Wasafi Media bado inawahitaji Jonijoo na Mtiga Abdallah

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
Kila mtu anajua leo hii kuwa Wasafi Tv na Wasafi FM ndiyo media ambayo zimepata nguvu ya kushabikiwa kwa muda mfupi na kupata watazamaji na wasikilizaji wengi.

Huenda labda ushawishi huo umekuja kwa sababu ya bosi wao Diamond platnumz kuipiga chapuo media hiyo lakini kuna kitu naona kabisa kimepungu pale Wasafi Media, na kama kila siku hii Wasafi Media itatagemea chapuo kwa kumuongelea Diamond platnumz na Zuchu kila siku.

Basi ipo siku hii media itaenda kufa na nafasi yake itachukuliwa na media nyingine kama media hii haitobadilika.

Wasafi Media inamuitaji mtu wenye ubunifu kama Jonijoo, walitakiwa kutumia nguvu ya kila namna kumzuia Jonijoo asiondoke ili kutengeneza vijana sahihi ambao walitakiwa kupata madini kutoka kwa Jonijoo. Kama wanavyofanya East Africa Radio kwa Dulla Planet na wale wadada.

Lakini kuondoka kwa Jonijoo na kumleta Lil Ommy naona kwangu haijakaa sawa. Jonijoo mmoja alikuwa anasimama kwenye The Bar Tender na msanii wake mmoja tu anafanya naye mahojiano wewe mtazamaji huku hautamani kipindi kiishe, hamlazimishi mtu kujibu maswali ila amamuuliza mtu maswali ambayo siyo mtazamaji wala siyo msanii ambaye alitegemea ataulizwa hilo swali.

Lakini leo hii kwenye wasafi TV kwenye Big Sunday Live Show unakutana na Lil Ommy, Ray Mshana na Ammy girl, wasanii zaidi ya watatu lakini kinachoendelea kwenye kipindi hakieleweki na wala hakina mvuto.

Raia tulikuwa tunafurahia mahojiano na Jonijoo pale Block 89, Jonijoo, Liyaah Naa mtu imara, tulikuwa tunafurahia kuwasikiliza. Unaweza ukawapotezea XXL B Dozen, Adam Mchomvu na Mamy Baby kule Clouds, leo hii Wasafi FM hakuna linaloeleweka, kelele tu na umarekani mwingi.

Kipindi The Story Book kinaanza watu tulikuwa tunafurahia maandiko ya Jamal April na masimulizi ya Mtiga Abdallah, lakini leo hii kipindi hakina mvuto kivile, naona kazi mbili kapewa mtu mmoja. Anayeandika ndiyo huyo huyo na anasimulia kwa njia ya sauti ni huyo huyo.

Ujumbe kwa Wasafi Media, inatakiwa kuwa makini sana, watu wanalalamika Wasafi haina maudhui kabisa zaidi ya umbea na kuongelea ngono kwa sana basi, ndiyo maana kila siku wanapigwa na rungu la TCRA.

Wanaopewa 'headlines' ni wale ambao hawana ubunifu kabisa.

Sasa Wasafi FM na Wasafi Tv kuweni makini msije mkampoteza Edo Kumwembe na George Ambagile.

20221110_090429.jpg
 
Nilikuwa namuelewa sana Mtiga alivyoingia Jamal nikaona ananipoteza kabisa yaani simuelewi,sasa hivi namuona yuko poa anasimulia vizuri sana.
 
Wana wanampa sifa nyingi sana Jamal April sometimes anazingua kutuletea story za upuuzi kuelezea maisha ya peponi, mara jehanam kupoje mambo ya dhahania dhahania yanakera sana. watu tunataka mambo yalioExist, mambo reality
Wasikilizaji wa huyo jamaa ni elimu hafifu wengi. Siwezi kaa zaidi ya dakika tatu unaniambia upuuzi wa motoni kuna nini. Mara zote huwa namsikia nikipita njiani na fatilia wanaokuwa wanashangaa ni wabeba guta wamepaki hapo wanafurahi kuambiwa ndege iliyopotea nje ya dunia na kurudi miaka 30 baadae. Hizo story hunipati
 
Jamal yupo sawa katika uandishi na sio usimuliaji naomba jamal anatumia nguvu nyingi ktk kusimulia mpaka anapoteza ladha ya kumsikiliza
 
Wana wanampa sifa nyingi sana Jamal April sometimes anazingua kutuletea story za upuuzi kuelezea maisha ya peponi, mara jehanam kupoje mambo ya dhahania dhahania yanakera sana. watu tunataka mambo yalioExist, mambo reality
Huyo jamal ashaanza upuuzi wake aisee
 
Wasikilizaji wa huyo jamaa ni elimu hafifu wengi. Siwezi kaa zaidi ya dakika tatu unaniambia upuuzi wa motoni kuna nini. Mara zote huwa namsikia nikipita njiani na fatilia wanaokuwa wanashangaa ni wabeba guta wamepaki hapo wanafurahi kuambiwa ndege iliyopotea nje ya dunia na kurudi miaka 30 baadae. Hizo story hunipati
🤣🤣🤣🤣🤣 watu wanataka true story yeye analeta nadharia
 
Nilikuwa namuelewa sana Mtiga alivyoingia Jamal nikaona ananipoteza kabisa yaani simuelewi,sasa hivi namuona yuko poa anasimulia vizuri sana.
jamaa hayuko sawa inahitaji umakini mkubwa sana kujua kama jamaa ana madhaifu meng sana kwenye eneo la usimuliaji
 
Wana wanampa sifa nyingi sana Jamal April sometimes anazingua kutuletea story za upuuzi kuelezea maisha ya peponi, mara jehanam kupoje mambo ya dhahania dhahania yanakera sana. watu tunataka mambo yalioExist, mambo reality
Sasa hamtaki Jamal kwasababu ya aina za stori au nini? Maana ata kipindi mtiga anatoa story book akiandikiwa na huyohuyo Jamal April, ila leo hii Jamali anafanya presentation ye mwenyewe
 
Sasa hamtaki Jamal kwasababu ya aina za stori au nini? Maana ata kipindi mtiga anatoa story book akiandikiwa na huyohuyo Jamal April, ila leo hii Jamali anafanya presentation ye mwenyewe
shida sio Jamal kufanya vitu viwili. ila kufanya vitu viwili kwa wakati moja kuna athari kubwa mfano jamal leo hii ana mvuto katika usimuliaji maana yake anataka kuandika pia anatka kusimulia hatima yake anakuta kuna kimoja anaharibu .

Jamal binadam kama binadamu wengine anatakiwa afanye kitu kimoja kwenye media yoyote lazima kuwa na mgawano wa majukumu .

Sio mtu moja huyo huyo awe producer, awe dj pia awe Radio presenter
 
Ukienda kwenye simulizi zake YouTube zaidi ya 90% ya watu wanamkubali,hiyo tunachukulia kama changamoto huwezi pata wapenzi bila haters

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
sina maana kuwa nachukia anachokifanya ila naitaj kuona uboreshwaj zaidi .

Kwenye football pep Guardiola alikuw na stricker km aguero , sterling na Gabriel jesus walikuwa wanafunga fresh ila aliwauza akalet wakina haaland akamtuamia na foden pia now n team hatar pale epl.

sasa swala la jamal anakuwa bora akiwa kama muandishi na sio msimuliaji .

watu hawajudge pale mtiga alipoanza kazi ila watu walijudge sana alipoanza jamal
 
jamaa hayuko sawa inahitaji umakini mkubwa sana kujua kama jamaa ana madhaifu meng sana kwenye eneo la usimuliaji
Kweli anayo ,lakini ninachomkubali huwa anayafanyia Kazi mapungufu yake na kuimprove .Zamani nilikuwa hata kumsikiliza siwezi nikawa nina dhana ya kuwa watu wenye uwezo mdogo wa kuchambua mambo ndio wanaoweza kumsikiliza na kushangaa watu wakimsifia ila nimeona video zake za karibuni amejigahidi sana.
 
Back
Top Bottom