Wasaidizi wa Rais Samia warekebishe makosa aliyofanya katika mahojiano na BBC, vinginevyo ataonekana siyo muungwana

..jamani tusijadili jinsia yake.

..tujadili kauli na matendo yake.

..na wewe unapaswa kuomba radhi.
Ndugu, wajitahidi kumsetiri, lakini huyu Mama alijianzishia mwenyewe, mara baada ya kuapishwa. Mwenyewe ndie aliyalitaka sijui alidhani litamjenga? Kwa kukosa busara/hekima kalikoroga swala ambalo kamwe hatoweza kulifuta hata ukimwombea radhi.
 
Porojo tu hizi, ulitaka aseme nn labda?

Siku ukijua nchi inaendeshwa kwa gharama kubwa kiasi gani, na maliasili zetu bado haziwezi kutunufaisha kwa kiwango tunachohitaji kwasababu wawekezaji wengi wanakuja na masharti ya kujinufaisha wao kwa kiasi kikubwa Basi utaacha mara moja kulalamika kama mjane
 
Porojo tu hizi, ulitaka aseme nn labda?

Siku ukijua nchi inaendeshwa kwa gharama kubwa kiasi gani, na maliasili zetu bado haziwezi kutunufaisha kwa kiwango tunachohitaji kwasababu wawekezaji wengi wanakuja na masharti ya kujinufaisha wao kwa kiasi kikubwa Basi utaacha mara moja kulalamika kama mjane

..mikataba yote ya kinyonyaji imesainiwa na viongozi wa ccm.

..tunatumia trillion 2 kununua ndege toka kwa wazungu wakati watoto wanakaa kwenye sakafu mashuleni.

.
 
..mikataba yote ya kinyonyaji imesainiwa na viongozi wa ccm.

..tunatumia trillion 2 kununua ndege toka kwa wazungu wakati watoto wanakaa kwenye sakafu mashuleni.

.
Kabla hujazitaja ndege lazima ujue lengo ni lipi?

Mbona ni mambo ya kawaida tu ambayo hayahitaji hata kusumbuka, kama unauliza habari za ndege Basi utauliza kwann mtu afungue biashara akati pesa iyo inatosheleza kujenga.

Uwekezaji si hadi uhakikishe umetimiza mahitaji yako yote, kwa kufanya ivo utachelewa sana.
 
... kipindi mfumo wa vyama vingi unaanza kati ya mambo yaliyoleta shida ni nafasi ya makamu wa rais. Kwa mujibu wa makubaliano ya muungano (wenyewe wanaita hati za muungano) na Katiba kwa ujumla, endapo rais akitoka upande mmoja wa muungano, basi makamu atoke upande wa pili na kwa utaratibu wao wa ki-CCM by default Rais wa Zanzibar alikuwa makamu wa Rais endapo Rais angetoka Tanganyika.

TATIZO: Baada ya vyama vingi, ikitokea Rais wa Tanzania (kichekesho) na wa Zanzibar wakatokea vyama tofauti itakuwaje? Ndipo solution ya haraka haraka ikaonekana waige utaratibu wa Marekani wa mgombea mwenza ambao automatically Rais akishindwa kutekeleza majukumu yake, VP (chama hicho hicho) anakalia kiti bila kuhitaji kuingia kwenye uchaguzi kwani kwa kufanya hivyo kuna uwezekano atakayechaguliwa akatoka chama tofauti na marehemu hali ambayo itainyima CCM kutawala pande zote. Of course hofu kuu ilikuwa Maalim Seif na huo utaratibu kimsingi ulimlenga yeye kutokana na hali ya kisiasa ya wakati ule!
Asante sana. Hii ndiyo shida ya kutunga sheria ili kumkomoa mtu badala ya kuangalia hali halisi. Sheria za namna hii zimekuwa zinatungwa sana na CCM kulenga wapinzani.
 
Hakuna binadamu aliye mkamilifu. Rais SSH alifanya makosa kwa kutoa kauli zisizo "sahihi" ktk interview yake na Salum Kikeke wa BBC.

Hilo siyo jambo geni kumtokea kiongozi yeyote yule. Kinachofanyika ktk mazingira kama hayo ni kiongozi mwenyewe, au wasaidizi wake, kujitokeza kuomba RADHI na kurekebisha makosa yaliyojitokeza.

Nashangaa kwanini mpaka sasa hivi hakuna mtu wa IKULU aliyejitokeza kurekebisha kauli alizotoa Rais. Ukimya huu wa Rais SSH, pamoja wasaidizi wake, unaweza kuleta hisia kwamba Rais hakukosea kibidamu, bali alifanya makusudi au alidhamiria kutoa majibu yale.

Zaidi ya kuharibu taswira ya Rais na kuporomosha heshima yake, hali hiyo inatoa mwanya kwa Rais kuitwa majina mabaya yenye kumvunjia heshima.

Hivi kweli Rais SSH ameridhika na majibu aliyotoa kwa BBC? Je, wasaidizi wake wanadhani Rais ametenda sawa, na kwa kukaa kimya wanamtendea haki Rais?

Nawasihi wasaidizi wa Rais wajitokeze kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza, na kuwaomba RADHI wananchi.

cc Richard, Nguruvi3 , Pascal Mayalla
Raisi hatakiwi kuomba radhi kamwe.huo ni bonge la udhaifu.kinachotakiwa ni kufafanua kile ambacho hakikueleweka kwenye statement yake.Raisi atoke hadharani aanze kusema ohooo nilighafirika sababu nilikuwa na hofu ya camera,what?Hayo atatafanya kwa mumewe tu.Akiomba radhi ataonyesha dhaifu kabisa kwamba huwa analopoka lopoka hovyo bila mpango.
 
Wafaransa hawaombi radhi hata kama ni kosa la wazi. Wanasema kuomba radhi ni sehemu ya kukubali udhaifu. Hiyo ni tabia ingawa siyo desturi ya wafaransa. Kule ni ubabe kwenda mbele!!!

Sisi mara nyingi twaomba radhi endapo tumefanya kosa kweli. Ingawa kundi fulani laweza kulazimika kuomba radhi hata kama halijakosa ili "yaishe".
====
Mkuu, kwanza orodhesha makosa yote yaliyotendwa ili tuwe na ujasiri wa kushauri hiyo radhi iombwe.
Nilikuwa naitafuta kauli kama hii; aonyeshe makosa ili na wengine tuyafahamu kwa kuwa watu wana mitazamo tofauti. Unaweza kuona hapa kajibu vibaya mwingine akaona amejibu vizuri hivyo anayesema kajibu vibaya basi ana wajibu wa kuonyesha huo ubaya badala kuandika tu kwa ujumla! Ukiandika kwa ujumla bila kudadavua nawe unakuwa umeandika vibaya na una wajibu wa kuomba radhi.
 
..kasikilize interview yake na Salum Kikeke wa BBC.
hajakosea popote, na sijawahi kusikia Rais yoyote akiomba radhi
mngemdanganya Trump akarekebisha Hotuba zake na tweeter alizozitoa enzi hizo,
JokaKuu wakati wa safari ya miguu ukienda kazini au kwenye biashara zako usisikilize mbwa wanavyobweka hutafika asilani, CHUKUA FIMBO /GONGO saonga mbele mbwa watanyamaza wote
tunataka maendeleo km hizo barabara tulizolipia TOZO kwa sasa, Siasa bado
Mama chapa lapa chapa fimbo
 
samia suluhu ni gaidi kaa magaidi wengine wa ccm, huyu mama hajui mbere au nyuma, hajielewi kabisa, hata akili hana kabisa, kasema uongo mtupu mbere ya dunia, kaa ni kwingine angekuwa amejiuzulu kufikia sasa
 
Hakuna kauli iliyoniuzi Kama kusema kuwa wananchi wameridhika na tozo!! Hivi kwa nin mheshiwa sulululu anatukejeli kiasi kile jamani,, kweli maumivu hayaaa anyway
 
kama unaona alikosea kwa nn usimuambie kikeke afanye masahihisho?! au unataka interview irudiwe?
kuna mambo mengi ya msingi yanapaswa yashughulikiwe sio jambo hili ambalo haliongezi dawa mahospitalini wala haliongezi kodi ya nchi, wala haliongezi chanjo ya corona, wala halipunguzi maendeleo ya watanzania.
watanzania wenzangu nawaomba tujikite kujadili mambo ya msingi kwa taifa letu sio hoja ambazo hazina maana ambazo zinapoteza uwezo wetu wa kufikiria changamoto zinazo tukabili kama taifa.
Nafikiri wewe ndiye mwenye hoja za hovyo na mtazamo wa mtu asiyetumia akili hata kama hajasoma hoja tunqzoziangalia hapa ni za msingi sana raisi wa nchi kutoa kauli za uongo ni hatari sana kwa nchi, kuminya democrasia kusingizia watu kesi za uongo kukumbatia washauri wabaya kupinga katiba isiyokidhi muda na hali halisi ya nchi hayo yote yana madhara ya moja kwa moja na mahitaji unayotaka tuyajadili.
 
Porojo tu hizi, ulitaka aseme nn labda?

Siku ukijua nchi inaendeshwa kwa gharama kubwa kiasi gani, na maliasili zetu bado haziwezi kutunufaisha kwa kiwango tunachohitaji kwasababu wawekezaji wengi wanakuja na masharti ya kujinufaisha wao kwa kiasi kikubwa Basi utaacha mara moja kulalamika kama mjane
Mbona tunaambiwa nchi inaongoza kwa rasilimali Africa nzima
 
Back
Top Bottom