Watanganyika wanaoitetea DP World wana matatizo ya akili?

Watanganyika wanaoitetea DP World wana matatizo ya akili?

Kuna vitu vinachekesha hope ulisikia mtu anasema hakuna faida tutakazopata .HAYA NAKUJUZA WEW NA HAO WENZIO MSIOFATILIA VITU ,ZIFUATAZO NI FAIDA ZA UWEKEZAJI [emoji116]

Zifuatazo ni faida 12 kubwa ambazo Tanzania inatarajia kuzipata kutoka na uwekezaji wa kampuni ya DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam:

1. Kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24 tu.

2. Kuongeza idadi ya meli zitakazokuja Bandari ya Dar es Salaam kutoka meli 1,569 zilizohudumiwa mwaka 2021/22 hadi kufikia takriban meli 2,950 ifikapo mwaka 2032/33;

3. Kupunguza muda wa ushushaji wa makontena kutoka wastani wa siku 4.5 mpaka siku 2

4. Kupunguza muda wa uondoshaji mizigo kutoka masaa 12 mpaka saa 1 tu kutokana na uboreshaji wa mifumo yạ TEHAMA;

5. Kupunguza gharama ya usafirishaji wa shehena kutoka nchi za nje kwenda nchi za jirani, kutoka USD 12,000 mpaka kati ya USD 6,000 na USD 7,000 kwa kasha

6. Kuongezeka kwa shehena inayohudumiwa kutoka tani milioni 18.41 kwa mwaka 2021/22 hadi kufikia tani milioni 47.57 mwaka 2032/33

7. Kuongezeka kwa mapato ya serikali yatokanayo na kodi ya forodha inayokusanywa katika shehena inayopitishwa bandarini kutoka Shilingi trilioni 7.76 kwa mwaka 2021/22 hadi Shilingi trilioni 26.70 kwa mwaka 2032/33

8. Kuongezeka kwa ajira zinazotokana na shughuli za bandari kutoka 28,990 kwa mwaka 2021/22 hadi 71,907 ifikapo mwaka 2032/33

9. Maboresho ya magati ya kuhudumia majahazi na abiria ikiwa ni pamoja na kushawishi uingiaji wa meli kubwa za kitali (cruise ships) zitakazo ongeza idadi ya watalii nchini na kuongeza pato la taifa

10. Mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa TPA katika Bandari zote (knowledge and skills transfer)

11. Uanzishaji wa maeneo huru ya kiuchumi na kuchochea ukuaji wa sekta zingine za kiuchumi zikiwemo: sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi; utali; viwanda na biashara

12. Kuchagiza ukuaji wa sekta ndogo za usafirishaji kwa njia ya reli (SGR, TAZARA na MGR) na barabara; na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia.

Chanzo: Takwimu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
Takwimu kutoka kwa mbarawa. Na hazijaandikwa kwenye mkataba. Na asipofanikisha hivyo unamfanyaje Chief
 
Takwimu kutoka kwa mbarawa. Na hazijaandikwa kwenye mkataba. Na asipofanikisha hivyo unamfanyaje Chief
Kwani hii IGA imeonesha DP ATAFAIDIKA VIPI.MORE CONTRACTS MORE AGREEMENT ZINAKUJA.IGA SIO MWISHO KUNA HGA PIA
 
Imani, Rangi
Mwaka 2000 nikiwa Malaysia kwenye kongamano la dini ya Buddha pale Malaysia university nilikutana na mhindi mmoja tajiri aliyewahi kuishi na kutajirikia bongo.

Kwa utani unaouma na kuakisi ukweli akasema usipotajirika Tanzania ni ngumu kutajirika pengine Niliumia sana naye aliyaona maumivu yangu lakini huo ndio ulikuwa ukweli

Mkataba mbovu wa bandari zetu zote na kampuni kubwa ya DPW umeshapigiwa kelele na kila kaliba ndani ya taifa hili lakini bado kuna mazuzu wajinga wachache wanaona unafaa

Kati ya hao kuna wale walioko mamlakani ambao wamepata chochote ili kuutetea.. Hawa kwangu ni wahaini na wasaliti wakubwa na hukumu yao kuna siku itafika

Ninaowahurumia ni hawa wafuata mkumbo kwasababu za kiimani, itikati za kisiasa jinsia na wote wenye fikra finyu kwamba nwafrika hawezi kitu bila msaada wa ngozi nyeupe ama manjano..

Kinachopiganiwa ni kwa maslahi ya watoto, vijukuu, vitukuu na vining'ina vya taifa hili la Tanganyika.. Bila kujali
Imani zao
Rangi zao
Itikadi zao nk

Haya yote hawayaoni.. Inafika mahali unajiuliza je wana matatizo ya akili?
Na itikadi ndipo wanasiasa wetu wameegemea na sio utetezi kama TAIFA LA TANZANIA.
 
Kwani hii IGA imeonesha DP ATAFAIDIKA VIPI.MORE CONTRACTS MORE AGREEMENT ZINAKUJA.IGA SIO MWISHO KUNA HGA PIA
Bro HGA si ni mikataba midogo itokanayo na huu mkubwa? Nauliza huu mkataba na hayo maelezo yako hapo juu kuna sehem inaonyesha asipotekeleza afanyweje? Umesahau kuwa ni teknolojia inakuja kuendesha hiyo mitambo so hizo ajira unaweza kutufafanulia zitapatikana vip mkuu?
 
Msitutishe
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Jongea tuunguze lehemu huku tukiperuzi ya waraka
20230820_132347.jpg
20230820_124935.jpg
 
Bro HGA si ni mikataba midogo itokanayo na huu mkubwa? Nauliza huu mkataba na hayo maelezo yako hapo juu kuna sehem inaonyesha asipotekeleza afanyweje? Umesahau kuwa ni teknolojia inakuja kuendesha hiyo mitambo so hizo ajira unaweza kutufafanulia zitapatikana vip mkuu?
Halafu hiyo mikataba midogo haiwezi kwenda kinyume na mkataba mama.. Sikio haliwezi kuzidi kichwa
 
Bro HGA si ni mikataba midogo itokanayo na huu mkubwa? Nauliza huu mkataba na hayo maelezo yako hapo juu kuna sehem inaonyesha asipotekeleza afanyweje? Umesahau kuwa ni teknolojia inakuja kuendesha hiyo mitambo so hizo ajira unaweza kutufafanulia zitapatikana vip mkuu?
HGA NI MKATANA MDOGO IGA NI MKATABA MKUBWA ?
NASHUKURU UTUKANI [emoji111].

IGA NI MKATABA WA MAKUBALIANO ILA HGA NI MKATABA WA UTEKELEZAJI HUKO NDO KUNA KILA KITU THAMAN YA MRADI ,MUDA ,NA MAMBO MENGINE
 
Q

Kijana, huwa sikisii.

Hakuna kongamano wala mkutano wa ma bhuddha uliofanyika Malaysia 2000.

Unaniandikia majina, ndiyo uth8bitisho wa kongamano huo? Majina na kongamano ni vitu tofauti.

Tena kasema chuo, chuo kipi hicho?

Msifikiri wote hapa JF ni wajinga ndiyo waliwao.

Acha upimbi,nenda kwenye hoja
 
Hiki kiajuza hovyo sana kimekimbilia google na hata hiyo university anayosema haipo
Namnukuu.. Chuo chenye jina pekee bila kibwagizo ni "University Malaya (UM)".

Jina lililopo ni hili hapa.. Hiki Kimalay ambapo ukitafsiri kwa kimombo ni University of Malaysia ama Malaysia UniversityView attachment 2721919
Dah mshana jr sikumbuki lini umekasirika hivi mkuu humu JF, nipo tayari kukosolewa kwenye ili mkuu kama ushawah kukasirika ivi
 
HGA NI MKATANA MDOGO IGA NI MKATABA MKUBWA ?
NASHUKURU UTUKANI [emoji111].

IGA NI MKATABA WA MAKUBALIANO ILA HGA NI MKATABA WA UTEKELEZAJI HUKO NDO KUNA KILA KITU THAMAN YA MRADI ,MUDA ,NA MAMBO MENGINE
Bro huongei na layman . IGA ni kama katiba na HGA ni sheria ambazo haziwez kuivunja katiba ndio maana nikakuambia hayo maelezo yako yapo kwenye IGA? Au ni maneno ya msemaji?
2.) Hizo ajira zinatokea wapi wakati karibu asilimia 80 ni mitambo inafanya kazi. Naamin ulishawah kufika Dubai Port au nsalalah pale Oman au Singapore Port. Au pale Hong Kong Port. Hiv kwa mitambo ile utahtaj watu wangapi kuiendesha ili hizo ajira unazosema tuamin.
 
Wewe unaogopa teknolojia? Kaangalie google imepunguza wafanyakazi wangapi? Juzi tu hapa Ellon musk chini ya twitter.

Wanaofanya kazi serikalini nafikiria wanajua kabisa jinsi kuna ulinzi wa ajira laiti ungekuwa unajua kuna taasisi zimepoteza mamlaka na wamepewa private tangu mwaka jana na kazi zilikuwa zikifanywa na watumishi wa umma zaidi ya 200 ila bado wapo na ajira zao..

Jaribu kufikria kuhusu teknlojia halafu baadhi ya point ni dhaifu sana.
 
Hao unaowaita hawana akili wanao uhuru wa kutoa maoni yao, na hiyo Ndiyo demokrasia.

Ila kujiona mawazo yako ni bora kuliko wengine na kuwaita hawana akili ndo kutokuwa na akili kwenyewe huko, Kwa sababu kama unaakili timamu utaheshimu mawazo yao na utaendelea kusimamia msimamo wako kwa kile unachokiamini

Acheni ushamba, wale wanaoona mkataba uko sawa wasikashifiwe Kwa sababu hawajamzuia yeyote kuupinga mkataba
 
Wewe unaogopa teknolojia? Kaangalie google imepunguza wafanyakazi wangapi? Juzi tu hapa Ellon musk chini ya twitter.

Wanaofanya kazi serikalini nafikiria wanajua kabisa jinsi kuna ulinzi wa ajira laiti ungekuwa unajua kuna taasisi zimepoteza mamlaka na wamepewa private tangu mwaka jana na kazi zilikuwa zikifanywa na watumishi wa umma zaidi ya 200 ila bado wapo na ajira zao..

Jaribu kufikria kuhusu teknlojia halafu baadhi ya point ni dhaifu sana.
Hiv umeelewa nilichohoji mkuu. Mi nahoji kutokana na maelezo yake sio hisia zangu by the Way hiv hujui tatizo la ajira dunian sio? Juz nimetoka china hali ni mbaya kuliko unavyofikir hela hamna na makampun mengi na viwanga vya wazungu yanafunga Shughuli zao China wanahofia soon ngoma kama ya Ukraine itahamia china soon pale Taiwan so mchina hela nyingi kapeleka kutengeneza silaha watu wanajipanga na mtanange. Tuache hayo.
 
Back
Top Bottom