Sina ugomvi sana na ushindi wa Wema coz tasnia ya filamu nayo ipo ipo tu, plus aina ya washabiki tulio nao ni rahisi sana kumtaja anayesikika na kuonekana kwao mara nyingi.
Sintofahamu yangu ipo kwenye mtangazaji anayependwa, mwanamuziki wa kiume anayependwa....hapa kuna mawili, either mfumo wa kupata mshindi sio sahihi au uchakachuaji ni mkubwa...kwa akili rahisi tu ni vipi mtu anayefuatiliwa na wengi ashindwe na mwenye wafuatiliaji wachache...kwa mfano Milard ameshinda kupitia blog yake, so nyie mnataka sie tuamini kwamba watu wanafuatilia blog yake kuliko kipindi/shughuli zake nyingine ?
Sioni ni kwa vipi hata waandaaji mnajiridhisha kwamba matokeo yenu yanatoa picha halisi ya kilichopo, na inawasaidia nini kumtangaza mtu ambaye hata bila kutumia nguvu kubwa ukweli upo wazi kuwa ni nani anapaswa kuwa juu.
Hivyo vigezo vinavyohalalisha mmoja kushinda hata kama kazi zake kwenye mitandao zinafuatiliwa na idadi ndogo ya watu kulinganisha na wenzake, ni dhahiri mnapaswa kujipanga upya...walau basi mtangaze kuwa ni tuzo za watu wa Tanzania tu.
Muweke wazi malengo yenu, otherwise SIELEWI....