Wananchi wanaweza kuona ofisi yao kama Wananchi wa Marekani wanaonyeshwa Ikulu yao kupitia website ya white house wanawaonyesha wananchi wao hata maua yaliopo ndani ya Ikulu.Watanzania wapatao Millioni Alobaini na Ushee wapate walau kujua Nyumba yao kuu uzuri wake na wanalo la kusema litakalo saidia kujua na kuchangia maendeleo ya ofisi hiyo ambayo pia ni makazi ya Rais wa Taifa letu.Bofya hapa uone ya Website White house ya Marekani.
Tena itakuwa na taarifa kadha wa kadha zikiwemo picha na hotuba za Marais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na wake zao waliopita ndani ya Mjengo huo.Dunia inabadilika hata kuonyesha machache kwa jamii ni moja ya mwamko wa kitekinolojia.Na itawapatia watoto wa shule na vyuo kupata taarifa na kupata jukwaa la kupata taarifa za masomo yao.Vile vle itatumika kujibu na kutoa picha maalumu za kutumika kwenye kutoa habari.
Kuwa na Website ya Kivukoni ni muhimu na wala halina mjadala, lakujiuliza Watanzania tuko committed (tayari) na mambo hayo kwani tunayo Website ya Taifa lakini inatushinda kuiupdate kila siku unachoona ni abuse - habari zisizoendana na wakati.