Waumini wengi wanapenda miujiza kuliko kumpenda Mungu na hapo ndipo wanapoibiwa wengi, mtu yuko tayari atende dhambi na machukizo ya kila aina hataki kuskia habari za Mungu ila akisikia kuna mtumishi flani anatenda miujiza na yeye huyo anajumuika
Halafu muujiza wenyewe Eti wa kupata gari la kutembelea, sasa sijui hiye service ya hilo gari nayo ifanyike kwa miujiza pia labda.
Hawajui kulihudumia gari linalo tembea ni ghalama zaidi ya kulinunua, kama huwezi kununua gari hata kulitunza hautaweza kabisa.
Hakuna muujiza mkubwa kama,
Jinsi ulivyoumbwa na kuwekwa duniani bila hiyari yako.
Jinsi ulivyo na afya njema na unaishi salama.
Jinsi unavyopata mahitaji muhimu kama chakula, hewa, maji, malazi na mavazi,
Jinsi ulivyopata bahati ya kulisikia Neno la Mungu aliyekuumba.
Jinsi Mungu alivyokuahidi kuwa hata ukifa atakufufua tena na utaishi maisha bora zaidi ya haya.
Jinsi unavyoshirikia kwa upendo na ndugu na jamaa zako.
Jinsi unavyojiweza hata kumudu kufanya kazi za kukupa ridhiki ya kila siku na kuhudumia familia yako.
Jinsi unavyo ishi kwa uhuru na amani.
Jinsi unavyopata nguvu ya kumwabudu Mungu aliyekuumba
Nakadhalika nakadhalika nakadhalika.
Hii ndiyo miujiza mikubwa zaidi uliyotendewa bila ghalama yoyote.
Utajiri wa mali sio muujiza ndiyo maana Yesu Kristo mtenda miujiza hakutaka kuwa tajiri, wala hakuwapa maskini utajiri.
Bali aliwapa afya njema kwa kuwaponya magonjwa yao, na pia aliwapa Uzima kwa kuwafufua wafu.
Kuna watu wakipata mali ndio wanaharibikiwa kabisa, na kuzama moja kwa moja kwa Shetani.
Tafuteni Kwanza Ufalme wa Mbingu hayo Mengine ni ya Ziada tu.