Wasi Wasi wa Udini

Status
Not open for further replies.
Rufiji,
Shukran kwa kuuliza isipokuwa tu nadhani hata wewe umeisha weka imani yako kutazama upande huo wa uwiano wa dini na makabila ktk kuchagua nafasi za watu serikalini.
Binafsi nalipinga na nadhani nimeeleza vya kutosha huko nyuma na yaonyesha wazi siwezi kubadilisha mtazamo wenu.
Utanisamehe kwa lugha niliyotoa kwa ndugu Augustine kwani haikuwa kabisa madhumuni ya hoja nzima isipokuwa niliweka timu ya mpira kwa makusudio ya kwamba kuna vitu ambavyo huwezi kabisa kutumia dini kuleta uwiano hasa pale ambapo hakuna ubaguzi. Na kama hamjaelewa hivyo basi itakuwa kazi kubwa. Sijui itakuwaje siku tukisikia Sheikh fulani anagoikmbea urais kama Mtikila.
Kuhusu hiyo list ya mabalozi nadhani unaweza ipata wizara ya mabo ya nje ama pitia balozi wote wa Tanzania nje kisha ondoa hao sita wapya! Waliobaki na wengine mawaziri leo hii warudishe Ubalozini mtapata hesabu kamili.
sasa huu ndio udini wenyewe maanake tunaanza kuhesabu vidole kuona huo uwiano wenu wa DINI ya mtumishi wa taifa.
 
Mkandara
Kwa kweli huwa sikuelewi kabisa tukianza kuzungumzia mambo ya dini, labda kuna mtu mwingine humu anieleweshe unaongelea nini. Wala sioni jambo la kujibu. Umefikia kiwango cha kuwatukana hadi wanafunzi wa Moshi hapo tumefika mbali. Moshi anafundisha hesabu, hesabu hazina uongo ama unajua au hujui na kama unajua unatakiwa u-prove hasa katika kiwango cha elimu ya juu.
Kwanza kabla sijaendelea Mtikila hajawahi kugombea uraisi, sielewi kabisa ni kitu gani ulikuwa unataka kusema au kuonyesha wanabodi.
Tuachane na hayo, unaposema utajiwe nchi ambazo zinatumia uwiano wa dini katika kujaza nafasi za kuteuliwa sijui unataka mfano gani. Achana na Vatican, Tanzania yetu serikali inaundwa kwa kuzingatia dini, ukabila, na jinsia ndiyo maana unaona tuna amani mpaka leo. BWM amefanya hivyo na ushahidi upo. Angalia Iraq ilimchukua muda gani mpaka Waziri Mkuu akaweza kupata mawaziri wale watatu kwa wizara muhimu za ulinzi? Unaweza kuniambia ni kwa nini? Mimi binafsi nisingependa kuona huu utaratibu huu but you can no stop people from thinking. Someone who can not think is the fucken dead meat. That's means you have to kill people ili uweze kutawala unavyotaka wewe Mkandara. Kama hautakuwa tayari kuua watu basi utawaua kwa lazima kama Mwembechai kwa maana kuna watu watachukua majambia kupigana kwa risasi hasa ukizingatia walio wengi wana elimu ya madrasa ambayo itawaweka nje katika uongozi. As a leader who have to consider wenye elimu hiyo kwa uwiano ambao utaleta amani na kutozoletesha uchumi wa nchi. Nitakubaliana na wewe kama ukisema watanzania hatuna udini kama unavyoongelewa hivi sasa, kwa sababu in the streets wote tunakula kitimoto na tende wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
Kama nilivyosema hapo mwanzoni, kama raisi akiamua aongeze idadi ya uongozi kwa kundi fulani katika jamii lazima ahakikishe anateua wale walio-qualify na kazi. Achana na uongozi wa Chama, hayo ni mambo ya kichama Mzee ES ndiye anaruhusiwa kuongelea kwani yeye ni mwanachama, position kama ubalozi akiteua mtu ambaye ana ufahamu mzuri wa foreign affairs na International Relations hakuna mtu atakaye fungua domo. Dr. Mahiga ni mfano wa mabalozi tunaowataka. Huwezi kuamini hadi UDSM wanafundishwa Internation Relations lakini hao watu wanaenda wapi? Toka uhuru nafasi ya ubalozi imekuwa ya kisiasa na kuwapoza watu wanaokusa ubunge au uwaziri lazima tufike mahali tuseme sasa basi mtu tunayempeleka kwenye nchi kama Uingereza lazima awe na elimu ya jinsi ya kuwasiliana na wenzake kitaaluma. Kwa mfano leo hii mtu ambaye ni "sex addict" ukaniambia nimsaidie kitaaluma nitaishia kukazana naye tu. Samahani Mh. Spika napenda kutoa hoja.
 
Sam,
Kusema kweli wewe ndiye uliyezungumza vitu vya ajabu. maelezo mengi na marefu yanayojichanganya.

Unapozungumzia siasa na nafasi za kazi umesema ni lazima tutazame dini, ukabila na hata jinsia kabla ya kufanya maamuzi. Hapa ukiwa na maana tulete uwiano wa vitu hivi. Lakini unapofikia swala la ramadhani umechagua kula Kitimoto... hapo hakuna uwiano na waislaam bali wakristu....We chose to ignore muslims faith.
kwa hiyo umerudi kwangu kwamba kuna vitu havina haja ya kutazama dini ila matakwa ya wananchi kwa ujumla kama Watanzania.
Swala la Iraq limetokana na uonevu wa kidni toka Saadam na Tanzania hatujawa na hali hiyo. Hujanitakia nchi yenye mfumo huo na imefanikiwa kuleta huo uwiano wa kidini kwani sio Tanzania pekee yenye dini mbili kubwa.
Tatu, sheria ndizo zinazompinga Mtikila lakini kisha pigania kutaka kugombea kiti cha Urais na kuahidi kutupa mapesa wananchi wote mwaka 1995. Vurugu la kuwapiga na kuwaita wahindi MAGABACHOLI alizianzisha yeye. I was in Dar my brother, pale Mnazi mmoja palijaa watu utafikiri mkutano wa Uhuru....
 
Asanteni sana wachangiaji wote. Nafurahi kuona kwamba haja ya kuzungumzia hili jambo imekubalika na wengi.

Uwiano tunaozungumzia katika teuzi za kisiasa haumaanishi idadi sawa kila mara. Hatuna maana kwamba Rais akichagua mawaziri achague nusu wanaume na nusu wanawake, nusu Waislamu na nusu Wakristu, na kila mkoa upate idadi sawa.

Maana yetu ni kwamba rais anapofanya teuzi zake za vingozi wa kisiasa asilete hisia za upendeleo wa kidini, kijinsia au kijiografia. Kuwe na idadi inayoridhisha ya Watanzania wa jinsia zote, wa dini zote na wa sehemu zote za nchi. Hivyo ndivyo alivyokuwa anafanya Mwalimu, na hili lilileta umoja nchini kwetu.

Rweyemamu ametumia logic ya hali ya chini sana. Amesema JK amechaguliwa na kukubalika na watu wa dini zote, kwa hivyo hawezi kutumia udini. In Logic we say: Non sequitur (It does not follow).

Rweyemamu ameandika: Ni watu wapumbavu ndio wanadhani Rais anawajibika kuchunguza dini na kabila za watu kabla hajawateua. Si watu wapumbavu, ni sisi watu wa kawaida kabisa. Ili kuwa na uwiano mzuri katika teuzi zake, ni lazima Rais atachunguza mambo hayo. Rais anajua kwamba hawezi kuteua mawaziri wote Wakristu. Sio upumbavu anapoangalia ateuwe pia baadhi yao wawe Waislamu. Lazima anaangali jinsia ya wateule wake vile vile, n.k.

Katika kuzidi kuonyesha ufinyu wa logic, Rweyemamu anaandika kwamba aliyeteuliwa kuwa Balozi wetu London ana sifa kubwa ya Uwakili. Sasa kwa nini hakuteuliwa kuwa Jaji? Huo Ubalozi London unataka mtu mwenye sifa kubwa ya Ubalozi, sio ya Uwakili tu.

Naomba tuwe makini katika logic. Haitoshi tu kuandika Kiswahili kizuri, na kuchomekea neno pumbavu, from time to time, kama pambo.

Augustine Moshi
 
Mkandara
Hakuna sheria ambayo inamzuia Mtikila kugombea urais, ana chama cha siasa DP ambacho kimesajiriwa kihalani. Labda tueleze ni sheria gani inamzuia Mtikila asigombee uraisi.
Mimi sina comments zaidi sidhani kama tunaweza kuelewana kwenye hili jambo.

peace
 
Sam,
Kusema kweli nashindwa kabisa kuwaelewa watu nyie.
WEWE ndiye ulisema MTIKILA hajawahi kugombea urais, nikakujibu kesha wahi sasa tena umegeuza dau nakuwa swala sio Mktikila kutogombea ila sheria.
Well, nilikujibu haraka kwa sababu naelewa mwaka 1995 kulikuwa na sheria za mgombea kuwa na chama cha kisiasa na sio mgombea binafsi pia mgombea akiwa kesha fungwa jela haruhusiwi. Kulikuwepo pia swala la mawakala au kitu kama idadi fulani ya wafadhili ama wabunge sina hakika lakini. Nakumbuka Mtikila alipeleka kesi yake mahakamani na CCM walijaribu kila njia kumsimamisha. Kifupi Mtikila kagombea urais kama nilivyosema awali na wewe ulipinga.
Swala hapa sio Mtikila kwani nilitoa hoja ya kuwepo kwa muislaam ktk kugombania urais, sijui hili litaonekana vipi kwenu.
Sam,
maneno yenu yote yanaweza kuwa na point lakini mnafikiri kwa kutumia imani zenu za dini yaani mnavyotaka wakristu nyie sio swala la Watanzania. Nitakubali sana mawazo yenu ikiwa udini umesha simama na mimi naamini kabisa nchi yeyote inayoingiza dini ama kabila ktk siasa huwa haina mwisho mzuri. Iraq wakati wa Saadam walikuwa dini moja kushika nchi nzima... hatari. Leo hii wametumia dini kuigawa Iraq kwa kufikiria wanaleta uwiano ndio hatari zaidi. Sababu kubwa ya kushindikana yote haya ni kuwa nchi hiyo tayari ilisha jenga tabaka za kidini kifikra na hii ndiyo hatari mnayoikaribisha.
NI vibaya kwa rais pia kuchagua watu kwa dini zao maana hii inakaribbisha cheche za Udini lakini tukiangalia mfano wa JK hauna Udini zaidi ya kwamba ni watu 6 kati ya mabalozi 22 waliobadilishwa na kupitia vyombo vyenu hivyo mmechambua kipande hiki na kukiweka mbele hali mabalozi wote nchini wana dini tofauti.
Mshikaji usije chukuliwa na wewe na huu udini kwani nasikia siku hizi Bongo dini ndio zinatawala mazungumzo ya watu. Sijaona nchi yenye demokrasia ikatawaliwa na dini isipokuwa zile zinazo amini dini kuwa msingi wa maendeleo ya watu wake.
Kesho tutakuja sikia waislaam wakidai Ijumaa pia iwe weekend kwa nini Sunday. These are just days wewe chukulia weekend ni siku ya mapumziko lakini ukisha anza kui-question sunday mshikaji ndio Udini huo. Na huwezi kuwaridhisha watu wote mahala hakuna udini.
Kuhusu Augustine, wewe hukuona alivyo-question elimu yangu kwa sababu ni mkristu mwenzako lakini nilipo-question knowledge yake imekuwa nongwa kwa sababu tu nipo upande wa pili. Mbona hukumuuliza kwa nini anataka kujua elimu yangu!
Hivi kufahamu Udini tunatumia elimu gani?
Mshikaji hata huko sipo mimi kafiri tu mhuni wa mtaani na wala sikusoma, lakini nafahamu 2+2 haiwezi kuwa 22.
 
Hizi ni takwimu zilizopostiwa kwenye podcast (mwanakijiji.podomatic.com) na mtu ajiitaye Salum Ahmed (nimemwomba anipatie majina):-

Unapo mtuhumu Kikwete kuwa anapendelea Waislam ni vizuri mtu ukatoa na takwimu sio malalamiko yasiye yakuwa na takwimu!

Baraza la Mawaziri full mimister 30 (hii haijumlishiki.. Mwanakijiji)
14 waislam
14 wakristo

Manaibu mawaziri 31

11 waislam
20 wakristo

Makatibu wakuu 28

7 waislam
21 wakristo

Naibu Makatibu wakuu 14

3 Waislam

11 Wakristo

Wakuu wa mkoa

13 Wakristo

8 Waislam
 
Mzee Mwanakijiji mimi bado naoina giza nene mbele .Kwa kuwa watu wote ambayo tunawaongelea ni viongozi wa Watanzania , na kaa umeweza kupata idadi yao ina maana unaweza kupata majina yao pia .Tafadhali endelea kutusaidia lete majina hapa.Mawaziri 30 lakini nimeshindwa hesabu zake jamaa.

Naomba tuleteeni majina na mikoa waliyopo tuwekane sawa hapa si dhambi kupeana fact maana sote tunataka suluhu na hil jambo.

Makatibu wakuu wako majina tunaomba pia .Manaibu waziri wapo majina tunaomba .Baada ya hapo tutaangalia teuzi zingine za tume na pia teuzi Wakurugenzi nk .

Hii yote ina nia njema weken data hapa tuanze mjadala badala ya kuweka figure tu .Taja wizara ama mkoa nk ili kuwekana sawa .
 
Deputy Ministers and Their Respective Ministries


Prime Minister’s Office

Disaster and HIV/AIDS
Hon. Dr. Luka Jelas Siyame

Regional Administration and Local Government
Hon. Celina Ompeshi Kombani

Foreign Affairs and International Co-operation
Hon. Seif Ali Iddi
Hon . Dr. Cyril August Chami

East African Co-operation
Hon. Dr. Diodorus Buberwa Kamala

Finance
Hon. Abdisalaam Issa Khatib


Hon. Mustafa Haidi Mkulo

Planning, Economy and Empowerment
Hon. Salome Joseph Mbatia

Industry, Trade and Marketing
Hon. Dr. David Mathayo David

Agriculture, Food Security and Co-operatives
Hon. Christopher Kajoro Chizza

Energy and Minerals
Hon. Lawrence Kego Masha

Infrastructure Development
Hon. Dr. Maua Abeid Daftari
Hon. Dr. Milton Makongoro Mahanga

Health and Social Welfare
Hon. Dr. Aisha Omar Kigoda

Education and Vocational Training
Hon. Mwantumu Bakari Mahiza
Hon. Ludovick John Mwananzila

Higher Education, Science and Technology
Hon. Gaudensia Mugosi Kabaka

Labour, Employment, and Youth Development
Hon . Jeremia Solomon Sumari
Hon. Daniel Nicodem Nsanzungwako

Lands, Housing and Human Settlements Development
Hon.Rita Louise Mlaki

Community Development, Gender and Children
Hon. Dr. Batilda Salha Burian

Public Safety and Security
Hon. Mohamed Aboud

Home Affairs
Hon. Bernard Kamillius Membe

Livestock Development
Hon. Dr. Charles Ogessa Mlingwa

Natural Resources and Tourism
Hon. Zabein Muhaji Mhita

Information, Culture and Sports
Hon. Dr. Emmanuel John Nchimbi
Hon. Joel Nkaya Bendera

Justice and Constitutional Affairs
Hon. Mathias Meinrad Chikawe

Defence and National Service
Hon. Omar Yussuf Mzee



For
 
Wanabodi ,

Nadhani watu mnataka kuharibu hii mada , wachangiaji wengi hawakuwa na lengo la kutaka kujua kuna waislamu wangapi mawaziri na wakristo wangapi ! Sual hili limenza ghafla baada ya JK kuchagua mabalozi sita.

Mimi binafsi , hata siku moja sijawahi kufikiri katika masuala haya ya dini ila baada ya uchaguzi wa hawa mabalozi hayo maswali yalinijia ,kama mtu atasema mimi ni mdini kwa kufanya hivyo then let it be ! Katika kipindi cha kampeni ya urais nilikuwa na hasira sana na maaskofu kwa kitendo chao cha kumindorse JK na niliyasema haya kule BCS ambapo niliweka wazi ya kuwa kitendo kile ni cha kishenzi na kina lengo cha kutuharibia uchaguzi wetu , kwani niliamini ya kuwa viongozi wa dini hawatakiwi kuwa na influence kwenye uchaguzi wetu .

Kipindi chote cha kampeni hakuna mtu hata mmoja aliyegusia suala la dini na hata ukiangalia ushindi wa JK auna uwiano na imani yoyote ya dini , kwani watu hawakutumia dini kama kigezo katika kumchagua ! Sasa tunapoona watu ghafla wanazungumzia tetesi za kuwepo udini then we have to ask ourselves kwa nini ? Suala la kukaa chini na ku-ignore autasaidia kitu , hata kama unahisi huyo mtu ni mjinga basi kaa chini na umwonyeshe ujinga wake !

Suala la watu kukurupuka kama Rweyemamu na kuwalabel wakristo ni wadini na wanaona gere kwa waislamu wamechaguliwa kwenye nafasi za uongozi hizi ni hoja zenye mtazamo wa chini sana........... kama kweli hawa watu ni wa dini kwa nini walimchagua JK at the first place ?

Tafadhali kama kuna mtu ana contact za rweyemamu naomba aziweke hapa .
 
Rufiji nadhani nakubaliana nawe kwa kuwa kuna watu wanavuta chao na wanaanza kutuvuruga sisi.Huyu Rweyemamu katoa habari za uongo sana .JK ana mtu anamwita Akukwetu ambaye yeye watu wasisema akaona watasema hadi Ubaya wa Serikali yao basi anaomba ushahidi kumzima sasa aje amzime Rweyemamu na uongo huu.

Swala Maaskofu mimi nilisha liona tangia mwaka 1995.Kadinali Pengo alikuwa anatoa matamshi ambayo yalionekana sana na wazi kuiunga CCM mkono .Huyu ni Mkatoliki ambaye anamekunywa maji ya bendera ya CCM.Uchaguzi wa mwaka jamna chuki zilizidi zaidi na hasa dhidi ya CUF.Nasema kama kuna siku CUF watasimama mahakani kupambana na Mahita basi lazima na Kanisa liwemo maana hotuba za Maaskofu wake zilikuwa mbaya na za ubaguzi na tuhuma ambazo hazina maana .

Mimi ni mkatoliki wa kuzaliwa lakini sikupenda jinsi walivyo kuwa wanakisema Chama cha CUF ni ubaguzi wa wazi ule .Kwa watu ambao hawana muono wa mbele kama wakristo wa kawaida na hasa wa Kanisa katoliki maneno yale ya Maaskofu basi yanawapa nguvu za kuchagua mapenzi ya Askofu na si wao .

Kanisa Katoliki lina mzigo mkubwa sana na kazi kwa waumini wake lakinji hawafanyi kazi kwa uaminifu wana ingilia siasa ambazo si sehemu yao .Wao kama Kanisa wana haki ya kuongelea maovu ya wanasiasa lakini si kutumia nafasi ya kuwagawa wananchi .Seikali haina dini ila watu wake wana dini zao .

Siasa mbaya kwenye Nchi ina maana maisha mabaya .Kila mara utaona watawa wamejifungia kwenye magari yenye AC hapo Dar ama mikoani wanakula raha lakini waumini wao wanakufa kwa njaa na malaria hawafanyi lolote ila kuwaombea kwenda kaburini nasema Rweyemamu uache mara moja hii tabia na Kanisa Katoliki pia .

Mbona hao maaskofu hawa hoji Kuuzwa KIA kwa pesa ndogo ? NIC ? NSSF na kashfa kubwa ? Mbuga kuuuzwa ? Mbona hawahoji mikataba ambayo hata sasa hatujui JK anawaza nini ? Mbona hawa hoji JK kumtumia Akukweti kuzima Sauti za watu Bungeni ??
 
Mkandara,
Kwanza, natumaini utaendeleza urafiki wetu tulioujenga behind the Internet for long time ingawa mimi na wewe huwa tunakubaliana kwenye mambo machache sana. It is very understandable for matured men.
Sielewi unaposema mgombea urais unamaanisha nini, ninavyojua mimi Kigoda hajawahi kuwa mgombea uraisi ila amewahi kuonesha nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania the same applied to Mtikila. Tatizo la Mtikila alikuwa anataka kugombea urais wa Tanganyika kama mgombea binafsi bila chama cha siasa.
Kuhusu ukristo, nilisha wahi kwenda kwenye forum moja nilijaribu kuwaelewesha watu kuhusu dini na ukristo mpaka naondoka hakuna aliyenielewa. Ukichukulia maana na ukristo pengine kwenye baraza zima la mawaziri hakuna mkristo, ndiyo maana mara nyingi tunachukulia mtu mwenye jina la kikristo ni mkristo kitu ambacho siyo kweli. Na Roman Catholic is more an empire than a church kama watu wengi wanavyofikiria na waislamu wengi wanajua mkristo yoyote ni Roman Catholic, which is 100% wrong. Hata kwenye discussion hii tunachukulia watu wenye majina ya kikristo tukiingia ndani zaidi tunaweza kuchanganyana.
Kama nilivyosema awali, inawezekana JK hakutumia udini wala hakufikiria hivyo katika uteuzi wa hao watu. Kwa nchi kama Tanzania ambambo tumeshashuhudia watu wakiuliwa kama kuku na risasi za moto Mwembechai na Zanzibar kwa ajiri ya mambo ya dini huwezi kuniambia kuwa rais asiangalie udini 100% katika uteuzi wake nikakubaliana na wewe. Ni nini tena mkandara unataka zaidi ya hayo matukio ya kinyama? Ndiyo, wote tunakubaliana kuwa watu wangekuwa wanateuliwa kwa uwezo wao wa kazi, ndiyo hicho ndiyo kigezo kikubwa lakini wakati huo huo wananchi wana mawazo ya udini vichwani mwao. what should we do? We can not never stop people from thinking. Solution ya kwanza kama ningekuwa raisi ni kuteua watu ambao wana uwezo wa kufanya kazi na kuwatumikia ipasavyo wananchi, pili kama umeshindwa kupata watu wanaofanya kazi kwa ubora wa juu uwiano wa makundi katika jamii ni kitu muhimu sana. Nadhani aliyeanzisha neno uwiano alifikiria vizuri, siyo usawa, usawa ni kitu ambacho kidogo hakiwezekani. Na hizi propaganda eti serikali haina dini sikubaliani nazo. Ni kwa nini kwenye wimbo wa taifa kuna neno Mungu? Who is Mungu anayeelezewa kwenye wimbo wa taifa. Kwa nini kwenye vikao vyote vya mbunge vinaanza na dua? Na kwenye dua hilo wanaliita Bunge tukufu? Ndiyo, hiyo dini inaweza ikawa siyo ukristo au uislamu lakini kuna imani hapo. Labda tuelezane maana ya dini ndiyo tuanzie hapo. Ni kitu kizuri kuweka neno Mungu lakini whom are we talking about? Christians beleive Jesus is GOD, are you guys talk about Jesus bungeni? Christians beleive that serikali yoyote imewekwa na Mungu. Mhh. Hapo ndipo tunapokuja na hoja kwamba you know what? Tunatakiwa tuwe na uwiano kwenye haya mambo au tusubiri kukatana mapanga.
 
Sam kwenye hili sina la kusema maana hata Udini na dini umeelezea vyema na hata majina mtu kudhaniwa ni mkiristo kwa jina lake ama Muilsma kwa jina si kweli .Ukristo ama Uislam ni matendo na ucga Mungu hawa jamaa hamchi Mungu ila wana mtukana Mungu kwa kula rushwa , kugandamiza Watanzania na kuwanyima haki .Bungeni dini na Imani yao na utiifu kwa Speaker at least ndilo naweza kusema maana sala zao bwana mimi sijui .Ila nakubaliana na point zako nyingi juu ya dini na imani .
 
Sam,
Sina beef na mtu kabisa isipokuwa lugha ya mtu hunipa hanjamu ya kurudisha lugha sio ngumi. Na hata siku moja siwezi kuondoa urafiki wangu kwa mtu kwa sababu kaeleza hofu yake ndani ya dini yangu.

Kuhusu swala hili nadhani yote haya yanayobainika sasa hivi ndiyo niliyokuwa nikisema toka mwanzo. Sikukubaliana na 2+2 kuwa 22, mabalozi 6 haiwezi kuwa hesabu ya 28. Wapo mabalozi na viongozi wengi wakristu kuliko Waislaam pia vyeo vyote vya juu, lakini hii sio hoja ikiwa hawa wote wanawakilisha Tanzania na sio kanisa. Na mara zote nimejaribu kuepa swala hili la kuhesabu vidole ili kupata jumla. WHY? kwa nini tufanye hivyo ikiwa sisi wenyewe tunadai hatuna udini. Kumbukeni TZ ni nchi isiyokuwa na dini. Hii ina maana dini zipo lakini sio mwongozo wa UMOJA wetu.
Maneno yako kuhusu wakatoliki ni sawa kabisa hata ukija kwa waislaam na umeyaona mwenyewe huko Iraq. Na kati ya viongozi wote wa serikali nadiriki kusema afadhali nyie wakristu viongozi hawa hufika makanisani na kusali ama kujishughulisha na dini. waislaam wengi ni kama mimi hapa. Waislaam jina wa kuzaliwa na sijui mara ya mwisho nimesali lini! Lakini nafaahamu lini nilikuwa na Peter ama Paul mitaani. Na trust me mengi wetu tupo karibu sana ktk kujenga urafiki, sio kwa kipimo cha dini.

Ukitaka kuondoa Udini, dawa yake ni kuifanya nchi haina dini, kama alivyofanya Nyerere kuondoa Ukabila. Alivunja kabisa uwezo wa watu kuwa - identified by kabila lake ingawa bado aliendelea kuwatumia Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa ktk vitengo muhimu. Kikubwa zaidi alihakikisha watu hawa hawawezi kuzitumia kabila zao ndani ya vitengo hivyo kwa faida ya kabila zao na aliwachanganya na watu wa makabila. Kiswahili kikawa lugha ya wote. Ukabila ukafa kifo cha nyani.
Lakini kama angejaribu kutafuta uwiano wa makabila kabla ya kujenga UMOJA wa Mtanzania tungekuwa kama Kenya ama huko west Afrika ambako wali-identify makabila makubwa na kuyapa nafasi serikalini eti kuleta uwiano hali watu hawa hawana umoja wala hawapendani. Badala yake walijenga chuki na kuzitazama position through a tribes mirror.

Kuhusu Mtikila mshikaji hata fomu za kugombea alichukua na kujiandikisha kama Mgombea. Nimesikia hata mwaka jana alichukua kwa kivuli cha chama chake sasa sijui bado tunabishana kipi hapa hali Mtikila mwenyewe sio issue. Nimesema huo ulikuwa mfano kutaka kujua mtalichukulia vipi mkisikia Sheikh fulani anagombea Urais.
Sam,
Nitasema ukweli wangu hapa kwa sababu siku zote nimemwona Mtikila kuwa na points kuliko Seif Shariff na naweza kumchagua Mtikila mbele ya Seif any given election. Simuoni Mtikila kama Mchungaji na maelezo yake ukiyasoma kwa makini hayana dini kabisa ila siasa tupu. Je, niache kumchagua Mtikila kwa sababu ni mkristu na kumchagua Seif Sharif?...
No brother, hapo mimi ndiye nitakuwa mdini sio Mtikila ambaye kamchagua Free kuwa makamu wake.
They are the only one who preach my language... Good politics.

Chie Ihunyo,
Ulikuwa wapi ndugu yangu maanake haya ndiyo maneno niliyotaka kusikia toka mwanzo. hawa jamaa tuwatazame kwa uwezo wao na ikiwa wote ni wala rushwa sio kwa sababu ni waislaam ila viongozi Watanzania wabovu hawatufai.
 
Mada yetu ni kuhusu hisia za udini. Tumekuwa tunajadiliana kuona kama teuzi za kisiasa za JK zimeleta hisia za upendeleo wa kidini. Tumelazimika kufanya hivyo kutokana na hofu yetu kwamba kama zipo hisia za aina hiyo, na kama zikiendelezwa, basi usalama wa taifa unahatarishwa.

Ndugu zangu Mugishagwe na Sam, naona mmechepuka kidogo na kushambulia Ukristu na hasa RC bila sababu ya kuridhisha. Mmeuliza Mkristu ni nani? Mkristu ni mfuasi yoyote wa Kristu. Sio lazima awe mfuasi mzuri. Hata hivyo, ni kweli msemavyo kwamba kuna lapsed Christians. They remain Christains, but of the lapsed kind.

Binadamu anaweza kuwa na dini, lakini asiifuatilie. Serikali ya demokrasia inatakiwa isifuatilie dini yoyote. Serikali haiwezi kuwa na dini, kwani ni binadmu pekee ndiye anaweza kuwa na dini.

Maaskofu wana wajibu wa kuwaonya kondoo wao kuhusu viongozi wabaya. Kwa mfano, akitokea mgombea ambaye ana sera ya kupinga baadhi ya amri za Mungu basi Maaskofu watalazimika kuwaonya kondoo wao wasimpe kura mtu huyo. Kwa mfano, mgomea ambaye atasema ana mpango wa kuweka sheria ya kuruhusu ndoa kati ya watu wa jinsia moja, au kuhalalisha utoaji mimba, ni lazima atawafanya Maaskofu kuwaasa kondoo wao wasimchague.

Shutuma za Mugishagwe kwamba wafanyakazi wa Kanisa wanafurahia tu maisha na hawasaidii watu sio za kweli. Wote tunajua huduma kuu za elimu na afya ambazo hutolewa na Kanisa. Vile vile, watu wasiojiweza, wakoma, yatima, n.k. wamekuwa wanahudumiwa na Kansia zaidi ya hata serikali. Mother Teresa wa Calcuta ni kielelezo kizuri cha upeo ambao watawa (ambao wameshutumiwa na Mugishagwe) wanaweza kufikia katika kujitolea kwa kuhudumia wale ambao jumuiya imewaacha wateseke. Bahati nzuri watawa wa Mother Teresa wako Tanzania, na wanafanya kazi nzito kimya kimya. Mshahara wao ni dharau kama hizi za Mugishagwe.

Ni tumaini langu kwamba tutaweza kurudi kwenye mada baada ya hapa.

Augustine Moshi
 
Ndugu Moshi
Kwanza naomba usipotoshe wanabodi, there is no such a thing "lapsed Christians", there is "lapsed Catholic". That is one of the differences betweem Catholic "The Empire" and other dominions. Catholic does not means christians. Give me a Break! Na mkristo siyo mtu anayemfuata Yesu tu, Mkristo ni mtu anayefuata mafundisho ya Yesu. Ukristo siyo jina la kikristo au kwenda kanisani au kusali rozali, hata wachawi wanaenda makanisani usiku wanaua watu na kusali rozali. Can we can them christians? Nashangaa unawatetea viongozi wa kanisa, there are just human beings for GOD sake. I am sorry, I hate them like a morning "sheet metal". Wengi wao wanashindia kuiba sadaka, kufira watoto wadogo, na kufirana wao kwa wao na kudai eti Mungu hakukataza mpaka dini tukufu inaonekana kama kundi la watu wendawazimu na mashetani kitu ambacho siyo kweli. Pamoja na discussion lote hili nashangaa hujui maana ya serikali. Unaposema Serikali haina dini ila watu ndiyo wana dini, hivi naomba nieleweshe vizuri wewe una define vipi serikali. Serikali siyo object eti uende dodoma ukaone serikali ya kijani na njano. Serikali inaundwa na watu ambao wameamua kufuata sheria au utaratibu fulani wa maisha kwa pamoja. Najua kuna watu wengi wanashindwa kutofautisha viongozi wa serikali na serikali lakini bottom like serikali ni watu.
Nadhani hii issue imefika mwisho naona tunaanza kutoka, nadhani wahusika wameshasikia tuliyoyasema na kwa busara za na heshima waliyopewa na watanzania wanaweza kuchambua zipi pumba na mchele ni upi na kufanyia kazi maneno ya watanzania fukara wanaopenda amani.
 
Sam,

Naona umesoma mchango wangu kwa hasira, kwani kwa kawaida huwa una michango iliyoandaliwa vizuri sana.

Umeandika: Kwanza naomba usipotoshe wanabodi, there is no such a thing "lapsed Christians", there is "lapsed Catholic".

Mtu yoyote aliyekuwa anamfuasa Kristu na sasa ameacha, ni lapsed Christian. Wako, tena wengi tu. All practicing Catholics are Christians, but there are many Christians who are not Catholic. You need not agree with this, but it is true nonetheless.

Umeandika: Catholic does not means christians. Give me a Break!

Bila shaka umekasirika ndio maana ukadhani kuna mtu amesema Catholic means Christian. We are slightly better informed than that.

Umeandika: Na mkristo siyo mtu anayemfuata Yesu tu, Mkristo ni mtu anayefuata mafundisho ya Yesu.

Sikusema Mkristu ni mtu anayemfuata Yesu. Nimesema Mkristu ni mtu anayemfuasa Yesu. Naamini unaelewa tofauti iliyopo. Amfuate Yesu wapi? Anamfuasa.

Umeandika: Nashangaa unawatetea viongozi wa kanisa, there are just human beings for GOD sake. I am sorry, I hate them like a morning "sheet metal".

Unamfuasa Yesu kweli? Kumbuka alisema kwamba tutawatambua wafuasi wake kutokana na upendo wao. Do not judge (Yesu alikataza). Huna haki kusema viongozi wa Kanisa wana dhambi na wewe huna.

Kanisa unalolishutumu linaongozwa na Yesu mwenyewe, kwa hivyo usihangake kulidhoofisha kwani hutaweza. Kama lina wadhambi, basi kwa vile wewe huna dhambi basi chukia dhambi yao, lakini usiwachukie wenyewe. Au utatenda dhambi kubwa kabisa.

Umeandika: Pamoja na discussion lote hili nashangaa hujui maana ya serikali. Unaposema Serikali haina dini ila watu ndiyo wana dini, hivi naomba nieleweshe vizuri wewe una define vipi serikali.

Serikali huundwa na watu. Serikali sio watu; ni umoja wa taasisi zinazoundwa na watu kwa ajili ya utawala. Kwa sasa, vingozi wa CCM ndio wameunda serikali yetu. Binadamu wameumbwa, na baadaye wakaunda serikali. Ni binadamu tu ndiye anaweza kuwa na dini. Viumbe wengine, na taasisi zote, haziwezi kuwa na dini. Zinaweza kuwa chini ya dini, lakini hazina uwezo wa kuwa na dini.

Imebidi nikujibu. Naelewa tuko nje ya mada, lakini mambo uliyoyaleta yalihitaji kujibiwa.

Nawaomba wachangiaji msiopendezwa na huu mchepuko mtuvumilie. Huenda tukaweza kurudi kwenye mada sasa.

Augustine Moshi
 
Moshi
Nilikuwa nasoma majibu yako natetemeka sielewi hivi huo ndiyo ueleo wako au unafanya maksudi.
Kwanza lazima ukubaliane na mimi madhahebu mengine hayatumii hilo neno neno "lapsed" ni RC peke yao wanatumia hilo neno, kama hujui basi jua hivyo. Niliandika nikiwa naelewa ninaloandika, wewe ndiyo badala ya kusema "lapsed catholics", umeondoa neno catholics na kuweke christians that is why I said Catholic does not means christians. Labda unieleze kwa nini umetoa neno Catholic ukaweka christians.
Sidhani kama nina muda kiasi hicho kukuelewesha mambo ya dini lakini ungekuwa makini na kuelewa mimi sijalaumu Kanisa, nimelaumu viongozi wa dini.
Hapa nimekaa najiuliza hivi hoja zako zote ulikuwa unazitoa ukiwa huelewe maana ya serikali au vipi, viongozi wa CCM hawaundi serikali, CCM ni chama cha kisiasa kilichopewa mamlaka ya kuongoza serikali. Serikali inaundwa na wananchi uwe mwanachama wa chama cha siasa au la. Nadhani wewe ni wale mnaosema serikali inatuonea, serikali haiwezi kukuonea, serikali ni wewe mwenyewe ila viongozi wa serikali wanaweza kukuonea. Do your homework mzee, tafuta maana ya serikali, chama cha siasa, viongozi wa serikali, na viongozi wa chama cha siasa. Unaposema viongozi wa Chama cha siasa wanaunda serikali hapo kidogo unanifanya nijiulize hoja zako unazitoa wapi. JK alipopata urais hakuwa kiongozi wa CCM, aliunda serikali kutokana na sera na maelekezo ya CCM. Na siyo lazima kiongozi wa serikali awe kiongozi wa CCM au mwanachama wa CCM. Ila kwa kuwa CCM imejiwekea utaratibu wa kuwapa uongozi watu ambao ni wanachama wa CCM hapo mnaona ndiyo hivyo inavyotakiwa. Mtu kama IGP anatakiwa asiwe mwanachama wa chama chochote, hebu nenda kafuatilie kama Mahita alitupa kadi yake ya CCM.
 
Augustine Moshi,

Please help me to understand, kwani umenichanganya kabisa na maelezo yako unasema Serikali aina dini , ila watu wake wana dini na ukuishia hapo ukasema serikali nitaasisi ! Unaweza ukanipatia tofauti kati ya Taasisi na serikali kwani you have lost me on that.

Kama ulivyosema mwanzoni wewe ni mathematician basi ningependa kutumia LOGIC katika kuonyesha duku duku langu , nadhani utakubaliana na mimi na statement nitakazotoa hapa chini

1. Watanzania ( watu ) wana dini

2. Serikali ni watu


Kwa maana hiyo basi kama watu wana dini na serikali ni watu that implies kuwa serikali nayo ina dini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom