Wataalam wa matibabu wa China waleta matumaini kwa wenye matatizo ya macho Burundi

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
gfdgdgs.jpg


fdsafsafa.jpg


Kikundi cha 20 cha madaktari wa China kilichotumwa nchini Burundi hivi karibuni, sasa kinaendelea kuwafanyia watoto upasuaji wa macho bila malipo katika mpango wa msaada wa matibabu Mkoa wa Giheta katikati mwa Burundi.

Katika utekelezaji wa mpango huo ulioanza mapema Aprili, wagonjwa 47 wenye mapato ya chini walifanyiwa upasuaji wa macho katika Hospitali ya Umugiraneza wilaya ya Giheta. Ubalozi wa China nchini Burundi pia ulitoa vifaa vya matibabu kwa kliniki za macho za eneo hilo.

"Tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na serikali ya Burundi ili kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika huduma za matibabu na afya. Na tutasaidia nchi za Afrika kuboresha uwezo wao wa afya ya umma na kujiendeleza," anasema Zhao Jiangping ni Balozi wa China nchini Burundi.

Katika ziara yake kwenye hospitali hiyo, Mke wa Rais wa Burundi Angeline Ndayishimiye akiambatana na Balozi Zhao na Waziri wa Afya ya Jamii na Udhibiti wa Ukimwi wa Burundi Sylvie Nzeyimana, walipongeza mchango wa China katika kuhimiza maendeleo ya afya ya umma nchini Burundi na kusaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu nchini humo.

Alisema Burundi itaendeleza ushirikiano wa kina na China katika matibabu na mafunzo ya wafanyakazi, ili kuimarisha urafiki kati ya watu wa pande zote mbili.

"Upasuaji wa macho unaweza kuwapatia watu binafsi na familia fursa ya kuondokana na umaskini na upofu. Na inaweza kuwa na athari chanya kwa jamii. Ni jambo zuri sana," anasema Wang Qian mmoja wa madaktari wa China.

Ujumbe wa 20 wa madaktari wa China uliotumwa Burundi umekuwa ukifanya kazi nchini humo kwa mwaka mmoja. Hapo awali, mwaka 2016 na 2018 China ilituma madaktari kutoa msaada wa matibabu hasa kwenye upasuaji wa macho.

Burundi na China zilianzisha uhusiano wa kibalozi mwaka 1963, huku ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ukilenga sekta kadhaa zikiwemo afya ya umma, nishati, elimu na miundombinu. China ilianza kutuma wataalam wa matibabu nchini Burundi mwaka 1987.
 
Xi jing Ping kashafanya yake hapo sio bure
Burundi ilipewa msaada wa kujengewa ikulu na China. Inashangazaaa
 
Xi jing Ping kashafanya yake hapo sio bure
Burundi ilipewa msaada wa kujengewa ikulu na China. Inashangazaaa
You are brilliant, si kila jambo toka China ni jema, usishangae kuna taifa karibu na hapo linanyemelewa, utakuja sikia "...si unaona jirani yako tulivyomsaidia!"
 
You are brilliant, si kila jambo toka China ni jema, usishangae kuna taifa karibu na hapo linanyemelewa, utakuja sikia "...si unaona jirani yako tulivyomsaidia!"
atashinda zabuni ya SGR kuja Tz kutokea Burundi...
 
Back
Top Bottom