Wasi Wasi wa Udini

Status
Not open for further replies.
Mkandara
Linapokuja swala la dini na ujamaa huwa sikuelewi kabisa unazungumza nini. Moshi amekueleza vizuri kabisa ila wewe naona hukumuelewa kabisa. Achana na mambo ya historia hayawezi kutusaidia kitu hapa. JK akitawala kama alivyotawala JKN hawezi kufika mahali popote. Dunia imebadilika na watu wamabadilika jinsi wanavyofikiria mambo. Huwezi kutumia historia kutawala. Tembelea forum nyingi utagundua kuwa watu wengi wanaona JK ni mdini. Inawezekana kabisa kuwa JK aliteua watu wale bila kuwa na lengo la kidini, wale ni binadamu na wanaweza kuwa na dini yoyote. Mkandara, nadhani watu wengi humu hawakuelewi tunaomba kwa maneno machache ikiwezekana sensensi moja tunaomba utueleze kama unadhani kama JK hana tatizo lolote katika uteuzi wake. Kila mtoa hoja hapa ameeleza mawazo yake na nimeelewa vizuri kabisa mawazo ya Mkwawa yanalingana kabisa na mimi ninavyofikiria, Moshi naye ametoa yake ambayo nimeona ni valid kama mawazo yangu au mkwawa yasipofuatwa. Kama mtu unataka uteue tu watu bila kujali uwezo wao wa kazi lazima uangalie uwiano wa makabila na dini au hata jinsia. Sasa wewe unasemaje?
 
Ndugu wasema ama wachangiajia na hasa wewe ndugu Augustine .Juu ya hii mada leo Mkandara anaizima kwa kuwa Mkandara ukisoma posting zake nyingi sana utagundua kwamba huyu jamaa ni mdini.Nina wasi wasi na michango yako Mkandara kama uko sincere.Nchi inaenda pabaya unataka kuangalia uwezo wa watu ?

Hivi Kibelo ana uwezo kweli ? Kalalamikiwa mara ngapi ?Adadi ana uwezo ? Kama anao mbona kaondolewa haraka toka kwenye u DCI ? Wengine sijwajui hata uwezo.Kuna mtu aliwahi kusema kwamba hata Karume akiwa Ujerumani baadaye ilionekana kwamba ni Balozi bora kuliko wengine nikashangaa .Mkandara wacha udini na uache mara moja kutuvuruga wacha watu waseme JK ni mnafiki mkubwa anatumia kuchekacheka kutugawa na atatuletea matatizo sisi Watanzania .

Augustine swala udini hujaliona wewe pekee hata watu wakulima wameanza kujiuliza .JK ni ni muongo na mnafiki wala hana nia ya kumkomboa Mtanzania ila kuwakomba watu wake wa pwani na waislam wenziwe .Inamchukua muda ganu kupitia mikataba na kutujulisha ? Mbona ni mwezi wa nane sasa kakaa kimya na hajasema lolote na anauza NIC na KIA kama kweli anaipenda TZ kwa gharama poa ?

Kwa nini Serikali yake ina side na Mramba kuchukua 17b na Lowasa ana mtetea an Kingunge ? Kwa nini anamtumia Akukweti kuzima sauti za wabunge kwa kuwatisha kila mara Bungeni ?

JK analeta udini na kuwaachia akina Mramba kuchukua pesa nyingi hivi anakaribisha Ukabila kutuchanganya .Tunangoja Mkuu wa majeshi mpya na Mkuu wa Usalama wa Taifa .Kuna mengi yanakuja huyu jamaa nina wasi wasi naye sana .Namaliza kwa kusema mimi huwa sijui kupanga mambo huwa nasema yalivyo Mkandara una udini sana una bahati umesoma lakini kwa akili hii ungaliweza kuvaa mabomu na kujilipua wewe .
 
Hii inanikumbusha Mzee Ngabu kule bcstimes na msemo wake

"takbiru allah walibalu........a true substance of life"

Kimbembe, tafadhali usituletee kimbembe hapa.

Kujenga au kujibu hoja ni jambo la msingi sana.

sam wrote
"Kama mtu unataka uteue tu watu bila kujali uwezo wao wa kazi lazima uangalie uwiano wa makabila na dini au hata jinsia. Sasa wewe unasemaje?"

This question is directed to Mkandara.

Hakuna anayejua kuwa JK aliwachagua hawa mabalozi sita kwa vigezo gani, isipokuwa, miongoni mwa jamii zimejitokeza hisia za udini.

baadhi ya mapendekezo ya wanabodi ni kama ifuatavyo
1.eti JK aelimishe umma kuwa uteuzi wake haukuwa na elements za udini
2.eti JK ateue watu kwa uwiano wa kijiografia, kikabila na hata kidini
3.eti JK aangalie uwezo wa watu na si watu wake/marafiki au watu wa kutoka kwao Pwani, na waislamu wenzake.

Nakumbuka ktk moja ya hotuba za JK wakati wa kampeni huko Dodoma alisema......"serikali haina dini, however mimi (JK) ni muislam, nitafanya kazi za serikali kwa kushirikiana na dini zote bila kubagua........"

1.Je ni kweli JK itabidi afanye kazi yake kwa mtindo wa kujikosha kila wakati akiamua jambo?
2.Je ni kweli uwiano wa kijiografia, kikabila au kidini unawezekana ndani ya CCM na makada wake? na je, hilo ni suluhisho la matatizo yetu wananchi?
3.Na je tunaweza kusema basi kuwa teuzi hii ya mabalozi ni uthibitisho kuwa JK anabagua dini na anapendelea waislamu wenzake au marafiki?
4.Wananchi tulimpa 80% JK, kwa imani kuwa ni mtu swaafi, sasa je imani yetu hiyo nikweli iko jeopardised na teuzi za hivi karibuni??.
5.Je ni kweli watu aliowateua hawana uwezo?

haya ni baadhi tu ya maswali ninayojiuliza
 
Ogah

Naomba uheshimu mawazo yangu kama vile ambavyo sijawahi kumgusa mgtu huwa nasema nikiona unazi unakuwa mwingi.Unasema JK alipata 80% si kura yangu .Nilijua tangia mwanzo kwamba JK hana uwezo wa uongozi .Kumbuka hata JK mwenyewe aliposikia kwamba kashinda kwa 80% hakuamini haya aliyasema mwenyewe siku ya kutangazwa rasmi kwamba hakuamini kama kapata asilimia hizo .

CCM ina nguvu nyingi na uana haramu mwingi asilimia hizi ziliongezwa na Mahita na Co huu ndiyo ukweli lakini CCM kupata kura halali 80% si kweli .

Nakubaliana nan baadhi ya maswali yako Ogah lakini kumbuka JK ahajali sasa ana dola na analitumia vilivyo ndiyo maana akipiga chafya tunasoma JK apiga chafya watu wanacheka .Issue ua ukabila na udini iko pale pale .Angali teuzi zake hata uundaji wa Tume zake utaona nini tunakisema .
 
Kimbembe,
Mtu kama wewe hunipi taabu kabisa na majibu yako mepesi sana kama maji.
Umewataja watu wawili Kibelo na Adai **** kweli wanao uwezo?
Jibu rahisi hapa hawana lakini usitake kunambia hawa watu hawana uwezo kwa sababu ni waislaam. Na labda wakichaguliwa wakristu kutakuwepo na usawa fulani na utendaji kazi mzuri. Sioni hoja yako kuwa na uhusiano wa mada nzima zaidi ya wewe kutunga vitu nje na kuvipaka wanja.

Kufupisha hadithi hii ndefu ebu niwape kazi wewe na huyo Augustine Moshi. Na mtumie vigezo vyenu ktk kazi hii bila kupotosha maana yenu na huo usawa.
Wewe na Augustine mmechaguliwa kuongoza timu ya taifa na mnatakiwa kuchagua wachezaji wa timu ya taifa itakayo wakilisha Tanzania. Haya nipeni uchaguzi wenu kwa kufuata hizo dini, kabila na kadhalika ili kuwepo na usawa kuliwakilisha taifa letu.
Mkinipa jibu ya hili swali na likakubalika kwa wenzetu wote basi mmeshinda nyie na niko radhi kutazama uchaguzi wa JK kwa mtazamo wenu.
 
Wanabodi ,

Kwanza ningependa kutumia nafasi hii kumshukuru Mzee Mwanakijiji kwa kutuwekea hotuba ya mwalimu , kusema ukweli hotuba ile inajitosheleza na inaweza kabisa kutupa majibu ya maswali tunayojiuliza hapa.

Swali ambalo nazidi kujiuliza ni kwa nini ghafla tuu watu wanaanza kuzungumzia udini na kum-accuse JK kuwa ni mdini ? Nadhani ili ni swali la msingi ambalo hatuna budi kujiuliza !

Kama wanabodi wengine walivyosema uchaguzi alioufanya JK unaleta picha mbovu sana kwa watanzania , na vitu kama hivi vinaweza kuinstigate udini katika nchi yetu. Hivi kama kiongozi angekuwa wa dini nyingine tofauti akachagua mabalozi sita wote toka dini yake kweli pangekalika hapo.
 
Kwanza napendakuwakumbusheni wanabodi kuhusu suala la udini,kumbukeni JK anauata nyayayo za Mkapa ambaye wengi walifikiri ni mdini wakati alipoingia nikiwemo mimi,kwanini tusiwaache viongozi kufanya kazi zao kama katiba inavyowaruhusu na kuwapa nguvu?,suala la udini tusipoangalia linaweza likatuletea matatio makubwa sananchini kama tusipoweka vyuchwa vyetu sawsawa ,kumbukeni Tanania ni nchi iliyokuwa na waislam na wakristo wengi number ya waumini isitumike kama kipimo cha uongozi ,tuangalie sana hasa kizazi hichi chetu cha leo tukiendekeza fikra za udinitutasambaratika kabisa na mwisho wa ke ni vita vya wenyewe kwa wenyewe ,angalieni Rwanda,Sierra Leone,Uganda n sehemu zingine duniani jinsi walivyoharibikiwa kwa ajili ya udini na ukabila.
Piece!
Willo
 
Willo,
Ndugu yangu kwanza karibu tena baada ya kupotea. Hapa tuna ubishi wa tafsiri ya Udini kwa mitazamo ya watu tofauti na sidhani kama kati yetu tunaweza kuzua hali hiyo isipokuwa kupotosha maana.

Mimi nachosema toka mwanzo ni kwamba dini, kabila na mengineyo sio kigezo cha uchaguzi wa viongozi watumishi ama nafasi yeyote ile isipokuwa uwezo wa mtu. Na sababu kubwa inayofanya uchaguzi uwe katika hali hiyo ni kwa sababu hatuna Ubaguzi wa aina yeyote toka makabila hadi dini isipokuwa kwa nchi zenye ubaguzi huo swala kama hili linaangaliwa kwa sababu wanyonge huonewa toka mwanzo wa kupata uwezo huo. Rwanda na nchi nyinginezo hata Marekani utakuta ubaguzi umeanza toka ktk shina - ELIMU. Tanzania hatuna kitu hicho kwa hiyo hakuna ubaguzi na lazima wananchi watazame maswala ya nchi yetu kwa black and white. Lakini ukisha anza kuondoa hiyo black na white na kuipaka rangi hoja, hapa mwenye matatizo ni mpaka rangi.

Rufiji, Nitarudia kusema Mkapa alichagua mabalozi zaidi ya sita wakristu na haikuwa hoja kwa sababu balozi hao walikuwa wakiwakilisha matakwa yake. Na baya kuliko yote mabalozi hao walikuwa na ukaribu nae kiukoo, wengine hadi leo bado wameshika nafasi hizo. Binafsi sioni kama ni udini kwani hawa ni mabalozi wanawakilisha maslahi ya nchi yetu na sio kanisa lake Mkapa. Pili, walioshindwa ubalozi sio kwa sababu ni wakristu ama waislaam isipokuwa hawakufaa nafasi hizo toka mwanzo kama Watanzania. Kuna habari kibao zilitembea stae house na wizara ya nchi za nje kuhusu Mkapa na udini. Na wapo waislaam walieneza habari na uvumi wa Mkapa na hata Nyerere kuwa wadini lakini ukweli ni kwamba watu hawa walichagua viongozi kwa kulingana na makubaliano yao ktk maswala ya politics. Huwezi kumweka balozi ambaye hakubaliani na uongozi wako hata kama ni msomi. Tazama wote hawa na hao ma- DC na RC kama wawakilishi wa rais ndani ya nchi badala ya dini zao. Hawa ni watu royal to him, kama alivyosema Mzee Es na wanaweza kuwa wote ni wanamtandao bila kujali dini ama makabila yao.

Nasubiri bado majibu ya Augustini na Kimbembe kuhusu timu yetu ya taifa.
 
Mkandara,

Inasikitisha kuona kwamba unadhani kuchagua mawaziri, mabalozi, wakuu wa majeshi n.k. kunafanyika kama kuchagua wachezaji wa mpira. Tena umesistiza ujibiwe kitu kama hicho.

Narudia kusema kwamba teuzi za mawaziri, mabalozi na nafasi nyingine za kisiasa hazizingatii uwezo peke yake. Zinazingatia uwezo pamoja na uwiano mzuri wa jinsia, jiografia na dini. Kila mtu angeshangaa kama mawaziri wote wangekuwa kina mama, au kama wote wangeteuliwa Wadengereko.


Kuna mtu hapa amedai kwamba wewe ni msomi. Could I please know whether that is true? I am curious.

Augustine Moshi
 
Haya waheshimiwa, kuna mtu amenipa takwimu za uwiano wa wakristu na waislamu katika nafasi mbalimbali za uongozi (mawaziri, manaibu waziri, wakuu wa mikoa n.k). Ni takwimu tu bila majina na sijui kama zina ukweli wowote. Kwa bahati mbaya siwezi kuaccess podcast yangu toka hapa ofisi ya kijiji. Kama kuna mtu anaweza kwenda kwenye podcast na kuangalia ile mada ya pili kwenye eneo la comments, kuna mwandishi ajiitaye "Salum Ahmad", basi kopi vile alivyosema na utupostie hapa.

Ukurasa wangu ni http://mwanakijiji.podomatic.com
 
NI dhahiri kuwa mpumbavu mmoja angejitokeza kujibu makala iliyochapishwa kwenye ukurasa huu wa gazeti hili wiki iliyopita, makala ambayo ililenga kumshutumu Rais Jakaya Kikwete kuwa amekuwa anatumikia udini katika kufanya uamuzi wa kuteua watu kushika nyadhifa mbalimbali katika utawala wake mpya, mpumbavu huyo ni mimi ambaye jina langu linaonekana mwanzoni mwa makala hii.

Nianze kwa kusema kuwa, kwa sababu mbalimbali, sikushangazwa na makala hiyo. Kwanza, uvumi na minong’ono ya mitaani katika wiki na siku za karibuni imekuwa inatajataja sana suala hilo.

Kwa hiyo, na kwa sababu nyingi na uzoefu wa nchi hii, nilitarajia kuwa suala hilo, kwa namna moja au nyingine, lingeingia magazetini hata kama ingechukua muda.

Hilo lilikuwa lazima kabisa. Sina shaka kuwa kama taasisi za serikali zinafanya kazi vizuri, basi hata Rais Kikwete mwenyewe bila shaka atakuwa pia amejulishwa kuhusu minong’ono hiyo.

Huo ni mtandao wa kawaida wa jinsi kiongozi wa nchi anavyopewa na kufikishiwa taarifa, hata kama mwenyewe hataki kuzisikia taarifa hizo au hata kama hataki zimfikie.

Pili; niharakishe kusema kuwa ilikuwa lazima kwa kelele hizo za rais kutumia udini kuteua watu kujitokeza, kwa sababu ukweli ni kwamba Tanzania bado inacho kiwango cha kusumbua cha ukabila na udini, hata kama tunajificha chini ya kivuli cha unafiki ili kuficha uozo huo.

Bado wapo viongozi wa shughuli za umma ambao wanaongozwa na ukabila na udini katika uamuzi mbalimbali, ukiwamo wa ajira na kuendeleza watumishi wa taasisi za umma, za binafsi na hata za kidini. Huo ndiyo ukweli halisi wa nchi yetu, hata kama tunataka kujidanganya vinginevyo.

Ukweli kwamba kuna watu; kwa mfano, wanatunza orodha za nani anateuliwa na rais pamoja na dini zao na pengine makabila yao, ni ishara tosha ya jinsi ukabila na udini vinavyoendelea kutusumbua.

Kwa hakika, uteuzi unatakiwa kuwa jambo la rahisi kabisa, kwa sababu ni lazima ufanyike kwa misingi ya sifa, uwezo, uzoefu, ujuzi na ufanisi. Na ukweli kwamba pengine watu wanatumia udini au ukabila kuwanyima watu wengine ajira, au vyeo, wenyewe ni ukabila wa kutosha.

Hakuna shaka kuwa tumefanya vizuri katika kudhibiti mwenendo wa udini, ukabila, rangi ya mwili na ubaguzi mwingine wenye athari za hatari kwa Tanzania. Lakini bado ukabila na udini unabakia.

Kama nilivyosema awali, wapo watu chungu nzima wanaosukumwa na kuongozwa na udini na ukabila katika shughuli za umma, iwe katika ajira au manufaa mengine ya kitaifa, ukiwamo hata upatikanaji wa tenda.

Vinginevyo, tunaelezea vipi malalamiko na ukweli kuwa mashirika kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wizara ya Fedha, au mashirika na wizara nyingine zina watu wa kabila moja? Na bado hakuna anayehoji hali hiyo kwa sababu tunaongozwa na unafiki tu.

Ukweli ni kwamba, pamoja na miaka yote ya kupambana na ukabila, udini na ubaguzi wa aina tofauti, ukiwamo wa rangi, bado tuna tatizo kubwa la mabalaa hayo. Mabalaa yote hayo yapo karibu sana na hisia zetu. Na ukijaribu kuhoji hali hiyo, utaambiwa wewe ni mkabila, mbaguzi wa rangi au mshiriki wa ubaguzi mwingine wowote.

Kiwango chochote cha kujidai kuwa hakuna ukabila wala udini katika Tanzania, hakitaondoa mabalaa hayo. Kujidai hakuna mabalaa hayo ni kuishi katika dunia ya mbuni, ya kuficha kichwa kwenye mchanga wakati kiwiliwili kilichobakia kiko wazi nje ya mchanga.

Tatu, sikushangazwa na madai hayo kwa sababu kila kiongozi mkuu wa nchi hii, kwa njia moja au nyingine, ameshutumiwa kuendesha nchi kwa misingi ya ukabila, udini, rangi ya mwili na ubaguzi mwingine miongoni mwa binadamu.

Julius Kambarage Nyerere, kiongozi wa kwanza wa nchi hii, alipata kushutumiwa kwa kuwapendelea Wakatoliki katika uteuzi wa nafasi za serikali. Alishangazwa mno na tuhuma hizo kiasi cha kwamba aliwaambia mawaziri katika mkutano wa Baraza la Mawaziri kuwa kabla ya shutuma hizo, alikuwa hajapata hata kuhangaika kuhesabu ni Wakatoliki wangapi alikuwa amewateua katika Baraza la Mawaziri.

Na wala hakuna shaka kwamba Mwalimu Nyerere ndiye kiongozi wa nchi hii ambaye alipambana kufa na kupona kupunguza makali ya udini, ukabila na ubaguzi mwingine. Kwa sababu bila Nyerere, baadhi ya makundi ya watu katika nchi hii wangeonewa sana.

Nne, sikushangazwa na shutuma hizo kwa sababu ya msimamo wa mwandishi mwenyewe wa makala hiyo. Huyu ni mtu ambaye amehama kutoka chama kimoja cha siasa za upinzani kwenda kingine kulingana na matakwa na maslahi yake. Kwa mtu kama huyo, shutuma za udini na ukabila ni mambo rahisi kuyatumia katika kufanikisha malengo ya kisiasa, hata kama ni ya muda mfupi; na yenye athari na hatari za kweli kweli huko tuendako.

Katika hali ya kubanwa mno ambamo wapinzani wa Serikali ya Jakaya Kikwete wamejikuta, baada ya kiongozi huyu wa Tanzania kupata ushindi mkubwa na wa kushangaza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, unafanya nini kuipinga serikali?

Kwa sababu hakuna hoja yoyote ya msingi ya kupinga serikali kwa sasa, na kwa hakika hali ya sasa ni ya kuwahurumia wapinzani kweli kweli, unafanya nini kama si kupakazia matope kwa kutumia hoja za ubaguzi ambazo nchi hii imepingana nazo tangu uhuru wetu tuliopata 1961?

Kuna hoja gani kwa sasa ambayo wapinzani wanaweza kutumia kuushutumu utawala wa Rais JK zaidi ya ile dhaifu ya ubaguzi wa dini, hata kama ilikwishaelezwa wakati wa mchakato wa kugombea urais kuwa Kikwete ni Mwislamu wa Kijamii (social) kuliko kuwa Mwislamu wa Kiitikadi (ideological) na huo ndio ukweli wa mambo.

Ama kuna hoja gani rahisi ya kuvutia na kuchochea hisia za watu kama kutumia hoja ya ukabila, hata kama mwenyewe rais anatoka kwenye kikabila kidogo cha Wakwere ambacho hata kama angetaka na kudhamiria kweli kweli kukipendelea, hakuna watu wa kutosha, kwa msingi ya elimu na uwezo, kuweza kuteuliwa katika nafasi za uongozi wa umma?

Kwa hakika, udhaifu huo wa kikabila wa Kikwete ulikuwa moja ya nguvu za kumwezesha kuteuliwa kuwa mgombea urais kupitia CCM na hata kuchaguliwa, kwa wingi mkubwa mno wa kura, kuwa Rais wa Tanzania.

Hata hivyo, jambo ambalo lilinishangaza katika shutuma hizo, ni ukweli kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, Wakristo sasa wanalalamikia kupendelewa kwa Waislamu katika uteuzi wa kushika nafasi za juu za uongozi.

Sikusudii kusema kuwa Wakristo hawajapata kulalamikia udini katika nchi hii.

Wamelalamika sana, kuhusu mihadhara ya Kiislamu, kuhusu matusi ya wahadhiri wa Kiislamu dhidi ya Ukristo, na tuwe wakweli, hasa wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Lakini kamwe, sisi Wakristo, mimi nikiwa miongoni mwao, hatujapata kulalamikia Waislamu kupatiwa nafasi kubwa za uongozi wa umma, kwa sababu ni sisi ambao siku zote tumenufaika na nafasi hizo.

Kuna wakati, hasa katika miaka 15 ya mwanzo ya uhuru wa nchi hii, nafasi zote kubwa katika uongozi wa serikali na umma, zilishikiliwa na Wakristo na tena kutoka makabila machache tu. Hali imebadilika kwa kadri Waislamu walivyozidi kupata elimu na watu wa makabila mengine zaidi kujiendeleza.

Kwamba sasa sisi tunalalamika, basi hili ni jambo jipya ambalo linahitaji kuelezwa zaidi na hasa kujibu swali kama kweli Kikwete anawapendeleza zaidi Waislamu katika uteuzi wa nafasi za uongozi wa umma.

Niongeze pia kuwa, sisi Wakristo tulikuwa hatulalamiki kwa sababu tulikuwa tunanufaika na kuneemeka. Na kwa sababu hali hiyo ilizoeleka kiasi cha kukubalika, sasa tunaona ni tatizo kwa Waislamu nao kuteuliwa kushika nafasi hizo. Ni hadithi ile ile ya ‘changu changu, chao changu’.

Nianze kwa kusema kuwa, mvutano wa kidini katika uteuzi wa nafasi za uongozi wa umma, ni mvutano wa kijinga na kipumbavu, lakini unaweza kuwa mvutano wa hatari kweli kweli na kusababisha zahma ambazo tumezishuhudia katika nchi nyingine duniani, zikiwamo za Kiafrika kama Ivory Coast, na nchi za maeneo mengine ya dunia, kama nchi iliyokuwa Yugoslavia ambayo sasa imemeguka vipande vipande.

Dalili zozote za kuwapo jitihada za kuupamba na kutumia udini katika uteuzi wa nafasi za madaraka ya umma, ni hatari. Na haziwezi kwa namna yoyote kukubalika au hata kusameheka. Lakini, sasa kauli hiyo inatuleta kwenye swali letu jingine ambalo ni; je, Rais Kikwete anatumia udini katika kuunda utawala wake?

Hata kabla sijaendelea, nataka kusema wazi wazi kuwa jibu la swali hilo ni hapana. Inawezekana vipi, kiongozi ambaye alipata zaidi ya asilimia 80 ya kura zote katika Uchaguzi Mkuu wa Desemba mwaka jana, ambaye alipata kiasi cha zaidi ya kura za Watanzania milioni tisa kati ya milioni 11 waliopiga kura, akatumia udini katika utawala wake?

Kwanza, hahitaji kutumia dhambi hiyo hatari, kwa sababu ni kiongozi ambaye alichaguliwa na kukubalika kwa watu wa dini zote.

Lakini pia, lazima iongezwe kuwa, kwa wale wanaomjua vizuri zaidi na mimi, lazima nikiri haraka haraka kuwa si mmoja wa watu hao waomjua vizuri sana, huyu ni kiongozi ambaye hatamani kwanza kuangalia pasi ya kusafiria ya mtu, kuona cheti chake za kubatizwa, rekodi yake ya kusilimishwa, cheti chake cha ndoa wala rekodi nyingine ya mtu yeyote, ili aweze kumteua mhusika kushika nafasi yoyote.

Tutaangalia rekodi yake ya uteuzi wa watu baadaye, lakini kama kweli kijana aliyelelewa chini ya utawala wa Mwalimu Nyerere, anaweza kusukumwa na ukabila, udini na madhambi mengine yoyote ya ubaguzi ukiwamo wa rangi, basi nchi hii iko katika hatari kubwa mno.

Na wale watakuwa ni watu wapumbavu kabisa ambao watatarajia kuwa rais atalazimika kwanza kusoma rekodi za maisha ya wateuliwa kwa maana ya dini, makabila, rangi zao za miili, kabla ya kufanya uteuzi wa watu mbalimbali kushika nafasi za umma.

Lakini vile vile, ni watu wajinga kabisa ambao wanatarajia Rais Kikwete ateue washika nafasi za umma kwa idadi ya sawa kwa sawa, kwa maana ya kwamba kwa kila mteuliwa Mkristo atateuliwa Mwislamu au kwa kila mteuliwa Mwislamu atateuliwa pia Mkristo.

Kwa mtu yeyote kuamini na kutarajia hali hii, ni kujidanganya na kujipumbazisha. Na wala hakuna kiongozi yeyote mwenye busara duniani anayefanya hivyo.

Katika uteuzi wake, hatutarajii kuwa Rais Kikwete atahangaika kuhakikisha kuwa, anateua idadi sawa ya Waislamu na Wakristo kushika nafasi za madaraka ya umma.

Kwanza, ukweli ambao ni mchungu kweli kweli, lakini hiyo ndiyo hali halisi, ni kwamba kama uteuzi wa kushika nafasi za umma unaongozwa na uwezo, ufanisi, elimu na uzoefu, ni dhahiri nafasi nyingi zitakwenda kwa Wakristo kwa sababu wao, kwa bahati nzuri au mbaya ya kihistoria, wamebahatika kupata elimu mapema kabla ya Waislamu na pengine kuliko Waislamu.

Huo ni ukweli wa historia ambao haukusababishwa na rika la sasa la Watanzania, na wa rika hili hawawezi kubeba lawama ya hali hiyo. Huu ni ukweli wa mpindo wa historia ambao si matakwa ya Kikwete wala Mtanzania mwingine yeyote. Hiyo ndiyo hali halisi.

Kwa sababu hiyo basi, hakuna mtu yeyote mwenye kufikiria sawasawa na kuitakia nchi hii mema, anaweza kudai kuwa ni wajibu wa Rais Kikwete, kama ambavyo haikuwa wajibu wa marais waliomtangulia, kuteua idadi sawa ya Waislamu na Wakristo katika nafasi za utumishi wa umma.

Kwa maama hiyo, hatuzungumzii uteuzi wa idadi sawa ya watumishi wa umma, bali tunazungumzia idadi linganifu (not equal but equitable numbers), ambako kila dini, kabila, rangi inapata haki yake ya kuteuliwa watu wake bila uonevu wala kubaguliwa kwa kadiri ya sifa za kazi ambazo wanateuliwa kuzishika.

Hivyo, kama kuna Mhaya ambaye ana sifa zaidi ya kazi ya utumishi wa umma kuliko Mkwere ambaye ameomba kazi hiyo, inatakiwa Mhaya huyo aipate kazi hiyo bila watu kutilia maanani kabila lake, dini yake au hata rangi yake ya mwili. Huu ndio msingi ambao nchi hii imeupigania hata kama hatujaufikia bado.

Naamini pia kwamba, inapokuwa lazima kabisa kwa rais kuangalia dini katika uteuzi wowote, hatasita kufanya hivyo, ilimradi mteuliwa awe na sifa za kuifanya kazi hiyo.

Hakuna anayetarajia kuwa kama rais angekuwa na madaraka ya kuteua Kadhi Mkuu wa Tanzania, angeteua Mkristo. Uteuzi huo ungekuwa ni matusi kiasi gani kwa Waislamu? Kwa bahati nzuri sana, rais, katika teuzi nyingi hachagui viongozi wa dini, bali viongozi wa shughuli za umma.

Shutuma dhidi ya Rais Kikwete katika makala ya wiki iliyopita, ilionekana kuchochewa na uteuzi wa karibuni wa kiongozi huyo wa viongozi wa Sekretarieti ya CCM ikiongozwa na Yusuf Makamba baada ya Kikwete mwenyewe kuwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, na kabla ya hapo uteuzi wake wa mabalozi wa nchi mbalimbali duniani.

Nakiri kuwa, katika uteuzi huo, walikuwapo Wakristo wawili tu katika timu nzima ya watu karibu 10 au zaidi. Je, huu ni udini? Jibu langu kwa swali hilo vile vile ni hapana.

Naamini ninayo matatizo kwa watu si zaidi ya wawili katika orodha ya watu hao walioteuliwa na Kikwete. Lakini matatizo yangu si kuhusu sifa zao. Hawa si watu walioteuliwa kwa sababu ya sifa za kuwa wamepata bahati nzuri au mbaya kuingizwa kwenye Uislamu na baba na babu zao, isipokuwa kwa sababu ya uwezo wao.

Kudai kuwa watu hao wameteuliwa na Kikwete kwa sababu ya Uislamu wao, ni matusi makubwa kwa wateuliwa hao na familia zao. Ni matusi yanayohitaji wateuliwa hao kuombwa radhi.

Kwa hakika ni matusi makubwa kwa mtu kuamini kuwa mwanasheria maarufu kama Mwanaidi Sinare Maajar, mtu mwenye sifa kubwa mno za uwakili na uanasheria nchini, anaweza kuwa ameteuliwa kwa sababu ya Uislamu wake.

Vivyo hivyo kwa Adadi Rajabu ambaye amepata kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Omar Ramadhan Mapuri ambaye alipata kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ahmed Rweyemamu Ngemera ambaye alipata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki au Juma Mwapachu ambaye ameshiriki sekta binafsi, ni msomi na amepata kuwa Balozi nchini Ufaransa.

Ni mtu gani asiyekuwa mnafiki na mkweli ambaye anaweza kuamini kuwa watu hawa wameteuliwa kwa sababu ya Uislamu wao? Tuambiwe ni sifa gani ambazo mabalozi Wakristo wanazo zaidi kuliko Waislamu walioteuliwa juzi kuwa mabalozi. Hawa ni wasomi waliobobea ambao wanazo sifa sawa au hata zaidi ya baadhi ya Wakristo ambao wanapiga kelele kuhusu uteuzi wao.

Kadhalika kwenye uteuzi wa Sekretarieti ya CCM. Nani asiyejua sifa za kisiasa za Makamba ambaye sasa amepewa kazi ya siasa ambayo naamini anaiweza zaidi kuliko ile ya ukuu wa mkoa ambayo inahitaji ujuzi na uzoefu zaidi ya kuendesha siasa tu?

Nani asiyejua ujuzi wa Rostam Aziz katika masuala ya uchumi? Unaweza vipi kumtilia shaka mchumi huyu kwa sababu tu ya jina lake kuelekea kwenye Uislamu? Kwa hakika, ni mtu asiyefanya utafiti wa kutosha ambaye atakuwa hajui kuwa Rostam si Mwislamu, bali mfuasi wa dini ya zamani mno ya Kiajemi iitwayo Zoroastrianism.

Zoroastrianism inakubalika kuwa moja ya dini za kale zaidi duniani na yenye asili yake miaka 5,000 iliyopita yenye kufananafanana na dini za kale za Kiafrika. Na kwa kweli unahitaji mchumi gani zaidi ya mtu mwenye sifa kama za Rostam kuendesha shughuli za fedha na uchumi za chama chako? Au mpaka aitwe Salvatory ndipo sifa zake zikamilike?

Naamini pia kuwa ni ukosefu huo huo wa utafiti na haraka haraka ya kushutumu ambavyo vilimsukuma mwandishi wa makala wiki iliyopita kudai kuwa Jaka Mwambi ni Mwislamu. Kasilimishwa msikiti gani huyo? Ama kaifanya shughuli hiyo kwa siri kubwa, kwa sababu ni kweli kwamba binadamu wanao uhuru wa kubadilisha dini zao wakitaka kwani dini ni sifa ambayo sote tunaikuta duniani ili ifungue njia yetu kwenda peponi.

Nani anayekataa dhana kuwa Kikwete ana haki ya kuteua watu ambao anaweza kufanya nao kazi kwa urahisi zaidi, kuliko kuteua watu ambao atavutana nao au wataanza hadithi ile ile ya kawaida ya Watanzania kuhalalisha uzembe kwa hadithi kibao na kuhujumiana?

Mwandishi wa makala ya wiki iliyopita, pia alionekana kukerwa na ukweli usiopingika kuwa, mabalozi wote walioteuliwa majuzi, wamepelekwa katika vituo muhimu na vikubwa kwa maana ya hadhi ya shughuli za kidiplomasia.

Nakubaliana na hoja hiyo kuwa vituo vya London (Uingereza), Paris (Ufaransa), Berlin (Ujerumani) ni vituo vikubwa kidiplomasia. Lakini hoja hiyo haiwezi kukamilika bila kwanza kuangalia vyeti vya ubatizo vya mabalozi wetu wa Washington (Marekani), Umoja wa Mataifa (New York), Ottawa (Canada), Pretoria (Afrika Kusini), Umoja wa Mataifa (Geneva), vituo vyenye ukubwa ule ule wa kidiplomasia kama vile ambako wanakwenda Maajar, Ngemera, Kibelloh na wengine.

Sikutaka kuingia kwenye takwimu, lakini ngoja tuangalie takwimu kidogo. Kwa sababu makala ya wiki iliyopita, ilitumia takwimu kujenga hoja, naomba na mimi nitoe takwimu chache kuhusu uteuzi wa Kikwete katika miezi saba iliyopita kuonyesha kuwa huyo si rais ambaye anaingia msikitini kuomba kwa Uislamu wake ili apate mwongozo wa kutosha wa kiroho kuweza kupata mawazo ya akina nani ni Waislamu ili awateue kushika nafasi za uongozi na madaraka ya umma:

Tunao mawaziri kamili 14 ambao ni Waislamu, na tunao mawaziri 15 ambao ni Wakristo, akiwamo Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi Serikalini, Philemon Luhanjo. Rekodi zipo kuthibitisha takwimu hizo. Kuhusu manaibu waziri, tunao Waislamu 11 na Wakristo 20.

Kuhusu wakuu wa mikoa, tunao Waislamu wanane katika mikoa ya Arusha, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Morogoro, Tabora na Tanga na Dar es Salaam ambako Yusuf Makamba alikuwa mkuu wa mkoa na sasa ameondoka, wengine 13 waliobakia ni Wakristo.

Kuhusu makatibu wakuu ni kwamba, makatibu wakuu kamili wa wizara 21 ni Wakristo kulinganisha na Waislamu saba tu. Kwa naibu makatibu wakuu, kuna Wakristo 11 na Waislamu watatu tu ambao ni Omar Chambo wa Wizara ya Miundombinu, Ramadhan Khijjah, mmoja wa naibu makatibu wakuu wawili wa Wizara ya Fedha na Mohammed Muya wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Lakini vile vile angalia uteuzi wake mwingine katika taasisi nyeti za ulinzi na usalama na hata uchumi. Chunguza uteuzi wake katika Jeshi la Polisi, na ni majuzi tu ambapo alimteua Luteni Jenerali Davis Mwamunyange kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mwislamu.

Mkuu wa Usalama wa Taifa anabakia Mkristo. Na bado wakuu wa taasisi kubwa za uchumi kama vile Benki Kuu, TRA na nyingine nyingi tu wanabakia Wakristo. Sasa hoja iko wapi, kama si kuzusha tatizo ambalo halipo?

Madai ya upendeleo wa Waislamu ni utani wa kiwango cha juu, lakini vile vile wa hatari inayoweza kuzaa zahma yenye athari kubwa. Awali, niliposoma makala ile ya wiki iliyopita, nilidhani kuwa Mhariri wa gazeti hilo alikuwa anashiriki kuzusha hoja hewa na za hatari.

Lakini, sasa naamini kuwa amefanya kazi nzuri kufungua mjadala wa jambo muhimu ambalo tumekuwa tunajidai kulipuuza na kujitia kuwa halipo kwa sababu ya unafiki wetu.
 
Ahsante sana ndugu Kigoma,
Nilipoisoma hiyo habari niligundua kuwa imeandikwa na mtu mdhoefu sana kwenye mambo ya habari na siasa. Hiyo link uliyonipa nimepata jina lake, huyu ni ndugu yetu Salva Rweyemamu, nadhani wenge wenu mtamkumbuka kwenye uandishi wake Habari Corporations Ltd.

4429046a1ca95_Picture_1_Salva_crop.JPG

Salva Rweyemamu
Nilipokuwa kwenye jitihada zangu za kutafuta nafasi yake katika jamii nilikutana na reaction ya wana CUF kwa makala aliyoandika juu ya viongozi wa CUF. Mwanachama mmoja wa CUF alisema haya,
Ni waumini wazuri wa chama chao kamwe hamuwezi kuwarubuni na propaganda za waandishi wanafiki kama za akina Rweyemamu. Unafiki wa akina Rweyemamu sio bure kuna mpango kabambe wa waandishi hawa kwa ajili ya kuutetea mfumo fulani ambao wao wana maslahi nao mimi nina shaka mfumo huo ni wa UDINI. Kwa vyovyote kanisa liko nyuma ya hivi vyombo vya habari katika kuripoti matukio yanayohusu viongozi wa CUF. Niwaambieni kitu kimoja fanyeni mnavyofanya iko siku na si muda mrefu HAKI itasimama nchini na wanyonge watapata HAKI yao na nyinyi wanafiki na madhalimu kama akina Rweyemamu mtalipa kwa yale madhara mliyoyasababisha kupitia kalamu zenu kama yale ya Mauaji ya watu wasio na hatia ya Januari 26 27 2001 yale ya Mwembechai 1998 n.k.

Haikunichukua muda mrefu kudhibitisha maneno hayo kama ni ya kweli. Check this out.

Rweyemamu reaction on Mapuri alipofungia magazeti
MISA-Tan chairman Salva Rweyemamu described the minister's action as "at best draconian and a negation of freedom of the press and freedom of expression which are core pillars of any democratic and tolerant society."

Kwa maneno hayo na habari yake anayomtetea Mapuri kuwa Balozi huo ni ushambenga wa hali ya juu. Mr. Rweyemamu ameweza kwa kiasi kikubwa kuwajibu watu wenye mawazo kuwa JK ametumia udini lakini ameshindwa kunijibu uwezo wa hao watu kuwa mabalozi. Nadhani wote tunakubaliana kuwa tunahitaji mabalozi wenye elimu ya Internation Relations kama alivyo Dr. Mahiga. Tunahitaji mabalozi kama hao wenye uwezo wa kuwa mabalozi.

Kwa wanaomjua Rweyemamu mwambieni sam anamsubiri TEF, yeye na Ulimwengu ndiyo walioongoza mashambulizi zidi ya BWM na sasa wanajifanywa wao ni CCM number one. Hiyo habari inaonyesha ametumwa na watu fulani kuiandika kwani ameandika kwa ufundi wa hali ya juu lakini hajanipata kwani habari ina mapungufu mengi na uongo mwingi.
 
Sam,
Habari Corporation imeshanunuliwa na Rostum. Nasikia Rweyemamu alikuwa mstari wa mbele kuunga mkono uamuzi huu wakati Jenerali alipinga. Kwa hiyo ndugu yangu usishangae sana. :p
 
sam said:
Filgga
Najua hujaandika wewe hiyo habari hebu tupe source.

Sorry, Nilisahahu kuweka source..


Ila nilitaka tuu kuweka ile habari ambayo mwanakijiji alisema kwamba ipo katika podcast yake sasa nikasoma alivyoandika nikajua kwamba hiyo habari inatoka katika makala ya gazeti la tanzania daima.
 
Wandugu Makala hii umejaa upigaji wa debe na uongo wa uwazi .Huu mwandishi na yeye katumwa kutumwagia uongo kama amavyodai kuna mtu kahama Chama katumwa ama ana andika kwa manufaa yake.Hii habari inaonyesha jinsi gani Salva alivyo tumwa lakini uongo mwingi sana katika hii habari yake .Hapa si mahala pa kuleta mawazo ya kutumwa .Yaani huyu anamtetea Rostam? Ama kweli Tanzania na waganga njaa .
 
Augustine Moshi,

Kumbe sikujua kama wewe ni mmoja kati ya wale waitwao:- Ambao kwamba.
Wee unataka kujua kama mimi msomi ili ufanye nini?..
Yaani ungejua kwamba pumba unazoandika humu hata huo usomi wako unatia wasiwasi sana. Na ikiwa kweli wewe mwalimu basi wanafunzi wako wana hatari kubwa, kambutas watupu!
Hapa tunazungumzia ubaguzi wa kidini na huwezi kufananisha kila kitu kwa mtazamo wako na hasa swala la dini linapohusika. Wanawake huchaguliwa bila kujali dini zao kwa sababu wanawake ni moja kati ya wanyonge wanaohitaji kupewa nafasi.
Hakuna kitu kinachoitwa usawa wa kidini ktk mazingira yoyote yale ya siasa na Tanzania peke yake itakuwa nchi ya kwanza duniani kuleta habari za usawa wa dini. Kama Nyerere alivyosema dini ni imani kesho mtu unaweza kubadilisha dini yako. Najua Waarabu na Wayahudi peke yao na ni asilimia 100... hakuna cha kuweka mtu kuwakilisha kundi la dini ktk siasa. Labda hufahamu hata sababu za kuchagua hao viongozi ndani ya nafasi hizi.
Haya kwa kukatisha hoja zako nambie nchi gani hapa duniani ambayo inafuata mfumo huo wa kuchagua viongozi wao kufuata imani za dini.
Wewe, msomi nipe hiyo!
 
Wanabodi ,

Naona kama kawaida yetu watanzania hatuna mazoea ya kushindana kwa nguvu ya hoja , badala yake tunakimbilia kwenye ishu personal za kudhalilishana kwa kusema wewe sio msomi na kutukana professional za watu . Hii yote inaonyesha ni jinsi gani tulivyo endelea.

Huyo mwandishi Rweyemamu ni mtu mwenye uwezo mdogo sana wa kuchambua mambo na mara nyingi hataishia huko huko kwenye magazeti yao ya mitaani , tafadhali kama kuna mtu ataweza ninaomba sana mumualike hapa . Kwanza jinsi alivyojenga hoja zake ni kichekesho kitupu hivi kweli huyu mwandishi anafanya critical reasoning kabla ya kuandika pumba zake ?

Suala la kujali uwiano wa dini au makabila katika position mbali mbali ni suala muhimu sana katika kujenga serikali itayokuwa inawajumuisha wananchi wote . Huwezi kusema kuwa vigezo katika kumchagua viongozi wetu ni elimu zao tuu ...Huku kutakuwa ni kujidanganya ! Pili ni muhimu kutambua each case is dfferent , aimaanishi kila jambo linalofanywa na marekani lazima na sisi tulifanye .Hizi case ni tofauti kabisa ni sawa sawa na kufananisha Kunguru na meza.

Mkandara umesema kwamba Mkapa alichagua mabalozi sita wakristo , jee unaweza kutusaidia majina yao ?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom