Wassira: CHADEMA kufa ni Ngumu

Wassira: CHADEMA kufa ni Ngumu

Hatimaye waziri wa Jk bwana Stephen Wasira kakili kuwa CHADEMA haiwezi kufa kirahisi na CCM wasibweteke na kudhani kitakufa kama walivyopanga huko nyuma na kuwaomba waangalie njia mbadala ikiwemo kumshawishi msajili wa vyama vya siasa kukifuta.

Source Gazeti Jamuhuri

Hizi ni baadhi tu ya ndoto zake anazoota mchana kama zile anazoota wakati akiwa amelala kule bungeni..
 
Hahahahahaha huyu mzee si ndo alisema kauli kuwa atahakikisha chadema kinakufa,kachemka kumbe
 
Mzee Wassira inabidi chama chako kijiandae na Tsunami ya CHADEMA ya 2015. Maana hiyo itakustaafisha siasa na kukurudisha GOMBE ukaungane na wenzako
 
Ritz, Simiyu yetu, HAMY-D, bungeni. Nadhani mmepata taarifa kwamba mzee wenu amekiri kwamba haiwezekani kukisambaratisha CHADEMA hivyo tafuteni namna mpya ya kufanya siasa lakini kwa mfumo huu wa siasa zenu uchwara mnakiangamiza Chama Cha Mapinduzi.

teh teh...huyo ni wassira..watamwita ni Chadema ndio maana anaiua CCM kila akifungua mdomo au kupanga jambo....Wassira soon atawapelekea Zawadi CDM...kukubali kuchindwa.Kisha tangaze amani halafu .....awe anajongea taratibu ili uzee wake usiishie ktk cello ndogo kwa ajili ya mwigulu.
 
wanahaha hawana pa kushika wasubili kumbe kufa kwa chama chao hawajui watanzania wameshachimba na kabuli kwa ajili ya ccm hahahaaaaaa!
 
Chadema kama saccos zingine inaweza filisika mda wowote
 
wassira tangu lini akawa na nia njema na CDM? ucku kucha anaota kifo cha CDM,maskini mzee wangu.Atafaulu ktk ndoto hizo?
 
Nyara ya taifa, hongera kwa kujua ukweli, japo njia mbadala haipo isipokuwa nyinyi na wanenu kukaa pembeni, ukipenda na wake zenu la sivyo tutakuwa nao CDM.
 
kila akiongea huyu mzee ni pumba tupu. Adui wake ni ESTHER BULAYA sio CDM
 
mwerevu huangalia upepo wa jambo, kama kuna mawazo mgando ndo haya, kuna vyama vinawanachama chini ya 1000 liakini vinaishi hiki ambacho kimeteka na wasomi wa Tanzania na wasio kuwa na elimu ndo kife?
 
Kamwe Chadema haiwezi kufa eti kwasababu ya wasaliti wachache kufika Bei.
Dhahabu inapopita kwenye Moto ili iwe Safi huwezi sema inaisha.
Zaidi ninaowaonea huruma ni watanzania maana wanakosa watetezi na wasemaji makini.

Jiulize swali Kama CCM wameweza kuiba mabilioni ya pesa na upinzani ukiwepo vipi wangekuwa peke yao.

Watumishi wa umma kwa miaka minne mmefanywa maskini na CCM wapinzani wamewatetea Sana na bado CCM ikawatwisha zigo la bodi ya mikopo bila huruma vipi Kama wapinzani wasingekuwepo si ajabu hata mishahara msingelipwa kumbukeni hii ni serikali inayotaka watu wake waishi kwa mateso na c furaha .

Ujinga wa watanzania ndio madhila Yao na CCM wanajua kwamba wananufaika na ujinga wa watanzania siku mkiamka ndio mtajua kwamba kumbe mlilala usingizi wa pono.

Kiufupi CCM inatakiwa iondolewe madarakani haraka Sana ila watanzania bado ni Kama makonokono pole sana nchi yangu.

Unafiki na USALITI unaofanywa na baadhi ya wapinzani hautauwa upinzani Bali utauimarisha na ipo siku mtajibu dhambi ya USALITI huu.

Mnaomsaliti Ben sanane Leo hivi mnajua damu yake iko wapi muda huu?

Mnaomsaliti Lisu Leo mnajua damu yake ilimwagika kwaajili ya ukombozi wa taifa? Ili watoto wenu waishi vizuri miaka ijayo? Sasa kwa USALITI wenu watoto wenu wataishi utumwani maana nyie baba zao mnayatengeneza haya maisha Yao Sasa.

Tulishafikia point ndogo Sana ya kuiondoa CCM nyie mnaturudisha nyuma .

Haina shida tutafika nchi ya ahadi ila ole wenu!!!
 
Njia zote mbili ulizozitaja zote zinawezekana hasa Ile moja ya Chama kufa endapo hakuna hatua zinazochukuliwa na viongozi wetu

Mimi na wewe ni wanachama tu, viongozi wetu na wanaokaa kutengeneza na kujadili namna Bora ya uendeshaji wa Chama wakiendelea kujitoa, hii ni ishara mbaya,

Hatuwezi kuwa tunaimba tu kila siku kwamba, Chadema haiwezi kufa wakati mwanzo wa kifo ni homa na sasa iko homa ikiendelea kama malalia na hatimaye inaweza ikawa ni malalia sugu na ndo kidokidogo mara mtu huyo....!!! watu... Hoooo katuacha na parapanda ikaimbwa.

Na hizo sjui sababu za watumishi kutokupandishiwa mishahara, na mambo kibao kuwa sababu ya watu kuwa na hasira ya kuiwajibisha CCM, hata Chadema ikifa wao hawana cha kupoteza, viongozi wa Chadema wajipange, wasidhani Chama kipo mitandaoni!!!! Huku tunawatia moyo tu na Wala hatuna lingine la kufanya zaidi ya kuwatia moyo, kazi ya kuhakikisha Chama hakifi ni wao
 
Hatimaye waziri wa Jk bwana Stephen Wasira kakili kuwa CHADEMA haiwezi kufa kirahisi na CCM wasibweteke na kudhani kitakufa kama walivyopanga huko nyuma na kuwaomba waangalie njia mbadala ikiwemo kumshawishi msajili wa vyama vya siasa kukifuta.

Source Gazeti Jamuhuri
Kuifuta cdm ni Kwa kutatua shida za watz,wameacha kutatua shida za watz kutwa kucha wanakimbizana na Mbowe badala ya shida za watz
 
Back
Top Bottom