Wajue viongozi wenye ulinzi mkali zaidi, mkubwa na wa masala 24 duniani

The Palm Beach

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
804
1,646
(Kwa hisani ya Shirika la Utangaji la Uingereza - BBC)

Viongozi wote walio madarakani kuongoza nchi zao,taasisi na mashirika mbali mbali ya kiserikali hupewa ulinzi .

Hata hivyo inafahamika kwamba marais na wakuu wa serikali ndio kitengo cha watu wanaopewa ulinzi wa juu kabisa kuliko wote .

Licha kuwa ni lazima kwa kila kiongozi wa nchi kulindwa kama 'raslimali' kuu ya nchi kwa sababu ya kuwakilisha umoja wa taifa lolote, hata hivyo kuna viongozi ambao ulinzi wao ni wa juu kuliko wengine. Kuna viongozi ambao katu huwezi kupenya 'kinga' ya ulinzi waliopewa na hasa wakiwa safarini nje ya mataifa yao .

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari katika nchi zao na makadirio mbali mbali ya matumizi ambayo hutolewa na wataalam wanaominika wa masuala ya usalama,watu hawa ni baadhi ya wanaolindwa sana duniani kwa sababu ya kazi zao na pia nafasi wanazoshikilia.

Maelezo mengine kuhusu usalama wao yapo wazi na yanafahamika kutegemea ulinzi wanaopata wakiwa katika hafla za umma na hata mipango ya serikali ili kuwalinda ama kufanikisha ulinzi wao. Hawa chini ndiyo viongozi wakuu wa nchi wanaolindwa zaidi duniani...

1. Vladimir Putin
Vladimir Putin Viongozi kama viongozi wengine wa kisiasa nchini Urusi analindwa na kikosi maalum cha kuwalinda viongozi hata hivyo kitengo kinachomlinda Putin kinaonekana kuwa spesheli na tofauti kabisa.

Mengi hayajulikani kuhusu kikosi kinachomlinda Putin lakini kinachofahamika ni kwamba kikosi hicho kina uwezo wa juu na wa kipekee .Lakini rais Putin alifafanua mengi kuhusu ulinzi wake katika mahojiano na mwandishi wa shirika la habari la Urusi la Tass News Andrei Vandenko mwaka wa 2020 aliposema kpia kwamba alikataa mpango wa kutumiwa kwa watu wanaofanana naye kama mkakati wa ulinzi wake. Katika mahojiano hayo Putin alisema pendekezo hilo lilitolewa miaka ya 2000 wakati nchi yake ilipokuwa katika vita na wanamgambo wa Chechnya.

Hakuna maelezo ya umma juu ya shughuli zake na hakuna ripoti zinazopatikana hadharani, ni za siri sana watu hutegemea uvumi kujua kikosi hicho huendesha vipi oparesheni zake.

Vladimir mwenyewe ni mtu wa kutatanisha ambaye amekuwa katikati ya kivutio kwa wanahabari tangu aliposhikilia nafasi hiyo kama kaimu wa rais na kisha baadaye kujenga kundi la wafuasi sugu ndani ya utawala wake.

Ingawa hakuna sanamu zake au minara ya kumanya kuwa maarufu ,Putin amejijengea sifa kama kiongozi mwenye ufuasi mkubwa sio nchini mwake tu bali katika nchi jirani na hata kimataifa.

Misimamo yake ya kizalendo haijakuwa tu na utata wa kuwaganya watu lakini pia ni hatua ambayo imemuweka hatarini na kuwa juu ya orodha ya viongozi wanaoweza kuwa katika hatari ya kushambuliwa au kuuawa na mahasimu wake .

Hofu ya Putin kuhusu usalama wake pia inatokana na utawala ambao ameujenga ambao kwa kiasi fulani na hasa katika nchi za magharibi unaoonekana kama wa kiimla.

Ufisadi ndani ya asasi za utawala pia unaifanya hali yake ya usalama kuhitaji uboreshaji wa kiwango cha juu .

2. Kim Jong-un
Ulimwengu ulivutiwa na ulinzi wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, walipoona kikosi cha ulinzi kilichokuwa kimeandamana naye akiwa ziarani huko Singapore .

Je Kim huendeleaje na shughuli zake za kila siku akiwa na wasiwasi juu ya majaribio ya kumuua na tishio la kupokonywa madaraka na watu wanapomzingira?

Baadaye iligunduliwa kwamba Kim Jong-un hana tu kikosi cha siri cha kumlinda bali pia ana jeshi lake zima la wapiganaji laki moja ambao wanaripoti kwake moja kwa moja .

Jeshi hilo linajulikana kama 'Kamandi maalum ya kiongozi mkuu'

Kitengo hiki hutumika kumlinda kiongozi wao lakini pia kinatumika kama chombo cha propaganda.

Kim Jong-un anajaribu kuleta dhana ya kukaribia 'utakatifu' machoni pa raia wake na lolote analoweza kufanya ili kuleta dhana hiyo ,basi atalifanya kwa gharama yoyote .

3. Joe Biden
Mengi yanafahamika kuhusu ulinzi wa rais yeyote wa Marekani na sio tu Joe Biden anayeshikilia nafasi hiyo kwa sasa .

Ulimwengu umejionea makubwa wakati rais wa Marekani anapozuru taifa lolote na hata mawasiliano ya simu na masafa yoyote ya mawasiliano huzimwa ili kumhakikishia usalama wake rais wa Marekani .

Msafara wake wa magari huandamana naye anakokwenda na hata vikosi vya kumlinda husimamia usalama mzima ya sehemu anayozuru na kuwaacha kama mashabiki maafisa wa ulinzi wa nchi anayotembelea

4. Papa Francis
Papa ni Askofu wa Roma na kiongozi asiye rasmi wa ulimwengu. Kama mkuu wa Kanisa la Katoliki na kama rais wa nchi, yeye pia anahitaji ulinzi wa hali ya juu. Akiwa ziarani nchini Iraq mwaka wa 2020,BBC iliripoti kwamba karibu maafisa elfu 10 wa usalama walitumika kumlinda papa Francis .

Papa anaishi labda katika moja ya miji iliyolindwa zaidi ulimwenguni, Jiji la Vatican, Roma, Italia. Hata unapotembea barabarani unaweza kuona walinzi wote wakiwa wamejihami silaha za kizamani wakiwa wamebeba mikuki.

Usishangae , Papa analindwa na mikuki, lakini msidanganyike - walinzi hawa wenye silaha ni jeshi la hali ya juu linaloundwa na wanajeshi wa zamani wa Uswisi, ambao wanaweza kukabiliana na tishio lolote kwa sekunde chache tu.

Mbali na mikuki, pia wana kila aina ya silaha za kisasa zilizofichwa na zinaweza kutumika inapohitajika. Walinzi wa Uswizi wamedumu kwa miaka zaidi 500, na kulifanya kuwa jeshi la kale zaidi ulimwenguni.

Wakati kilianzishwa rasmi na Papa Julius II mnamo 1506, kikosi hicho kilikuwa kama jeshi la mamluki, ambalo bado linajulikana hadi leo kwa ushindi mkubwa zaidi wakati wa mapigano yaliyokuwa yakifanyika ndani na karibu na Roma.

Nani bora kumlinda papa Francis kuliko jeshi ambalo limedumu kwa miaka 500 na kustahimili mengi katika historia ya mapigano.

5. Mark Zuckerberg
Hakuna chochote kuhusu Facebook ambacho ni siri tena, pamoja na bajeti ya ulinzi ya Mkurugenzi mkuu Mark Zuckerberg.

Walinzi wake wakati mwingine huitwa 'polisi wa siri wa Zuckerberg' kuna uvumi kwamba kikosi chake cha ulinzi kina watu 16 kwa wakati mmoja wanaofanya kazi kwa zamu kwa mujibu wa ripoti nyingi za vyombo vya habari zinazofuatilia shughuli zake za kikazi .

Ukilinganisha na zaidi ya muongo mmoja uliopita Larry Ellison wa Oracle aliyekuwa akiongoza kampuni hiyo ya teknlojia alikuwa na gharama kubwa zaidi za usalama zilizoripotiwa kuwa $ 1.8 milioni kwa mujibu wa ripti za vyombo vya habari wakati huo zilizotegemea makadirio ya wataalam wa usalama.

Ikizingatiwa kwamba kampuni yake ipo chini ya shutuma za kukusanya data nyingi za kibinafsi kutoka kwa watumiaji wake na kuuza habari hizo kwa walio tayari kulipia kwa bei ya juu, Zuckerberg anaonekana kupendelea kuweka maisha yake ya kibinafsi siri ili kuweza kujihakikishia usalama wake.
 
Kwa io mark Zuckerberg analindwa kuliko hata Marais waataifa mengine? Ndo maana umemueka namba 5 sio?

Ni Bora hata ungemuweka Samia hapo....
Si Mimi.

Hawa ni BBC ndo waliofanya utafiti huu mwaka 2020...

Bado Samia alikuwa hajawa Rais na hata kama angekuwa, hawezi kuingia kwenye orodha hata ya top 50..

Vigezo vilivyotumiwa kuja na conclusion hii vikubwa ni viwili ambavyo ni;

1. Bajeti ya ulinzi ya kiongozi husika...

2. Uwezo wa jeshi la ulinzi na teknolojia..

##Je, Samia na Tanzania tuaweza kuingia hapo?
 
Navutiwa sana ulinzi wa viongozi wakubwa, wakiwa kwenye ziara/safarini huwa namakinika kuangalia kila pembe kuliko na ulinzi.

Binafsi navutiwa zaidi na walinzi wa kike wa Rais wetu Mama Samia, huwa sichoki kuwaangalia wakitekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
 
Si Mimi.

Hawa ni BBC ndo waliofanya utafiti huu mwaka 2020...

Bado Samia alikuwa hajawa Rais na hata kama angekuwa, hawezi kuingia kwenye orodha hata ya top 50..

Vigezo vilivyotumiwa kuja na conclusion hii vikubwa ni viwili ambavyo ni;

1. Bajeti ya ulinzi ya kiongozi husika...

2. Uwezo wa jeshi la ulinzi na teknolojia..

##Je, Samia na Tanzania tuaweza kuingia hapo?
Hujaelewa kwanini nimemtaja Samia hapa.... Ni kama sarcasm.... Huyo Marc pia hawezi kua top 5 hata iweje...

Kwa io bajeti yake ya ulinzi anawazidi viongozi wakuu wa china,Saudi Arabia,Iran.... Pm wa uingereza? Rais wa ufaransa? Au anamzidi hata vice president wa us tu?? Hapo hamna kitu...

Viongozi wengi tu wa afrika Wana bajeti za kukufuru kwenye ulinzi wao
 
Hujaelewa kwanini nimemtaja Samia hapa.... Ni kama sarcasm.... Huyo Marc pia hawezi kua top 5 hata iweje...

Kwa io bajeti yake ya ulinzi anawazidi viongozi wakuu wa china,Saudi Arabia,Iran.... Pm wa uingereza? Rais wa ufaransa? Au anamzidi hata vice president wa us tu?? Hapo hamna kitu...

Viongozi wengi tu wa afrika Wana bajeti za kukufuru kwenye ulinzi wao
Naskia museven nae si haba
 
Naskia museven nae si haba
Kama anavyoonekana pichani
JamiiForums1024264035.jpg
 
Kwakua umesema viongoz wa hapo duniani bas na Mimi naomba nitie namba Moja yangu

Kiongoz anayelindwa Zaid hapa duniani ni king na queen wa siafu, Kuna siku niliona Hawa wadudu wakihamisha viongoz wao kutoka sehemu Moja kwenda nyingne, sio Siri Hawa viumbe mungu kawaumba kiajabu sana...ulinzi ulikua mkali sana sidhan kama Kuna mdudu anaweza kutia pua yake kukatiza kwenye ule msafara

Unaweza kuhisi nimecomment Kwa kuchekesha ila huo ndo uhalisia wake
 
duh, si muwakilishi wa Mungu mbona anahitaji ulinzi mkali?
Lakini huyu huyu Mungu ndiye aliyetupa akili ili tuzitumie kujua jema au baya..

Ingekuwa hivyo, tusingekuwa tunakimbia unapomwona nyoka anakuja kukung'ata kwa hoja kuwa Mungu yupo..!

Yupo ndiyo. Lakini tumia akili kujiepusha na hatari zinazoonekana wazi.
 
Kwakua umesema viongoz wa hapo duniani bas na Mimi naomba nitie namba Moja yangu

Kiongoz anayelindwa Zaid hapa duniani ni king na queen wa siafu, Kuna siku niliona Hawa wadudu wakihamisha viongoz wao kutoka sehemu Moja kwenda nyingne, sio Siri Hawa viumbe mungu kawaumba kiajabu sana...ulinzi ulikua mkali sana sidhan kama Kuna mdudu anaweza kutia pua yake kukatiza kwenye ule msafara

Unaweza kuhisi nimecomment Kwa kuchekesha ila huo ndo uhalisia wake
Haa haa😂

Hao wako ktk dunia yao tu.

Likely, ktk ulimwengu wao wa wadudu/wanyama, ni wazi kuwa malkia wa siafu hulindwa sana kuliko Rais wa Korea Kaskazini..

Lakini pengine yule wa nyuki naye anaweza kuwa kwenye list ya ushindani na huyo wa siafu..
 
Back
Top Bottom