Watambue madalali wa shetani

Watambue madalali wa shetani

Hongera sana mtoa hoja, je kumpa Mungu asilimia kumi ya mali yako imekaaje? Mungu amechoka kiasi cha kuhitaji pesa yako?
 
hii ya leo ni kibokoooo
nimefurahi sana, kumbe uko pande zote mkuu maana naona watu wakishindwa kulala usiku wanakukumbuka sana,
hii imedhihirisha kuwa ushauri pande zote uko makini
big up mkuu
 
Sawa kwa kutoa unapokea, sipeleki kanisani au msikitini, nawapa mwenyewe watu wanaonizunguka kwani ninawafahamu. Nimekosea?
 
Hawa si wengine bali ni mitume na manabii wa uongo (sio wote, namaanisha mitume na manabii wa uongo)
Utawambuaje?
Hawatoi bali wanapokea
Hawafuati bali wanafuatwa
Hawachangi bali wanachangiwa
Hawalishi bali wanalishwa
Hawahudumii bali wanahufumiwa
Kwao kila kitu ni fedha
Mahubiri yao ni utajiri na kutenda miujiza... Wanashindana kwa vitu vya kidunia.. Utajiri, vyombo vya usafiri, (magari boat, meli ndege nk) mavazi ya bei ghali, majumba ya gharama kubwa nknk... Ni watu wasiopitwa na fasheni yoyote
Ni wachoyo na ni wa binafsi wamepiliza! Pesa zao zinazotokana na kuwakamua waumini maskini na wenye uhitaji hawazitumii kwa manufaa ya jamii bali wao wenyewe na watu wao wa karibu
Pamoja na mabilioni wanayomiliki daima utawakuta mitandaoni wakishindana kupost vitu wanavyomiliki vya bei ghali...
Wakiamua kuwekeza pesa zao hizo ni kwenye biashara na kamwe sio kwenye huduma za kijamii kwa wasiojiweza kama lishe elimu afya na vituo vya misaada kwa walemavu yatima na yeyote mwenye uhitaji wowote .. Haya sio yao haya hayawahusu. ..
Watu wa kaliba hii wanaojipenda kujikweza na kupenda kutukuzwa, wapenda Mali na ibada za karamu zilizojaa ukakasi mwingi ni makuwadi wa kuzimu na madalali wa shetani

NB: Niombe radhi kwa wale watakwaza na hii mada
Mukuu naona unamchokoza gwajima jiandae kama bashite koromije malyangili.
 
Kwa kweli hili kama janga fulani hivi.

Mi nina maza yangu mdogo kawa mteja wa huyo bulldozer mwamposa basi kutwa ni stori zake tu huyo jamaa na jinsi anavyosaidia watu ukijumlisha na yeye mwenyewe maana ni mfanyabiashara sasa anadai tangu aende kule biashara yake iliyokuwa inataka kufa imefufuka ghafla na anauza kweli kweli yani! Hapa alipo anatusumbua wanae tumpe picha zetu azipeleke zikaombewe ili tulio mazuzu darasani tuwe vichwa,tusio na kazi tujaliwe kuzipata nk.. Imekuwa kero sasa maana kila siku simu akitaka tumpelekee hizo picha....hapa yenyewe kila wiki tunaletewa mafuta na maji ya kunywa 'aliyoombea' jamaa hahahaha
naona maza kashatafunwa tayari,chezea mchungaji anapotamani kondoo.
 
Tutawatambuaje hali ya kuwa wanatenda miujiza ya kuponya na kufufua kama manabii walio tangulia?

Kuhusu utajiri wao ni neema zitokanazo na kulishwa shambani mwa Bwana.
Waumini tumeaswa kwenye maandiko matakatifu tuwalishe watumishi wa Mungu.

Hata wateule wa zamani kina Daudi na Suleimani walikuwa matajiri wakubwa kupitia ukulima, ufugaji na uhunzi wa zana mbalimbali.

Mkuu mshana jr unataka kutuaminisha ya kwamba dhana ya uwepo wa dini ni utapeli uliotukuka?
Je, hujawahi kushuhudia matendo makuu ya Mungu ktk kuishi kwako hapa Duniani?

Tusiwahukumu kwa matendo yao na umiriki wao wa mapambo ya Dunia, vyote tutaviacha hapahapa.

Kwa Mungu kila goti litapigwa.
Kila mmoja apambane kuurithi ufalme wa Mbinguni.
kama Yesu angeamua kutumia hii neema angekua tajiri wa kupitiliza mpaka sasa. aliweza kufufua mpaka wafu na kujifufua mwenyewe.lakini bado aliishi na kufa kimasikini kabisa.
 
Geor Davie ni Nabii wa uongo,Muhuni wa wanawake na Tapeli

Mwamposa ni nabii wa uongo na Tapeli

Lusekelo ni mhuni, chapombe na mpenda pesa

Gwajima ni mpenda pesa, Mwanasiasa na Msanii ila mwenye ujasiri wa kuwatetea watanzania.

SAFINA RADIO ina watumishi wapenda pesa wasio na huruma kwa wamama masikini wanaochukua pesa zao. wa kwanza ni mkurugenzi wao DANIEL LEMA.

Akina manyau nyau na Sheikh sharrif majini ni wasanii wenye majini na ujinga kichwani.

Wengi wao wanarushwa na Channel 10.

Ashakhum si matusi
Baba umenena kweli.hawa ni wapiga dili wakutupwa.pesa wanazowakamua waumini wao Mungu anawaona
 
Mi nafikiri tunashindwa kutofautisha mambo hapa.Wale watu si kwamba wao wanakuponya au wanatatua shida zako,bali imani yako.Wanachokifanya kikubwa ni kukuongoza tu ili imani yako itokee kwenye maandiko matakatifu.Ndio maana mzazi wako alipoongozwa na huyu mchungaji na yeye akaweka imani basi akaanza kuona mabadaliko.Kwa mjadala huu tutaaminishwa kuwa watumishi wote ni manabii wa uongo.Ni seme tu kwamba hawa jamaa wamejikita kutafasiri neno la mungu physically yaani katika mambo ambayo ni matamanio ya mwili na si spiritually.Kutafasiri neno la Mungu kiroho unahitaji roho mtakatifu,hapo dipo nguvu za kumbadilisha muumini zinakuwa za kudumu.Kimsingi hawa manabii wengi wao wamekosa nguvu za roho mtakatifu ndio maana wamebaki kutumia nguvu zao wenyewe kuwaaminisha watu kwa kuonyesha utajiri.Na kwa sababu imani yako ndio inakuponya basi wanajithidi wavute imani za watu ili waonekane wana Mungu.Changamoto ni kwamba wale wanaotengeneza imani zao kwa kuangalia uwezo wa nje wa hao jamaa wanakuwa katika matatizo yasio isha kila siku unakuta wanatoka kwa huyu wanaenda kwa huyu matatizo yao yanapoa kwa muda tu.Utawatambua kwa kauri zao,wanavyowasifia hao manabii kwa majina bila kutambua jina la kristu.
Hawa manabii ni mara chache sana kuubiri injiri ya kutoa kwa masikini,kwa wajane,kwa wakimbizi,kwa wagonjwa,na kwa yatima au kwa kifupi injiri ya Upendo kwa wengine.Kwa sababu injiri hiyo ndipo kristu alipo na wao hawapo kwa ajili ya kristu hapo ndipo nakubaliana na mleta mada.
Tambua ndugu kuwa mtu yeyote anaweza akauubiri injiri,lakini si kila mtu anaweza kuubiri injiri takatifu,Mtu yeyote anaweza kubeba Biblia na hata kuisoma mpaka akapata Phd,lakini si kila mtu ana uwezo wa kubeba Biblia takatifu,na kuisoma.Hata sadaka wanazotumia kujenga na kununua magari ya kifaari na ndege,si kwamba wanatumia sadaka takatifu kwa sababu mtu yeyote ana uwezo wa kutoa sadaka awe ameua,awe ameeiba wao wanachukua tu,ila si kila mtu ana uwezo wa kutoa sadaka takatifu na hata kuitumia sadaka takatifu utaongozwa na roho mtakatifu.Si kwamba yesu Kristu waumini waliokuwa wanamfuata walikuwa hawatoi sadaka za kumfanya awe tajiri kimwili,bali alizigeuza na kuwa sadaka takatifu kwa kuimiza Upendo kwa walio masikini na wenye shida.
Amen kwa somo
 
Dada zetu na mama zetu ndio wahanga wakubwa wa hawa madalali,wanaume ni wachache.
 
Hongera sana mtoa hoja, je kumpa Mungu asilimia kumi ya mali yako imekaaje? Mungu amechoka kiasi cha kuhitaji pesa yako?

Nijuavyo ikiwa sijakosea...kuna Sadaka maalum za aina 3, sawasawa na maagizo ya Biblia Takatifu.

Sadaka ya moja ya kumi (Ten percent) inayotokana na jasho lako la kuajiriwa ama kujiajiri. Inaitwa ZAKA.

Sadaka ya Shukran kwa yale aliyokufanyia Mungu wako, haijalishi ni mazuri au mabaya...Biblia inatuambia Shukuruni kwa kila jambo. Inaitwa DHABIHU

Sadaka ya Mzaliwa wa kwanza wa Mazalia ya mifugo au kilimo chako. Mfano unaanza kufuga ng'ombe au mbuzi dume na jike, watakapozaa kwa mara ya kwanza kabisa...yule ndama usimwache pale zizini mpeleke kama sadaka katika madhabahu ya Mungu....Inaitwa MALIMBUKO.

Sasa katika sadaka hizo...hiyo DHABIHU/SHUKRAN unaweza kuamua kuipeleka kwa Watoto yatima,kwa wagonjwa mahospitali, Masikini na wenye shida na taabu mbalimbali.

LAKINI : Nathubutu kukuambia katika sadaka hizo zote usije ukacheza na ZAKA yaani 1/10. Mungu mwenyewe anasema usipoitoa umemwibia.

Madhara ya kutotoa ZAKA ni makubwa sana na ni mengi kama:-

1) Kufilisika kabisa

2) Pesa/Mshahara wako kutokufanya chochote cha maana mpaka unakwisha

3) Kufutwa kazi / kufa kwa Ajira kabisa kwakuwa unakosa ulinzi na utetezi wa Mungu katika Ajira yako.

4) Kuaibika, kutokutoa ZAKA pia kunakusababishia AIBU katika maisha.

USHAURI: Jitahidi sana usiache kutoa SADAKA haswa ZAKA ila hakikisha unatoa katika MADHABAHU SAHIHI kwa MTUMISHI SAHIHI.

Barikiwa.
 
Kichwa changu kimeathiriwa na kirusi sisiem, hicho kichwa cha habari nilikisoma "Watambue madalali wa madiwani" serious.
 
umenena kweli tupu mkuu!
 
Back
Top Bottom