Wataalam wa bajeti za ndoa njooni hapa

Kwa kweli umefanya la maana tatizo ni kwamba ulivyoiandika inachekesha maana hapa ni kicheko tu kama tuko 8 hapa ndani kumbe peke Yangu.

Suala la harusi linagarimu fedha nyingi sana na likiisha unaanza kuwachangia waliokuchangia yaani mfumo mbovu sana huu .

Baada ya miaka kadha ndio mnaanza kufikiria maendeleo binafsi

MKUU,

NA UPUUZI WA MICHANGO NISHAUKATAA!!!

SITAKI NIJE KUSUMBULIWA NA WATU WANAODAI MICHANGO YA HARUSI MIMI!!!
 
Wakuu,

Baada ya mbinde ya miezi kama mitatu hivi ya kubishana na upande wa ukweni kuhusu kipengele cha mahari hadi nikaweka mgomo na kuzila kuwa nimeghairi kuoa kwenyewe,
Hatimaye jana wamekubali kushuka kutoka Milioni 2.5 mpaka 145,000/= ambayo angalau inakaribia laki 1 ambayo nd'o niliipanga kwa upande wangu.

Na nimeshawapiga biti kuwa sitaki wanihusishe kwenye gharama za upuuzi wa sendiofu wala pumba gani.

-----------
Sasa wakuu,
Hapa nataka wataalam wa bajeti wanichanganulie hii elfu 95 yangu niliyobakiwa nayo
ili niweze kukamilisha shughuli ya ndoa.

Angalizo:
Usafiri nishapata Starlet ya mchizi wangu ya kutupakia maharusi,
kaniambia,

"Do not have worry #SENETA_WA_MTWIZ,
I'll offer you for free".

Na kuna jirani yetu hapa kitaa anamiliki Suzuki_Kirikuu na ina turubai- hivyo ndugu watabebwa humo.

Watu wengine watajitegemea usafiri,
Hata wakitembea kwa miguu sio mbaya,
itawasaidia kufanya mazoezi.

Wakuu,
Pigeni bajeti ya gharama zingine tu,

Ila kanzu na barakashia ninavyo,
Na gauni la Bi. Harusi kuna dada'angu atatoa msaada katika hilo.

Na nimewaambia vitu vingine vya kijingakijinga sijui Koti la babu, Shuka ya bibi, Chupi ya shangazi n.k
Sivitaki kabisa!
Kwani siku zote walikuwa wanavaa nini?!?!

HAIWEZEKANI SHUGHULI YA SIKU 1
INIGHARIMU HELA YA KUJUTIA KIPINDI KIREFU!

SHENZI KABISA!!!
Hahaha mkuu wewe n zaid ya hatar....
 
Ndoa in raasisi mhimu na nyeti sana naona unaifanyia mzaha au kukejeli baadhi ya tamaduni za watu.pia ndoa no muungano wa hiari kama uliona huna uwezo nalo ungepitezea yanini kuanika hapa?pili mm ni mkristo ila nimelelewa na jamii Islam nilifundishwa kuwa ukiona umeoa mwanamke na hajui kutunza siri za ndani make ujue huna mke.nafikiri kipengere hiki hakimlengi mwanamke tu hata sie wanaume tunapaswa kuwa na staha kwa wake zetu na jamii kwa jumla.samahani kama nitakuwa nimeenda tofauti mdau ila hapo staha kwa wazaa chema ujaonesha.

MKUU,
PUNGUZA POVU!

NYIE ND'O MNAOENDEKEZA UNYONYAJI KWA KIGEZO CHA NDOA NYIE!

EEEEEEEEBOH!
 
Wakuu,

Baada ya mbinde ya miezi kama mitatu hivi ya kubishana na upande wa ukweni kuhusu kipengele cha mahari hadi nikaweka mgomo na kuzila kuwa nimeghairi kuoa kwenyewe,
Hatimaye jana wamekubali kushuka kutoka Milioni 2.5 mpaka 145,000/= ambayo angalau inakaribia laki 1 ambayo nd'o niliipanga kwa upande wangu.

Na nimeshawapiga biti kuwa sitaki wanihusishe kwenye gharama za upuuzi wa sendiofu wala pumba gani.

-----------
Sasa wakuu,
Hapa nataka wataalam wa bajeti wanichanganulie hii elfu 95 yangu niliyobakiwa nayo
ili niweze kukamilisha shughuli ya ndoa.

Angalizo:
Usafiri nishapata Starlet ya mchizi wangu ya kutupakia maharusi,
kaniambia,

"Do not have worry #SENETA_WA_MTWIZ,
I'll offer you for free".

Na kuna jirani yetu hapa kitaa anamiliki Suzuki_Kirikuu na ina turubai- hivyo ndugu watabebwa humo.

Watu wengine watajitegemea usafiri,
Hata wakitembea kwa miguu sio mbaya,
itawasaidia kufanya mazoezi.

Wakuu,
Pigeni bajeti ya gharama zingine tu,

Ila kanzu na barakashia ninavyo,
Na gauni la Bi. Harusi kuna dada'angu atatoa msaada katika hilo.

Na nimewaambia vitu vingine vya kijingakijinga sijui Koti la babu, Shuka ya bibi, Chupi ya shangazi n.k
Sivitaki kabisa!
Kwani siku zote walikuwa wanavaa nini?!?!

HAIWEZEKANI SHUGHULI YA SIKU 1
INIGHARIMU HELA YA KUJUTIA KIPINDI KIREFU!

SHENZI KABISA!!!

safi sana lazima wakwe wakukome
 
Ukubwa huu wa mahari ndo unawafanya vijana wengi wasiowe ,maana unatoa mahari kubwa alafu mke anakuja kukuvuruga ndani ,dah unaweza uwa mtu maana ukifikiria mahari uliyotoa ni mtaji tosha

MKE AKUVURUGE AU ASIKUVURUGE,
KIPENGELE CHA PUNGUZO MURUWA LA MAHARI NI MUHIMU!
 
Mie nasubiria ukishaoa tumgawane wote huyo mke maana inaonekana bahili sana nitakula deal tu na wazazi wake anakua anaaga anaenda kwao anakuja kwangu kazi inakuwa kuwawezesha tu wazazi wake.

NAMUOA DADA'AKO,
SASA SIJUI TUTAMGAWANA HIVYOHIVYO!
 
Hivi kwani mke unamnunua kwanza hiyo umewapa nyingi mkuu ungekomaa na kilo yako moja swaafii kabisa ...

Hiyo iliyobaki nenda kwa supplier wa vinywaji vya azam nunua full sana zisizidi za 9800
Kuna yake maandazi ya azam chukua mifuko ya kutosha ..ata ya 9600 apo wanakula kabisa mengine bajet

HUU ND'O USHAURI MWEMA KWA MAENDELEO YA NCHI HII!
 
Wakati nasoma post hii nje nasiki kigoma cha arusi sijui kaolewa nani wanapita njiani......mkuu iyo 95 ndio yakuanzia matumizi yakumwachia wife pindi uendapo job.....pi waambie harus ni 24 hrs baada ya hapo unaingia kazini kama sio wewe uliye owa jana yake...

NA NDIO MIKAKATI YANGU.
 
Back
Top Bottom