Hivi akina Invisible, Pasco, Halisi na wengineo. Mkienda kwenye hizi press briefings za hawa wawili kwa nini hamuwaulizi kuhusu website ya ikulu ambayo iko under construction kwa takriban miaka 6 sasa.
Surely kuuliza si vibaya and its really embarrassing kama taifa na sasa naona its about time hili suala nikalivalia njuga upya kama nyie hamtaki.
These guys promised us transparency na pesa za kutengenza hiyo website zilishatolewa sasa cha kujiuliza pesa zimefanya kazi gani na nani kazila?
SlidingRoof, kwa asante kwa kuliuliza hili.
1. Kwanza ni kweli mimi ni mwandishi ila ni wa kujitegemea, freelancer, sijaajiriwa na chombo chochote na wala sijajiatach na media yoyote, hivyo ni miongoni mwa wale waandishi ambao kamwe hatuwezi kualikwa Ikulu. Huko wanaalikwa waandishi waandamizi kwenye media.
2. Kwa vile wote wawili nawafahamu na pia uwezo wao naufahamu, nadhani pale Ikulu kuna matatizo, maana performance yao hapo walipo ukilinganisha na kabla hawafika hapo, was much much better, hivyo kwa vile wote ni watu wenye uwezo, kama wanashindwa kuperform au kudeliver, then penye matatizo ni Ikulu.
3. Naomba binafsi nimpongeze Premmy, mara ya mwisho tumekutana pale hotel ya Al-Awadarby Mkuu alipokuja kwenye Mkutano wa CTO. Jukumu langu pale lilikuwa ni kuandaa special program itoke siku hiyo hiyo. Mkuu akahutubia kwa Lugha ya Kiingereza, alipomaliza akatoka nje kutembelea maonyesho na kujichanganya na watu. Nikawasiliana na Premmy kuwa ninafanya program ya Kiswahili, naomba kupata insert ya Kiswahili. Premmy akanipa changamoto, 'you have to fight and get it', hapo hapo nikatafuta security clearence almanusura nifanikiwe, ndipo wale 'jamaa' wakanisukumia kule, as if ile mic yangu ni mtutu!. Jamaa akaniambia Mkuu hana muda kabisa, he is rushing to his nest appointment. Hivyo at leat Premmy aliniruhusu, wale jamaa, wakanizibia!.
4. Kweli nami nikajikalia pembeni wakapiga group photo nikitegemea akimaliza ni mbio kwenye gari kuiwahi hiyo next appointment.. ala kumbe!,
Kilichofuatia hapo naomba nikiache private ila Mkuu aliondoka hapo baada ya 20 minutes!. Wakati wote huo nimewasha kamera ili angalau
aseme japo neno moja la Kiswahili, wakati akielekea kwenye gari, nililazimisha kuuliza swali ...alichonijibu rais wangu, naomba nikihifadhi
kama heshima ya mkuu wangu wa inchi ... huyo akaishia zake kwenye gari!.
5. Nikawaambia waandalizi, this is very unfair, mkutano uko kwetu, walengwa ni Watanzania, ukiamua kuhutubia kwa Kiingereza, its fine, ule ni international conference lakini ukimaliza, basi malizia japo kwa neno moja la kiswahili!.
6. Sikuificha embarassment yangu kwenye makala yangu, nilipiga nyundo kuwa Wakoloni Waingereza, wametufanya vibaya sana kwa kutokolonize mpaka kwenye mind hata kwenye nchi huru Tanzania, viongozi wetu bado wanajikomba kwa wakoloni mamboleo hawa kwa kuzungumza lugha yao hata mahali pasipopaswa.
7. Kama nilivyosema mwanzo, Ikulu pana matatizo, ila matatizo mengine, yanachangiwa na wasaidizi wa rais kwa kumuover protect wakiamini ndio wanamsaidia, kumbe ndio wanamuangusha, na wengine ama wamezidi kujikomba komba mno kwa rais, hadi kumwambia ukweli wanaogopo kwa kujua huku ndiko kumsaidia, kumbe ndio kwanza wanazidi kumuangusha!.
8. Kwa vile Ikulu ni mahali patakatifu na kila kitu mule ni siri, website ya nini?. Zile release za 'Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu' zinatosheleza kabiisa!.