Warioba: Wanaotaka Tanganyika wasipuuzwe!

Lini itakuwa ni priority?

Kwa sasa tunaelekea mchakato wa kuwa na katiba mpya, je hiyo katiba itakuwaje?
hilo ni lazima lifikiwe maelewano mazuri.

Kuna swala la EAF nalo linahitaji intergration ya hizo nchi, sasa kama Zanzibar na Tanzania tu kwa sasa migogoro na makelele ni mengi tu sembuse na hilo shirikisho, si itakuwa ni kichekesho tu??

Kutakuwa na tatizo kati ya zanzibar na Muungano kama ilivyyozoeleka na kutakuwa na Tatizo kati ya Zanzibar na hiyo federation pia kutakuwa na tatizo kati ya Muungano na hilo federation..hapo patakalika kweli???

Yes he has balls, however utanganganyika sio priority kwa sasa, ANGESEMA JK nchi imemshinda ajiuzulu angekuwa amesema la maana zaidi, au angehamasisha watu kuandamana, ilikuwa bora pia....
 
Warioba anakula pension yake kutoka serikali dhalimu ya CCM iliyopata nafasi ya kuongoza nchi kwa njia za Wizi. Hivi kweli inaingia akilini kutaka kuungana na nchi kama Kenya ambayo kila kukicha wanachinjana kama kuku? Au Uganda ambao wamekuwa wakipigana na waasi kwa zaidi ya miaka 20?

Zanzibar wanataka U-zanzibari wao kwa nini sisi tusitake Utanganyika wetu? Sio siri nchi nyingi sana Yugoslavia, Ukraine ilikuwa Russia etc wameachana na miungano ya kulazimishana sasa sisi ni nini hasa wanachong'ang'ania tuungane na Manyang'au let alone huu muungano wetu unatushinda. Maloloso kila siku, Zanzibar wameendelea kutumia umeme wa bure kutoka bara sijui kwa miaka mingapi hata hiyo bajeti yao inachangiwa sana na walipa kodi wa Bara haya mambo yakiwekwa hadharani hakuna atakayepona hapo magogoni.

Warioba ni kuwadi tu anayetaka kujificha na madhambi yao wanayofanya. Hata Gadafi alikuwa anataka kuwa kiongozi wa umoja wa Afrika ati shujaa?
 
Turudi nyuma kidogo tuangalia chanzo hasa cha huo Muungano. Lengo kuu la Muungano ilikuwa ni kuimarisha umojaa wa Afrika kuanzia kiwango cha majirani kwa lengo la kufikia United States of Africa. Kabla ya Muungano wa Tanzania wazee wetu walikuwa na plani ya kuwa na federation of East Africa, lakini kwa sababu mbalimbali juhudi za kuuanda federation ile zikafeli.

Kwa vile kuna effort mpya za kuwa na jumua ya afrika ya mashariki, muungano wa Tanzania katika muundo wake wa leo unaweza usiwe na umuhimu tena. Ama kuwe na Taifa moja la Tanzania lenye serikali moja au tuwe na mataifa mawili ya tanganyika na zanzibar kila moja ikiwa na sauti yake ndani ya EAC.

Hapo umeongea pointi tupu mkuu, nakubaliana na wewe.
This is BIG YES
 
Turudi nyuma kidogo tuangalia chanzo hasa cha huo Muungano. Lengo kuu la Muungano ilikuwa ni kuimarisha umojaa wa Afrika kuanzia kiwango cha majirani kwa lengo la kufikia United States of Africa. Kabla ya Muungano wa Tanzania wazee wetu walikuwa na plani ya kuwa na federation of East Africa, lakini kwa sababu mbalimbali juhudi za kuuanda federation ile zikafeli.

Kwa vile kuna effort mpya za kuwa na jumua ya afrika ya mashariki, muungano wa Tanzania katika muundo wake wa leo unaweza usiwe na umuhimu tena. Ama kuwe na Taifa moja la Tanzania lenye serikali moja au tuwe na mataifa mawili ya tanganyika na zanzibar kila moja ikiwa na sauti yake ndani ya EAC.

Watanzania wengi hawaitaki EAC kutokana na mchakato uliotangulia sasa mambo ya kulazimishana hayana tija tena wakati huu wa 21st century.
 
Kuwepo kwa serikali ya Tanganyika na ya Muungano vina mantiki kisheria lakini madhara yake ya muda mrefu ni mawili (1) Kutakuwa na mashindano ya ukweli katika kila nyanja ya kiuchumi, kijamii na kisera. Ikumbukwe kwamba kwa Sasa Rais wa Zanzibar ni "loyal" kwa rais wa Muungano. Structure ilivyo sasa ilibuniwa kiufundi sana kiasi ambacho miaka inaweza kupita mingi sana bila kutia mashaka kama 1+1 ni 2 na siyo 1 (2) Tunapoingia katika shirikisho la Afrika mashariki kuwa na serikali ya Muungano juu ya serikali nyingine mbili siyo tu ni gharama kama wengine walivyosema bali pia kuna rahisisha utengefu. Kila upande unaweza kuamua kujitoa hata kama upande mwingine hauna mpango huwo.

Kwa maoni yangu huu siyo wakati muafaka kwa serikali ya Tanganyika. Ni wakati wa kuzifanyia kazi kero nyingine nyingi ambazo zinasababisha (directly or indirectly) kuweko kwa ombwe (vacum) ambalo wengi wanafikiri dawa yake ni serikali nyingine. Serikali in its very basic meaning ni chombo cha kimaamuzi chenye uhalali wa kisheria na kimaadili (legal and legitimate) kuongoza kwa niaba ya watu wa eneo fulani. Hata serikali za mitaa ni serikali na zaidi sana tunahitaji serikali za majimbo kama ndugu zetu wa chadema wanavyo tukumbusha mara kwa mara. The latter makes perfect social-economic sense.
 
Tatizo wengi wanao support Muungano na serikali mbili wana support kwa ajili ya mazoea tu. Kwamba ndiyo mfumo uliyo kuwepo muda mrefu na ndiyo mfumo wengi wetu tulio zaliwa ndani yake. Kumbukeni mazoea ni kama sheria. Ila kiukweli logic ya mfumo wa serikali mbili ulio kuwa na mantiki 1964 hauna mantiki sasa. Ndiyo maana kuna migogoro mingi ndani ya muungano.

Mimi sisemi tuvunje muungano ila pia tuangalie options zote. Kama hii ya serikali mbili una dosari kwa nini tusifanye tathmini ya serikali tatu au hata kuto kuwa na muungano kabisa? It is all about looking at all your options. Ila hii ya kutegemea tufanye yale yale kisha tupate matokeo tofauti tuna jidanganya.

In short matatizo ya muungano yameanzia na mfumo huu. Tungekua na serikali moja leo tungejiona ni wamoja. Hivi mna dhani ni coincidence upande wenye serikali yake yenyewe ipo very nationalistic na sisi ambao hatuna serikali yetu tuna jitambulisha tu kama Watanzania? Zanzibar ina serikali yake ndiyo maana wananchi wana jiona ni Wazanzibar. Tanganyika hatuna serikali ndiyo maana tuna jiona kama Watanzania tu.

Sasa hapa tuamue tuwe na serikali tatu ili Wananzibar wajione Wazanzibar na Watanganyika wajione Watanganyika japo ni Watanzania au tuwe na serikali moja sote tujione ni Watanzania.
 
Hivi tukiwa na serikali mbili za Tanganyika na Zanzibar na kisha kukawa na serikali ya shirikisho ya Tanzania wananchi wa hizi nchi mbili watajitambulisha vipi? Yaani ukienda nje ya nchi utajiita mtanzania, mtanganyika, au mzanzibar? Au itategemea na muktadha wa utambulisho?
 
Kwa hiyo tukiwa na serikali tatu hakutakuwa na mtanzania. Kutakuwa na mtanganyika na mzanzibari.
 
Kuta kuwa na Watanganyika na Wazanzibar chini ya mwamvuli wa Tanzania. Au una prefer sasa ambapo kuna Tanzanians na Zanzibar-Tanzanians? Kama wao wana jivunia Uzanzibar wao kwa nini na sisi tisijivunie Utanganyika wetu?
 
Mimi siitaki Tanganyika!

Mkuu Tanganyika ni JINA tu watu wadai zaidi ya jina...kama jina linakukwaza tunaweza kubaki kama TANZANIA lakini yakle ya msingi ya watu BARA lazima yarejeshwe...mfano hatutaki mawaziri kutoka ZANZIBAR wawemo huku BARA wakati sisi wa BARA hatuna mawaziri ZANZIBAR
 
Kuna Mzanzibari Mmoja, kule kwenye jukwaa lao, anadai yuko tayari kulipua vile vitu Watanganyika wanavyoringia. Kiufupi jamaa yuko tayari kutumia mbinu za kigaidi kulipua na kuharibu mali za Watanganyika kwa sababu yeye haridhiki na huu Muungano ambao anaona kama ni ukoloni wa Tanganyika dhidi ya Zanzibar.

Mzanzibari mwingine anadai kuna wale wanaojiita Wazanzibar wakati asili yao ni msumbiji, Bara n.k, kwake yeye hao wanaotoka OMAN ni wazanzibari halisi kuliko hao waliotoka bara .

Mzanzibari mwingine akajenga hoja kwamba waarabu walikuwepo zanzibar kabla ya Wabantu, akadai walikuwepo wale ambao jamii zao zinarandana na Uarabu kama vile "wenye asili ya somalia na wahabeshi" lakini si wabantu. jamaa anajaribu kujenga hoja kwa kuimply kwamba Wabantu ndo wakuja na waarabu ndo wenyeji. Ila sasa cha Ajabu Zanzibar maana yake ni "ZINJIBAR" inkimaanisha "LAND OF BLACK PEOPLE", na hiyo waliita waarabu wenyewe, sasa sijui watu weusi wenyewe ni hao Wahabesh na wasomali na si Wabantu ?"

Kusema kweli Zenji kuna matatizo, hawa jamaa baadhi yao wanaubaguzi mbaya sana!, tena Ubaguzi baina ya wao kwa wao ni mbaya mno, kuvunja muungano ni dhahiri wanaweza, wakitaka wanaweza kabisa na wala hili halina shaka yoyote!, isipokuwa watakuja kujuta baadae kwa sababu muda si mrefu wataanza kubaguana wao kwa wao. baadhi ya Wapemba wana kasumba ya "Usuperiority", wanawaona wenzao wa unguja kama "non-deserving". hawa ndo wenye chokochoko za kuvunja Muungano, au kama hauvunjiki basi Zanzibar ifaidi to a Maximum at the expense of Tanganyika.

Kwa kuwa Tunakwenda katika East-Africa Community, hii ikifanikiwa kutakuwa hatuna haja ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa sababu tutakuwa na Federation kubwa Zaidi na yenye tija, Zanzibar tunaweza kuwaacha Wakaenda kivyao, wakitaka kujiunga kwenye EAC wakaribishwe!!, kwa sababu ninajua hawawezi kukaa nje ya EAC, nchi yao ni ndogo, na itakuwa haina tija kuwa nje ya EAC,watageukana wao kwa wao muda si mrefu kwa sababu ya ubaguzi mbaya wa baadhi miongoni mwao. then wakitaka kujiunga na EAC ndo watafahamu kwa uzuri, muungano ni mbaya ukiwa ndani, ukiwa nje Muungano ni lulu, wenye akili wanajua hili ndo, maana kuna UNITED STATES OF AMERICA, EUROPIAN UNION, etc.
 
Hapo kwenye red:
Ndio maana nasema kuwa kama wanataka kujiondoa tuwaache wajiondoe kivyao na utashangaa mda si mrefu watakapoanza kuwa na civil war wao kwao.
kwanza wao kwa wao wanachuki, hwapendani hata kidogo ,wanabaguana huwezi kuamini..yaani wanchokifanya ni kama mchezo wa kitoto
 
Kwa hiyo tukiwa na serikali tatu hakutakuwa na mtanzania. Kutakuwa na mtanganyika na mzanzibari.
Ndio maana unaona wao wanajiita Wazanzibar wawapo nje ya nchi ni kwa sababu ya kuwapa huo uhuru.
The best way to do, ni kutoa kabisa huo uraisi wa huko Zanzibar ( ingawa sio rahisi) na kuweka majimbo.
Hapo kutakuwa na Utanzania wa ukweli, lasivyo ni sawa na kujilisha na upepo tu
 
Hivi tukiwa na serikali mbili za Tanganyika na Zanzibar na kisha kukawa na serikali ya shirikisho ya Tanzania wananchi wa hizi nchi mbili watajitambulisha vipi? Yaani ukienda nje ya nchi utajiita mtanzania, mtanganyika, au mzanzibar? Au itategemea na muktadha wa utambulisho?
maswali yako ni ya msingi sana na yanahitaji kupatiwa majibu ya msingi
 
THAT IS WHY I LIKE WARIOBA.......ILe Tanganyika ALso
Warioba anaongea pints sana SISIEm wana kamafledge watuwasifahamu . SISI em inataka tuungane na watu kama wakenya na waganda ambao hata kutupenda hakupoo. Hivi kweli inaingia akilini kutaka kuungana na nchi kama hizo ambazo kila kukicha wanafikiria kupata malighafi ya Tanganyika. Angalia kwanza walivyo wanaguzi mfano Wakenya, Au Uganda ambao wamekuwa wakipigana na waasi kwa zaidi ya miaka 20? Leo eti unataka nchi iwe moja inakuja akilini kweli. labda kama sisi vichaa!

TANGANYIKA HOYEEEEE!
 
Back
Top Bottom