Wasomi wa Tanzania wametoa mchango gani kwenye Taifa letu mpaka sasa?

wasanii kama kanumba walikua na jina kubwa, na wanasiasa wanapenda sana publicity, wasomi wengi hawajulikani nje ya fraternity kubwa zao za usomi yaani nje ya vyuo, wanafunzi wao, na wasomi wenzao (ambao kwa tz ni wachache mno)..mimi kama mwanasiasa ningechukua point pale mtu mwenye nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari anapokufa haijalishi ni msanii au la..

ila kwenye hali nyingine wasomi hawapewi sapoti nzuri na serikali kama mambo ya utafiti, ushauri wa karibu kwa serikali, kuhusishwa kwa vyuo na taasisi nyingine za elimu ya juu katika kutunga na kufuatilia sera za kitaifa n.k ila wasanii JK kawapa nyumba, na anawaita ikulu, anawato jela wakihukumiwa n.k
 
Jibu ni rahisi, kwa wana siasa sanaa ni jimbo kwa sababu inavuta na kuwagusa wengi wasomi na wasiowasomi. Hivyo, kushiriki kwenye matukio yanayohusu sanaa na wasanii ni katika mbinu ya kuongeza idadi ya kura. Bahati mbaya wasomi hawajulikani sana isipokuwa kwa wasomi wenzao na wanafunzi wao. Kwa sababu hiyo kushiriki kwenye issue za wasomi hakuwafanyi kuwa watu wa watu kama wanavyotaka kujinasibisha.
 
unadhani kukaa na kubuni kuandika pepa za kuomba funds kwa wazungu inatosha? Kanumba alipokufa kuna watu kama 20 na zaidi ajira zao zimeyeyuka. Msomi kaaajiriwa na anatengeneza tu liability kwa taifa kutikana na uchakachuaji anaoufanya kila mara... Fikiria pande zote
Huna akili hata kidogo..unamlinganisha kanumba aliyekuwa anafundisha watu uzinzi na Prof. wa Chuo kikuu aliyefundisha watu kibao ambao ni nguvu kazi ya taifa hili? Kanumba alikuwa role model wa mahouse girl, waswahili ambao ni wavivu wa kufikiri na wanafunzi wa shule za kata; na ww nafikri ni mmoja kati ya makundi haya!
 
Mkuu, dunia nzima ndivyo ilivyo wasanii wanathaminiwa kuliko wasomi hata mazishi yao watu wengi wanaudhulia tofauti na wasomi mfano mmoja ni Marekani kwenye hao wasomi wengi...angalia mazishi ya Whitney Houston,Michael Jackson, yalitangazwa dunia nzima kuzika kwenyewe watu walivyokuwa wengi mpaka card, lakini wanakufa Maprofesa wanazikwa kawaida tu na wana familia.
 
Hapo ndio umeonesha matatizo yetu sie watanzania, nchi hii haiwezi kutoka kwnenye umasikini kwa sababu ya mawazo kama yako best.....fikiri hizo paper unazoongelea matokeo yake yangekua yanafanyiwa kazi na wananchi pamoja na serikali kwa michango yetu wenyewe bila kutegemea fund toka nje zingetenzeneza ajira zaidi ya hizo 20 unazosema tena mara 7*70.

Hao wanaoandika hizo pepa wanaishi angani? Kwanza hao wanaoandika hizo pepa lengo lao ni kupata pesa, na haohao walitakiwa kutekeleza walichoombea fedha. Mbona hawatekelezi? Wasomi ni wengi lakini hawana impact ya kutosha kwenye taifa hili. Mtu anayekufa akililiwa analiliwa kwa mengi
 
Mkuu, dunia nzima ndivyo ilivyo wasanii wanathaminiwa kuliko wasomi hata mazishi yao watu wengi wanaudhulia tofauti na wasomi mfano mmoja ni Marekani kwenye hao wasomi wengi...angalia mazishi ya Whitney Houston,Michael Jackson, yalitangazwa dunia nzima kuzika kwenyewe watu walivyokuwa wengi mpaka card, lakini wanakufa Maprofesa wanazikwa kawaida tu na wana familia.
Wanathaminiwa na mashabiki wao na wasanii wenzao..katika huo umati uliohudhuria msiba wa MJ & WH ulimouna kiongozi gani wa serikali wa Marekani? Kanumba alikuwa anapendwa na mahouse girl na vilaza ambao wanapenda movie za kijinga za kinijeria zilizotafsiriwa kwa kiswahili. Hao ndio walistahili kumzika kanumba sio viongozi waandamizi wa serikali. Ni aibu kubwa!
 
FJ, hili halina cha kujadili maana ni kweli tupu na kuwa sahihi kabisa mada ingekuwa "Kwa nini Wasomi, Waadilifu na Watendaji wazuri hawapendwi / hawapewi nafasi?

Inabidi tujitokeze tuweke mkakati mahili kama ule wa maajeti mahili katika movie ya 'Mission Impossible' tuokoe Taifa letu. Mtengeneza hiyo 'movie' nabook nafasi sasa ya kuwa mmoja wa ma- actor! Angalia mguu wangu kwenye avatar yangu uone jinsi teke langu litakavyoshughulikia Wanaume Majasusi wasiotufaa kati ya miguu yao, panapouma kuliko popote.
 
Hao wanaoandika hizo pepa wanaishi angani? Kwanza hao wanaoandika hizo pepa lengo lao ni kupata pesa, na haohao walitakiwa kutekeleza walichoombea fedha. Mbona hawatekelezi? Wasomi ni wengi lakini hawana impact ya kutosha kwenye taifa hili. Mtu anayekufa akililiwa analiliwa kwa mengi

Kwani hao wasanii wanaishi angani?hakuna anayefanya kazi humu duniani hata huyo msanii asiye na lengo la kupata pesa. wasomi ni wengi lkn hawapewi nafasi na hoja zao zinatupwa nje au kuwekwa pembeni maana zinaharibu msingi wa wasanii,na wanapojaribu kutekeleza tu wanaharibiwa na wasanii...ni kweli mtu akifa analiliwa kwa mengi nakubaliana na hilo kwa maana kubwa ambayo ni binadamu yeyote kumpoteza inasikitisha hata msomi sio msanii tuu.
 
Ni ukweli ulio wazi. Msanii ni maarufu zaidi kuliko professor, kila mwananchi anamjua msanii, lakini professor ni maarufu kwa watu wachache/wanachuo/na wasomi wacahche

Hata mimi ningekuwa politician msiba wa msanii ndio mahali pa kuonyesha ukaribu na wananchi..

Hivyo msiba wa Kanumba kuvutia wana-siasa sio ajabu
 
Wakuu,tanzania tuna wasomi wa kila aina ktk nyanja tofauti kitaaluma waliosomeshwa kwa kodi zetu(wengi wana nyadhifa),matatizo yamezidi je wapo na dhima yao iwapi kabla hawajagoma madaktari basi wenye busara wanusuru uhai wa watz kwa kutumia weredi wao.nawasilisha
 
Wapo maprofesa na madaktari wengi serikalini na wastaafu wengi,hata nikiorodhesha majina wengi wanafahamika,naomba tujadili uwajibikaji(responsbilities)wao katika jamii
 
Walaji ni wengi maslai yao wameya weka mbele zaidi ya utaifa.

Hawana uwajibikaji wanasababisha serikali kupoteza pesa nyingi kuwa undia tume kuwachunguza kila kukicha.

Wengi wao wachumia tumbo.
 
WASOMI WA TANZANIA WAMEKUWA WASALITI?

Nchi zote zilizoendelea na zinazozidi kuinuka kiuchumi duniani zimepata maendeleo makubwa kwa kuwasomesha watu wake. Napenda niwagawe wasomi wote katika makundi mawili makubwa kama ifuatavyo:

Kundi la kwanza ni la wasomi ambao ni wanasiasa kama Rais, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, nk. Kundi la pili ni la wasomi waajiriwa ambao sio wanasiasa. Kila kundi linategemewa kwa namna yake kuleta maendeleo nchini. Nchi yenye wasomi wengi wa makundi yote mawili inatarajiwa kuwa na maendeleo zaidi kuliko nchi ambayo ina wasomi wachache. Jambo hili kwa Tanzania ni tofauti kabisa. Kwa Tanzania kuwa na wasomi wengi kumekuwa ni chanzo cha kupiga hatua kubwa nyuma maana kila msomi wa Tanzania anafikiria ni jinsi gani ya kupata maendeleo binafsi ya haraka kwa njia zisizo halali. Kwa kudanganya, kuiba, kula rushwa, nk. Msomi wa Tanzania akipata kazi anafikiria jinsi ya kutoka haraka haraka ili marafiki zake waone kuwa ni mjanja kweli.

Kutoka kwenyewe ni kwa wizi. Ni wachache sana wanaofikiria kupata kazi na kuitumikia nchi kwa uaminifu. Msomi wa Tanzania akipata kazi anafikiria kununua gari na kununua kiwanja kama sio kuanza kujenga ndani ya mwaka mmoja. Hata akifanikiwa kutimiza hayo ya msingi katika muda mfupi bado haridhiki. Starehe kwa mbele na kwa kina. Hulka hii ni kubwa sana kwa wasomi waliopata fursa ya kuwa viongozi wa kisiasa. Viongozi wa kisiasa ni viongozi wa umma. Vitu alivyoibiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Adamu Kighoma Malima akiwa hotelini huko Morogoro ni ushuhuda mzuri wa starehe zilizokithiri za wasomi. Wasomi kama hawa ndo wamechangia sana kuwaharibu wasomi waajiriwa wasiokuwa wanasiasa. Kuwa msomi wa kuheshimika Tanzania siku hizi maana yake ni kuwa mtu wa dili.

Dili ni mipango ya wizi tu wala hakuna kitu kingine. Kama hujaiba au kufisadi unakofanyakazi unaonekana huna maana, unaonekana umezubaa, unaonekana mpumbavu, unaonekana usomi wako ni wa kutiliwa mashaka. Ukiwa mtu wa kufuata maadili ya kazi unaonekana una matatizo katika kichwa chako. Siku hizi kumpata msomi asiyefikiria kuiba ni kazi kubwa kweli. Naye akipatikana usalama wa kazi yake unakuwa hatarini. Hakubaliki kwenye jamii kubwa ya wasomi. Kuanzia kwa Rais mwenyewe hakuna aliye na moyo wa kuiletea maendeleo nchi yake. Kitendo cha Rais kunyamazia vitendo vya ufisadi vya akina Andrew Chenge na wenzake kinaonesha wazi kuwa Rais naye anahusika katika ufisadi. Tena yeye ndiye fisadi mkuu.

Lakini wasomi hawa wanapotembelea nchi zilizoendelea ndo wa kwanza kuanza kusifia hatua ya maendeleo iliyofikiwa katika nchi hizo. Utafikiri maendeleo hayo yalikuja yenyewe. Wakirudi wanaishia kutoa takwimu tu kutoka katika nchi hizo ili waonekane mbele ya jamii kuwa wamefika huko. Usomi wao unadhihirishwa kwa kutoa takwimu tu. Hawajifunzi na kufanya chochote cha kubadilisha maisha hapa nchini. Kazi yetu ni kwenda kuomba misaada kwa nchi hizo bila aibu hata kama nchi zenyewe zina raslimimali chache kuliko zetu.

Wasomi wetu hawa ndo wa kwanza kuingiza nchi katika mikataba ya kinyonyaji isiyo na masilahi kwa nchi. Wanafanya hayo wakijua wala sio kwa bahati mbaya. Hawa hawana njaa ya fedha wala nini, ni uchu wa utajiri uliopitiliza mipaka. Kama watu hawa wanaosaini mikataba hiyo wangekuwa hawana ujuzi wa kutosha tungeona tunanyonywa kutokana na ukosefu wa wasomi. Tungejihurumia sana kwa kukosa wasomi.

Wasomi wetu hawa ndo wa kwanza kula njama na makampuni ya kigeni kuleta vitu feki nchini. Hata kama vitu hivyo vina athari za kiafya. Wako tayari watanzania na ndugu zao wafe lakini wamesaidia wageni kutajirika.

Wasomi hawa ndo wa kwanza kula njama za kuwasaidia wafanya biashara kukwepa kodi mbalimbali wakati wanajua maendeleo ya nchi yanategemea kodi. Maendeleo ya nchi yetu kwao sio muhimu. Muhimu ni maendeleo ya nchi nyinginezo. Ndo wasomi wetu tuliowalilia kuwapata tangu enzi za ukoloni.

Wasomi wetu hawa ndo wa kwanza kwenda mahakamani kutetea mikataba ya kifisadi nchini. Hivi kuwa mwanasheria mahiri ni kutetea hata kitu ambacho hakina uhalali? Mimi nafikiri mwanasheria mzuri ni yule anayehakikisha haki inapatikana. Kama mtu kaiba kweli na kama haki yake ni kwenda jela, basi mwanasheria ahakikishe mtu huyo anaenda jela na sio kumsaidia asiende jela kwa kupindisha ukweli. Wakili wa mtu sio kumwepusha mtu adhabu kwa kuficha au kupindisha ukweli bali ni kumtetea mteja asikandamizwe na vifungu vya sheria ambavyo sio halali na kumsaidia apate adhabu sahihi. Na mahakimu wanatoa hukumu zisizo za haki wakijua kabisa wanaumiza nchi. Ndo wasomi wetu tunaowategemea kuleta maendeleo.

Wasomi wetu hawa ndo wanaotunga, kupitisha na kusaini sheria za kuifilisi nchi. Mfano sheria ya manunuzi. Sheria ya manunuzi inahitaji wazabuni ndo wanunue bidhaa kwa ajili ya serikali. Wazabuni hawa wanauzia bidhaa serikali kwa bei mara tatu zaidi ya bei iliyoko sokoni. Serikali yetu inalipa tu licha ya kujua ukweli kuwa bei iliyotolewa ni ya kugushi. Wanapitisha malipo kwa kuwa tayari wameishapewa kitu. Hata kama makampuni ya uzabuni ni ya viongozi WETU kuna shida gani kutoa bei ya kweli? Tatizo kubwa la wafanya biashara ni kupata soko. Sasa umeishapata soko, kwa nini usiuze kwa bei ya haki?

Wasomi wetu hao ndo wa kwanza kulilia maendeleo duni kwa nchi yetu wakati wao wakipata nafasi ndo wanachangia uduni huo. Hawafanyi kazi kwa uaminifu. Wasomi hawa wanakuwa kazini kwa ajili ya kupata utajiri usio wa haki. Hawaoni kwamba kuwa tajiri katika kundi la masikini ni hatari. Unakuwa tajiri katika kundi la watu walio na njaa. Utaendeleza utajiri wako kwa amani? Unakuwa na gari lako la kifahari lakini hakuna barabara nzuri ya kupita kutokana na ufisadi wako. Utajiri wako unaufurahiaje?

Wasomi hawa ndo wa kwanza kutoa kauli kuwa nchi bila wasomi haiwezi kuendelea na wakati huo wao ndo wanahujumu elimu nchini kwa kutotatua matatizo ya elimu yanayoikumba nchi yetu. Elimu ya Tanzania inazidi kushuka kila kukicha. Wasomi waliosomeshwa kwa pesa ya watanzania wote hawataki tena kujishughulisha na matatizo ya elimu nchini. Kutatua matatizo kwao ni kukaa vikao lukuki na kulipana posho kibao. Mwisho wa yote hakuna kinachofanyika. Hawa ndo wasomi tunaowategemea watuletee maendeleo.

Wasomi hawa ndo wa kwanza kukimbilia nje kwa matatibabu wanapougua. Sijui wanadhani hao wataalamu wa afya walioko nje wameshuka kutoka mbinguni! Hao wataalamu wamesomeshwa vizuri na serikali zao. Hospitali nzuri wanazoenda zimejengwa na wananchi wao kupitia kodi zao. Serikali zao zimewekeza vya kutosha kwenye elimu ambayo wasomi wetu wanaikandamiza.

Wasomi hawa ndo wanatoa lawama kali kwa wakoloni waliotutawala kwamba walikuja kutunyonya. Wakoloni waliotutawala ndo wanaotuonea huruma na kurudisha fedha zilizoibiwa nchini na wenzetu kutokana na mikataba ya kifisadi ya rada. Ni nani mkoloni mzuri basi? Anayekuambi kuwa umeibiwa na kukurudishia ulichoibiwa au anayejifanya mzalendo na kukuibia hicho kidogo ulicho nacho na kwenda kukificha ughaibuni? Ebu watanzania tutoe hukumu ya haki kati ya pande hizo mbili. Akili za wasomi hawa zinasikitisha sana.

Wasomi hawa ndo wanaolaumu na kudharau sana mababu zetu walioingia mikataba ya ulaghai na wakoloni akina Karl Peters. Kwamba walidanganywa kwa kuwa hawakuwa na elimu. Sasa leo wao wana elimu lakini wanaingia mikataba bomu kuliko ya enzi hizo. Bora hata wao waliingia mikataba hiyo wakiwa hawajui hata kusoma. Mikataba waliyoingia wao ni bora mara mia kuliko hii inayosainiwa sasa.

Tanzania ni nchi nzuri iliyo na raslimali za kumwaga. Kila mtu sasa hivi anajua ukweli huu. Lakini nchi yetu imebaki katika umaskini wa kutisha. Viongozi wa nchi hii ambao ni wasomi waliopewa madaraka ya kutumikia wananchi wamegeuka wanyonyaji na maharamia wakubwa wa uchumi katika nchi yao. Ni viongozi ambao hawana shida za maisha. Kiu yao kubwa ni utajiri wa kukufuru, tena wa wizi. Hata wasomi wasio kuwa viongozi wamekuwa hali moja. Wanafanya mashindano ya kutafuta utajiri wa haraka.

Kwa ujumla nashindwa kuona faida ya kuwa na wasomi wengi nchini. Enzi za uhuru wakati wasomi walikuwa wachache nchi haikuwa na matatizo ya ukosefu wa maadili ya kazi kama yaliyoko sasa baada ya kuwa na wasomi wa kumwaga. Je wasomi wa sasa hivi wamekuwa ni wasaliti wa nchi yetu? Wasomi wasio wanasiasa ni kawaida kuwashutumu na kuwanyooshea vidole wasomi wenzao ambao ni wanasaidia. Lakini nao kwa nafasi zao wanafanya hayo hayo ya wizi. Kwa nini wameamua kuiga tabia hiyo ovu? Wao watajitenga vipi na uozo huo? Wanachokilalamikia ni nini basi kama hata wao hawawezi kuridhika na vipato vyao halali? Nchi yetu inaenda wapi? Rais wetu ambaye ni kiongozi wa kwanza mwenye dhamana ya kuongoza nchi hii anawaza nini? Anafurahia hali hii? Haoni kuwa yeye ndo anachangaia matatizo haya? Yeye akiwa kwenye mstari bila kuweka upendeleo naamini kila mtu atageuka na kufuata mstari. Lakini kwa kuwa yeye anawachekea wezi basi wizi utaendelea tu. Hao wezi wanamwona hana nguvu za kuwafanya lolote. Ni kama nchi haina rais.

MUNGU ISAIDIE TANZANIA.


Ruberts Witta

mrtrusted@hotmail.com
 
ccm haitumii wasomi ktk kazi zake kuhofia kujulikana kwa wizi wao, ccm inaishi kwa kutumia Ujinga wetu, wasomi huwezi kuwalaumu hawatumiwi na Magamba,
 
Wewe BOB G unataka utaingizaje UCCM kwenye hoja kama hii ambayo ipo wazi, iliposemwa Uanasiasa au Uongozi wa juu serikalini hauangaliii maslahi ya taifa, hii ina maana chama chochote hata cha cha upinzani ni wanasiasa na kinaweza kushika hatamu ya uongozi nchi hii. Na kama hakutawekwa sheria kali/misingi dhabiti ya utumishi wa umma hali itakuwa ileile.

ZILONGWA MBALI, ZITENDWA MBALI.
 
Wanabodi,

Tanzania is one of the poorest countries in the world, with a per capita income estimated a at about $250 per year.

Kila siku tumekuwa watu tukijiliwaza na kujifariji humu JF kuwa Tanzania tuna wasomi wengi wenye huwezo na maarifa ya kutosha mchango wao ni upi kwenye ujenzi wa taifa letu. Tukiangalia historia ya taifa letu toka wakati wa Mwl. Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete wasomi wetu wengi wanaounda serikali wametoka University of Dar es Salaam.

Tumeona hawa wasomi wetu ndio wamelifikisha taifa letu hapa tulipo wamebinafsisha mabenki makampuni ya umma, wamegawana nyumba za serikali, wameuza migodi yetu kwa wazungu. Mikataba yote mibovu ya taifa letu imefanywa na hawa wasomi wetu.

Ni kipi cha kujivunia sisi watanzania kutoka kwa wasomi wetu...CC to Mkandara, chama, Nguruvi3, Ngongo, zomba,
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom