Husninyo
Platinum Member
- Oct 24, 2010
- 24,286
- 10,572
Kumetokea nini humu JF siku hizi? hii ni ile ile JF ninayoijua ama nimepotea njia? yaani kila nikichungulia mada ni hizi hizi, zile mada zetu zileee za wakati uleee za kuelimishana/kufundishana zimeishilia wapi? nini kimetokea? kwamba hakuna maisha zaidi ya kuoa na kuolewa, sijui 30+ na ujinga mwingine mwingi? hakuna maisha zaidi ya hayo?na hawa wanaume wanaoanzisha hizi mada huko kwenye koo zao dada zao wote wameolewa? kumetokea nini mpaka mnafatana matakoni kwa mambo ya kijinga kiasi hiki? kwamba mtu anataka mwenzie aishi jinsi anavyotaka yeye? kwamba hajaolewa basi amekuwa na kilema ama vipi? kwanini mnapangiana maisha? kwanini mtake mtu mwingine aishe utakavyo wewe? umeoa poa, hajaolewa ni maisha yake hayakuhusu, kwamba wewe ulieoa/olewa ndio una amani zaidi kuliko wengine? baadhi ya watu humu wana fikira za kiupuuzi sana, tena upuuzi uliopitiliza, kila mtu anaishi atakavyo jamani!
yaani siku hizi jf inatia hadi uvivu kuingia. upuuzi kibao na kufatana fatana. zamani tulikuwa tunakesha humu mada moto moto tunachat tunafurahi. siku hizi ukisign in tu lazma mawili matatu ya kukukera.