Dramatizing serious narratives: Journalism itazamwe upya kwa Wasafi Media na EFM

NIPOSINGO

Member
Jul 24, 2022
11
39
Matukio ya siku za hivi karibuni yamenitafakarisha maana na dhamira ya kuwa mwanahabari

Kuanzia saga ya Wasafi Media vs Lissu, controversy ya TCRA vs Waziri Nnauye, na dhihaka kadhaa za EFM

Uanahabari sio guarantee ya kukosa heshima au ku-act unprofessional in the pretext of professionalism, tena kwa waandishi ambao “tunajuana” elimu na uwezo wetu.

Something somewhere is not serious, I think. Hapa nitazungumzia matukio mawili tu ya hivi karibuni; wengine mnaweza kujazia wanajamvi kwa ajili ya mjadala.

KATAZO LA KUSOMA MAGAZETI KWA HISIA

“Impartiality” ni nadharia inayoeleweka vyema kwa wanataaluma wa habari. Kanuni kubwa iongozayo nadharia hii ya uyakinifu inamtaka mwandishi kutoandika/husisha/weka maoni au hisia zake katika habari anayoiandaa au kuiwasilisha — kinyume na walivyokuwa na wanavyoendelea kufanya baadhi ya watangazaji wa EFM na Wasafi

Uandishi wa habari unaofuata taratibu ni ule unaotenganisha kwa uwazi uhalisia wa jambo na maoni kuhusu jambo hilo. Waandishi wengi wa zama hizi hawaliishi hilo.

Mwanahabari wa redio hapaswi kutoa maoni yake kama ilivyo kwa mwandishi wa makala/tahariri gazetini. TCRA wqliligundua hilo na wali-address kama ni kosa na kutoa onyo

Ikumbukwe kuwa TCRA ndio regulator wa online and broadcasting content nchini, kwa mujibu wa sheria.

TCRA hufanya kazi zake kwa kanuni na miongozo mbalimbali, lakini pia kazi hufanyika katika baadhi ya kamati mathalani Kamati ya Udhibiti Maudhui (Content Committee Team), ambayo pamoja na mambo mengine yote, Waziri (wa Habari) ndiye last say wake (this is unquestionable)

Binafsi sikupendezwa na approach ya Nape kutuma kombora mtandaoni dhidi ya TCRA lililowapa “pointi tatu” walengwa (sisemi waandishi, ni walengwa) na kupelekea watu hao kufanya dhihaka kubwa kesho yake dhidi ya TCRA. This is both disgusting and unprofessional.

DHIHAKA KWA SANAMU LA MWL NYERERE MJINI ADDIS ABABA

Leo tena nimeona team ya EFM iki-dramatize issue ya sanamu la Mwl. Nyerere lililosimikwa na kuzinduliwa hivi karibuni katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, nchini Ethiopia.

Wasichokijua ni kwamba, ile sio tu komedi bali ni dhihaka kubwa kwa Kiongozi Mkuu wa nchi (Rais Samia Suluhu Hassan) aliyehudhuria na kuridhia uzinduzi huo. It means that yeye naye “alipigwa” kwa kukubali kuzindua “Nyerere feki”. Ni kukosa heshima.

EFM wamekuwa na tabia ya ku-dramatize mambo serious na kuwakosea watu/viongozi heshima. Sio Rais SSH pekee, bali ni dhihaka kwa marais wote wa Afrika waliohudhuria pale.

Sawa, ni role ya media kuhabarisha, lakini wajifunze kwa vyombo vingine kama BBC walivyoripoti kimaadili na kuzingatia taaluma, sio wao.

Ni tatizo linaloletwa na kuajiri wachekeshaji na watumbuizaji kama watangazaji katika tasnia ya habari. Vichwa vyote vikifanana, of course no critical mind huzaliwa.

Nimeandika roughly nikiwa safarini, nitairudia vyema makala hii ikiwa imeambatana na ushahidi na rejea za kisheria

Ahsanteni!
 
Mkuu NIPOSINGO umeandika suala mihimu sana.Hawa watangazaji wa hizi media hawafuati kwa kiasi kikubwa maadili ya utangazaji.TCRA wananyamaza kimya ! nashindwa kuelewa tunakoelekea ! Chombo cha habari hakipaswi kuegemea upande mmoja au kutoa maoni binafsi ya watangazaji ! nitatoa mfano, wiki iliyopita tulisoma na kusikia katika chombo cha habari cha wasafi FM eti Baba Levo akisimulia kuwa Harmonize alimkaba na kumpora pesa alizopewa na tajiri fulani huko Casino flani ili wagawane na baadhi ya watu.Kwa hiyo huyu Baba Levo anaitumia radio anayoifanyia kazi kuutangazia umma hizo habari ! Hapa tumepata upande wake, je Harmonize mbona nae hatujamsikia kwa upande wake ? Je Baba Levo anamchafua Harmonize mbele ya jamii ? Je Baba Levo anatumika ?? TCRA mmekaa kimya ?? Tumeona Radio kama Wasafi FM , watangazaji muda wote wanashambulia watu wasioendana nao na kuwatukuza wamiliki ! Je hilo ndo lengo la kuanzisha hizi Radio ?? Je Harmonize akienda mahakamani kuwa mmemdhallisha na kumvunjia hadhi yake mbele ya umma mtalalamika nyie Wasafi FM ?? TCRA mnafanya nini na radio hizi ?? Kwa nini msizifungie ?? Muda wote badala ya kutangaza maudhui wao wao kumsifia mama nani sijui, mara chui sijui mara nani , ilimradi kelele tupu utadhani genge la wahuni wako kijiweni !
TCRA Chukueni hatua isije ikatokea kama ya Rwanda !
 
Matukio ya siku za hivi karibuni yamenitafakarisha maana na dhamira ya kuwa mwanahabari

Kuanzia saga ya Wasafi Media vs Lissu, controversy ya TCRA vs Waziri Nnauye, na dhihaka kadhaa za EFM

Uanahabari sio guarantee ya kukosa heshima au ku-act unprofessional in the pretext of professionalism, tena kwa waandishi ambao “tunajuana” elimu na uwezo wetu.

Something somewhere is not serious, I think. Hapa nitazungumzia matukio mawili tu ya hivi karibuni; wengine mnaweza kujazia wanajamvi kwa ajili ya mjadala.

KATAZO LA KUSOMA MAGAZETI KWA HISIA

“Impartiality” ni nadharia inayoeleweka vyema kwa wanataaluma wa habari. Kanuni kubwa iongozayo nadharia hii ya uyakinifu inamtaka mwandishi kutoandika/husisha/weka maoni au hisia zake katika habari anayoiandaa au kuiwasilisha — kinyume na walivyokuwa na wanavyoendelea kufanya baadhi ya watangazaji wa EFM na Wasafi

Uandishi wa habari unaofuata taratibu ni ule unaotenganisha kwa uwazi uhalisia wa jambo na maoni kuhusu jambo hilo. Waandishi wengi wa zama hizi hawaliishi hilo.

Mwanahabari wa redio hapaswi kutoa maoni yake kama ilivyo kwa mwandishi wa makala/tahariri gazetini. TCRA wqliligundua hilo na wali-address kama ni kosa na kutoa onyo

Ikumbukwe kuwa TCRA ndio regulator wa online and broadcasting content nchini, kwa mujibu wa sheria.

TCRA hufanya kazi zake kwa kanuni na miongozo mbalimbali, lakini pia kazi hufanyika katika baadhi ya kamati mathalani Kamati ya Udhibiti Maudhui (Content Committee Team), ambayo pamoja na mambo mengine yote, Waziri (wa Habari) ndiye last say wake (this is unquestionable)

Binafsi sikupendezwa na approach ya Nape kutuma kombora mtandaoni dhidi ya TCRA lililowapa “pointi tatu” walengwa (sisemi waandishi, ni walengwa) na kupelekea watu hao kufanya dhihaka kubwa kesho yake dhidi ya TCRA. This is both disgusting and unprofessional.

DHIHAKA KWA SANAMU LA MWL NYERERE MJINI ADDIS ABABA

Leo tena nimeona team ya EFM iki-dramatize issue ya sanamu la Mwl. Nyerere lililosimikwa na kuzinduliwa hivi karibuni katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, nchini Ethiopia.

Wasichokijua ni kwamba, ile sio tu komedi bali ni dhihaka kubwa kwa Kiongozi Mkuu wa nchi (Rais Samia Suluhu Hassan) aliyehudhuria na kuridhia uzinduzi huo. It means that yeye naye “alipigwa” kwa kukubali kuzindua “Nyerere feki”. Ni kukosa heshima.

EFM wamekuwa na tabia ya ku-dramatize mambo serious na kuwakosea watu/viongozi heshima. Sio Rais SSH pekee, bali ni dhihaka kwa marais wote wa Afrika waliohudhuria pale.

Sawa, ni role ya media kuhabarisha, lakini wajifunze kwa vyombo vingine kama BBC walivyoripoti kimaadili na kuzingatia taaluma, sio wao.

Ni tatizo linaloletwa na kuajiri wachekeshaji na watumbuizaji kama watangazaji katika tasnia ya habari. Vichwa vyote vikifanana, of course no critical mind huzaliwa.

Nimeandika roughly nikiwa safarini, nitairudia vyema makala hii ikiwa imeambatana na ushahidi na rejea za kisheria

Ahsanteni!
kwa hiyo unataka tuendelee kuimba kuwa mnaupiga mwingi ndo mfurahie hadi sirini huko
 
Back
Top Bottom