Wasomi na kiingereza

Wasomi na kiingereza

Tatizo ni waalimu mkuu. Maana waalimu ktk ufundishaji wao hawawezi kwenda mbali zaidi maana nao hawana msingi mzuri wa lugha na wanachofanya ni kufundisha kanuni zilizopo ktk vitabu tu na si kwenda mbali zaidi nje ya kanuni na mafanunuzi kutoka ktk vitabu.
Kama vp hebu toa mifano kile ambacho hao waalimu walitakiwa kufanya.
 
huu ni uongo mbona wachina hawajui kiingereza lakini wana uwezo
kwani china wanasoma kwa kiingereza? China elimu yao yote wanasoma kwa kichina hiki kiingereza ni cha kujifunza tu ukubwani. Sisi huku tunajifunza kiingereza toka shule ya msingi hadi chuo kikuu lakini bado kuandika na kuongea inakuwa shughuli lakini mchina anaweza kujifunza kiingereza ukubwani na akajua kuongea na kuandika vizuri tu.
 
Hao sidhani kama wanasoma kwa kutumia English.
That's why hawawezi kumudu English hivyo hakuna cha ajabu.

Cha ajabu ni yule anayesoma kwa kutumia English for 6 or 10 years lakini anatoka mweupe.

Hapo lazima kuwe na tatizo linalohitaji solution na sio kutafuta justifications ili kujipa faraja.

Na hakuna tatizo kujua lugha zaidi ya moja maybe kama una plan za kuishi Tanzania milele.
Ila hata hizo nchi ambazo hawatumii kiingereza kwenye masomo bado wana somo la english na nia waweze kujua kiingereza,sasa kama hawaelewi utasemaje si ajabu? maana kuna watu kiingereza wamejifunzia kwenye hizi english course na sasa wanakiongea.
 
kwani china wanasoma kwa kiingereza? China elimu yao yote wanasoma kwa kichina hiki kiingereza ni cha kujifunza tu ukubwani. Sisi huku tunajifunza kiingereza toka shule ya msingi hadi chuo kikuu lakini bado kuandika na kuongea inakuwa shughuli lakini mchina anaweza kujifunza kiingereza ukubwani na akajua kuongea na kuandika vizuri tu.
Unataka kusema huko China hakuna somo la english mashuleni?
 
Walikuwa hawana hilo somo labda kama wameanzisha miaka ya karibuni. Lakini hata hivyo kuna tofauti kubwa sana ya kusoma masomo kwa kiingereza na kusoma kiingereza kama somo. Kwa anyesoma masomo yote kwa kiingereza including somo la kiingereza lenyewe anakuwa more fluent kama atapata walimu wazuri kuliko anayesoma kwa lugha yao halafu akasoma kiingereza kama foreign language. Hapa kwetu TZ hapo ndipo shida ilipoanzia unasoma kuanzia darasa la kwanza hadi la saba masomo yote kwa kiswahili na kiingereza kama somo halfu unakuja kuwa introduced kwenye english kama lugha ya kujifunzia kuanzia form one up to university level. Na bahati mbaya walimu wenyewe wanaotufundisha english wao wenyewe wanahitaji kufundishwa english. What do you expect?

Msingi wa kumudu lugha yoyote ile unaanza katika umri mdogo wakati kichwa akijawa na matakataka mengi. Kujifunza lugha ukubwani ni kazi sana na inabidi ume committed kwelikweli ili uwe fluent au uishi kwenye jamii wanayoongea hiyo lugha muda wote vinginevyo broken haikwepeki hata kama si kwa sana.
 
Na siku hizi wameanza kusoma biblia za kiingereza... Hakika utumwa tulionao bado tuna safari ndefu sana ya kujikomboa
Kuna kitu una kosa mkuu. Nafikiri ungefanya utafiti wa lugha kwanza nazani usingeweza kusema hivi mkuu.... Biblia ya kiingereza ni tamu sn kuliko na inaeleweka zaidi kuliko ya kiswahili
 
Unafikiri kwa nini nchi kama Kenya, uganda, Zambia wapo fluent? Kwamba wao wana akili za kujua sana kiingereza kuliko sisi? No, ni kwamba wao tangu shule za awali (elementary school) wanasoma kwa kiingereza. Hivyo wanaizoea lugha at an early age.
 
Nitakujibu kitaaluma na si kishabiki.

Lugha huwasilishwa na namna mbili written na spoken. Mara nyingi mashuleni tunatumia written na si spoken.

Sasa basi spoken language inahitaji practice ya kutosha kuanzia matamshi n.k lakini pia unapozungumza huna muda wa kufikiri ndo maana mara nyingi tunashindwa.

Sasa huyo Ph. D holder huenda alitumia zaidi written na si spoken
Sema alitumia njia ya kukalili ndio njia inayotumika mashule maana hiyo unayosema Written inahitaji uwe na uelewa mkubwa ambao ni Sawa na spoken.... Hakuna tofauti ktk written na spoken. Kwafano unakuta swali la kujieleza na kutolea mafafanuzi na si la kuchagua. Yaani swali linakutaka utoe maelezo. Hapo kwa kanuni yako ya written ktk maana yako uliyokusudia lazima ufeli. Ndio maana wengi wanafanya vzr ktk maswali ya kuchagua kwasbbu wanasoma kwa kukalili na si kuelewa kitu kwa mapana ma ndio sbbu ktk maswali ya kutoa maelezo wanachemka....
 
Unafikiri kwa nini nchi kama Kenya, uganda, Zambia wapo fluent? Kwamba wao wana akili za kujua sana kiingereza kuliko sisi? No, ni kwamba wao tangu shule za awali (elementary school) wanasoma kwa kiingereza. Hivyo wanaizoea lugha at an early age.
Labda useme Kenya lkn sio Uganda. Uganda hawajui kiingereza kabisa bora ata ya watz....
 
kwani china wanasoma kwa kiingereza? China elimu yao yote wanasoma kwa kichina hiki kiingereza ni cha kujifunza tu ukubwani. Sisi huku tunajifunza kiingereza toka shule ya msingi hadi chuo kikuu lakini bado kuandika na kuongea inakuwa shughuli lakini mchina anaweza kujifunza kiingereza ukubwani na akajua kuongea na kuandika vizuri tu.
Ata hivo China wameshindwa kutawala dunia au kua na usemi mkuu ktk dunia kwasbbu wameshindwa kupenyeza lugha yao ktk dunia. Kwahiyo wameshindwa kupenyeza tamaduni zao duniani. Maana lugha ni tamaduni ya jamii Fulani
 
Sema alitumia njia ya kukalili ndio njia inayotumika mashule maana hiyo unayosema Written inahitaji uwe na uelewa mkubwa ambao ni Sawa na spoken.... Hakuna tofauti ktk written na spoken. Kwafano unakuta swali la kujieleza na kutolea mafafanuzi na si la kuchagua. Yaani swali linakutaka utoe maelezo. Hapo kwa kanuni yako ya written ktk maana yako uliyokusudia lazima ufeli. Ndio maana wengi wanafanya vzr ktk maswali ya kuchagua kwasbbu wanasoma kwa kukalili na si kuelewa kitu kwa mapana ma ndio sbbu ktk maswali ya kutoa maelezo wanachemka....
Hujaelewa nilichoandika labda.

Kiingereza unapoongea na unavyoandika ni tofauti, unapokuwa unaandika unaweza pata muda wa kufiliria neno sahihi la kuweka katika andiko lako.

Lakin uongeapo huna muda wa kufikiri, na kwakuwa lugha ni ngeni basi inakuwa shida.

Mkuu kiingereza kukielewa na kuzungumza ni vitu vilwili tofauti,

Unaposema kukariri, mkuu huwezi kukariri essays hata siku moja, labda definitions kadhaa.
 
Unafikiri kwa nini nchi kama Kenya, uganda, Zambia wapo fluent? Kwamba wao wana akili za kujua sana kiingereza kuliko sisi? No, ni kwamba wao tangu shule za awali (elementary school) wanasoma kwa kiingereza. Hivyo wanaizoea lugha at an early age.
Hapa umemaliza mkuu
 
Hujaelewa nilichoandika labda.

Kiingereza unapoongea na unavyoandika ni tofauti, unapokuwa unaandika unaweza pata muda wa kufiliria neno sahihi la kuweka katika andiko lako.

Lakin uongeapo huna muda wa kufikiri, na kwakuwa lugha ni ngeni basi inakuwa shida.

Mkuu kiingereza kukielewa na kuzungumza ni vitu vilwili tofauti,

Unaposema kukariri, mkuu huwezi kukariri essays hata siku moja, labda definitions kadhaa.
Unapoongea na kuandika lazima ufikirie mkuu. Na kusema la ukweli elimu zetu sisi ni za kukalili tu na si za kuelewa kitu kimapana zaidi.
 
Ukiongea lugha ambayo umeizoea let's say kiswahili huna haja ya kuwaza maneno ya kuchomeka ili mazungumzo yaendelee.

Lakin kama lugha ni ngeni narudia lazima uwaze msamiati wa kupachika kama huna au uko mbali (umeusahau).

Sasa basi huo muda huwa unakuwa mwingi kwenye kuandika ila kuongea muda unakuwa mchache ndo maana wengi hushindwa.

Kiingereza cha kuongea ni zaidi ya darasani, nchi zote wanazozungumza vizuri kiingereza wamezaliwa wanongea kiingereza si cha kujifunzia ukubwani kama sisi.
 
Inakuwaje msomi ama graduate wa chuo kikuu aliespend miaka kama minne chuo kikuu na ana degree, masomo yake yote ni kiingereza tupu anafanikiwa kugraduate, lakini ukimwongelesha kiingereza haelewi

Akiamua yeye sasa Hata kuandika ujumbe kwa kiingereza anashusha broken ya hatari hadI unashangaa? Wengine wamefanikiwa kupata kazi kabisa unakuta bonge la engineer from ardhi university English mbovu mkichat yuko kwenye bonge la kampuni

Mbaya zaidi graduate kamaliza chuo few days anaambiwa andika barua ya kuomba internship anaweweseka..Mara nipe google..maelezo yake binafsi yanamshinda kujieleza kwa kiingereza anatafuta CV za wengine akopi.sasa najiuliza huyu mtu kafanikiwa kumaliza successful report zake aliandikaje?kama kiingereza cha kuandika anababaika presentation alihudhuriaje akapata marks
Research zake?

Au ndo wale wa kukariri? Sawa basi hata kama kukariri unashindwa kujifunzia hapo mpangilio wa grammar.

Boss mzima ananitext "is you coming or no"
Kiingereza nacho ni kipaji?
Kwa bongo ni kawaida,mfumo wetu wa elimu haufundishi kiingereza vzr,ukimtoa Mkapa,nitajie kiongozi gani anaweza kuongea kizungu kilichonyooka,Hata Mkapa Elimu ya juu,kasoma Makerere university Uganda,
Ukienda Zanzibar,Kuna beach boys,wanaongea kizungu,kiitaliano,kirusi,kilichonyooka,na Hawa vijana unakuta hata Darasa la Saba hawakusoma,
Ila tusiwaponde sana wahandisi wetu,maana hata wachina wanaotujengea flyover hawajuhi kizungu,
Muhandisi akishindwa,kufanya kazi yake ya ujenzi aliyosomea,asemwe,ila siyo kushindwa kuongea kizungu.
 
Inakuwaje msomi ama graduate wa chuo kikuu aliespend miaka kama minne chuo kikuu na ana degree, masomo yake yote ni kiingereza tupu anafanikiwa kugraduate, lakini ukimwongelesha kiingereza haelewi

Akiamua yeye sasa Hata kuandika ujumbe kwa kiingereza anashusha broken ya hatari hadI unashangaa? Wengine wamefanikiwa kupata kazi kabisa unakuta bonge la engineer from ardhi university English mbovu mkichat yuko kwenye bonge la kampuni

Mbaya zaidi graduate kamaliza chuo few days anaambiwa andika barua ya kuomba internship anaweweseka..Mara nipe google..maelezo yake binafsi yanamshinda kujieleza kwa kiingereza anatafuta CV za wengine akopi.sasa najiuliza huyu mtu kafanikiwa kumaliza successful report zake aliandikaje?kama kiingereza cha kuandika anababaika presentation alihudhuriaje akapata marks
Research zake?

Au ndo wale wa kukariri? Sawa basi hata kama kukariri unashindwa kujifunzia hapo mpangilio wa grammar.

Boss mzima ananitext "is you coming or no"
Kiingereza nacho ni kipaji?
Kama imekukela kufa 🤣 mwache boss ajimwage
 
Back
Top Bottom