Wataalam wa bajeti za ndoa njooni hapa

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
3,601
4,085
Wakuu,

Baada ya mbinde ya miezi kama mitatu hivi ya kubishana na upande wa ukweni kuhusu kipengele cha mahari hadi nikaweka mgomo na kuzila kuwa nimeghairi kuoa kwenyewe,
Hatimaye jana wamekubali kushuka kutoka Milioni 2.5 mpaka 145,000/= ambayo angalau inakaribia laki 1 ambayo nd'o niliipanga kwa upande wangu.

Na nimeshawapiga biti kuwa sitaki wanihusishe kwenye gharama za upuuzi wa sendiofu wala pumba gani.

-----------
Sasa wakuu,
Hapa nataka wataalam wa bajeti wanichanganulie hii elfu 95 yangu niliyobakiwa nayo
ili niweze kukamilisha shughuli ya ndoa.

Angalizo:
Usafiri nishapata Starlet ya mchizi wangu ya kutupakia maharusi,
kaniambia,

"Do not have worry #SENETA_WA_MTWIZ,
I'll offer you for free".

Na kuna jirani yetu hapa kitaa anamiliki Suzuki_Kirikuu na ina turubai- hivyo ndugu watabebwa humo.

Watu wengine watajitegemea usafiri,
Hata wakitembea kwa miguu sio mbaya,
itawasaidia kufanya mazoezi.

Wakuu,
Pigeni bajeti ya gharama zingine tu,

Ila kanzu na barakashia ninavyo,
Na gauni la Bi. Harusi kuna dada'angu atatoa msaada katika hilo.

Na nimewaambia vitu vingine vya kijingakijinga sijui Koti la babu, Shuka ya bibi, Chupi ya shangazi n.k
Sivitaki kabisa!
Kwani siku zote walikuwa wanavaa nini?!?!

HAIWEZEKANI SHUGHULI YA SIKU 1
INIGHARIMU HELA YA KUJUTIA KIPINDI KIREFU!

SHENZI KABISA!!!
 
Du kweli yani mwanamke amekua cheap kiasi hicho. Wakati mm niliambiwa nilipe 2 m nikawaambia mm sina. Nikawaambia keshi mfkoni natoa 1 m na sina nyingine wao wakaniambia basi tupe 1.8 nikawaamba sina nina hyo 1m wakaniambia nilipe 1 m. Ila mahari kamili 1.5 m nikawapa na nikawaambia hyo ingine sku nikija nitamaliza. Mpaka leo sijarudi na mke nilimpa mimba ikabidi nilee mimba na mtoto mpaka akajifungua. Sasa nina mpango wa kwenda kumalizia mahari ili nifanye sherehe tu ya kubariki ndoa.
 
Unadhambi ya zinaa
 
Kwa waislamu mahari ni kiasi kidogo sana nasikia. Sisi wakristo ndio wazee wanatafutia mtaji kabisa hapo hapo
 
Wakuu,

Baada ya mbinde ya miezi kama mitatu hivi ya kubishana na upande wa ukweni kuhusu kipengele cha mahari hadi nikaweka mgomo na kuzila kuwa nimeghairi kuoa kwenyewe,
Hatimaye jana wamekubali kushuka kutoka Milioni 2.5 mpaka 145,000/= ambayo angalau inakaribia laki 1 ambayo nd'o niliipanga kwa upande wangu.

Na nimeshawapiga biti kuwa sitaki
Hwanihusishe kwenye gharama za upuuzi wa sendiofu wala pumba gani.

-----------
Sasa wakuu,
Hapa nataka wataalam wa bajeti wanichanganulie hii elfu 95 yangu niliyobakiwa nayo
ili niweze kukamilisha shughuli ya ndoa.

Angalizo:
Usafiri nishapata Starlet ya mchizi wangu ya kutupakia maharusi,
kaniambia,

"Do not have worry #SENETA_WA_MTWIZ,
I'll offer you for free".

Na kuna jirani yetu hapa kitaa anamiliki Suzuki_Kirikuu na ina turubai- hivyo ndugu watabebwa humo.

Watu wengine watajitegemea usafiri,
Hata wakitembea kwa miguu sio mbaya,
itawasaidia kufanya mazoezi.

Wakuu,
Pigeni bajeti ya gharama zingine tu,

Ila kanzu na barakashia ninavyo,
Na gauni la Bi. Harusi kuna dada'angu atatoa msaada katika hilo.

Na nimewaambia vitu vingine vya kijingakijinga sijui Koti la babu, Shuka ya bibi, Chupi ya shangazi n.k
Sivitaki kabisa!
Kwani siku zote walikuwa wanavaa nini?!?!

HAIWEZEKANI SHUGHULI YA SIKU 1
INIGHARIMU HELA YA KUJUTIA KIPINDI KIREFU!

SHENZI KABISA!!![/QUOTE
Hongera sana mkuu tukiongezeka watu wenye philosopher kama hii tutavuka haraka kwenda kwenye uchumi wa kazi!
 
Back
Top Bottom