Watangazaji wa 360 Clouds tv kama hamtojali nitaomba mnijibu maswali yangu haya yafuatayo...

Mkuu hizo alama za funga na fungua semi zina haribu maandiko yako sana, maana unaziweka kwenye maneno mengi sana kwenye sentensi moja.
Jaribu kuzipunguza ili maandiko yaonekane vizuri na yenye kuvutia.
nasisitiza hapa,yani zinakera sana. Unakuta ana hoja nzuri ili ukifikiria hizo alama unaona hata uvivu kusoma
 
  1. Je ni kwanini kila mnapomualika ' Mgeni ' anayezungumza lugha ya Kiingereza ni Babie Kabae tu ndiyo anauliza maswali mengi ila mwenzake Hassan Ngoma anauliza machache?
  2. Je ni kwanini kila Mtangazaji Hassan Ngoma anapouliza ' swali ' la Kiingereza mara nyingi sana huwa anatetemeka?
  3. Je ni kwanini kila Mtangazaji Babie Kabae anapouliza swali la Kiingereza anakuwa ' comfortable ' kabisa na anauliza maswali ya maana?
  4. Je ni kwanini kila Mtangazaji Hassan Ngoma anapouliza ' swali ' la Kiingereza huwa ' anatupatupa ' mno mikono na hatulii ' Kitini ' kama ' Swala ' aliyekamatwa na Simba?
  5. Je ni kwanini kila Mtangazaji Babie Kabae akimwona Mtangazaji mwenzie Hassan Ngoma anauliza ' swali ' la Kiingereza huwa anaonekana ' anacheka ' kichinichini?
  6. Je ni kwanini kila Mtangazaji Hassan Ngoma anapokuwa ' anatafsiri ' kwa Kiswahili kile ambacho amekisia kwa Kiingereza huwa anachukuwa muda mwingi kukieleza huku akichanganya tena maneno ya Kiingereza tofauti na mwenzake Babie Kabae ambaye ' akitafsiri ' tu kwa Kiswahili huwa yuko ' brief ' na anaeleweka vizuri na kwa haraka?
  7. Je ni kwanini kila Mtangazaji Hassan Ngoma akimaliza tu kuuliza ' swali ' lake kwa lugha ya ' Kiingereza ' hupumua kwa nguvu na ni kama vile anaona ' ameutua ' mzigo fulani ' mzito ' sana uliokuwa umemuelemea?
Nitashukuru sana kama nikijibiwa hayo ' maswali ' yangu ' Kuntu ' kabisa na naamini na nina uhakika wa 100% kuwa ' Watajwa ' au ' Watangazaji ' wote hao wa Kipindi cha 360 wapo humu JF na ni ' Members ' wa ' Kutukuka ' kabisa hivyo watanipa ' ushirikiano ' wao katika kunijibu.

Nawasilisha.
Brother hii misumari yako ni ya moto sana.
 
Maswali yote ni yakijinga tu! Na jibu ni jepesi kwamba jamaa hakijui kingereza vizuri ma labda nikuweke sawa kutoka kwenye ulimbukeni wa watanzania wengi kwamba kujua kingereza sio ujanja na kutokukijua sio ujinga pia lugha mama kwetu ni kiswahili sio kosa unaposhindwa kuongea lugha nyingine kwa ufasaha mbona wengine kiswahili kinawasumbua na tunaona sawa tu. Nachukia sana watu wanaotukuza kingereza, ni vizuri kukijua lakini kama nitaweza kuongea na wewe na tukaelewana inatosha ujinga ni pale tu unapoanza kumcheka mtu kwa sababu hiyo
Kama ambavyo mleta mada hapa kiswahili kimemgonga kweli. Inabidi uitengeneze mwenyewe habari ili kuelewa anacho maanisha. We all lack when it comes to languages.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hao Wanaume wenyewe unaowasema ni wa wapi Je ni Nyie ( Wewe ) wa Dar es Salaam au mnaojulikana kwa ' matatizo ' yenu ya ' Kutukuka ' na ya kutia ' aibu ' au Sisi wa Mikoani na Afrika ya Mashariki? Mkuu kumbe na Wewe pamoja na ' Ujanja ' wote huo ni Mwanaume wa Dar es Salaam?

Kazi ipo hakyanani!
Tafadhali nisaidie kujua, hivi wewe ni ke au me?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ambavyo mleta mada hapa kiswahili kimemgonga kweli. Inabidi uitengeneze mwenyewe habari ili kuelewa anacho maanisha. We all lack when it comes to languages.

Sent using Jamii Forums mobile app
Katika lugha kuna kuongea na kuandika unaweza ukawa unajua kimoja zaidi kingine
lakini tunatumia keypad kuandika wakati mwingine hatupitii tulichoandika kwa hiyo makosa kama hayo msomaji unasahihisha mwenyewe tu
 
Katika lugha kuna kuongea na kuandika unaweza ukawa unajua kimoja zaidi kingine
lakini tunatumia keypad kuandika wakati mwingine hatupitii tulichoandika kwa hiyo makosa kama hayo msomaji unasahihisha mwenyewe tu
Primary school tulifundishwa kusoma na kuandika. Yote yanawakilisha uelewa wa lugha. Asione kibanzi kwenye jicho la mwenzie wakati yeye ana boriti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom