Wasomi wa Tanzania wametoa mchango gani kwenye Taifa letu mpaka sasa?

ritz msindikize dadii kula shangwe amemaliza kutupiga fix alafu huyooooo! Hahahahahaha!
 
Wasomi hawapewi nafasi, zaidi ya kupigwa mabomu. Kwani we hujashuhudia mabomu vyuo kikuu???

Hahaha, achana na hiyo.....
wasomi wetu, wanaitwa "wataalaam" a.k.a madaktari hukuona waligoma ili wapatiwe haki zao.

Tanzania ndo nchi pekee duniani haijali wataalamu wake. Hivi wewe umeshasikia tuzo za ubunifu kwenye nyanja za elimu au za wataalamu?? Umeshasikia watu wanapatiwa tuzo kwa tafiti flani za ki-elimu??

Zaidi tunasikia tuzo za kisiasa tu. JK anawaita kina Pinda, Tambwe hiza kuwapa tuzo za siasa bora ikulu..haha
 
wasomi kazi yao iliyobakia ni kulalamika tuuu. Sasa nyie ambao taifa linawategemea mnalia, je wasoenda shule? Arrgh. Wasomi wanaboa sana. Hawawezi kitu, walamba viatu na wabeba makoti wa wanasiasa, hamna kitu.
 
Wasomi hawapewi nafasi, zaidi ya kupigwa mabomu. Kwani we hujashuhudia mabomu vyuo kikuu???
Nafasi akupe nani? wasomi wanahitajika, wapigane! haki haiombwi inapiganiwa. Sema wasomi kwa sabau kwa kiasi furani wanashiba, hawapo tayari kuwapigania wengine, wachoyo.,waoga, wanafiki,we si ulimsikia VC wa UDSM alivyokuwa anasifia mswaada wa katiba mpya hao ndo wasomi wetu.
 
tupo hapa jf tunasuppy maujanja ili wadanganyika kama kina ritz waweze kuijua kweli!

Haitoshi kuwapa maujanja, tunawahitaji frontline kwenye mapambano! nani kakuambie uwatwishe wengine mzigo ambao wewe huwezi kuugusa hata kwa kidole? ule wenu mungu kasema, mnaowatwisha wengine mizigo mizito amabo nyinyi wenyewe hamwezi kuigusa hata kwa kidole.
 
Wasomi wa nchi nyingine wanafanya yepi ili kuonyesha kuwa wanashughulika? Mi sidhani kama ni sawa na wao wajihusishe na siasa. Kazi ya wasomi ni kuchambua hali halisi kisomi na kisha kuishauri serikali na viongozi wengine wa kisiasa juu ya nini kifanyike na sidhani kama hilo halifanyiki. Kazi ya msomi ni kushauri kisomi lakini ni uamuzi wa serikali na viongozi wa siasa kuuchukua ushauri huo au kuacha.
 
wasomi wa nini wakati serikali yenyewe haiambiliki.ndio maana wengi wao wanaacha taaluma zao na kukumbilia siasa.
 
Majira ya saa moja jioni ya leo, nilikuwa na rafiki yangu maeneo ya Mlimani City, Dar er Salaam tukijadili masuala ya kimaisha na kisiasa sawia. Katikati ya mazungumzo yetu, rafiki yangu huyo aliibua hoja ambayo ilituingiza katika tafakuri nzito. Alinieleza kuwa jirani tu na eneo tulilokuwepo kulikuwa na pilika pilika na hamasa zisizo kifani za watu wakijiandaa kuingia Mlimani City Conference Hall kushuhudia utoaji tuzo za Kilimanjaro Music.

Akikubaliana na kauli iliyopata kutolewa na Ernesto Che Guavara, mara baada kutoka kusaidia harakati za ukombozi nchini Congo, kuwa Waafrika kwa hulka zao, wanapenda sana starehe,waoga na wasio tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya kujikomboa wao wenyewe, rafiki yangu huyo,alitanabaisha kuwa tabia na matendo ya wanasiasa wetu,kama zao la jamii yetu, yanaweza kuthibitisha dai hili:

Wakati Mhadhiri mwandamizi wa UDSM, Prof. Chachage S. Chachage, anafariki dunia, wakati huo yeye akiwa mwaka wa mwisho Mlimani, hakuona viongozi wa ngazi za juu wa kisiasa na kiserikali wakati wa kuaga mwili wa marehemu Chachage katika ukumbi wa Nkurumah. Aidha, kila mwaka UDSM hufanya kongamano la kumkumbuka Chachage, lakini viongozi wetu wa kisiasa na kiserikali,kama kawaida yao, hawahudhurii kabisa.

Nikakumbuka matukio kadhaa ya miaka ya karibuni:
Prof. Haroub Othumani aliaga dunia, wanasiasa na viongozi wachache wa serikali walihudhuria mazishi. Hali ilikuwa hivyo pia siku chache baada ya kifo chake, Jumuiya ya Wanataaluma wa UDSM, UDASA ilipoandaa mhadhara wa kumbukumbu ya marehemu.

Mwaka mmoja, baada ya kifo chake, UDASA waliandaa tena mhadhara wa wazi kumkumbuka marehemu na kama ilivyo ada yao, wanasisa na viongozi wetu wa serikali hawakujitokeza.

Mwaka 2010, Prof. Jwani Mwakyusa wa UDSM alifariki dunia, na mwili wake uliagwa katika ukumbi wa Nkurumah. Mbali na Dkt. Harison Mwakyembe na Prof. Mark Mwandosya na wanasheria wengine waandamizi, viongozi wetu wengine wa kitaifa, kwa mara nyingine tena, hawakuonekana. Hali ilikuwa hivyo pia katika misiba ya Prof. Christant Kamuzora, Prof. Sam Mushi, Dkt. Ndibalema Alphonce na wengine wengi.

Hivi karibuni, taifa limempoteza ndugu yetu mpendwa, Steven Kanumba ,ambaye kwa kweli ana mchango mkubwa katika kukuza sanaa yetu kimataifa. Sote tumeshuhudia jinsi viongozi wetu wa kisiasa na kiserikali walivyojitokeza kwa wingi kabisa na kikamilifu kabisa nyumbani kwa Marehemu, katika kumuaga na hatimaye katika mazishi yake.Sitaki nieleweke kuwa ninapinga viongozi wetu kuhudhuria mazishi ya wasanii wetu.

Hoja yangu ni kuwa kwanini sasa inaonekana ni kawaida, wanasiasa na viongozi wetu na Watanzania kwa ujumla wetu tunakuwa wazito kuhudhuria katika misiba ya Wanataaluma wetu ambao wamepata kutoa mchango mkubwa katika maeneo yao ya kitaaluma ikiwemo kuandaa wataalamu mbalimbali na michango yao katika kuleta maarifa mapya kupitia tafiti, machapisho na vitabu vyao?
Kwanini tunaenenda hivi? Na kwanini tusibadilike?

Karibu tujadili.
 
Yaani umeongea point sana, ila hawa viongozi wengi wanaongoza kisanii sana ndio maana wanajiona ni sehemu ya hao wasanii na wala sio wanataaluma
 
Viongozi wetu wanapenda sana umaarufu na hiyo quite honestly inatokana na ulimbukeni. Ndiyo maana hata Raisi wetu safari za nje anazithamini kuliko maendeleo ya waTanzania, au mazishi ya aliyekuwa IGP wetu anayakacha.

We kama rais mzima anakuja Marekani na anaona ni jambo la maana sana kupiga simu na watu kama 50 Cents, unategemea wale walioko chini yake watakuwaje? Umuhimu wa wasomi wetu kwa taifa letu hauthaminiwi na viongozi wetu na ndiyo maana elimu inazidi kushuka kila siku.

Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya jinsi tunavyo-view wasomi wetu (hasa professors, waalimu, wataalamu, madaktari, etc) na level ya elimu yetu hapa Tanzania na kwa bahati mbaya viongozi wa kitaifa hawaoni hili.

Funding ya elimu haitakuwepo mpaka hili libadilike. In other words tutaendelea kuchangia hela ya madawati na quite soon, wazazi watatakiwa watume watoto wao shule na mchango wa majengo kama madarasa. I think it is already happening.
 
FortJeasus

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kwenye issue ya Chachage jamaa anakudanganya. Mwaka 2005 nilikuwepo kutoa heshima za Mwisho pale Nkrumah Hall na nadhibitisha kwamba JK alihudhuria.

Tena nakumbuka siku hiyo alikuwa ametoka safarini kati ya Angola au Namibia aliomba sana akiwa huko kuwa wasisafirishe mwili wa marehemu kwenda Njombe kabla hajaaga. Kweli alivyotua JKNIA msafara wake ulikuja moja kwa moja mpaka UDSM na alivyotoa salamu zake za mwisho safari ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Njombe ilianza.

Sijui kwa mengine uliyotaja ila kwa issue ya Chachage I was there, mpeni haki yake pale panapo staili
 
Last edited by a moderator:
unadhani kukaa na kubuni kuandika pepa za kuomba funds kwa wazungu inatosha? Kanumba alipokufa kuna watu kama 20 na zaidi ajira zao zimeyeyuka. Msomi kaaajiriwa na anatengeneza tu liability kwa taifa kutikana na uchakachuaji anaoufanya kila mara... Fikiria pande zote
 
unadhani kukaa na kubuni kuandika pepa za kuomba funds kwa wazungu inatosha? Kanumba alipokufa kuna watu kama 20 na zaidi ajira zao zimeyeyuka. Msomi kaaajiriwa na anatengeneza tu liability kwa taifa kutikana na uchakachuaji anaoufanya kila mara... Fikiria pande zote

Hapo ndio umeonesha matatizo yetu sie watanzania, nchi hii haiwezi kutoka kwnenye umasikini kwa sababu ya mawazo kama yako best.....fikiri hizo paper unazoongelea matokeo yake yangekua yanafanyiwa kazi na wananchi pamoja na serikali kwa michango yetu wenyewe bila kutegemea fund toka nje zingetenzeneza ajira zaidi ya hizo 20 unazosema tena mara 7*70.
 
Usiseme wanasiasa wetu... Sema CCM wanathamini sana wasanii kuliko wasomi.

Jibu; kwasababu CCM wenyewe ni wasanii.
Katika wanachama 100 wa CCM, wawili ndo intelectual. Waliobakia wote ni kaole. Kuanzia mwenyikiti wao mpaka kina Lusinde
 
1) Wanasiasa wetu ni wasanii halisi hivyo wanathibitsha usahihi wa mithali ya "ndege wa aina moja huruka pamoja".
2) Wasomi wengi wa Tz ni tishio kwa hao vilaza (wanasiasa) ila kwa vile hawajijui na kwa sababu ya njaa hujiuza kwa bei ndogo sana....kwa hivyo wanaishia kusababisha tasnia iliyotukuka ya usomi kudharauliwa.
3) Pia inaonesha moral balance. Kama Kanumba "alikuza" na "kutengeneza ajira kwa vijana" kwa njia ya sanaa yake bila kujali madhara/faida za hicho alichokuwa anafanya kwa jamii.
4) Tanzania kinachohitajika ni technical "know-who" na sio technical "know-how". So you see wasanii wanajuana na ndicho kinacho -matter hapa.
5) .........ongezea
 
Jagermaster

Hata kama JK alienda, mwaka 2006, Nkurumah kumuaga Chachage,hoja inayojengwa ni hulka za wanasiasa kama zinavyojionyesha katika mwitikio wao katika matukio ya kijamii.

Kwamba viongozi wetu wa kisiasa hawana hulka ya kushiriki misiba ya wanataaluma na hata wakifanya hivyo, huwa si katika viwango vya kuridhisha, kama ilivyojidhihirisha katika msiba wa Chachage.

UDSM wana kawaida ya kufanya tafakari ya maisha ya Ernesto Che Guavara takribani kila mwaka, kwa nini watawala wetu hawatokei?

Kama ni kweli wanaguswa na vifo vya wasanii na wanahudhuria misiba yao ipasavyo, kwanini basi inakosekana hiyo consistency inapokuja misiba na kumbukumbu za wanataaluma?

Tabia halisi za watawala wetu ni zipi? Tayari majawabu yameanza kupatikana kutoka kwa wachangiaji wengine.
 
Last edited by a moderator:
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom