Wataalam wa bajeti za ndoa njooni hapa

Hivi kwani mke unamnunua kwanza hiyo umewapa nyingi mkuu ungekomaa na kilo yako moja swaafii kabisa ...

Hiyo iliyobaki nenda kwa supplier wa vinywaji vya azam nunua full sana zisizidi za 9800
Kuna yake maandazi ya azam chukua mifuko ya kutosha ..ata ya 9600 apo wanakula kabisa mengine bajet
 
Wakati nasoma post hii nje nasiki kigoma cha arusi sijui kaolewa nani wanapita njiani......mkuu iyo 95 ndio yakuanzia matumizi yakumwachia wife pindi uendapo job.....pi waambie harus ni 24 hrs baada ya hapo unaingia kazini kama sio wewe uliye owa jana yake...
 
Haaaaahahah
Seneta ni Nyokoooo sana wewee.
Yaan nimecheka kuanzia aya ya kwanza mpaka conclusion yako.
Big up Seneta wa Mtwiz.
 
Wakuu,

Baada ya mbinde ya miezi kama mitatu hivi ya kubishana na upande wa ukweni kuhusu kipengele cha mahari hadi nikaweka mgomo na kuzila kuwa nimeghairi kuoa kwenyewe,
Hatimaye jana wamekubali kushuka kutoka Milioni 2.5 mpaka 145,000/= ambayo angalau inakaribia laki 1 ambayo nd'o niliipanga kwa upande wangu.

Na nimeshawapiga biti kuwa sitaki wanihusishe kwenye gharama za upuuzi wa sendiofu wala pumba gani.

-----------
Sasa wakuu,
Hapa nataka wataalam wa bajeti wanichanganulie hii elfu 95 yangu niliyobakiwa nayo
ili niweze kukamilisha shughuli ya ndoa.

Angalizo:
Usafiri nishapata Starlet ya mchizi wangu ya kutupakia maharusi,
kaniambia,

"Do not have worry #SENETA_WA_MTWIZ,
I'll offer you for free".

Na kuna jirani yetu hapa kitaa anamiliki Suzuki_Kirikuu na ina turubai- hivyo ndugu watabebwa humo.

Watu wengine watajitegemea usafiri,
Hata wakitembea kwa miguu sio mbaya,
itawasaidia kufanya mazoezi.

Wakuu,
Pigeni bajeti ya gharama zingine tu,

Ila kanzu na barakashia ninavyo,
Na gauni la Bi. Harusi kuna dada'angu atatoa msaada katika hilo.

Na nimewaambia vitu vingine vya kijingakijinga sijui Koti la babu, Shuka ya bibi, Chupi ya shangazi n.k
Sivitaki kabisa!
Kwani siku zote walikuwa wanavaa nini?!?!

HAIWEZEKANI SHUGHULI YA SIKU 1
INIGHARIMU HELA YA KUJUTIA KIPINDI KIREFU!

SHENZI KABISA!!!
Nina mashaka huyo mke atakua ni wakichina na wazazi wake wanafahamu, ndiomaana wakakubali kutoka Hero to Zero
 
Du kweli yani mwanamke amekua cheap kiasi hicho. Wakati mm niliambiwa nilipe 2 m nikawaambia mm sina. Nikawaambia keshi mfkoni natoa 1 m na sina nyingine wao wakaniambia basi tupe 1.8 nikawaamba sina nina hyo 1m wakaniambia nilipe 1 m. Ila mahari kamili 1.5 m nikawapa na nikawaambia hyo ingine sku nikija nitamaliza. Mpaka leo sijarudi na mke nilimpa mimba ikabidi nilee mimba na mtoto mpaka akajifungua. Sasa nina mpango wa kwenda kumalizia mahari ili nifanye sherehe tu ya kubariki ndoa.

FOMULA ZA MAISHA NA MIPANGO ZATOFAUTIANA MKUU.
 
Hahaha, nimecheka sana mkuu.
Asubuhi yangu imekua mujarabu, hao wakwe kabla ya kuja kwako kukusalimia watakua wanajipanga kwanza hahaha.

Hiyo bajeti ya 90s nimeielewa ww kaza ivo ivo ikiwezekana hata washkaji wenye maguta nao wakupe sapoti

NAAAAAM,
NI MWENDO WA KUKAZA TU HAPA.

KUNA GUTA MBILI ZA WANA ZIMEPATIKANA.
 
Du kweli yani mwanamke amekua cheap kiasi hicho. Wakati mm niliambiwa nilipe 2 m nikawaambia mm sina. Nikawaambia keshi mfkoni natoa 1 m na sina nyingine wao wakaniambia basi tupe 1.8 nikawaamba sina nina hyo 1m wakaniambia nilipe 1 m. Ila mahari kamili 1.5 m nikawapa na nikawaambia hyo ingine sku nikija nitamaliza. Mpaka leo sijarudi na mke nilimpa mimba ikabidi nilee mimba na mtoto mpaka akajifungua. Sasa nina mpango wa kwenda kumalizia mahari ili nifanye sherehe tu ya kubariki ndoa.
Mahari huwa haimalizwagi kaka,mie nilianziwa 1.6mill nikalia nao mpaka nikala pin kwenye lak8 nikatoa nusu 400,000/= nyengine nikaahidi kulipa hadi leo ndoa imefungwa mwaka wa nne huu cent tano sijapeleka naona wenyewe wamekaa kimya sasa sijui wameelewa kiutu uzima sijui.ila vijana wanaogopa kuoa maana wakifikiria suala la mahari basi wanakata tamaa ni vizuri kama wazazi wakaliangalia hili kwa kupanga kiasi cha mahari kitakachokuwa nafuu kwa vijana.
 
Back
Top Bottom