Muungano uwe wa serikali moja tu, kama sio hivyo ufe tu

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,363
12,708
Manufaa ya muungano tumeyaona, ni matamu sana kwa watanzania walio wengi. Kila kijana mzanzibar anatamani kwenda kuishi Tanzania bara, na wako watanzania bara ambao wanatamani kwenda Zanzibar kwasababu moja au nyingine. manufaa ya muungano kila mtu anaweza kuyasimulia bila kuambiwa wala kusoma pahala popote.

Mwalimu Nyerere na Karume nina uhakika wote au mmojawapo alitaka muungano wa serikali moja, na wako wazee ambao wanajua dhamira ya muungano na aina ya muungano ambayo waasisi waliukusudia lakini kwa unafiki na woga wao wamenyamaza kimya na hatimaye kufa na siri hiyo.

Wazee wa hivi hawafai kupewa heshima tunayowapa, maana ni wanafiki, waoga na wasioona mbele. Nyerere sio mjinga kuifuta serikali ya Tanganyika na asiifute ya Zanzabar, lazima kuna jambo ambalo tunafichwa na kupewa sababu za kijinga na uongo juu ya muungano wa serikali mbili. G55 hawakuwa wajinga kudai kuirudisha serikali ya Tanganyika; bila shaka ilikuwa kujibu mkwamo wa kupata serikali moja.

Wakati tunaelekea kuadhimisha sikukuu ya Muungano ni aibu nchi moja kuwa na serikali kamili mbili bila kuwepo ya Tanganyika. Wazee kama Pius Msekwa, Warioba, Butiku, Mongella, Malecella, Msuya, Sumaye, Kikwete, na wengine ambao wanafahamu sababu za kweli na halisi juu ya kwanini serikali ya tanganyika ilifutwa na ya zanzibar akabakizwa hadi Sasa waitoe siri hiyo kabla hawajaiaga dunia na kuondoka nayo hata kama kwakufanya hivyo kutaleta shida kwao. maana watoto wajao hawataujua ukweli halisi juu ya kwanini kuna serikali 2 badala ya 1 au 3.

Muungano wa aina hii utahojiwa na kila kijana wa leo na wa kesho mwenye akili timamu. Hii haitaleta afya ya muungano siku zijazo wakati wazee wote wanaoijua siri ya muungano watakapokuwa wameondoka duniani. Vijana watatafuta njia zao za kusawazisha ujinga, uzembe na woga wa mababu zao.
 
Usijidanganye eti kuna mtu ana siri hiyo. Hilo ni suala la kitaalamu. Ebu jaribu kusoma miungano ya nchi mbalimbali duniani kati ya nchi ndogo na nchi kubwa uone kama hawajafanya kama Tanzania. Mfano, ushawahi kujiuliza kwanini Wales, Ireland ya Kaskazini na Scotland Zina mabunge na Serikali zao za ndani lakini England haina?
 
Kwani muungano wao umetulia kama ule wa marekani? Muda simrefu utavunjika tu.
 
Nimekwambia, fanya stadi ujiridhishe aina za miungano na changamoto zake. Unaweza ukafikiri Marekani wametulia kumbe Wana yao!
Tusiongelee UK, US na miungano mingine, bali tujikite kwenye huu wa kwetu. Kuna shida gani itatokea kama serikali ya zanzibar itafutwa pia kama ile ya Tanganyika? Maana mpaka sasa hakuna sababu ya kumezana, hakuna mtu anaweza kumeza wala kuwahamisha wazanzibar kwenye makazi na majumba yao kama serikali ikiwa moja.
 
Manufaa ya muungano tumeyaona, ni matamu sana kwa watanzania walio wengi. Kila kijana mzanzibar anatamani kwenda kuishi Tanzania bara, na wako watanzania bara ambao wanatamani kwenda Zanzibar kwasababu moja au nyingine. manufaa ya muungano kila mtu anaweza kuyasimulia bila kuambiwa wala kusoma pahala popote.

Mwalimu Nyerere na Karume nina uhakika wote au mmojawapo alitaka muungano wa serikali moja, na wako wazee ambao wanajua dhamira ya muungano na aina ya muungano ambayo waasisi waliukusudia lakini kwa unafiki na woga wao wamenyamaza kimya na hatimaye kufa na siri hiyo. Wazee wa hivi hawafai kupewa heshima tunayowapa, maana ni wanafiki, waoga na wasioona mbele. Nyerere sio mjinga kuifuta serikali ya Tanganyika na asiifute ya Zanzabar, lazima kuna jambo ambalo tunafichwa na kupewa sababu za kijinga na uongo juu ya muungano wa serikali mbili. G55 hawakuwa wajinga kudai kuirudisha serikali ya Tanganyika; bila shaka ilikuwa kujibu mkwamo wa kupata serikali moja.

Wakati tunaelekea kuadhimisha sikukuu ya Muungano ni aibu nchi moja kuwa na serikali kamili mbili bila kuwepo ya Tanganyika. Wazee kama Pius Msekwa, Warioba, Butiku, Mongella, Msuya, Sumaye, Kikwete, na wengine ambao wanafahamu sababu za kweli na halisi juu ya kwanini serikali ya tanganyika ilifutwa na ya zanzibar akabakizwa waitoe siri hiyo kabla hawajaiaga dunia na kuondoka nayo hata kama kwakufanya hivyo kutaleta shida kwao. maana watoto wajao hawataujua ukweli halisi juu ya kwanini kuna serikali 2 badala ya 1 au 3.

Ni muhimu sana badala ya hivi ilivyo sasa ambavyo muungano wa aina hii utahojiwa na kila kijana wa leo na wa kesho mwenye akili timamu. Hii haitaleta afya ya muungano siku zijazo wakati wazee wote wanaoijua siri ya muungano watakapokuwa wameondoka duniani.
Wazanzibar wanaitazama Tanganyika kwa matazamio ya kiuchumi.

Watanganyika wanaitazama Zanzibar kwa matamanio ya kupata wanawake shombeshombe.
 
Muungano uvunjwe hauna faida yoyote
kuvunjwa sio sawa lakini kutoa sababu za uongo kwa watanzania sio jambo zuri wala afya kwa muungano wenyewe. Uongo huu utaendelea kuhojiwa na vizazi vyote bila kupewa majibu ya kweli. Iko siku vitukuu vitachoka kudanganywa na kusawazisha mambo unguided. Wazee wanaotembea na uongo huu vifuani mwao watawajibika hata kama wamekufa. Bahati mbaya sana wazee wanaoshikilia kuwepo kwa serikali ya Zanzibar ndio wanaofaidi sana matunda ya Muungano, karibu wote wanaishi tanganyika na wana nyumba na vitegauchumi (ardhi kubwa, biashara, majumba, mifugo, nk) tanganyika. wanawadanganya vijana watoto wa maskini tu.
 
Tusiongelee UK, US na miungano mingine, bali tujikite kwenye huu wa kwetu. Kuna shida gani itatokea kama serikali ya zanzibar itafutwa pia kama ile ya Tanganyika? Maana mpaka sasa hakuna sababu ya kumezana, hakuna mtu anaweza kumeza wala kuwahamisha wazanzibar kwenye makazi na majumba yao kama serikali ikiwa moja.
Kabla hujafikia hitimisho hilo, ungejishughulisha kujua kwanini kuna aina tofauti tofauti za miungano. Mwanadamu ni yule yule na sababu ni zile zile. Usifikuri sababu za UK, US, USSR, SPAIN, FRANCE na kwingine ni tofauti na za Tanganyika na Zanzibar.
 
Back
Top Bottom