Mimi nafikiri wewe Teknolojia umejikita zaidi katika hisia zaidi kuliko uhalisia. Mtu kufananishwa na mtu mwingne ni jambo la kawaida na binafsi sioni tatzo lolote. Na kama hukubaliani na mtoa hoja ni vizuri pia na wewe kutoa hoja mbadala, sababu na ushahidi ili kutetea madai yako. Kwa mfano, unaposema hao wawili wanakwapua fedha za chama chao kwa maslahi binafsi, je una ushahidi wa kuthbitisha hilo au madai yako umeyajenga zaidi kwenye hisia na chuki binafsi dhidi ya hao viongozi? Mimi nafkri kwenye siasa huwezi kumpenda kila mwanasiasa. Lakini si vizuri hata kama humpendi mwanasiasa fulani kumzushia habari ambazo ni za hisia zaidi kuliko uhalisia. Kama hujafanya utafiti juu ya madai yako, ni dhahiri tu una chuki tu binafsi dhidi ya viongozi hao. Mimi natamani Watanzania hata kama tunatofautiana kimitazamo, kiitikadi na kisiasa tusifike hatua ya kutumia tofauti hizo kwa ajili ya kubomoa bali tuzitumie kujenga.