Kwanini baadhi ya viongozi wa dini Elimu zao ni ndogo?

Kwanini baadhi ya viongozi wa dini Elimu zao ni ndogo?

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,625
Reaction score
27,440
Awamu hii nimejiona ufinyu wa akili za baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu, ufahamu na uelewa wao ni tatizo kubwa kwa watu ambao wanawaongoza; kwamba RAISI akiwa Muislamu, akifanya makosa asielezwe kwa kigezo cha dini?

WAKRISTO hawajaanza kukosoa leo, TUNDU LISU alipigwa risasi kwenye utawala wa Rais muislamu? Godbless Lema na mwenzie EZEKIA DIBOGO WENJE, walikuwa wakimbizi kwenye utawala wa RAISI muislamu?

Waislamu hawa hawa wamesahau kuwa wakati wa utawala wa Hayati Mkapa, wahadhiri wa kiislamu walizunguka Nchini kusema kuwa, "CCM NI CATHOLIC CHURCH MOVEMENT" lengo ikiwa watu waichague CUF ya IBRAHIMU HARUNA LIPUMBA, na marehemu, MAALIM SEIF SHARIFU HAMAD, kwa sababu wao ni waislamu.

Mpaka Sheikh Mohammed Isa wa SHINYANGA amewahi kutukusanya Pale THAQAAFA Mwanza kueleza mambo hayo.

Wakati DR. WILLBROD SILAA, anagombea kiti cha URAIS, kwa tiketi ya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) wahadhiri wa kiislamu akiwemo marehemu HUSSEIN MSOPA (SHEIKH SHARIFU MAJINI) walizunguka Nchi nzima kuwahamasisha waislamu wasimpe kura Padre kura, wampe DR. JAKAYA KHALIFANI MRISHO KIKWETE kupitia Chama kile kile ambacho waliikita Catholic church movement, yaani CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) watu hao waliobadili maana halisi ya Chama cha CCM wakageuka tena wema, kisa anayegombea ni muislamu mwenzao.

Mpaka LIPUMBA, akiwa msikitini, pamoja na SHEIKH KUNDECHA, na marehemu, Baswalehe, wakawa na mtazamo wa LIPUMBA kuwa mgonbea wa Waislamu mwaka 2015, ndiyo maana baada ya kuwepo kwa Ukawa, mgombea akawa Hayati EDWARD NGOYAYI LOWASA, LIPUMBA akajiondoa, maana malengo yao hayakutumia.

Sasa mnapokuja kuleta mambo ya Udini, nani mdini? Nchi ni yetu sote, hakuna muislamu, Mkristo wala mpagani, RAIS akifanya makosa akosolewe sio kwa misingi ya DINI, bali KISIASA.

SHEIKH PONDA ISA PONDA, alikuwa na mgogoro sana na Kikwete muislamu mwenzie, huyu hajawahi kuwa mdini, nitampa pongezi RAIS sio kwa sababu ya dini yake, bali kwa kazi njema anayofanya, TUACHE UDINI kwenye mambo ya KITAIFA.

Anaandika Rafiki yangu Abel
 
Kwahili na kuunga mkono ila sio viongozi tu wa dini ya kiislamu, hata madhebu mengine cardinal Pengo alikua Bega kwa benga na magifuri licha yakua magufuri aliuua watu wengi, na wakuristo wengi makada wa chama bado wanasupport chama cha wauuaji bila kujali, na wengine wamechaguliwa bila kukata uteuzi wao, mkuu jitahidi kubalace story yako, usionyeshe chuki ya upande moja.
 
ITIKAD KALI AKILI ZAO ZIMEWEKWA HOSTAGE.

NDIO MAANA COMMENTS ZAO HAPA ZINAPROVE AKILI NA TAFAKURI ZAO ZIMETEKWA NA UJINGA WA ITIKADI YAO.

THUS HAWAWEZI KUJA NA KITU MTAMBUKA CHA KUENDANA NA MCHAKATO WA TAFAKURI YAO.

Eti ndugu Covax gallow bird Dume la Dar Shanily kipi kitukufu zaidi, kutokula nguruwe au kulinda uhai wa asie itikadi kali, 🤣🤣 mnajua jibu lake ndio maana nawaambia tafakuri yenu sio ya utashi binafsi bali itikadi uchwara consciousness.

Karibuni mnitukane

🚮🚮🚮🚮
 
Mkianza usenge wenu wa udini ndo hapo nawaona wapumbavu kwani wale walokufa kwenye maandamano unaweza sema wakristo tupu? Au watanzania?

Acha usenge na utumwa wa dini, wenye akil tunajua kwamba wanaosapot wote wamekua compromised tatzo sio dini wala elimu bali njaa zao.

Kwan huko serikalni hakuna wakristo, hakuna mapadre na wachungaj wapo upande wa serkali?

Acha usenge wako wewe kafir mbobevu, hichi ni kipind cha kuunganisha nguvu iwe kafir iwe kobaz lengo ni Moja tu.
Haya matusi ulitakiwa kuwatukana pia Masheikh wako wa Bakwata ambao hawataki kusikia TEC wakikemea maovu yanayofanywa na serikali kwa kisingizio Rais ni Muislam!
 
Kwahiyo tukusaidieje labda!?.
Acheni kuwatumia vibaya Masheikh wa Bakwata kwenye propaganda zenu za udini, huku mkiwadanya kwa kuwalisha ubwabwa! Kama kweli mnajielewa, jaribuni kwanza kuwatumia wale Masheikh wa Shura ya Maimam! Halafu tuone.
 
Awamu hii nimejiona ufinyu wa akili za baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu, ufahamu na uelewa wao ni tatizo kubwa kwa watu ambao wanawaongoza; kwamba RAISI akiwa Muislamu, akifanya makosa asielezwe kwa kigezo cha dini?

Elimu unayoiongelea wewe ni Elimu ipi ?

Mtu kama muadilifu ukiwasikiliza viongozi wa kiislamu walio ongea wako makini na wameelezea mambo kielimu na utulivu kuliko hao mnao wataja wana Elimu.

Kingine kama wao Maaskofu wana Elimu, watuambie kwa mujibu wa mafundisho ya Yesu, kiongozi akiwa muovu wanatakiwa wafanye nini au ukosoaji wake unatakiwa uweje ?

Kingine hakuna kiongozi yoyote wa Kikristo mwenye uwezo wa kuwasilisha jambo kwa ufasaha na ustadi na kujenga hoja kuwazidi hao masheikh walio zungumza, japokuwa wana madhaifu yao.
 
WAKRISTO hawajaanza kukosoa leo, TUNDU LISU alipigwa risasi kwenye utawala wa Rais muislamu? Godbless Lema na mwenzie EZEKIA DIBOGO WENJE, walikuwa wakimbizi kwenye utawala wa RAISI muislamu?

Sifa ya Wakristo ni kutokuwa waadilifu, Sasa unajiita vipi una Elimu au msomi na hutendi uadilifu katika uwasilishaji wa jambo lako. Elimu kama haikufundishi uadilifu hayo ni kama mavi tu.
 
Elimu ni nini labda Tunakosea sana kuhusisha mavyeti na Elimu, Babu zetu walikuwa hawajaenda hizo formal schools ila kwa uelewa wao walikuwa head above shoulders kwa upuuzi mwingi unaoendelea sasa hivi on both sides....; Na kuhamia kwenye vijembe vya Elimu ni kutoka kwenye reli - Tujikite kuwabana wauwaji

 
Sifa ya Wakristo ni kutokuwa waadilifu, Sasa unajiita vipi una Elimu au msomi na hutendi uadilifu katika uwasilishaji wa jambo lako. Elimu kama haikufundishi uadilifu hayo ni kama mavi tu.
Uadilifu na dini, wapi na wapi! Je, Chura Kiziwi ni Mkristo? Na kama siyo mkristo, pale alipo ana uadilifu gani?
 
Uadilifu na dini, wapi na wapi! Je, Chura Kiziwi ni Mkristo? Na kama siyo mkristo, pale alipo ana uadilifu gani?

Uadilifu na dini ni vitu visivyoachana.

Mitume na manabii wote walitumwa kwa ajili ya kutenda uadilifu. Sasa kama dini yenu haiwafundishi uadilifu na mnajiita wasomi huko ni kuikosea adabu Elimu.
 
Uadilifu na dini ni vitu visivyoachana.

Mitume na manabii wote walitumwa kwa ajili ya kutenda uadilifu. Sasa kama dini yenu haiwafundishi uadilifu na mnajiita wasomi huko ni kuikosea adabu Elimu.
Ila hujanijibu swali langu la msingi! Narudia tena; Je, Samia naye ni mkristo? Na kama ni Muislam! je, ni muadilifu?
 
Back
Top Bottom