Mdeke_Pileme
JF-Expert Member
- Aug 24, 2013
- 1,563
- 2,126
Baada ya jukwa la JamiiForums kuchapisha nakala kwenye mitandao ya kijamii inayosema :-
Bodi ya Maabara Binafsi za Afya ambayo ipo chini ya Wizara ya Afya imesema inayafanyia kazi madai kuwa baadhi ya Maabara zinatoa majibu ya uongo ili Zahanati ziuze Dawa, ikiwa ni ufafanuzi uliotolewa baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuibua hoja hiyo.
Soma:
Bodi hiyo imesema kwa kushirikiana na Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi imeanza ufuatiliaji na itachukua hatua kwa wote watakaobainika kufanya vitendo hivyo
Bodi imetoa wito kwa Wananchi kutoa taarifa za vitendo vya aina hiyo ya Wataalam wanaotoa majibu yenye mashaka au ya uongo ili waweze kuuza Dawa kwa kupiga simu ya bure na 199 na kutoa taarifa.
MAELEZO YA WATAALAMU WA MAABARA YALIYO TOLEWA KUPITIA UKURASA WAO WA INSTAGRAM :-
KWA HESHIMA KUBWA.
• Tunapenda kuwasilisha ushauri kuhusu suala la uchache wa wataalamu wa maabara kazini katika vituo vya afya, na athari zake kwa huduma za afya. Hali hii inahitaji kuchukuliwa hatua madhubuti ili kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa wananchi.
• Athari za Vipimo Kupimwa na Wasio Wataalamu wa Maabara au watu ambao hawana mafunzo sahihi ya maabara, kuna hatari kubwa ya matokeo potofu au ya uongo kutolewa. Hii inaweza kusababisha kutopata tiba sahihi au matibabu yasiyo na ufanisi, hii ni pamoja na kutokuajili wataalam wa maabara wa kutosha katika vituo vya afya, Hali hii inaleta athari mbaya kwa utoaji wa huduma za afya. Kutokana na hali hii, tunapendekeza serikali ichukue hatua zifuatazo:
1• kufuta Sheria ya mwaka 2007 inayo ruhusu wasiokuwa wataalam wa maabara kufanya vipimo vya mkojo na damu katika vituo vya afya, zahanat pamoja na hospital, kwa sababu wataalam wa maabara wapo wa kutosha na bado wapo mitaani bila ajira.
2• Tunapendekeza serikali iweke mikakati ya kuacha kuwapa vipaumbele watu ambao si wataalamu wa maabara [ NON LAB TESTERS ] katika vituo vya afya serikalini pamoja vituo vya afya binafsi . Hii itahakikisha matokeo sahihi ya vipimo na ubora wa huduma za afya. Njia za kufikia lengo hili ni pamoja na kuimarisha mchakato wa ajira kwa kutoa kipaumbele kwa wataalamu wa maabara wenye sifa sahihi, kutoa mafunzo kwa wafanyakazi ikiwemo semina kwa wataalamu wa maabara , pamoja na kuweka masharti ya kisheria ya kuajiri wataalamu wa maabara.
3• Kuunda sera na mipango ya kuhamashisha wataalamu wa maabara kufanya kazi katika vituo vya afya, ikiwa ni pamoja na kuweka mishahara stahiki.
4• Kuweka mifumo imara ya udhibiti wa ubora ili kuhakikisha vipimo vinapimwa na wataalamu wa maabara wenye ujuzi na matokeo yanatolewa kwa usahihi.
KWA HESHIMA,
• Tafadhali tunaomba Wizara ya Afya itoe kipaumbele katika kuajiri wataalamu wa maabara kwa kuzingatia ripoti iliyotayarishwa na wataalam wa maabara inayobainisha upungufu mkubwa wa wataalamu wa maabara katika vituo vya afya. Kufanya hivyo kutaimarisha huduma bora za afya na kukuza ustawi wa jamii.
TANZANIA MEDICAL LABORATORY ASSOCIATION- TMLA
[ EMAIL : TMLA@secretary.net ]

- https://www.jamiiforums.com/threads...ambayo-hawana-ili-zahanati-ziuze-dawa.2185841[/URL]
- Ofisi ya Msajili Bodi ya Maabara Binafsi za Afya yasema inafanyia kazi Madai ya Maabara kutoa majibu ya Uongo