Watu 15 wenye matatizo ya moyo kunufaika na Kambi maalumu ya siku tano inayowahusisha wataalamu kutoka JKCI na Marekani

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Katika jitihada za kuboresha zaidi utoaji wa huduma,Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Shirika la Cordiostart International la Nchini Marekani wanatoa mafunzo ya siku tano kwa wataalamu mbalimbali wa hospitali hiyo yanayojikita katika kuwaongezea ujuzi kwenye michakato ya upasuaji wa moyo.

Akizungumzia mafunzo hayo yanayoambatana na kambi maalumu Mach 11, 2024 , Mkurugenzi wa JKCI, Dr. Peter Richard Kisenge amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea ujuzi wa kuwahudumia wagonjwa watakaopandikizwa moyo, ambapo ujuzi huo ni kabla ya zoezi, baada ya zoezi, na wakati wa zoezi la upandikizaji wa moyo.

Amesema kuwa "Tunategemea mpaka hii wiki itakapoisha tutakuwa timewafanyia wagonjwa karibia 15 lakini pia wataalamu wetu 160 watapata elimu mbalimbali kuazia wauguzi, wataalamu wa vifaa tiba, madaktari bingwa wote watapata elimu katika hii wiki nzima wa kitengo cha upasuaji na tiba ya moyo."

Amesema ujio wa wataalamu hao nchini unaifanya taasisi hiyo kuokoa zaidi ya milioni 500 kama wagonjwa hao 15 wangeenda nje ya Nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu hayo ya kibingwa, ameeleza kuwa watu hao watapatiwa matibabu ya upasuaji wa moyo na upasuaji wa mishipa ya damu kupitia kambi maalumu ya wataalamu kwa muda wa siku tano.

Amesema kuwa wadau hao kutoka Marekani kwa kushirikiana na wadau wengine wamewezesha pia upatikanaji wa zaidi ya vifaa vyenye thamani ya Milioni 200 ambavyo vinatumika katika kuwahudumia wagonjwa wa moyo.

Pia ameeleza kuwa ni zaidi ya miaka 5 sasa tokea JKCI ianze kutoa huduma za upandikizaji wa moyo na kuwa huduma hizo zimeendelea kuimarika kutokana uwekezaji wa vifaa vya kisasa ambavyo vimeongeza ubora wa huduma ikiwemo kuwavutia watu wengine kutoka nje ya Tanzania hususani ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kufika hospitalini hapo kupatiwa huduma.

Lakini amesema kuwa mazingira hayo pia yamechangia kuvutia wadau zaidi ya 20 ambao wameingia nao mashirikiano mbalimbali katika kuboresha huduma mbalimbali.

Ambopo amebainisha wazi kuwa JKCI ilianza kushirikiana na Shirika la Cordiostart International mwaka 2019 na kuwa tayari wameshafanya kambi maalumu za matibabu moyo tano.

Aidha kwa upande Shirika la Cordiostart International wameeleza tija ya ushirikiano huo kuwa unasaidia kukuza ujuzi kwa wataalamu na wamepongeza jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na taasisi hiyo.

Screenshot_20240312-131959_1.jpg
 
Back
Top Bottom