Shemsa Mohammed Katika Mapokezi ya Makonda Mkoani Simiyu, Akitawazwa Jina la Bagolole

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

Cde. Shemsa Mohammed Katika Mapokezi ya Makonda Mkoani Simiyu, Akitawazwa Jina la Bagolole.

KATIBU wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda amewasili Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kufanya ziara ya kikazi, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya mikoa 20 backo to back.

Akiwa Mkoani humo, Umoja wa Machifu wa kabila la Wasukuma wamemtawaza Makonda kwa jina la Bagolole ikimaanisha WANYOOSHE, huku akisema muda wa kuwanyoosha Wakandamizaji umefika.

Akizungumza leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika stendi ya zamani Bariadi, Makonda amesema kilimo cha Mkoa wa Simiyu ni kilimo cha kujikumu na siyo kilimo cha kusubiri Amcos wawalipe wakulima.

‘’Maelekezo ya Chama, hawa wakina mama waachwe wauze sokoni kwa mteja wanayemtaka kumuuzia, nafahamu mpango wenu wa stakabadhi ghalani ni mwema lakini katika hili tupeni muda, kilimo kinahama kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kimataifa’’ amesema Makonda na kuongeza.

‘’Maafisa kilimo ni marufuku kukaa ofisini, nendeni kwa wakulima, Chama kilishamwelekeza Waziri Bashe, Mnafahamu Rais Samia katoka pikipiki kwa watendaji wa kilimo nchi nzima, katoa pikipiki, ipad na vipimo vya udongo’’

Amewataka kumwamini na kumwombea Dk. Samia Suluhu Hassan, huku akisisitiza kuwa kuna baadhi ya watu wamepewa nafasi kwenye ofisi za umma na kwamba majibu wanayotoa siyo maelekezo ya Dk. Samia bali ni majibu yao.

MWISHO.
 
Attachments

  • DSC_4222.JPG
    DSC_4222.JPG
    51.3 KB · Views: 5
  • DSC_4215.JPG
    DSC_4215.JPG
    40.2 KB · Views: 5
  • DSC_4265.JPG
    DSC_4265.JPG
    43.7 KB · Views: 5
  • DSC_4217.JPG
    DSC_4217.JPG
    46.1 KB · Views: 6
  • DSC_4221.JPG
    DSC_4221.JPG
    54.9 KB · Views: 5
  • DSC_4209.JPG
    DSC_4209.JPG
    46.2 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-01-30 at 00.11.48.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-30 at 00.11.48.jpeg
    422 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-01-30 at 00.11.56.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-30 at 00.11.56.jpeg
    251.1 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-01-30 at 00.11.57.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-30 at 00.11.57.jpeg
    618.4 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-01-30 at 00.11.58.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-30 at 00.11.58.jpeg
    472.7 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-01-30 at 00.11.52.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-30 at 00.11.52.jpeg
    219.8 KB · Views: 5
Eti majibu wanayotoa sio maelezo ya Raise ni yao binafsi, hii nchi changamoto sana. Sasa hao watu walijiteua wenyewe?
 
Mzee piga kazi hizi kelele zimekua nyingi sababu unaweka mchanga kwenye kasungura kao kalikokua tayari Kwa kuliwa.
 
Cde. Shemsa Mohammed Katika Mapokezi ya Makonda Mkoani Simiyu, Akitawazwa Jina la Bagolole.

KATIBU wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda amewasili Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kufanya ziara ya kikazi, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya mikoa 20 backo to back.

Akiwa Mkoani humo, Umoja wa Machifu wa kabila la Wasukuma wamemtawaza Makonda kwa jina la Bagolole ikimaanisha WANYOOSHE, huku akisema muda wa kuwanyoosha Wakandamizaji umefika.

Akizungumza leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika stendi ya zamani Bariadi, Makonda amesema kilimo cha Mkoa wa Simiyu ni kilimo cha kujikumu na siyo kilimo cha kusubiri Amcos wawalipe wakulima.

‘’Maelekezo ya Chama, hawa wakina mama waachwe wauze sokoni kwa mteja wanayemtaka kumuuzia, nafahamu mpango wenu wa stakabadhi ghalani ni mwema lakini katika hili tupeni muda, kilimo kinahama kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kimataifa’’ amesema Makonda na kuongeza.

‘’Maafisa kilimo ni marufuku kukaa ofisini, nendeni kwa wakulima, Chama kilishamwelekeza Waziri Bashe, Mnafahamu Rais Samia katoka pikipiki kwa watendaji wa kilimo nchi nzima, katoa pikipiki, ipad na vipimo vya udongo’’

Amewataka kumwamini na kumwombea Dk. Samia Suluhu Hassan, huku akisisitiza kuwa kuna baadhi ya watu wamepewa nafasi kwenye ofisi za umma na kwamba majibu wanayotoa siyo maelekezo ya Dk. Samia bali ni majibu yao.

MWISHO.
huyu mjamaa ana kasi ya mwendokasi na hana mpango wa kupumzika hadi October 2025 🤣

vibaraka na wengine mpaka sasa pumzika ingekua imeshakata siku nyiiiiingiiii🐒
 
Back
Top Bottom