Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,131
- 35,159
Kumekuwa na dhana ya uongo na upotoshwaji mkubwa dhidi ya utendaji wa rais wetu Mama Samia Suluhu. Kumekuwa na maneno ya mara kwa mara, tena yakurudiwa rudiwa ya kusema wasaidizi wa karibu wa mheshimiwa Rais Samia wanampotosha kwenye mipango na maamuzi ya serikali.
Hii dhana sio tu inamkosea heshima rais wetu (kwa kumuonyesha ni kiongozi dhaifu) bali imelenga kumchonganisha rais na wasaidizi wake. Hili sio jambo jema na lenye afya kwa mustakabali wa nchi yetu.
Sote tunapaswa kutambua, Rais Samia yuko pale kikatiba, na mamlaka yake yanalindwa kikatiba, chochote kile kinachoamuliwa na serikali yake kitaifa basi kiujumla ni maamuzi yake kamili kwa 100%, na ikiwa kitakuwa tofauti na matakwa yake atatangaza kukitengua ndani ya muda mchache sana ndani ya masaa kadhaa katika siku hiyo hiyo.
Ukimya wowote wa rais kwenye jambo lililoamuliwa kitaifa na serikali yake unamaanisha ndio uamuzi wake. Mfano rahisi sana ni suala la mkataba wa bandari na waarabu. Yale maamuzi yaliyopitishwa bungeni ndio takwa rasmi la rais Samia, na kama litahitaji kutiwa saini baada ya kutoka bungeni, mpaka kufikia leo litakuwa limetiwa saini na rais Samia!
Sasa kuliko kumkosea heshima rais wetu, kumkosanisha na wasaidizi wake, ni vyema kila jambo ambalo limeamuliwa na serikali yake halafu kama kuna watu ambao hawakubaliani nalo wapambane kwa hoja na rais Samia moja kwa moja kuliko kumkosanisha na wasaidizi wake.