Mtarajiwa,
Tatizo la Masha ni kubwa zaidi ya unavyotaka kuonyesha. Mimi nilikuwa na imani kubwa sana na masha kwasababu najua ana uwezo na pia kakulia kwenye mazingira ambayo yanaweza kukufanya ufikiri na uachane na ujinga ujinga wa kwenye mitaa ya waswahili.
Lakini looh! ukimsoma huyu mheshimiwa kuanzia speeches zake mpaka alichotaka kufanya kwa Mengi, huwezi kushindwa kukubaliana na Nyani Ngabu, Miafrika ndivyo tulivyo.
Muhimu kwa yeye si kuanza kutafuta wabaya wake au kufikiri kuna watu wanamuonea wivu, bali kuchapa kazi. Yuko wizara ambayo ukiamua kufanya kazi, kila mtu ataona. Wakati anapoteza muda kujibizana na akina Mengi, kuna Albino wanaendelea kuuawa. Asipokuwa mwangalifu hata hilo jimbo lake hapo Mwanza linaweza kuota magugu 2010.