Watangazaji wa TV wapunguze maneno wanapokuwa katika vipindi mubashara ili wataalam watoe maarifa kwa kina

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Oct 27, 2019
1,876
5,443
Wakuu salaam, moja kwa moja kwenye mada,

Kuna watangazaji wa vipindi mubashara ambavyo kuna wataalamu wa afya, elimu, viongozi nk hualikwa kwa ajili ya kudadafua mambo fulani kwa kina.

Natambua watangazaji wanajukumu muhimu la kuongoza mijadala kwa kuuliza maswali au kupokea simu za watazamaji nk, sasa unakuta mtangazaji yeye ndio mzungumzaji mwanzo mwisho.

Hapa niko natazama kipindi cha Mahakama cha ITV sasa mtangazaji anaongea ni yeye tu. Anauliza swali refuuuuuu humo humo anaelezea mawazo yake afu mgeni mualikwa akianza tu kujibu anamkatisha anauliza swali jingine refuuu huku akisimulia uzoefu wake na visa alivyoshuhudia mgeni mualikwa akianza tu kujibu swali la pili anamkatisha tena na kuanza kuchambua swali lake upya huku swali lenyewe lishaeleweka na hata hakimu alishaanza kujibu vizuri tu.

Haya baada ya dk kama mbili za porojo ndefu mgeni mualika (hakimu) anaanza kujibu na anaomba kupatiwa muda wa kutosha kuelezea na anaelezea kidogo anakatishwa tena kuna tangazo la biashara tangazo linaisha.

Tangazo linaisha msura wa mtangazaji unarudi kwenye screen anaanza kuelezea kipindi kinaruka lini mda gani, anataja majina yake anaenda mbele na kuanza upyaa kuelezea kipindi cha leo kinahusu bla bla bla tuko na hakimu flani tunazungumzia bla bla bla haya sasa hakimu anakaribishwa kabla hata hajasema neno inapigwa simu anakatishwa

Mtazamaji aliepiga simu anauliza swali akimaliza mtangazaji badala ya kumkaribisha mgeni hakimu kujibu anaanza kudadafua na kuchombezea swali (kwa mbwembwe na madaha) swali ambalo limeshaeleweka.

Cha ajabu zaidi hata zile sekunde chache anazozungumza mgeni camera ziko kwa mtangazaji, sijui hata hawaoni kasoro hii ya wazi kabisa.

Aise kipindi cha dk 30 nadhani jamaa atatumia dk 25 peke yake sasa hapa unajiuliza kulikua na mantiki gani kualika mgeni alafu mtangazaji anabwabwaja mwanzo mwisho.

20220527_141043.jpg
 
Back
Top Bottom