliko lugha yetu ya Kiswahili?,ningefurahi mno vyombo vyetu vya habari vitumie zaidi lugha yetu na kupiga zaidi nyimbo zetu

Kwani kuna Mtu yoyote labda amekataa hilo? Hivi kwanini Watanzania mnakuwa wagumu kama siyo wazito kuelewa? Hivi katika Content yangu ya ' uzi ' kuna mahala popote nimesema kuwa sipendi Kiswahili au nakitukuza Kiingereza au sijui Mtangazaji Hassan Ngoma hajui Kiingereza? Kumbe sasa nimeshajua ni kwanini hata Wanafunzi wengi wa Kitanzania hufeli mno ' Mitihani ' yao huko Shuleni na Vyuoni kwani huwa ni ' wazito ' kuelewa jambo na hupenda kukurupuka.
 
Hao watangazaji wote wana taaluma za habari??maana huko vyuoni wanasoma na lugha na namna ya kudeal na maswali...sasa Tanzania saiv kuna redio na Tv chungunzima na uwanahabari unaupata tokana na umaarufu sio taalama.Ukiona huwaelewi achana nao angalia VoA na BBC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom