Warioba: Wanaotaka Tanganyika wasipuuzwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba: Wanaotaka Tanganyika wasipuuzwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Feb 27, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,275
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Na Richard Makore
  26th February 2011


  Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema kuna baadhi ya Watanzania wanaohitaji kuwepo kwa serikali ya Tanganyika badala ya ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo umefika wakati wa kuheshimu mawazo yao.

  Jaji Warioba alitoa maoni hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye mjadala uliozungumzia Muungano wa Tanzania na mchakato wa kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki.


  Alisema mawazo ya Watanzania ya kutaka kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika bado yapo na yamekuwepo kwa kipindi kirefu na kwamba hivi sasa yana maana zaidi wakati wa kuelekea Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC).


  "Kuna watu wanatoka Tanganyika na kuna watu wanatoka Zanzibar hivyo mawazo yao ya kutaka kuwa na serikali zao yamekuwepo kwa kipindi kirefu na sasa umefika wakati wa kuyaheshimu," alisema.


  Kuhusu visiwa vya Zanzibar, Warioba alisema kunahitajika kuwepo kwa katiba mpya kwa kuwa hii ya sasa inawanyima wananchi haki ya kuchagua viongozi wao.


  Alisema kwa kutumia katiba ya sasa ili mtu aweze kupiga kura ya kumchagua kiongozi anatakiwa awe ameishi visiwani humo mfululizo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu, hatua ambayo alisema ni kinyume na demokrasia.


  Akizungumzia shrikisho la EAC, Warioba alisema kinachokwamisha juhudi hizo ni viongozi wa nchi wanachama wasiotaka kuachia nafasi zao za kisiasa wanazoshikilia.

  "Viongozi wengi wa EAC hawapo tayari kuachia nafasi zao na kuunda shirikisho la pamoja hatua ambayo inazidi kukwamisha mpango huo," alisema.

  Kwa upande wake, mwanasheria maarufu, Mabere Marando, akizungumza na NIPASHE baada ya kumalizika mjadala huo alipingana na mawazo ya Warioba kuhusu Serikali ya Tanganyika kwa maelezo kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndicho kinachokwamisha mpango wa kuwepo kwa serikali hiyo.


  Alisema Warioba ni mwanachama wa CCM kwa kipindi kirefu lakini anashangaa kuona anatoa mawazo nje ya chama badala ya kuyatoa ndani ili yafanyiwe kazi.


  Mjadala huo wa siku moja ulijadili masuala ya muundo wa Muungano wa Tanzania, Tanzania kuandika katiba mpya muda mfupi baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana pamoja na mchakato wa kuelekea Shirikisho la Afrika Mashariki.
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Warioba: Wanaotaka Tanganyika wasipuuzwe


  Na Richard Makore
  26th February 2011

  Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba

  Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema kuna baadhi ya Watanzania wanaohitaji kuwepo kwa serikali ya Tanganyika badala ya ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo umefika wakati wa kuheshimu mawazo yao.
  Jaji Warioba alitoa maoni hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye mjadala uliozungumzia Muungano wa Tanzania na mchakato wa kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki.
  Alisema mawazo ya Watanzania ya kutaka kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika bado yapo na yamekuwepo kwa kipindi kirefu na kwamba hivi sasa yana maana zaidi wakati wa kuelekea Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC).
  "Kuna watu wanatoka Tanganyika na kuna watu wanatoka Zanzibar hivyo mawazo yao ya kutaka kuwa na serikali zao yamekuwepo kwa kipindi kirefu na sasa umefika wakati wa kuyaheshimu," alisema.
  Kuhusu visiwa vya Zanzibar, Warioba alisema kunahitajika kuwepo kwa katiba mpya kwa kuwa hii ya sasa inawanyima wananchi haki ya kuchagua viongozi wao.
  Alisema kwa kutumia katiba ya sasa ili mtu aweze kupiga kura ya kumchagua kiongozi anatakiwa awe ameishi visiwani humo mfululizo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu, hatua ambayo alisema ni kinyume na demokrasia.
  Akizungumzia shrikisho la EAC, Warioba alisema kinachokwamisha juhudi hizo ni viongozi wa nchi wanachama wasiotaka kuachia nafasi zao za kisiasa wanazoshikilia.
  "Viongozi wengi wa EAC hawapo tayari kuachia nafasi zao na kuunda shirikisho la pamoja hatua ambayo inazidi kukwamisha mpango huo," alisema.
  Kwa upande wake, mwanasheria maarufu, Mabere Marando, akizungumza na NIPASHE baada ya kumalizika mjadala huo alipingana na mawazo ya Warioba kuhusu Serikali ya Tanganyika kwa maelezo kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndicho kinachokwamisha mpango wa kuwepo kwa serikali hiyo.
  Alisema Warioba ni mwanachama wa CCM kwa kipindi kirefu lakini anashangaa kuona anatoa mawazo nje ya chama badala ya kuyatoa ndani ili yafanyiwe kazi.
  Mjadala huo wa siku moja ulijadili masuala ya muundo wa Muungano wa Tanzania, Tanzania kuandika katiba mpya muda mfupi baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana pamoja na mchakato wa kuelekea Shirikisho la Afrika Mashariki.
   

  Attached Files:

 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Kuna watu wanatoka Tanganyika na kuna watu wanatoka Zanzibar hivyo mawazo yao ya kutaka kuwa na serikali zao yamekuwepo kwa kipindi kirefu na sasa umefika wakati wa kuyaheshimu," alisema.

  Ni kweli tunahitaji Tanganyika yetu.
  Wenzetu zenji si katiba yao imeshawaruhusu kufanya kila kitu wana bendera,rais n.k... isipokuwa waategemea sisi tuwaongozee serikali yao interms of funds ila mengine yote wanafanya kama wao ni nchi.
  Sasa kwa nini sisi tukiomba Tanganyika inakuwa nongwa? mbona ni kitu cha kawaida tu?
  Hapa kuna mwiniliano mkubwa sana wa kimasilahi kuingia EAC F bila ya kuwa na Tanganyika maana hapo kutakuwa na shirikisho ndani ya shirikisho, kila kitu kitaharibika sana, bora tusiingie kwenye hilo shirikisho kabisa.
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 201
  Trophy Points: 160
  Yeye Warioba haitaki Tanganyika ? Hebu muulizeni atupe jibu,awache katabia cha uchonganishi.
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,169
  Likes Received: 1,823
  Trophy Points: 280
  Huyu Jaji Warioba anazeeka vibaya....Hii katiba ya 1977 na madudu yake yote yeye ndie aliyeiandika na timu yake.
  Baada ya kuwahilikisha, kuwaadhibu Watanganyika na wazanzibari kwa miaka 47 ndio hawa CCM wanasema wanataka wananchi wasikilizwe.
  Warioba ni CCM, kwa nini haanzi huko kwenye vikao vyao vya vyama?
  Kama anatubia baada ya miaka yote hii basi asiishie kwenye makongamano tu.
  Hata hivyo, anastahili hongera kwa kauli yake hii. Sasa tunasubiri vitendo kutoka CCM na serikali wanayoiongoza.

  http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 11,572
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  ..kuwa na serikali 3 ni kujiongezea gharama[haswa kwa wa-Tanganyika] zisizo na ulazima.

  ..ukiongeza na uanachama wetu kwenye EAC naona muungano wa Tanganyika na Zanzibar unakuwa redundant.

  ..kama Rwanda na Burundi ni wanachama kamili wa EAC kwanini Zanzibar wasipewe haki kama nchi hizo?

  ..Muungano huu umepitwa na wakati, hauna faida wala mantiki.
   
 7. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kama hamjui huyo mzee riceyoba(waliyoba) kakosea kusema? Yeye alimaanisha tunaotaka ''DANGANYIKA''(hasa KIWETE) wacha tusikilizwe. Huyo ni mwana kondoo aliyevaa ch*p* ya ''MAFISADI''. Ako*e kutudanganya.
   
 8. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kama hamjui huyo mzee riceyoba(waliyoba) kakosea kusema? Yeye alimaanisha tunaotaka ''DANGANYIKA'' wacha tusikilizwe. Huyo ni mwana kondoo aliyevaa ch*p* ya ''MAFISADI''(hasa KIWETE). Ako*e kutudanganya. MPUUUUUUUUUUUUUU..
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,094
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Turudi nyuma kidogo tuangalia chanzo hasa cha huo Muungano. Lengo kuu la Muungano ilikuwa ni kuimarisha umojaa wa Afrika kuanzia kiwango cha majirani kwa lengo la kufikia United States of Africa. Kabla ya Muungano wa Tanzania wazee wetu walikuwa na plani ya kuwa na federation of East Africa, lakini kwa sababu mbalimbali juhudi za kuuanda federation ile zikafeli.

  Kwa vile kuna effort mpya za kuwa na jumua ya afrika ya mashariki, muungano wa Tanzania katika muundo wake wa leo unaweza usiwe na umuhimu tena. Ama kuwe na Taifa moja la Tanzania lenye serikali moja au tuwe na mataifa mawili ya tanganyika na zanzibar kila moja ikiwa na sauti yake ndani ya EAC.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Feb 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,208
  Trophy Points: 280
  Mimi siitaki Tanganyika!
   
 11. T

  Taso JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,526
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Warioba ametumia strategic language kusema tuvunje Muungano. Ni vigumu sana kwa mtu mwenye kutambulika kijamii kutangaza hadharani "Tuvunje Muungano." Ndio maana anaanzia mbaali, "tuheshimu mawazo ya wanaotaka Tanganyika." Lakini anastahili pongezi kwa kuwa na balls.

  Muungano ni zigo la pakacha kwa Tanganyika, bora tulituwe, ni kongwa la uhuru wa Zanzibar kuwa nchi kamili kama wanavyotaka, bora tuwataliki.

  Tuvunje Muungano.
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 10,419
  Likes Received: 2,663
  Trophy Points: 280
  Yes he has balls, however utanganganyika sio priority kwa sasa, ANGESEMA JK nchi imemshinda ajiuzulu angekuwa amesema la maana zaidi, au angehamasisha watu kuandamana, ilikuwa bora pia....
   
 13. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tanganyika imekosa nini kwa watu wake hadi kufika kuikataa isimarishwe rasmi
   
 14. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mzeemwanakijiji wewe endelea kula kuku wako kwa mrija ,wenye kuishi hapa Tanganyika ndio wenywe uchungu wa Tanganyika yao ,sipingi kutoipenda kwako Tanganyika na heshimu sana na kwa maana hiyo ndio umeikimbia Tanganyika kwakuwa huipendi na huitaki kuwepo kwake sasa waache wenye kuitaka waipiganie irudishe hadhi yake
   
 15. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  sisi tulio watanganyika tunaitaka
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mimi naitaka na kuitamani sana Tanganyika. Japo nime zaliwa Mtanzania mimi nimefundishwa darasani kwamba waasisi wetu wali gombea uhuru wa Tanganyika na si Tanzania. Utanzania hauja wahi kuuwa Utanganyika wetu.

  Mimi binafsi naji tambulisha kama Mtanzania wala si Mtangayika. Ila tuwe wakweli wenzetu wa Zanzibar wamekunywa na kulewa Uzanzibar. Iweje upande mmoja wajione ni Watanzania na wengine wajione ni Wazanzibar? Kama tumeshindwa kuwa nchi moja basi bora tuwe nchi mbili ndani ya mwamvuli wa serikali moja.
   
 17. T

  Taso JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,526
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Lakini mada ya hiyo forum aliyoongea Warioba haikuwa "tuandamane .... JK nchi imemshinda." Hata hapa huwezi kuposti maswala ya u-Tanganyika kwenye jukwaa na "Nimelala na Mama Mkwe wa kaka yangu," watakutimua.

  Umejuaje huko aliko anakula kuku kwa mrija? Kuna ma ghetto ya Detroit suburbs huko aliko yana tabu kuliko kuliko wewe wa Tanganyika. Mikuku ya kule unanunua liko kwenye deep freezer, wewe kuku unakula wa kuchinja fresh off the farm. Usimtukane bana.
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  It is his opinion and he is entitled to it. Ingekua vyema uka muuliza kwa nini haitaki Tanganyika...
   
 19. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 293
  Trophy Points: 180
  Ndiyo sisi tulio wa-Tanganyika tunaitaka Tanganyika yetu. Mheshimiwa Njelu Kasaka uko wapi, zile ajenda za Tanganyika yetu zishushe hapa jamvini.:A S 13:
   
 20. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Well, hapo ndipo hata mimi ninapochukia.

  Sisi kama watanzania tunapenda na kujisifu tu Watanzania kila sehemu tuwapo nje na ndani ya nchi

  lakini cha kushangaza Wazanzibar wao walishajitangazia nchi yao , si hata katiba yao mpya imeeleza wazi kabisa?? kwani ni siri??

  Hawa watu siku zote wanauchukia sana Utanzania, wanadharau sana kwa ujumla ,kama ukifatilia mijadala na forum zao walai unaweza usiamini kama hao ni watu wanaoishi kwa kodi zetu kwa jinsi wanavyotudharau wabara.


  Wakiwa nje ya nchi ndio basi kabisa, wanajitambulisha wanatoka Zanzibar yaani hapo hapo tukiwa nao pamoja...


  Sasa mimi utaniambia nikumbatie Utanzania na kuukana utanganyika ,kweli hii ni akili au mimi ni kichaa ,mpuuzi au mwendawazimu???


  Huwezi ukaimarisha kitu fulani kwa kutegemea upande mmoja, la hasha huwezi hata siku moja..ndio maana tunasema kwa kuwa wenzetu hawauthamini huo muungano basi ni bora nasi tukadai Utanganyika wetu.

  Natamani tuwe na shirikisho basi linatosha labda tutaheshimiana.

  Ukiwasikiliza hao jamaa wao kila siku ni malalamiko tu, hawana jema hata moja..kwa nini tuendelee kubembelezana na watu ambao ni wazima??


  Hata mke wako akikukana huna budi kumwacha aidha kwa kumpa taraka au yeye mwenyewe unamwomba akupe taraka .


  Kwa kifupi ni kwamba kwa kuwa wao hawatutaki basi wao wajiondoe na tuwape uhuru na kama wakihitaji basi wajiondoe na tubaki na shirikisho tu.


  Natumaini na kodi zetu zitaanza kufanya miradi mingine ya maendeleo nchini kwetu Tanganyika kuliko sasa jamaa tunawabeba karibu kwa kila kitu lkn bado jamaa wanachuki kwetu za ajabu sijwahi kuona..

  Yes we need our beloved nation Tanganyika

   
Loading...