Wassira: Nitagombea urais 2015

Rais wetu awe Sokwe? Haiwezekani. Kwanza anauelewa mdogo kuliko sisimizi, anasura mbaya, roho mbaya, kauli mbaya.hana elimu ...... yaani nashindwa kumuelezea ......!

Sijui hayo mengine,kwa upande wa elimu ana masters 3 tofauti za mambo ya uchumi......jama nchi hii tusiipeleke ki shabiki mponde mtu si kwakumwonea jamaa elimu ipo.
 
Mhe. WASSIRA amekuwa kielelezo cha utendaji uliotukuka hivyo kila wizara anayopelekwa anafanya vizuri na kumfanya rais awe anampa majukumu ya ambayo mawaziri wengine yamewashinda.Naomba uelewe Gwangambo sura na utendaji haviendani hii inanipelekea nikutilie shaka juu ya uwezo wako wa kufikiri na kupambanua mambo.WASSIRA ndiye kiongozi bora kati ya wote waliotangaza nia hivyo tumuunge mkono atuletee mabadiliko ya kweli nchini.
 
Last edited by a moderator:
Hapa kwenye jina la TYSON LILITOKANA NA KUMSHINDA UBUNGE WARIOBA NDANI YA CCM na NJE YA CCM.
Alipo hojiwa na waandishi wa habari ndio walimlinganisha na jina hilo kwa kumtoa Warioba kwa Knock Out.
Wasira anauwezo mkubwa kama utajadili hoja na si vihoja.
 
kuna watu hata aibu hawana sasa huyu babu niwakumpigia promo?

Alipaswa kujipambanua wakati wa BMK, uzalendo wake wa kutetea watanzania masikini angeuonyesha ndani ya BMK kwa kuikataa katiba inayopendekezwa. Tofauti na hapo ni porojo tu ambazo zimezoeleka. Halafu na nyie waandishi wa habari mlio pungukiwa uzalendo ipo siku tamaa zenu za visenti zitawatokea puani. Mmekosa kabisa journalistic ethics kisa tumbo.
 
Nakupongeza kwa kujitahidi kumuelezea wasira hakika umemtendea, Kwa sifa hizo anafaa kuwa raisi.achana na huo upuuzi mwingine.
 
Bwana mkubwa kila jina la NYERERE ina maanisha ni yule Baba yake Makongoro? Nyerere nyingine inamaanisha Vicent,,,,
Nini Hoja yangu?
HOJA YANGU HAPA WASIRA ALIYE TAJWA SI HUYU RAIS MTARAJIWA NI KAKA YAKE.......JARIBUNI KUPUNGUZA UVIVU WA KUJISOMEA KUMBUKUMBU ZA NCHI.
 
Nyerere aliwahi kumteua Wassira kuwa RC wa Mara... Kwa kutumia wadhifa wake alimwandikia barua GM wa Mutex kumtaka kiwanda kiwaajiri watu wa Mara pekee!!! GM alikasirika sana kiasi cha kupeleka ile barua kwa JKN! ... JKN alimwita wassira Butiama! Katika Mazungumzo Wassira alijikojolea baada ya kugundua kuwa Barua yake ilimfikia JKN aliekuwa anapinga Ukabila kwa nguvu zote... Baada ya hapo, wassira alipotezewa hadi Rostam alipompa fedha kwaajili ya Kampeni ya JK 2005 ... Huyu Mkabila, Mdini na Mkanda Gaidi mwenye kuabudu nguvu dhidi ya wapinzani Hastahili kamwe kuongoza hata Tarafa ndani ya nchi yetu ... Kama mnampenda sana Mpelekeni akawe msimamizi wa Mapori ya Gombe ...
Awamu ya Tano inahitaji Rais mwenye kuijua vema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anahitajika mtu ambaye anaijua nchi kwa kadiri inavyotakiwa. Awe kiongozi ambaye anaelewa ukweli huu kwamba ujio wake ni kutatua changamoto ambazo jinsi zinavyoonekana, zinatisha kuzidi mafanikio.

Hata hivyo, anapaswa kutambua na kuheshimu kazi kubwa iliyoanza kufanywa na waasisi wa taifa hili. Hahitajiki kiongozi anayekuja kuanza upya, isipokuwe aje mwenye mawazo mapya yenye ukomavu zaidi.

Akaribishwe anayetambua Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa ni tunu ya Watanzania wote, Bara na Visiwani. Mwenye kuujua vema na aliyeishi ndani yake, aliye na maarifa ya kuulinda utaifa wa Watanzania. Hapa ni ufafanuzi kuwa Rais anayetakiwa ni Mtanzania kutoka ndani kabisa ya moyo wake.

Je, mwaka 2015 ni wa Stephen Masato Wasira? Tumwangaze katika pande zote ili kuona ubora na udhaifu wake. Mwisho tutaona jinsi gani anaweza kuisaidia Tanzania, endapo Watanzania watamwamini na kumchagua kuwa Rais wa Awamu ya Tano.

Kuhusu kuulinda Utanzania, historia inampendelea Wasira kwa sababu ni mmoja kati ya viongozi wachache waliobaki ambao walikuwepo serikalini, akiwa memba wa Baraza la Mawaziri tangu utawala wa awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kama maono, mitazamo, misimamo na falsafa za Mwalimu Nyerere ni muongozo wa vizazi vyote katika Taifa la Tanzania, basi tukubaliane kwamba Wasira anafaa, kwa maana kwamba Baba wa Taifa alimwamini na kumpa uongozi katika wizara inayoongoza sekta ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi.

Wasira akiwa na umri chini ya miaka 40, aliteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa Naibu Waziri wa Kilimo. Ni mmoja kati ya vijana wachache wakati huo ambao walimvutia Baba wa Taifa na kuwapa nafasi ili watumie elimu zao kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Kama Serikali ya Awamu ya Pili, chini Rais Ali Hassan Mwinyi, ni kielelezo cha daraja la mabadiliko makubwa ya mfumo na mtazamo wa kiuchumi katika nchi. Serikali iliyobadili dira iliyokuwepo ya Ujamaa na Kujitegemea hadi Ujamaa Mamboleo (Ujamaa wa Kisasa), basi Wasira anafaa, kwa maana alikuwa mmoja wa waliounda serikali.

Serikali ya Awamu ya Kwanza, ilijenga misingi halisi na imara ya Ujamaa na Kujitegemea (Ujamaa Kindakindaki), ikawekewa njia madhubuti katika Azimio la Arusha. Awamu ya Pili ilibadili baadhi ya vifungu vikali vilivyokuwemo katika Azimio la Arusha, ikaurahisisha Ujamaa Azimio la Zanzibar, hivyo kuibua mfumo wa Ujamaa Mamboleo.

Wasira alikuwa Naibu Waziri wa Serikali za Mitaa na baadaye alipandishwa kuwa waziri kamili katika Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, wakati wa utawala wa Rais Mwinyi. Hivyo kama mabadiliko hayo ya dira ya uchumi kwa taifa ni bora, basi naye alikuwemo katika Baraza la Mawaziri.

Ni dira hiyo ya Ujamaa Mamboleo ambayo ilipokelewa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa ambaye aliuzimisha Ujamaa jumla na kuukaribisha Upepari kwa mlango wa Utandawazi (Globalization), kisha kuuwekea mizizi inayoibeba mpaka Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete.

Anahitajika kiongozi ambaye siyo mroho wa madaraka? Basi Wasira anafaa, kwa maana mwaka 1990, aliamua kwa hiari yake kutogombea ubunge wa Jimbo la Bunda ili kumpisha aliyekuwa Waziri Mkuu kwa wakati huo, Jaji Joseph Sinde Warioba.

Wasira alikuwa Mbunge wa Bunda kati ya mwaka 1985 na 1990 lakini aliamua kujitoa kwenye kinyang'anyiro ili kumwacha Warioba awe mgombea pekee, kwa heshima kwamba alikuwa Waziri Mkuu wa nchi. Alizingatia itifaki ya ukubwa (protocol of seniority).

Kingine ambacho kilimsukuma Wasira kujitoa kwenye kuwania ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 1990 ni utambuzi kwamba nafasi ya Warioba ya kuwa Waziri Mkuu ni fahari kubwa kwa jimbo na wilaya yao ya Bunda. Hivyo kwa uungwana, aliamua kujiweka pembeni. Ni watu wachache ambao wanaweza kuchukua uamuzi huo.

Na kwa sababu wakati huo uchaguzi ulikuwa ukifanyika chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa (CCM peke yake), Warioba alishinda kiulaini na kuapishwa kuwa Mbunge wa Bunda kwa mwaka 1990 hadi 1995. Ila Wasira aliwahi kukaririwa akilalamika kwamba Warioba hakuwahi hata kumshukuru kwa uamuzi wake wa kumwachia jimbo kwa heshima.

Je, anatakiwa kiongozi mwenye uthubutu wa kuchukua uamuzi mgumu? Wasira anatosheleza viwango kwa sababu mwaka 1995, baada ya jina lake kukatwa kwenye kura za maoni, kuwania ubunge Jimbo la Bunda kwa tiketi ya CCM, na kupitishwa Warioba, aliamua kuachana na chama hicho, hivyo kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi, kilichokuwa tishio sana kwa wakati huo.

Kama kauli ya Mwalimu Nyerere kuwa "CCM siyo mama yake mzazi", kwamba anaweza kuachana nacho wakati wowote pale anapoona hakiendeshi mambo yake kwa utaratibu unaokubalika, ni dira ya kila mwanasiasa. Basi Wasira ana maono ya ki-Mwalimu Nyerere kwa kitendo chake cha kuhama CCM na kujiunga NCCR-Mageuzi.

Sababu aliyoitoa baada ya kuhama CCM ni kwamba alishinda kura za maoni lakini alichakachuliwa kwa sababu ulikuwepo mkakati kwamba lazima Warioba ashinde na kusimama kama mgombea ubunge wa chama hicho. Na alipopeleka malalamiko kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM wakati huo, hayati Lawrence Gama, kwamba matokeo yake yalichakachuliwa, alijibiwa kuwa rufaa yake itasikilizwa baada ya kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu 1995.

Lengo lake ni rufaa yake kusikilizwa ili apewe ushindi ambao aliamini ndiyo haki yake, hivyo apate fursa ya kukiwakilisha chama chake (CCM) katika kuwania ubunge Jimbo la Bunda kwenye Uchaguzi Mkuu 1995, kwa hiyo alipojibiwa hivyo, aliona hakuna njia nyingine zaidi ya kutafuta haki yake akiwa nje ya chama. Akahama, hivyo kutekeleza kauli ya Mwalimu Nyerere: "Mama CCM si mama yangu mzazi."

Alikuwa na hoja? Wasira alisema kuwa wananchi wa Bunda walimshinikiza sana kugombea. Ilifika wakati walimtaka ahame chama na kumwahidi kumpigia kura nyingi endapo atagombea kwa kupitia chama chochote kile cha siasa. Bunda walihitaji tu huduma yake.

Ukweli wa hoja yake; Wasira alishinda ubunge Jimbo la Bunda kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi mwaka 1995 na kuongoza jimbo hilo mpaka mwaka 2000. Sura inayobeba matokeo ya hapa ni kwamba alikuwa na hoja kuwa wananchi walimhitaji, ndiyo maana hata alipohama chama, aliweza kumshinda Warioba aliyekuwa mwakilishi wa CCM.

Anatakiwa msomi wa kiwango kisichotia shaka? Wasira anapita hapa kifua mbele, kwani ni mmoja wa wasomi wazuri, waliopata bahati ya kusoma katika vyuo bora kabisa duniani wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. Enzi hizo, wasomi wa elimu ya juu, wanahesabika. Tena adimu kweli!

Shahada zake zote za Chuo Kikuu, Wasira alizipata nchini Marekani katika Chuo Kikuu cha Marekani (American University), kilichopo Washington DC. Alianza kunutukiwa Shahada ya Kwanza ya Uchumi na Elimu ya Kimataifa (BA in Economics & International Studies) na baadaye Shahada ya Pili ya Uchumi (MA in Economics *Applied Economics*).

Vilevile Wasira, alisoma na kutunukiwa Shahada ya Umahiri katika Uongozi wa Umma (Masters in Public Administration) katika chuo hichohicho, yaani Chuo Kikuu cha Marekani. Bila shaka utaona ukweli huu kwamba elimu ya Wasira inatosheleza mahitaji ya kiongozi wa zama za sasa.

Kama hoja ni kuwa na kiongozi mwenye uzoefu; Wasira anatosha! Maana serikali za awamu zote yupo kazini. Awamu ya Kwanza kama Naibu Waziri, Awamu ya Pili, akawa Naibu na baadaye Waziri kamili, Awamu ya Tatu akawa mshauri wa serikali (jukumu lake kama mbunge), Awamu ya Nne, waziri kipindi chote.

Kwa mantiki hiyo, ana uzoefu wa kutosha. Kwa muda mrefu katika Serikali ya Awamu ya Nne, alifanya kazi Ofisi ya Rais, akiwa Waziri wa Nchi, akishughulikia Uhusiano na Uratibu. Hivyo hakuna kitu ambacho hakijui Ikulu, namna ya uendeshaji wa serikali. Utawala wa nchi na uhusiano kati ya serikali na mihimili mingine ya dola kama bunge na mahakama.

Wasira amekuwa ndani ya jiko na ana uzoefu wa kutosha. Atakapokabidhiwa rungu hataanza upya isipokuwa ataanza kwa kushughulikia changamoto ambazo zimeshindwa kutatuliwa na awamu zote zilizopita, kwa maana anazijua ipasavyo. Kama msemo wa kufuatwa ni "bunduki mpe mwenye ujuzi nayo", basi Wasira anajua.

Uzoefu wake bungeni katika awamu nne za uongozi wa nchi hii, peke yake unatosha kumpa turufu ya kuchaguliwa kuongoza taifa hili. Hii ni kwa sababu anajua kila kilio cha kila mbunge kadiri alivyowasilisha kero za jimbo lake katika kipindi chote hicho. Anaujua ugumu wa uwaziri na changamoto za kila wizara.

Ana uzoefu mkubwa kisiasa, kama hivyo mbali na ubunge, alishakuwa mwanachama hai na kiongozi NCCR-Mageuzi. Alikuwepo wakati chama hicho kilipopata mtikisiko mkubwa na kusambaratika. Kwa hiyo, anajua nini afya ya chama cha siasa, anelewa adui kirusi au adui ni nini.

Ndani ya CCM, tangu aliporejea kundini akitokea NCCR-Mageuzi, ameaminiwa na wanachama wenzake kushika nafasi muhimu kabisa ya ujenzi wa chama hicho tawala. Kwa sasa, ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), nafasi ambayo alikuwepo tangu mwaka 2007, na katika uchaguzi wa chama mwaka 2012, alichaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Yaani mpaka 2017.

Mwaka 2011, alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (CC) na mwaka 2013, alichaguliwa tena kuendelea na nafasi hiyo. Itambulike kwamba NEC na CC, ni vyombo vikubwa vya CCM, ambavyo husimamia na kutoa uamuzi na miongozo kwa serikali iliyopo madarakani kwa sasa. Hivyo basi, kwa uzoefu, hutapata kasoro ya Wasira.

Katika zama za sasa, kiongozi ambaye anaweza kukubaliwa na Watanzania sharti awe msafi na mwenye kuheshimu kiapo cha utumishi wa umma; Wasira siyo mwizi. Katika miaka tisa ya Serikali ya Awamu ya Nne ambayo amekuwemo, huku ikishuhudiwa mawaziri wengi wakikumbwa na kashfa za rushwa kubwa (ufisadi), hata mara moja Wasira hajawahi kujeruhiwa.

Hii hali kwamba mawaziri mbalimbali wanajeruhiwa kwa kuhusika na ufisadi, wengi wao wakiwa wameondolewa katika Baraza la Mawaziri kwa sababu ya uzembe au kuhusika moja kwa moja na rushwa, halafu wengine kuwa salama, hawajaguswa. Ni alama nzuri kwa Wasira.

Novemba 2014, wakati Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lilipotikiswa na kashfa ya ufisadi mkubwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, ambapo zaidi ya shilingi bilioni 300 ziliporwa, Wasira alikuwa mmoja wa mawaziri wachache, waliojenga hoja dhidi ya wenzao waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na wizi huo.

Wakati wapo mawaziri waliotaka kuwalinda wenzao, wakaibuka na wabunge waliopinga hoja ya kwamba zile zilizoibiwa ni fedha za umma, na kwamba ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitungwa tu kwa minajili ya kisiasa, Wasira aliposimama alizungumza bila kuwaonea aibu watuhumiwa.

Alisema, lazima serikali ishughulikie taarifa za PAC. Akasema taarifa kwamba wapo watu waliochota fedha kwa magunia, sandarusi, malumbesa, viroba na kadhalika katika Benki ya Stanbic, ni nzito na haziwezi kuachwa zipite tu, lazima vyombo husika vifanye kazi na wahusika wakamatwe.

Ilihitaji mtu mwenye uchungu na nchi, kuweza kuwageuka mawaziri wenzake. Suala la watu kuchota fedha kwa magunia, sanadarusi na kadhalika, lilikejeliwa na baadhi ya mawaziri pamoja na wabunge walioamua kuwatetea watuhumiwa. Wasira alisimamia ukweli ambao leo hii unamuweka huru katika suala la Escrow. Angetetea watuhumiwa, angekuwa amejiharibia sana.

SURA YA PILI YA WASIRA:

Hapo ndipo kwenye swali. Je, anaweza kujidhibiti akiwa na madaraka makubwa ya Urais au ndiyo atakuwa amepata rungu la kuwanyoosha wananchi, wabaya wake au wapinzani kwa misingi ya udikteta? Kiulizo hicho kinatokana na ukweli kwamba wasifu mkubwa wa Wasira ni mtu asiye na subira.

Wasira anayo rekodi ya kumpiga mwandishi wa habari kipindi akiwa NCCR-Mageuzi. Ni kipindi hicho alitungiwa jina la Tyson, akifananishwa na bondia wa zamani wa Marekani, aliyepata kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani, Mike Tyson. Jina hili amedumu nalo, japo mwenyewe hapendi kuitwa hivyo.

Katika kipindi cha Bunge la Tisa, chini ya Spika Samuel Sitta, Wasira aliwahi kuonya na kutishia kugombana na wabunge ambao walikuwa na kawaida kila akiitwa kwa ajili ya kutoa mchango wowote bungeni, walitoa sauti za chinichini "Tyson… Tyson… Tyson…" Akasema ole wake amsikie mtu mwingine anamwita hilo jina.

Kwa kawaida, Wasira ni mtu ambaye anapenda kuogopwa. Hata mkwara wake kwa wabunge kuwa "ole wao awasikie", ulikuwa na maana hiyohiyo, wamwogope na wasiendelee. Je, ni sahihi kuwa na Amiri Jeshi Mkuu ambaye anapenda watu wawe wanamwogopa? Katika zama hizi ambazo demokrasia inanadiwa kila kona ya dunia? Na inahitajika sana!

Hili la Wasira na ubabe, hata mimi limewahi kunitokea. Mwaka 2010, nikiwa bungeni Dodoma kwa ajili ya kuripoti habari za bunge, hususan kuwapiga picha wabunge ili kutengeneza maktaba mpya ya kampuni yetu, ukizingatia kuwa ndiyo tulikuwa tunatoka kwenye Uchaguzi Mkuu 2010 na bunge lilikuwa na sura nyingi mpya.

Ajabu ni kwamba Wasira alinikimbiza. Kwa lugha ya vijana ni kwamba ‘alinitoa nduki'. Kosa langu kumpiga picha tu! Eneo hili linatia shaka sana kwa Wasira. Binafsi napata tabu kuamini kama anaweza kubadilika na kuwa kiongozi mzuri, aliye na uhusiano mzuri na watu.

Hajawahi kupewa mamlaka ya kuongoza wizara nyeti kama Mambo ya Ndani au ya Ulinzi, pengine tungeweza kupata tathmini ya uvumilivu wake dhidi ya vishindo vya hapa na pale, au uwezo wake wa kuhimili mikikimikiki ya wapinzani, waandamanaji na kadhalika.

Pengine tungeweza kushuhudia jazba zake na uamuzi wake wa haraka wa kutumia nguvu kwa sababu tu Jeshi la Polisi lipo chini yake. Au Jeshi la Wananchi (JW) na lile la Kujenga Taifa (JKT), yapo chini yake. Hajawahi kuwa na mamlaka hayo, hivyo ni ngumu kumuwekea dhamana hata ya maneno.

Kawaida ni kama sheria! Kwa maana hiyo, hulka ya Wasira ya ubabe ndivyo alivyo na itakuwa ngumu sana kumbadilisha. Kwa tabia ya Wasira labda tutarajie kwamba atakwenda kujifunzia uhusiano mwema na watu akiwa Ikulu, jambo ambalo haliwezekani hata kidogo.

Wanasema ukitaka kujua kama mtu anaweza kutunisha mabega au akawa mnyenyekevu siku zote, jaribu kumpa madaraka ndiyo utaona. Sasa kama akiwa na nafasi za chini amekuwa katika sura hiyo, itakuwaje pale ambapo ameshaapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Wapo watu ambao wamekuwa wakipendekeza kwamba umefika wakati mwafaka kwa Tanzania kuwa na Rais dikteta. Kwa aina hii ya watu, Wasira anaweza kuwafaa sana. Maana yeye hatakuwa na hulka ya kucheka wala subira kama Rais Jakaya Kikwete ambaye wanaona hafai, wanamtaka anatakayeongoza kiimla, kibabe! Amri kwa kwenda mbele!

Taifa linapita katika migogoro na nchi za Rwanda na Malawi. Uvumilivu wa Rais Kikwete katika kutafuta majibu kwa njia za kidiplomasia umekuwa ukionekana. Kama angekuwa Wasira, pengine leo tungekuwa tunazungumza lugha tofauti. Kwa kawaida Wasira hapendi kuchezewa.

Sura nyingine ya Wasira ni usaliti! Mwaka 1992 akiwa mwanachama hai wa CCM, alishiriki vikao na michakato yote ya awali ya kukiasisi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliwahi kutaja orodha ya waasisi wa chama hicho, akamtaja na Wasira.

Baadaye, Wasira alijikausha na uanachama wake wa CCM na mwaka 1995 akataka kugombea ubunge Jimbo la Bunda kwa tiketi ya CCM. Alipokataliwa na kupitishwa Warioba, ndipo alijiunga na NCCR-Mageuzi.

Zipo taarifa kuwa uamuzi wa kumzuia asigombee ulitoka makao makuu ya CCM, baada ya kuwa na taarifa zote za kiintelijensia kwamba Wasira alikuwa mmoja wa waasisi wa Chadema, wakati akiwa ni mwanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi. Kwa hakika huu ni usaliti, na haipendezi kiongozi kuwa nyendo za usaliti wa chinichini.

HATABIRIKI:

Wasira hajajipambanua yeye anaamini katika njia zipi za uchumi. Japo hili ni tatizo la karibu watu wote ambao wameonesha nia ya kuutaka Urais mwaka 2015. Tupo kwenye ulimwengu wa gesi na Tanzania kuna ugunduzi mkubwa umeshafanyika, ni vizuri tukajua au kuhisi kuwa Rais mtarajiwa ana makusudio yapi.

Kuna kasoro kubwa sana hapa! Wanasiasa wengi hawana hulka ya kuandika, kwa hiyo inakuwa vigumu kupata mawazo yao ya namna wanavyoutazama uchumi wa nchi, tafsiri na majibu yao. Mawaziri wengi kwa vile wao wana wizara zao, jukumu la uchumi na bajeti ya nchi, humwachia Waziri wa Fedha.

Jukumu la gesi asilia, linaachwa kwa Waziri wa Nishati na Madini. Kwa maana hiyo, ni vigumu kumtabiri Wasira na mbinu zake za kuujenga uchumi wa nchi kwa sababu hajawahi kuyapambanua mawazo yake japo kwa maandishi. Kwa hapa japo ni msomi wa uchumi, ila hatabiriki.

Kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa hili. Ni wakati mwafaka wa kuwa na viwanda vingi, vilivyokufa vifufuliwe, mchezo wa kuuza malighafi ufe, serikali iwajengee uwezo wananchi na kuwawezesha kuuza bidhaa zilizopita kiwandani badala ya mazao. Hapa pia hatabiriki.

By Luqman Maloto
 
Hapo Mkuu marekebisho...aliyekuwa miongoni mwa waasisi wa CHADEMA ni kaka yake George Wassira...wakati huyu ni Steven Massatu Wassira
Kwa sifa hizo,huyu ni mtu ndani ya chama anayestahili kuppeperusha bend era,hayo mengine ya maumbile nk si hoja,hakuna mwanadamu aliyejitengeneza
 
Back
Top Bottom