Wasifu wa Masha: Maswali na Majibu

Wasifu wa Masha: Maswali na Majibu

Mheshmiwa mtarajiwa;

hivi humu JF unaelewa mafanikio ya kila mtu?. Kwa wengine unachoandika ni kichekesho. Mafanikio ni subjective. Kama una maana kuwa na hela ni mafanikio basi wapo wengi wanaomzidi Masha na wamo humu. Kama ni cheo ndo kwako mafanikio basi wapo humu wengi wanaomzidi Masha.

Ukiacha mengine tunayoandika kama utani. Waziri Masha pamoja na exposure yake kubwa ameongea chini ya uwezo kabisa. Ndio maana watu wanasikitishwa. huwa tunatagemea mtu kijana na ambaye ana exposure kama yeye kufanya zaidi ya aliyofanya.

Habari ndio hiyo kaka/dada

Nadhani na wewe hukunielewa mkuu!Hakuna niliposema kuwa mafanikio ni hela au cheo,hayo ni yako!Nimeongelea kukwamishana kwetu wenyewe kwa wenyewe na wala sikumaanisha kwa Masha peke yake.
 
Haya ndiyo tunaita majungu,chuki ama fitna mkuu.Hivi unadiriki kusema CV ya Masha haifai hata kwa ujumbe wa nyumba kumi?Are u serious mkuu?Labda kwanza uniwekee CV ya kuwa mjumbe wa nyumba kumi maybe nakuelewa vingine lakini kusema mwanasheria wa LLB na LLM kutoka vyuo vinavyojulikana na kuheshimika hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi kisa umesikia habari zisizokuwa na uthibitisho wowote kuwa alipendekeza wamsilifi Mengi ni matusi makubwa sana mkuu.Ingekuwa bungeni tungekulazimisha ufute kauli yako!

Mheshimiwa sana Mtarajiwa
Ubalozi wa nyumba kumi si shahada wala stashahada kama unavyotaka tuamini. Ni uwezo, ari na hadhi ya kuongoza. Masha hana hadhi hiyo, hata kama utakesha hapa JF kumsafisha, hatasafishika kirahisi hivyo. Hana haiba ya uongozi, tena kwa kuwa ni kijana ndio amechafua zaidi harakati za vijana kuaminika.
Pili kama unafikiri mambo ya Masha ni majungu...time will tell
Mwisho, nimegundua nachambua hoja na mtu asiyejua hoja zaidi ya vioja. I wish you all the best Mkuu
 
Mtarajiwa;

Post ya kiingereza iliandikwa kama utani, kufurahisha baraza. Ungesoma katikati ya mistari ungeelewa.

Asante

FP
 
Mheshimiwa sana Mtarajiwa
Ubalozi wa nyumba kumi si shahada wala stashahada kama unavyotaka tuamini. Ni uwezo, ari na hadhi ya kuongoza. Masha hana hadhi hiyo, hata kama utakesha hapa JF kumsafisha, hatasafishika kirahisi hivyo. Hana haiba ya uongozi, tena kwa kuwa ni kijana ndio amechafua zaidi harakati za vijana kuaminika.
Pili kama unafikiri mambo ya Masha ni majungu...time will tell
Mwisho, nimegundua nachambua hoja na mtu asiyejua hoja zaidi ya vioja. I wish you all the best Mkuu


Mwalimu Zawadi majungu ni pale unaposema Masha hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi.Kama nilivyosema mwanzo leta CV ya mtu ambaye unadhani anafaa kuwa mjumbe wa nyumba kumi ili tuilinganishe na CV ya Masha tuone kama hafai.Usipoleta basi futa hii mijungu yako mkuu!
 
Mama;

Wakati huo (mwaka 1991 ambao pia nilikuwa UDSM) kama ni raia wa Tanzania lazima ilikuwa upitie JKT.

Sielewi kama aliukana uraia wake wa USA ama la!.

FP


Jamii ya kitanzania inajiuliza maswali mengi kweli kumhusu Masha, ambayo majibu yake hayawezi kupatikana. Pengine wananchi wamtupe 2010 na pia atolewe katika baraza la mawaziri. Inaonekana umma namchoka sana Masha

Hivi vipi nasikia jana kazushiwa kifo ni kweli jamani? Hapa Dar nimesikia tetesi kwenye Bar kwamba katutoka?
 
Ndugu zangu,
I am concerned about corruption in the privatization process in our motherland? The country is currently under 'siege' of oil companies. Bei ya mafuta inaendelea kuumiza watanzania kwa kuendelea kufanya maisha kuwa magumu. kwa sababu hiyo naomba mwenye kufahamu atusaidie kufichua ufisadi kwenye eneo hili. Maswali yafuatayo yananiumiza kichwa sana

1. Who killed(Tanzanian and Italian Petroleum Refining Company Ltd) TIPER?. In whose interest did TPDC abandon its refinery in favour of importation by private sector?
2. Je, kweli hakuna rushwa kwenye maamuzi hayo na sera nzima ya ubinafsishaji wa sekata hiyo? Ni akina nani walihongwa na nani ili kufikia maamuzi ambao yataendelea kuliumuiza Taifa kwa muda mrefu?

mapambano daima,


mpambanaji
 
Lawrence Kego Masha aka Lau alimezaliwa March 11 mwaka 1967!!! Na sio 1970 as stated on his CV na anavyodai mwenyewe. Alianza shule ya vidudu pamoja na darasa la kwanza na la pili Mwanza. Hizi habari sio za kusimuliwa. Nilisoma nae shule moja enzi hizo.

Baada ya hapo waliondoka kwenda kumfuata Mzee Masha senior at the Big Apple. Huko UN huyu mzee alipokuwa anamepata kazi wana policy ya kusomesha watoto mpaka watakapofikisha miaka 18 au 21 (correct me if am wrong). Masha senior alirudisha nyuma umri wa Lau miaka mitatu ili aweze kuendelea kulipiwa shule. Kumbuka waliondoka TZ katika mazingira ya kutatanisha na hivyo it was very possible for documents to be played with. Huwezi kumlaumu sana huyu mzee maana watz wengi tu wanacheza huu mchezo. US walikataa kumwingiza darasa la tatu kwa kuwa ana "umri mdogo" hivyo akarudia darasa la pili. Actually Masha finished high school akiwa mzee kuliko wenzake yaani 19 lakini akipretend ana umri wa miaka 16. Alikuwa anatutambia kwamba He was called the whiz kid. He was and still is bright though he was no kid.

Nakubali kuna wengine humu JF wanamfahamu Lau sana na wasifu wake hasa wakati akiwa Marekani lakini huyu Mzinza ninamfahamu tangu akivaa nepi. Alizaliwa Sengerema na sio marekani. Mdogo wake Mgisa (mjeshi) ndio alizaliwa New York lakini huyu ni mzalendo kwelikweli aliukataa uraia wa marekani alipofikia umri wa miaka 18. But for the devious 41 year old Lau.....waziri wetu wa polisi...........well, leaves a lot to be desired??....pathetic at least
.

Mzee Jembe Ulaya,

Unao ushahidi?
 
Originally Posted by Jembe Ulaya
Lawrence Kego Masha aka Lau alimezaliwa March 11 mwaka 1967!!! Na sio 1970 as stated on his CV na anavyodai mwenyewe.

- Wakuu sometimes muwe munamuogopa Mungu japo kidogo, Lau anamfuatia kaka yake anayeitwa John K. Masha, msomi aliyebobea na nyanja ya uchumi aliyeko Missouri State, bado hajafikia miaka 41 sasa inakuwaje mdogo mtu anakuwa na umri mkubwa kuliko kaka, au?

- Unajua kama nilivyosema huko nyuma, labda aliyoyafanya Lau toka awe mbunge na waziri ndiyo yana walakini, lakini elimu yake na background yake kwa ujumla, sidhani kama kuna anything serious politically!
 
Lakini FMES; je, ni kweli kwamba masha alisomea kindergarten, STD 1 and 2 Tanzania kabla ya kwenda US? Na kama ni hivyo je itakuwa basi alianza STD 1 akiwa na mwaka 1 na miezi 9? Naomba ufafanuzi kwa hilo!
 
Lakini FMES; je, ni kweli kwamba masha alisomea kindergarten, STD 1 and 2 Tanzania kabla ya kwenda US? Na kama ni hivyo je itakuwa basi alianza STD 1 akiwa na mwaka 1 na miezi 9? Naomba ufafanuzi kwa hilo!

- Mkuu Nurujamii, ni kwamba nikiwa mdogo nilikuwa ninamjua sana baba yake kwa sababu enzi hizo yeye akiwa katibu mwenenzi wa TANU taifa, Kambona, Chiume, na Lusinde walikuwa ni marafiki wakubwa sana,

- baadaye nilikutana naye tena US, NY wakati huo Lau alikuwa anasoma High School, baadaye najua kuwa alienda Mlimani kwa hiyo ya nyuma ya hapo siyajui ila ninayajua tu kuanzia hapo nilipomkuta. Yaaani alisoma Mlimani, na baadaye Georgetown.
 
..hivi kwanini wananchi wanahangaika kumjadili huyu jamaa wakati huu ambapo tumepokea matokeo ya mitihani std 7 na almost 47% wa wanafunzi wamefeli?

..nadhani wakati mwingine ni kutumia muda wetu vibaya kujadili watu, badala ya masuala muhimu ya kitaifa.
 
Mkuu; kulikoni unafufua ya kale? Ya kale hayanuki yakhee hata kama kamwekea pingamizi mtu na limekubalika. Yeye ni Mbunge ati . . . anasubiri kuapishwa tu.

Ha ha haa.....yeye kama waziri mwenye dhamana na uhamiaji....
 
Na yeye ni RAIA HALALI wa Tanzania lol

Ndio maana siku za huko nyuma niliwahi kusema kuwa huyu Masha hana nguvu ya kushughulikia mambo yanayohusu Uraia wa watu,kwa sababu hata Uraia wake una walakini.....muangalieni vizuri huyo,maana kipindi alichokaa Marekani kuna habari kuwa alishawahi kuomba Uraia sio kuishi na Green Card tu.

Huyu Bwana alishawahi kuandika email ndefu wakati alipokuwa anaondoka USA ambayo ilikuwa na maelezo mengi kuhusu haja ya kulitumikia Taifa,ukiisoma vyema email ile utagundua wazi kuwa alikuwa ameahidiwa wadhifa fulani...Kwa kumpamba na kuanza kumtengenezea njia mama Mwenegoha akamualika awahutubie vijana pale American Embassy na kuwaambia umuhimu wa kurudi nyumbani kulitumikia Taifa.Kuanzia hapo akaanza kujitengenezea njia ikiwa ni pamoja na kumuajiri Mshauri Mkuu wa Rais,Ridhiwan kufanya intern yake kwenye kampuni yao ya Uwakili (IMMMA).Masha kama walivyo viongozi wengine wengi ni opportunist na wala si msafi na makini kama anavyozungumzwa hapa.

Kuna kila Haja ya kuanzishwa vetting ktk muundo wetu wa kuomba Kazi za kuwatumikia Watanzania....Huu mtindo wa Watanzania wababaishaji kujiona bora au patriotic kuliko wenzao unauma sana.Katika Jimbo la Nyamagana Masha alikuwa na Wapinzani wawili Ezekiah Wenje wa Chadema na Omar Mbalamwezi wa CUF,lakini wote wameondolewa na Tume ya Uchaguzi na kumbakisha Masha peke yake.Bado tutasikia mengi kuelekea Oktoba/2010.
 
Back
Top Bottom