Wasomi wa Tanzania wametoa mchango gani kwenye Taifa letu mpaka sasa?

Usitegemee maendeleo kwa Taifa la watu wanaokamata madaraka kwa kuhonga, kupewa vimemo, na kuteuliwa kutokana na kuwa na ushikaji au nasaba na Rais, au mwandamizi mwingine.

Wasomi wapo, hilo halina ubishi, tena ni wengi.

Shida ya kukosekana kwa maendeleo ni kwamba hao viongozi wa hapo juu niliowasema wanakosa guts za kusimamia effectively utendaji ndani ya serikali na mashirika kwa vile wao wenyewe ni toothless, hawapo pale kwa qualities zinazotakiwa.

Pia wataalam siku hizi wanaongozwa na wanasiasa.

Ulishawahi kusikia mwanasiasa anaagiza wataalamu wa kuleta mvua wewe? kama hujasikia hiyo ipo Tanzania.
Katika medium na context kama hiyo unategemea wataalamu na wasomi wana nafasi gani?

Ni mara ngapi umesikia loggerheads kati ya ushauri wa kitaalamu na mapendekezo ya wanasiasa?

Una habari UDOM imejengwa kwa matakwa ya wanasiasa?

Na unajua jinsi sasa wananchi watakavyoanza kulipia gharama za maamuzi hayo ya mwanasiasa? Je wataalamu na wasomi hawakuwepo? na je wangekuwana guts za kumstopisha mwanasiasa huyo asiliingize taifa katika maisha ya mashaka ya kubadilishiwa taratibu za mafao ya akic zao?

Wasomi wetu wamekatwa miguu na mikono short n clear.
 
Wasomi wengi hapa Bongo si wazalendo.. they are selfish.. Akilini wanaplan ''Individual gain'' watoke vipi, wapige kivipi (waibe).. wajilimbikizie mali binafsi kivipi. .. wachukue rushwa kivipi???

tutaendelea kuwa masikini kama hatutabadilika.
 
Wanabodi,

Tanzania is one of the poorest countries in the world, with a per capita income estimated a at about $250 per year.

Kila siku tumekuwa watu tukijiliwaza na kujifariji humu JF kuwa Tanzania tuna wasomi wengi wenye huwezo na maarifa ya kutosha mchango wao ni upi kwenye ujenzi wa taifa letu. Tukiangalia historia ya taifa letu toka wakati wa Mwl. Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete wasomi wetu wengi wanaounda serikali wametoka University of Dar es Salaam.

Tumeona hawa wasomi wetu ndio wamelifikisha taifa letu hapa tulipo wamebinafsisha mabenki makampuni ya umma, wamegawana nyumba za serikali, wameuza migodi yetu kwa wazungu. Mikataba yote mibovu ya taifa letu imefanywa na hawa wasomi wetu.

Ni kipi cha kujivunia sisi watanzania kutoka kwa wasomi wetu...CC to Mkandara, chama, Nguruvi3, Ngongo, zomba,

Wasomi wamesaidia kuiingiza kwenye umaskini usio mfano hii nchi. Kwanza wanafikiria matumbo yao, kwani msomi wa kwanza kushika madaraka aliwanyima kila kitu hata kula ilikuwa taabu, kuja Mzee Mwinyi kuwafungulia, wakawa na tamaa ya ajabu.
 
Usitegemee maendeleo kwa Taifa la watu wanaokamata madaraka kwa kuhonga, kupewa vimemo, na kuteuliwa kutokana na kuwa na ushikaji au nasaba na Rais, au mwandamizi mwingine.

Wasomi wapo, hilo halina ubishi, tena ni wengi.
Shida ya kukosekana kwa maendeleo ni kwamba hao viongozi wa hapo juu niliowasema wanakosa guts za kusimamia effectively utendaji ndani ya serikali na mashirika kwa vile wao wenyewe ni toothless, hawapo pale kwa qualities zinazotakiwa.

Pia wataalam siku hizi wanaongozwa na wanasiasa.
Ulishawahi kusikia mwanasiasa anaagiza wataalamu wa kuleta mvua wewe? kama hujasikia hiyo ipo Tanzania.
Katika medium na context kama hiyo unategemea wataalamu na wasomi wana nafasi gani?

Ni mara ngapi umesikia loggerheads kati ya ushauri wa kitaalamu na mapendekezo ya wanasiasa?

Una habari UDOM imejengwa kwa matakwa ya wanasiasa?
Na unajua jinsi sasa wananchi watakavyoanza kulipia gharama za maamuzi hayo ya mwanasiasa? Je wataalamu na wasomi hawakuwepo? na je wangekuwana guts za kumstopisha mwanasiasa huyo asiliingize taifa katika maisha ya mashaka ya kubadilishiwa taratibu za mafao ya akic zao?

Wasomi wetu wamekatwa miguu na mikono... short n clear.
WASOMI TUNAO WENGI ILA HAWATUMII AKILI ZAO NA TAALUMA ZAO KWA MAENDELEO YA TAIFA ILA WAPO KWA MASLAHI YA CCM, MFANO MUKANDARA, KIKULA, MLACHA NA WENGINE WENGI, NA WACHACHE WAZALENDO WANAISHIA KUUWAWA AU KUKANDAMIZWA NA SERIKALI MFANO Dr Kitila Mkumbo, Prof Shivji, Sungusia, na wengine wengi, ila CCMna mapupet wao wote their days are numbered.
 
Mi nadhani wapanga mipango na watekelezaji ambao ni watawawala ndiyo hovyo. Kwa sababu wanatumia kodi zetu kuwasomesha hawa watu ndani na nje ya nchi lakini wanashindwa kuwatumia kwa maslahi ya Taifa. Wakati wa Mwl. JK Nyerere wasomi walikuwa wachache lakini viwanda na mashirika ya Umma yalikuwepo lakini leo wasomi wengi viwanda na mashirika ya Umma yamekufa na mengine kubinafsishwa kwa wageni. Kwa waliosoma history sidhani kama hawatakubaliana na mimi kuwa mikataba wanayosaini viongozi wetu (watawala) ambao tumewaamini haina tofauti na ile ya wakoloni kina Karl Peter na wenzake.
 
Wanabodi.

Kila siku najiuliza sipati jibu sahaihi kuhusu wasomi wetu wa Tanzania..

Kwa mujibu wa data za World Bank na IMF Tanzania ipo kwenye kundi la nchi 20 maskini wa kutupwa duniani.

Baadhi ya nchi zimekuwa masikini kutokana kuwa na vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe kama vile Rwanda, DRC, Burundi, Somalia..

Hawa wasomi wetu kila kukicha wanajitapa na kijisifia na wengine wapo humu JF kuwa ni wasomi..

Ni kipi cha maana hawa wasomi wetu wa Tanzania wamelisadia taifa letu kutoka kwenye dimbwi la umasikini?

Kama kuna wasomi tunaomba mnijibu ni kipi mlichoifanyia taifa letu la Tanzania..
Nawakilisha...

Wewe si miongoni mwa wasomi hao? Umetoa msaada gani?
 
Hii topic labda sijailewa, maana serikali ya CCM ndio yenye resource zote za kuleta maendelea, Hiyo nafasi ya wasomi individually kuonyesha michango yao itapatikana wapi? Ukizingatia ukiwa na kiherehere cha kuwakosoa wanakata mirija yako yote ya riziki zako, wakati mwingine wanaweza kukuangamiza.Siasa chafu za serikali ya CCM is one of the greatest obstacle for them to deliver the best to their country.
 
Shida ni mfumo wa ccm usiotaka kubadilika wala kuachia madaraka. Ccm inawenyewe ambao ndio mafisadi na hawataki kubadilika wala kuachia madaraka.

Taifa la TANZANIA LITAKOMBOLEWA NA WASIO WASOMI. Tena watu wadogo sana. Mark my word utaniambia. Mungu anauwezo wa kutumia chombo dhaifu sana.
 
wanabodi.

Kila siku najiuliza sipati jibu sahaihi kuhusu wasomi wetu wa tanzania..

Kwa mujibu wa data za world bank na imf tanzania ipo kwenye kundi la nchi 20 maskini wa kutupwa duniani.

Baadhi ya nchi zimekuwa masikini kutokana kuwa na vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe kama vile rwanda, drc, burundi, somalia..

Hawa wasomi wetu kila kukicha wanajitapa na kijisifia na wengine wapo humu jf kuwa ni wasomi..

Ni kipi cha maana hawa wasomi wetu wa tanzania wamelisadia taifa letu kutoka kwenye dimbwi la umasikini?

Kama kuna wasomi tunaomba mnijibu ni kipi mlichoifanyia taifa letu la tanzania..
Nawakilisha...

majibu mbona yapo humu?
 
Serikalini ndio kumejaa wasomi na ndio watendaji wanapanga mipango ya uchumi baada ya kukusanya kodi zetu, labda wewe tuambie na mwingine mwenye jukumu la kuitoa Tanzania kwenye dimbwi la umasikini?

kiukweli si wote walioko serikali ni wasomi,vipi inssues za vyeti feki? Ikumbukwe kwamba msomi ni yule tu anayesaidia jamii/taifa lake vinginevyo si wasomi hawa bali ni makanjanja tu.Kwa wale ambao ni wasomi wa kwelix2 siasa imewateka kabisa,maana Tanzania yetu hii siasa ndio kilan kitu kuliko utaalam.Mwanasiasa anaweza kumchapa kibao mtaalamu ilihali mtaalamu yule anachekelea tu akisema sirudii tena mzee ili kuinusuru nafasi yake.Wacha kabisa,jiulize kwanini kura moja tu ya mjumbe ni karibu 1m.kwa sekunde tu ilihali 1m. unaweza kujifunza kozi fupi ya computer kwa mwaka.
 
Hii topic labda sijailewa, maana serikali ya CCM ndio yenye resource zote za kuleta maendelea, Hiyo nafasi ya wasomi individually kuonyesha michango yao itapatikana wapi? Ukizingatia ukiwa na kiherehere cha kuwakosoa wanakata mirija yako yote ya riziki zako, wakati mwingine wanaweza kukuangamiza.Siasa chafu za serikali ya CCM is one of the greatest obstacle for them to deliver the best to their country.

Serikali ya CCM iliasisiwa na nani? nikupe jibu au unalijuwa?
 
Mi nadhani wapanga mipango na watekelezaji ambao ni watawawala ndiyo hovyo. Kwa sababu wanatumia kodi zetu kuwasomesha hawa watu ndani na nje ya nchi lakini wanashindwa kuwatumia kwa maslahi ya Taifa. Wakati wa Mwl. JK Nyerere wasomi walikuwa wachache lakini viwanda na mashirika ya Umma yalikuwepo lakini leo wasomi wengi viwanda na mashirika ya Umma yamekufa na mengine kubinafsishwa kwa wageni. Kwa waliosoma history sidhani kama hawatakubaliana na mimi kuwa mikataba wanayosaini viongozi wetu (watawala) ambao tumewaamini haina tofauti na ile ya wakoloni kina Karl Peter na wenzake.

Nyerere alipopewa madaraka, Tanganyika ilikuwa ndio msafirishaji mkuu wa mazao katika Afrika. Hii nchi ilikuwa inasafirisha mazao ya mkonge kuliko nchi yeyote duniani, inasafirsha Korosho kuliko nchi yoyote Afrika, inasafirsha pareto kuliko nchi yoyote Afrika, inasafirisha Kahawa, Chai na Almasi. Inasafirsha nyama hai na za makopo, beef swaaaafi katika mikebe.

Baada ya kuja yeye kwa miaka saba tu ya mwanzo tukawa sisi ndio waagizaji wakuu wa chakula tena cha kusaidiwa.

Hivyo viwanda unavyovisema, vilikuwa ni ujinga wa hali ya juu na vyote vilianza kufa kabla yake.
 
Samahani wadau....mleta mada hajatujuza msomi ni nani........labda anavigezo vyake vya mtu kuwa msomi.......UDSM imetajwa......labda ili kuwa msomi lazima upite pale.....tujuze basi msomi yupi unayemzungumzia......mie kwangu msomi ni mtu yeyote mwenye busara na maarifa....
 
Lakini mkuu wakati huo wasomi hawakuwa wengi na pengine inaweza kuwa sababu ukiacha ushindani wa kibiashara kutoka mataifa makubwa ikiwepo Uingereza iliyotutawala wakitukwamisha kwa kila mbinu ionekane tumeshindwa kujitawala. Leo huduma nyingi za jamii tunalipia hasa elimu na afya, huduma za bure zimebakia kwa watawala na familia zao tofauti na kipindi cha Nyerere. Ukweli unabakia kuwa Serikali yetu siyo bunifu ila ni wataalam wataalam wa kutumia wasivyozalisha.
 
Tanzania ina rundo la watu wenye vyeti vya vyuo vikuu lakini hao ndio wajinga kuliko nursery school drop outs.
Nadhani education is a failed project in TZ.
 
Samahani wadau....mleta mada hajatujuza msomi ni nani........labda anavigezo vyake vya mtu kuwa msomi.......UDSM imetajwa......labda ili kuwa msomi lazima upite pale.....tujuze basi msomi yupi unayemzungumzia......mie kwangu msomi ni mtu yeyote mwenye busara na maarifa....

Nadhani anaongelea watawala wa nchi.
 
Ritz, heshima mkuu..

Ningependa kuchangia thread yako NZURI, lakini kabla ya kufanya hivyo, ningependa kujua definition yako ya msomi/wasomi? Na je, wewe ni miongoni mwao(wasomi)?
 
Serikali ya CCM iliasisiwa na nani? nikupe jibu au unalijuwa?

Kina bibi titi, kawawa na wazee wa kiswahili wengine labda walikuwa na Phd?
Michango mingi ya wasomi wa leo haitakaa ionekane kwa serikali hii ya sasa iliyoko madarakani(dhaifu) na mfumo uliyopo (ufisadi,Ubinafsi na Kulindana).
 
Tatio unachanganya CCM na TANU, au unalijuwa hilo?
 
Back
Top Bottom