Watambue madalali wa shetani


 
Sawa kwa kutoa unapokea, sipeleki kanisani au msikitini, nawapa mwenyewe watu wanaonizunguka kwani ninawafahamu. Nimekosea?
Kusaidia maskini ni kazi takatifu, kutoa Zaka na Sadaka ni kazi njema pia, hapa jambo linalo zumgumziwa ni kwamba Viongozi wa dini wanazitumiaje nafasi zao hizo ?
Ivi utapenda sadaka yako itumike kununulia pombe au kuhonga wanawake za watu au waumini ?
Sadaka inabidi ifanya kazi njema ya kueneza Injili na kusaidia maskini.
Sadaka au zaka inapaswa impe mahitaji muhimu (kama kula na malazi) kiongozi wa Dini na inayobaki ajenge Kanisa Bora, na inayobaki aitumie kupanua kazi ya Uinjilishaji, na inayobaki awekeze katika huduma za kusaidia jamii kama Hospitali Shule nk.
Zaka na Sadaka zifanye kazi iliyokusudiwa na siyo nje ya hapo.
Ndiyo Lengo La Mada hii.
 
Waumini wengi wanapenda miujiza kuliko kumpenda Mungu na hapo ndipo wanapoibiwa wengi, mtu yuko tayari atende dhambi na machukizo ya kila aina hataki kuskia habari za Mungu ila akisikia kuna mtumishi flani anatenda miujiza na yeye huyo anajumuika
Halafu muujiza wenyewe Eti wa kupata gari la kutembelea, sasa sijui hiye service ya hilo gari nayo ifanyike kwa miujiza pia labda.
Hawajui kulihudumia gari linalo tembea ni ghalama zaidi ya kulinunua, kama huwezi kununua gari hata kulitunza hautaweza kabisa.
Hakuna muujiza mkubwa kama,
Jinsi ulivyoumbwa na kuwekwa duniani bila hiyari yako.
Jinsi ulivyo na afya njema na unaishi salama.
Jinsi unavyopata mahitaji muhimu kama chakula, hewa, maji, malazi na mavazi,
Jinsi ulivyopata bahati ya kulisikia Neno la Mungu aliyekuumba.
Jinsi Mungu alivyokuahidi kuwa hata ukifa atakufufua tena na utaishi maisha bora zaidi ya haya.
Jinsi unavyoshirikia kwa upendo na ndugu na jamaa zako.
Jinsi unavyojiweza hata kumudu kufanya kazi za kukupa ridhiki ya kila siku na kuhudumia familia yako.
Jinsi unavyo ishi kwa uhuru na amani.
Jinsi unavyopata nguvu ya kumwabudu Mungu aliyekuumba
Nakadhalika nakadhalika nakadhalika.
Hii ndiyo miujiza mikubwa zaidi uliyotendewa bila ghalama yoyote.
Utajiri wa mali sio muujiza ndiyo maana Yesu Kristo mtenda miujiza hakutaka kuwa tajiri, wala hakuwapa maskini utajiri.
Bali aliwapa afya njema kwa kuwaponya magonjwa yao, na pia aliwapa Uzima kwa kuwafufua wafu.
Kuna watu wakipata mali ndio wanaharibikiwa kabisa, na kuzama moja kwa moja kwa Shetani.
Tafuteni Kwanza Ufalme wa Mbingu hayo Mengine ni ya Ziada tu.
 
Hakuna Nabii , wanaponya wapi kiini macho na mipete yao ya Nigeria
 


Kwa hiyo ndugu yangu mshana jr baadhi ya hawa ndugu zetu tunaowachangia michango ya harusi na wao hawatoi chochote kumbe nao ni mashetani na wanafunga ndoa na mashetani wenzao?
 
Hakika dini ya Haki mbele ya Allah au Mwenyezi Mungu muumba was mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake ni UISLAM.
 
Umeongea point mkuu
 
Mshana jr leo umekuja kivingine
Niongezee tu moja pia hupenda kuita kufuatwa badala ya kufuata
Huku wakiamini Mungu wa kweli hupatikana walipo tu
 
Soma Biblia yako muujiza ni kwa watu wasioamini
Je sisi ni kipi tusichokiamini au hatujaambiwa
Na wao wanatumia nafasi vizuri
 
Mshana jr leo umekuja kivingine
Niongezee tu moja pia hupenda kuita kufuatwa badala ya kufuata
Huku wakiamini Mungu wa kweli hupatikana walipo tu
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji115] [emoji106] [emoji123]
 
baphomet goddess wa ashki..beelzebub...memphis.horus wanawasaidia watu kupata wateja kanisani inexchange of their souls
 
Hakika dini ya Haki mbele ya Allah au Mwenyezi Mungu muumba was mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake ni UISLAM.
Uislam sio DINI ni mfumo wa maisha unaowapasa watu kuishi kama alivyoishi Mudy.

Unajua maana ya Dini?

Unaweza kuthibitisha kuwa uislam ni dini?
 
Endelea kuwaamini
Mkuu kama hujamwelewa mshana hutokuja mwelewa yeyote pole yako evidence + reality hujamwelewa....
Endelea kutoa sadaka ukijua ni sadaka inaenda kunakopaswa..
 
ni kweli usemayo na ndio maana sijasema watumishi wote ni feki...ila wengi wao ndio wanachafua wenzao mifano mizuri wakiwemo hao tajwa hapo juu.


Neno mwenyewe alisema watu wake tunapotea kwa kukosa maarifa. haya yote yasingekuwepo kama watu wangeshika Neno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…