Nimeshindwa kukusaidia leo usinichukie, kesho yetu ni fumbo

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
NIMESHINDWA KUKUSAIDIA LEO USINICHUKIE, KESHO YETU NI FUMBO.

Based On True Story

Miaka kadhaa iliyopita, rafiki yangu wa miaka mingi alipata ajali mbaya sana. Ilibidi afanyiwe operation ili kuokoa maisha yake.

Nikiwa kama rafiki yake wa karibu, alinipigia simu kuniomba nimtumie kiasi fulani cha fedha ili kimsaidie katika matibabu.

Lakini sikuweza kumpatia chochote kwani hali yangu kifedha ilikuwa sana.

Nilishindwa hata kufika hospitali kumjulia hali, kwani nilikuwa mbali na sikuwa hata na pesa kidogo ya nauli kutoka mahali nilipo hadi hapo hospitali.

Mbaya zaidi niliishiwa hata pesa ya kula. Kila mtu niliyemfikilia kumkopa alikuwa ananidai. In short, nilionja joto ya jiwe.

Rafiki yangu alipata msaada kutoka kwa watu wengine, baadae akapona japo alikuwa amepata ulemavu wa mguu wake wa kushoto.

Lakini alinikasirikia sana na alinichukia kupita kiasi, kwani kama rafiki aliona nilishindwa kumsaidia.

Miezi miwili baadae nilibahatika kupata kazi fulani ya muda mfupi ambayo ilinipatia kiasi fulani cha fedha.

Nilifanikiwa kulipa madeni yangu na nikaamua kwenda kumjulia hali na kumuomba msamaha rafiki yangu, kisha nimpatie chochote kitu.

Uwezi amini, rafiki yangu alinifukuza nyumbani kwake lakini baada ya watu kumsihi alikubali kunisikiliza.

Nilimweleza hali ngumu niliyokuwa nikipitia wakati ule. Nikampa na kiasi fulani cha fedha.

Nilifurahi, kwani alipokea na kunishukuru sana. Kiasi kile kilimsaidia kulipa madeni aliyokopa katika kipindi cha kujiuguza.

Baada ya siku chache nilipata nafasi ya kuajiliwa katika kampuni moja kubwa hapa nchini.

Lakini sikuwa na elimu ya kutosha kuajiliwa katika kampuni ile. Niliambiwa nigushi hata vyeti lakini nilikataa.

Niliamua kumuunganisha rafiki yangu katika kampuni ile kwakuwa yeye alikuwa na elimu kubwa inayohitajika lakini alikosa kazi kwa muda mrefu kutokana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini.

Ni kweli, kupitia mimi rafiki yangu alipata kazi na kufanikiwa kubadilisha maisha yake na familia yake kwa ujumla. Kiufupi kwa sasa jamaa ni tajiri mkubwa sana.

Nami kwa upande wangu, maisha sio mazuri sana, lakini pia sio magumu. Urafiki wa kweli umetusaidia kupiga hatua kadhaa mbele.

JIFUNZE,
Mtu akishindwa kukusaidia leo USIMCHUKIE. Huwezi jua kuna magumu kiasi gani ambayo naye anayapitia. Kesho yetu ni FUMBO pengine atakufaha sana kuliko kumchukia na kuvunja undugu au urafiki.

#no_learning_no_earning
So we have to Learn.

Prepared By
Mr George Francis
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
IMG_20231019_220420_056.jpg
 
View attachment 2817547
 
Back
Top Bottom