Haya ndiyo mahangaiko ya vijana wa Tanzania

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Ila we are being very unfair kwa vijana wa Tanzania. Everyone is pointing fingers at them but no one is ever saying “this is how I’ll help them”. Vijana hawawi tu, vijana wanatengenezwa. Na linapokuja suala la uwezo wa vijana wa tanzania they’re the victims, not the enemies.

Ujuzi na uwezo na umakini ambao tunautaka uwe ndani ya vijana hauwekwi muda sahihi. By the time kijana wa Tanzania ana miaka 23, anawaza kusaidia wadogo zake, Jumanne rejesho la mama, kupata connection na kujiuliza kila wakati kama amepoteza miaka yake maana haoni matunda.

Unahitaji level fulani ya kujitambua, na kujiamini kuweza kutoboa nje ya mazingira uliyokulia hapa Tanzania. It’s a tough place kama udogoni haukubadilishwa mindset. Ukubwani ni kama kama unataka hiki inabidi usacrifice kile. Ujichange usome masters au hiyo hela ufanye biashara?

Uendelee kuvumilia kazi ambayo inakutesa au utafute nyingine? Na hiyo nyingine utapata?
Ukweli ni kwamba kijana wa kawaida wa Tanzania anakosa muda wa kufanya mambo ya muhimu kwa sababu anahangaika kutatua mambo ya haraka. Hana luxury ya kuwaza kesho maana leo inakaribia kumuua.
Kuweza kuwa wa kipekee, na kuwaza kesho yako kwa umakini zaidi, unahitaji kutokuwa na wasiwasi na leo yako. Na vijana wengi hawana uhakika na leo yao. So tuwaelewe tu na tukubali ni matunda ya mazingira yetu.

Kama tunataka vijana wa tofauti, tutengeneze mazingira tofauti.And the way tunaweza kufanya hivi ni either:

1. Tangu wakiwa wadogo tujenge values za kufikia kipekee kuhusu maisha. Maana wakiwa wakubwa muda wa kuwaza kesho wakati leo inakuua huna.

2. Vijana wakubwa watengenezewe centers nje ya mazingira ya nyumbani wanapoweza kujiboresha.Umaskini ni jambo expensive sana. Unakunyima nafasi ya kijibadilisha maana kila siku linazuka jambo. Ndio maana inabidi kusaidia vijana kujikaza na kuonyesha njia PRACTICAL za namna ya kutoboa kwenye mazingira yetu.

Sio kila siku kutoa maneno cliche ya work hard, be aggressive sijui, plan long term. HOW? Tuwaelezee HOW can they plan long term huku mshahara laki 4? Sio kwamba haiwezekani but show them HOW.

Hili suala naweza kuongea mpaka kesho na linaniuma maana nimekuwa nikifanya kazi kwenye sekta ya elimu kwa miaka 9 sasa nikideal directly na vijana.

It’s not as easy as it seems. Vitabu vya nje haviangalii context yetu so ushauri mwingi haufanyi kazi. We need our own blueprint.

We want different vijana, we need to be a different community. Simple. But to complain about the product of our environment is just myopic.

Chukua kijana mmoja, jaribu kumbadilisha ndani ya mwaka. Utajifunza mengi sana yanayomzunguka.

Muwe na siku njema.Na kwa vijana hii haimaanishi kwamba inabidi uridhike hapo ulipo. Excuses zako zinaweka kuwa za kweli ila hazitabadilisha maisha yako. No one is coming to save you.

My advice ni kwamba kama upo kwenye mazingira ambayo hayakubadilishi, HAMA. Huwezi kuwa bora kuliko mazingira yako.Bora uanze 0 kwenye mazingira mapya kuliko kuwa hapo hapo ulipokuwa kwa miaka 10 na unaona kabisa hakuna mtu amewahi kutoboa hapo.

Ukishafanya hivyo jambo ya pili ni kuformat ubongo. Kuna aina fulani za kufikiri mazingira ya shida yanakupa. Haya ya kuformat.

Nakumbuka baba alisemaga hata kujitolea (volunteering) ambayo wengi wanahamasisha vijana ni Privilege na inadiscriminate against the poor. Ukiwa maskini huwezi kuafford kujitolea BURE, yani nyumbani huna shock absorber; nauli unatoa wapi? Wadogo zako wanakula nini? Kodi unalipaje?

Imeandikwa na @givenality
 
Ila we are being very unfair kwa vijana wa Tanzania. Everyone is pointing fingers at them but no one is ever saying “this is how I’ll help them”. Vijana hawawi tu, vijana wanatengenezwa. Na linapokuja suala la uwezo wa vijana wa tanzania they’re the victims, not the enemies.

Ujuzi na uwezo na umakini ambao tunautaka uwe ndani ya vijana hauwekwi muda sahihi. By the time kijana wa Tanzania
Asante kwa madini
 
Mfumo wa maisha ya kibepari ndio upo hivyo. Wachache ndio wananufaika na jasho la wengi.

Kodi tunazotoa ndio zinatumika kuwalipa watawala ambao hawana muda kuangalia namna ya kutatua changamoto na msoto wa vijana.

Watawala wanakuja na short term solutions tu hawafikiri miaka 50 mbele. Mfano wanaweza kuwapa mikopo vijana wa elimu ya juu na diploma kisha kuwatelekeza bila kutengeneza ajira.

Yapo mengi ila hii nchi kundi linalonufaika ni la watawala. Vijana ni sauti ya umma iliyosahaulika.
 
PLANS=>GOALS=>DREAMS.
Take risk, be Focused, Committed and Consistent=> DESTINY.
No one is coming to live your life on your behalf, but only yourself.
 
Back
Top Bottom