Watambue madalali wa shetani

Watambue madalali wa shetani

Mshana kwasasahivi Safina Radio ya Arusha kwakweli wanachofanya ni Biashara tu.

Wanauza mpaka maji na fruto ambazo wamepiga brand kwenye vichupa.

Mungu ni Roho...wamwabuduo wanapaswa kumwabudu katika ROHO na KWELI, ila wao wanaweka Imani za watu katika vitu kama Maji n.k badala ya katika Kristo.

Ikiwa basi ni hivyo, JE kwanini wasiwafundishe watu namna ya kuombea hayo maji kisha wakaombee maji yao nyumbani na kutumia kiimani?
Yeah imagine kitu kama hicho kinafanyiwa biashara
 
Tutawatambuaje hali ya kuwa wanatenda miujiza ya kuponya na kufufua kama manabii walio tangulia?

Kuhusu utajiri wao ni neema zitokanazo na kulishwa shambani mwa Bwana.
Waumini tumeaswa kwenye maandiko matakatifu tuwalishe watumishi wa Mungu.

Hata wateule wa zamani kina Daudi na Suleimani walikuwa matajiri wakubwa kupitia ukulima, ufugaji na uhunzi wa zana mbalimbali.

Mkuu mshana jr unataka kutuaminisha ya kwamba dhana ya uwepo wa dini ni utapeli uliotukuka?
Je, hujawahi kushuhudia matendo makuu ya Mungu ktk kuishi kwako hapa Duniani?

Tusiwahukumu kwa matendo yao na umiriki wao wa mapambo ya Dunia, vyote tutaviacha hapahapa.

Kwa Mungu kila goti litapigwa.
Kila mmoja apambane kuurithi ufalme wa Mbinguni.
Kwani wewe huamini bible juu ya kuwepo manabii wa uongo?
 
Yesu aliwalisha watu elfu tano wakala wakasaza .
Nabii Au mtume wa uongo analishwa Na watu elfu tano.
Wewe tulishawahi kukutana sehemu nini? maana niliwahi kusema sentensi hiyo watu walicheka sana
 
Geor Davie ni Nabii wa uongo,Muhuni wa wanawake na Tapeli

Mwamposa ni nabii wa uongo na Tapeli

Lusekelo ni mhuni, chapombe na mpenda pesa

Gwajima ni mpenda pesa, Mwanasiasa na Msanii ila mwenye ujasiri wa kuwatetea watanzania.

SAFINA RADIO ina watumishi wapenda pesa wasio na huruma kwa wamama masikini wanaochukua pesa zao. wa kwanza ni mkurugenzi wao DANIEL LEMA.

Akina manyau nyau na Sheikh sharrif majini ni wasanii wenye majini na ujinga kichwani.

Wengi wao wanarushwa na Channel 10.


Ashakhum si matusi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom