Wataalamu na masuala ya teknolojia naombeni msaada wenu

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,425
9,818
Mimi ni kijana wa kiume umri miaka 30 nina tatizo la usikivu hafifu ambalo lilinianza nikiwa na miaka 14 au 15 hivi. Nashindwa kumsikia vizuri mtu akiwa mbali, anaeongea kwa sauti ya chini sana, mtu anaeongea haraka, mtu mwenye kigugumizi, mtu akiniongelesha tukiwa kwenye makelele na pia nashindwa kusikia vizuri sauti ambayo inatoka kwenye vyombo vyenye spika mfano tv, kompyuta, simu, redio n.k ila mtu ambae tupo karibu sehemu yenye utulivu namsikia vizuri tu

Pamoja na kuzunguka hospitali kadhaa sijawahi kupata suluhisho mara ya nilienda CCBRT niliambiwa nina tatizo la nerves, nikapewa dozi lakini hazikusaidia chochote, niliambiwa pia naweza kutumia hearing device lakin gharama yake ni kubwa na pia kuna risk ya kuongezeka kwa tatizo nikaachana na huo mpango kwa sasa nimekubali hali halisi labda siku nitakayopata msaada wa kwenda kutibiwa nje., naskia Marekani na India wanatibu hili tatizo.

Maombi yangu kwenu kwa wataalamu wa masuala ya teknolojia naomba kujua kama kuna program au app yoyote ninayoweza kuinstall kwenye simu ili mtu akinipigia anapokua anaongea yawe yanakuja na maandishi kueleza anachoongea yaani kama subtittle kwenye movie maana nakoswa na fursa nyingi sana kwa kushindwa tu kuwasiliana na mtu kwa maongezi kwenye simu.

Asanteni sana
 
Pole mkuu!! Geukia hata kwa Mungu,anaponya hayo mkuu! Jaribu hata kwenda kwa Mwamposa ukatumie maji na mafuta
pole Sana ndugu yangu Hilo ni tatizo na nikushauri ungeenda kuonana na ma specialist pia nikutoe hofu sio wewe Tu yupo mwenzako mwenye tatizo kama Hilo ila yeye anasema tangu utoto yupo hivo na ataendelea kuwa hivyo nadhani kwako ni damage uliipata labda uliwahi kusikia sauti kubwa zaidi ya uwezo wa masikio ikapelekea damage huko ndani au uliwahi kupata ule ugonjwa wa kutokwa usaha masikioni ukaharibu baadhi ya viunda mitetemo huko ndani pia linaweza likawa tatizo la ubongo all in all my friend nakushauri ungeenda kuonana na ma specialist
 
Pole sana kwa changamoto hata mimi ninayo hiyo changamoto
tatizo lilianza baada ya kutumia dawa za quinine
 
Back
Top Bottom