Huyu zee la nyani la Gombe si alisema kuwa CHADEMA itakuwa imekufa na kupotea katika miaka 2 ijayo?
Sasa baada ya mikakati yake akisaidiana na kina Mchembe,Polisiccm na Usalama wa Taifa wamegundua kuwa CHADEMA ni maji marefu.
Ifuatayo ni mikakati iliyoshindwa ya Wassira na Magamba wenzake:
- Wamejaribu kutengeneza video fake zimeshindwa
- Wametunga kesi za kubambikiza kwa Viongozi na Wanachadema zimekwama.
- Wamejaribu kufuta au kutengua Ubunge wa baadhi ya Wabunge wa CHADEMA wameshindwa.
- Wameteka waandishi wa Habari na Viongozi wa Madaktari wameshindwa.
- Wamemwua mwandishi wa Ch.10 Daudi Mwangosi wakashindwa.
- Wameua watu kwenye mikutano na maandamano ya CHADEMA bado wameshindwa.
- Wamechochea udini,ukabila na itikadi wameshindwa.
- Wametumia Bomu la Kivita la kutupa na mkono kwenye mkutano wa kampeni wa CHADEMA pale Soweto na kutaka kumwuua Mwenyekiti Taifa na Mbunge A Town bado wakashindwa.
Sasa wanataka kumtumia kiranja wao Mkuu John Tendwa aifute CHADEMA kwa sababu dhaifu kabisa ati ya kutaka kuanzisha vikundi vya ukakamazu na ulinzi shirikishi ndani ya CHADEMA. Vikundi kama hivi vipo hata ndani ya CCM na jamaa zao wa CUF lakini Tendwa amenyamaza kimya!!!
Nataka tu nimshauri Tendwa ushauri wa bure kabisa kuwa Watanzania ni wapole sana na waungwana sana.Watanzania ni wavumilivu na wastahimivu sana. Watanzania ni wapenda amani. Lakini kwa namna Serikali ya CCM inavyotawala(siyo kuongoza) kwa sasa Watanzania hawahawa wenye sifa nilizozitaja hapo mwanzo wanabadilika kidogokidogo! Kama Tendwa ana macho ya kutazama na aone sasa, kama Tendwa ana masikio ya kusikia na asikie sasa. Kwamba Watanzania wameshachoka na siasa za CCM za kutaka kuwaburuza Watanzania kama vile hawana akili.
Namsihi Tendwa akae,atafakari na aone kama ana macho kile kilichotukia Arusha kwenye Bomu la Soweto na mrejesho wa hisia za Wana Arusha kwenye matokeo ya Chaguzi za Kata 4 za Udiwani hapo Arusha. Kama ana macho ya kuona na aone sasa.
Lakini pia namsihi Tendwa akae na atafakuri kile kilichotokea Mtwara kuhusu Gesi asilia na kinachoendelea kufukuta chini kwa chini hukohuko Mtwara kwa sasa.Bila shaka amesikia na kama hajaona basi afike Mtwara ajionee mwenyewe uhalisia na mambo asingoje kusimuliwa.
Akisha tafakari yote haya sasa ndipo apime na aone kama itakuwa ni busara kwake kuifuta CHADEMA kwenye daftari lake la kuandikisha vyama. Kama hana akili na busara za kutafakuri basi aendelee na mpango wake na hao magamba wenzake kuifuta CHADEMA ambao bila shaka kwao ni mpango PLAN B au C. Tendwa atangaze hata kukifuta leo halafu aone nini kitafanyika nchi nzima.Kama ana simu ya Mohamed Morsi wa Misri ampigie amwulize nini walichofanya Wamisri kwa serikali yake!
Na ndipo Tendwa atakapojua kwamba hupashwi kuchezea nguvu ya Wananchi(Umma) kwa namna yoyote ile.