Ndugu mwandishi wa huu uzi sidhani kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa Wasafi media. Ndio nasema kwamba wewe sio mfuatiliaji kwasababu zifuatazo:
1. Kwanza inaonekana unazungumzia hisia binafsi na maoni tu ya kwako binafsi na wala sio kwamba unawasemea watu wote.
2. Block 89 unayoizungumzia kuwa ilikuwa poa sana, kuna wenzako waliikataa na kusema ni kipindi kibovu na kilikuwa kwenye bad timing. Japo hapa nakiri kwamba binafsi nilikipenda sana hiki kipindi. Ila unaposema pia kwamba mtu anaweza kuacha kusikiliza Clouds XXL kwasababu ya block 89 sio kweli kwasababu vipindi hivi vilikuwa muda tofauti.
3. Mtiga na Jonijoo: nakubali na kuheshimu mchango wao kwa wasafi Media na pia nikiri ubora wao walipokuwa wasafi Media. Lakini unajua kwa sasa wako wapi na wanafanya nini?

Mpaka hapo utagundua pia kwamba Wasafi Media pia ilikuwa inawabeba. Kwa mfano huyu Mtiga alikuwa mwanafunzi wa Jamal, aliandikiwa stori na kuelekezwa pia jinsi ya kuzisoma. Kipaji chake kikubwa ni sauti yake nzuri
4. Wasafi Media kumtegemea Zuchu na Diamond


Ni kweli kwanza Diamond ni msanii anayezungumziwa zaidi Tanzania na nje ya Tanzania na suala la kumzungumzia halikwepeki. Hakuna namna....ndio maana hata Media zilizokuwa na tofauti naye zimerudi zenyewe na zinapiga nyimbo zake. Zuchu ni dhahabu, nyimbo kali, kipaji na ubunifu wake unamfanya kuwa mmoja wasanii bora kabisa wa kike kwa Tanzania na Afrika kwa sasa. Utaachaje kumzungumzia?
5. Wasafi TV: Africa Is watching. Hii ina maana kwamba maudhui na mtazamo mzima umebadilika na hivyo lazima ilenge kuhudumia Africa nzima.