Warioba: Mimi na Salim urais basi

Warioba: Mimi na Salim urais basi

Mpitagwa,
Wewe umeona hili, wengine wanachoangalia bora tu kuwa na rais bila kuangalia mazingira na hali ya siasa na kiuchumi ilivyo sasa nchini. Mgombea urais anatakiwa aonyeshe yale ambayo wananchi wanaona ni tatizo kwa maisha na maendeleo ya nchi. Pamoja na kutokuwa na nafasi ya kutenda, lakini hata kauli tu inaweza kutoa picha ya kile anachokifikiria ndani ya moyo wake. Ndio maana siku hizi kuna debate kwa wagombea, licha ya debate, kuna vigezo ambavyo kabla ya uteuzi vinaangaliwa kama mtarajiwa anafaa kutokana na mwenendo wake wa maisha katika taifa letu. Mtazamo wake kwa watanzania, ubunifu wa mipango ya maendeleo na mfumo wa serikali.

Tunahitaji rais licha ya kuwa na panga la makali kuwili, aonyeshe ubunifu wa kuigeuza Tanzania kuwa taifa lenye kuwa na dira ya maendeleo kwa ulimwengu wa leo tokana na utajiri wa mali asili tulizo nazo. Ahadi za barabara zimekuwepo tangu tunapata uhuru, shule hali kadhalika, lakini sijaona hoja mbadala kwa marais waliomfuata Nyerere kujenga msingi wa uchumi wa kitaifa unaotegemea utajiri wa rasilimali za nchi yetu.

Tahadhari:
Vigumu kumgeuza aliyezoea kuruka angani aanze kutembea kwa miguu, kupanda baiskeli na kwenda vijijini kwa wananchi, kuamua kula mihogo Ikulu kwa kikombe cha tangawizi, kuzoea kula bilinganya zinazozalishwa na bustani za bonde la msimbazi badala ya vyakula vya mahoteli ya kitalii duniani.
Nadhani hoja yangu mwaipata. Somo tunalo, tumeliona. Je, tumejifunza nini na tumejenga tahadhari gani?



Acha kuwa na mawazo mgando

nchi hii ina watu milioni 45 ambaoa kati ya hao walio na umri wa chini ya miaka 20 ni asilimia 70

bado tuu unalalamika kwa mtu mmoja kutosema jambo?

Mbona husemi kitu kuhusu kimya cha Mzee ABOUD JUMBE?
 
Acha kuwa na mawazo mgando

nchi hii ina watu milioni 45 ambaoa kati ya hao walio na umri wa chini ya miaka 20 ni asilimia 70

bado tuu unalalamika kwa mtu mmoja kutosema jambo?

Mbona husemi kitu kuhusu kimya cha Mzee ABOUD JUMBE?

Jumbe alifungua makucha, system ya mfumo uliopo ikamwadhibu kwa kumweka chini ya ulinzi mkali asijitutumue, ndio maana kizazi cha leo ni kingine kwani kuna njia nyingi zikiongozwa na dot com.
 
L.Col_Members_SalimSalim.jpg
images

Dr. Salim Ahamed Salim (Tanzania) and Henry A. Kissinger (USA)

Dr. Salim Ahmed Salim ana jina kubwa nchini na kimataifa katika masuala ya kimataifa. He is a diplomatic figure. Naweza kumlinganisha na baadhi ya wanadipolamasia kama Henry Kissinger pamoja na umaarufu wao kimataifa hawakufaa kushika dola katika taifa.

Majukumu mazito aliyowahi kuyafanya kitaifa na kimataifa ni pamoja na:
  • Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa
  • Katibu Mkuu Umoja wa nchi Za Afrika
  • Mgombea Ukatibu Mkuu umoja wa Mataifa - hakupita
  • Nafsi ya juu aliyowahi kuishika Tanzania ni kuwa Waziri Mkuu
Pamoja na umaarufu alioweza kuwa nao katika masuala ya kimataifa na kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania:

  1. Hajaonyesha msimamo wake katika masuala ya kitaifa,
  2. Hayuko wazi
  3. Mkimya asiye weza kushirikisha aliyo nayo.
  4. Pamoja na kwamba ni mwana CCM sijawahi kuona ushirikishaji wa uongozi wake kwa CCM zaidi ya kuwa mhudhuriaji.
  5. Anaonekana kupokeleka zaidi kwa sura badala ya vitendo na fikra.
  6. Anaonekana kufaa shughuli za kiofisi zaidi kuliko siasa za majukwani.

Kwa mtazamo huu ana dira gani katika kuongoza Tanzania ya leo kama atagombea urais?
Je, Tanzania tuendelea kunadishwa majina makubwa ya wagombea urais pasipo kuonyesha uwezo wao?


Huyu Bwana Salim alionekana chaguo la wengi wenye kumwona ana uwezo wa kuongoza nchi yetu. Tangu mizengwe ya kuenguliwa kipindi kile akiwa Waziri MKuu na Nyerere kumpisha Mwinyi basi danadana imeendelea. CCM wakaja na single ya kumsifia Mtu wa kimataifaa, na mara nyingine wakimuenzi kwa uanadiplomasia, ili mradi aridhike na hayo, na aliridhika.

Kwa kipindi hiki naona kama ni vigumu kwa huyu Bwana kwa vile siku za nyuma hatukuangalia sana mtu ajenge hoja za kutetea nafasi anayotaka, kuuza sura na kunadishwa na wakubwa au chama ilitosha. Lakini leo hii na ukimya alio nao hali kadhalika sifa ulizoainisha hapo juu, naona amepitwa na wakati, atulie tu na kula pensheni yake. Choko choko za siasa za leo zitamshinda, na pia ule uungwana anaoonekana kuwa nao wenzake CCM sidhani kama watamkubalia maana wao wanataka mtu mwenye mlengo wa kifitina zaidi dhidi ya sianza pinzani kuliko ustaarabu.
 
Aaah Wapi,

Mmeshaanza siasa zenu za majitaka sasa,,

Hebu niambie wewe sasa.humpendi huyu kwa chuki zako binafsi au humpendi kwa kuwa yuko CCM??

Akisimama huyo 2015 hatuna budi kumpatia nchi hii,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni..

Au kwa kuwa ni Muislam??

Nadhani wanafanya vizuri ili nawe uweze kumfahamu kwa undani zaidi, sidhani makosa kuonyesha anavyofikiria juu ya mtu huyo.
 
Si tu hafai kuwa Rais wa nchi hii bali, kitendo cha Vurugu za Kidini zinawakosesha baadhi ya Watarajiwa uhalali wa kuliongoza taifa hili linajinasibu kutokuwa na Dini....Je kama CCM watamteau kugombea na ikatokea kwa BAHATI MBAYA akawa rais hataweza kutuliza mukari na hasira za kundi la dini linalodai linaonewa na kukandamizwa.

Maana kwa sasa Viongozi walioko madarakani wanatoka upande huo na mambo ndio haya.. Je yeye akibahatika kuunyaka Urais je anayomikakati gani ya Kuyalinda makundi ya dini zote......Tumechoka sana kuona pande hizi mbili zinanyanyasana, hasa upande mmoja unaonekana kuwa na jazba na kusababisha madhara makubwa kwa upande wa pili...."

Watanzania bado tuna wasiwasi na wagombea wengi toka CCM, vinginevyo watamke waziwazi ni mbinu gani watazitumia kuondoa kirusi hiki cha Udini kilichotamaraki kwa sasa..Vinginevyo tuwajaribu wapinzani kwani kwao pana uwezekano wa kukiua kirusi cha udini, na labda tutapambana na swala na rushwa na ukabila ambao kwa nchi kama Tanzania si tatizo kuukemea na kuuzika kabisa... Udini ni noma...

Umenena yakhe, maana madudu yote haya yatokeayo nchini amekaa kimya tu, maana hayuko na simanzi kwa yanayojilia? Hata nchi ikiangamia hana uchungu nayo, maana ana mafao mengi huko kimataifa alikofanyia kazi. Watu hawa tuwe macho na makini sana nao.
 
Watakao jitokeza kugombea na kuwa na sifa za kuwaridhia wananchi tutamchagua mmoja wao.

Tatizo walio na nafasi za majina makubwa ndio wanaojitanguliza kifua mbele na wanao wapiga debe wao wakati sisi tutafumbwa vinywa tusiwe na cha kuwauliza na hata debate za wagombea kukatazwa tusiwaulize haya.
 
kuna ka ukweli pamoja na heshima yake atuonyeshe msimamo wake ktk masuala ya madini, gesi, umeme, n.k
 
kuna ka ukweli pamoja na heshima yake atuonyeshe msimamo wake ktk masuala ya madini, gesi, umeme, n.k

Hicho ndicho kilichomgusa mleta mada kwani wengi wamejaribu kuonyesha msimamo wao hata kama wana kashfa, lakini huyu pamoja na uadilifu wake, bado haonyeshi msimamo wake katika masuala ya taifa, je tumweleweje?
 


Hapa ndipo pale Watanzania wengi tunapokosea,tunaangalia majina makubwa zaidi,PhD zaidi,vituko zaidi kuliko 'track records' za wagombea urais. Tusipobadilika tutaendelea kuumia..​

Hapo ndipo tatizo linapojitokeza kwa mazoea ya siasa za Tanzania, watakapopitisha jina la kigogo wanayemtaka watambeba kwa kila njia na kumsemea mazuri tu hadi kuwachukua watu kwa malori kwa gharama yo yote ili mradi kuonyesha kwamba ndiye anayefaa, na kitakachotokea baada ya uchaguzi "MAJUTO NI MJUKUU."
 
Hz sio siasa za majitaka wakuu. Binafsi sijawahi kumsikia huyu ndugu akijadili au kutoa kauli yeyote kupinga, kukubali au kusisitiza jambo. Kwa ujumla haeleweki. Penye ukweli tuzungumze jamani. Inaonyesha hana msimo.

Nikitaka kumwona huyu Bwana Salim Ahmed Salim nifanyeje, maana anaonekana kama yuko mbali kusikofikika na mtu wa kawaida, hata isue fulani huko nyuma serikali na CCM yenyewe hupata taabu namna ya kumfikia isipokuwa kuna kigogo fulani aliye karibu naye ndiye wanayemtumia kumfikia Salim. Haonekani kujumuika katika mazingira ambayo wananchi wa kawaida wako isipo kuwa katika vikao vichache sana vya juu vya CCM, hata hivyo sijazoea kusikia tamko lake katika vikao hivyo wala mtazamo wake kwa mambo mazito yatokeayo nchini. Mbona Mwinyi katoa kauli hukusu uchunjaji, Mkapa naye kaonyesha kusikitikia kwa yatokeayo nchini ambayo kipindi chake hayakuwepo.

Huyu bwana hata haonyeshi kusikitikia yatokeayo, anakula kuku kwa mrija tu kutoka matunda yake kwenye utumishi wa kimataifa. Huyu bwana kuwa Rais wa Tanzania hapana, ziwezi kufanya makosa hayo, tunao wengi tu bora hata mzee Samwel Sitta kuliko Salim.
 
watu wakimya sana na watu wanaopenda kuchekacheka hovyo na kutabasamu hovyo waogope kama ukoma wamejaa unafiki,visasi,vinyongo,ni watu wanaopenda matabaka.
 
watu wakimya sana na watu wanaopenda kuchekacheka hovyo na kutabasamu hovyo waogope kama ukoma wamejaa unafiki,visasi,vinyongo,ni watu wanaopenda matabaka.

Kuna point mohimu hapa kwani kuchekacheka ni njia kisaikolojia kuficha kilichomo sana na kufunika chungu mwanaharamu apite. Ukimya nao huzua mambo ya ajabu yasiyotegemewa kabisa. Hata katika familia watoto wakimya huleta mtafaruku sana katika familia kuliko watoto walio wazi. Maana walio wazi utajua nini wanataka, nini wanafikiri na nini wanakisudia tofauti na mkimya utakuja kushtukia matendo ambayo hukuyategemea.
 
makamanda huu msiba upo lumumba pale karibu na mahakama ya mnazi mmoja huku kinondoni naona shwari ila kwenye msiba lazima tuende kama observers tuangalie kama tumekanyagwa bahati mbaya tunalipua makusudi CCM MWISHO WENU 2015 KIVYOVYOTE ITAPASUKA VIPANDE VITATU EL,MEMBE NA DR SALIM.

"PEOPLESSSSSS POWEEEEEEEER" SALAMU YA MAKAMANDA.
 
Aaah Wapi,

Mmeshaanza siasa zenu za majitaka sasa,,

Hebu niambie wewe sasa.humpendi huyu kwa chuki zako binafsi au humpendi kwa kuwa yuko CCM??

Akisimama huyo 2015 hatuna budi kumpatia nchi hii,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni..

Au kwa kuwa ni Muislam??

Hapo kwenye nyekundu naona hujamtendea haki Dr. Salim na sisi wanajamvi, maana sijaona mahali mwandishi kamtuhumu kwa vile ni mwislamu. Kwangu hoja ingekuwa hivi akina Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Slaa, Lipumba, Cheo, nk waliogombea na wengine wakashinda kuwa maraisi walikuwa na CV kubwa kuliko ya Salim? Labda tumtoe Nyerere kwa kwenda UN na kueleza kuwa tunahitaji kujitawala nchi ikiwa na wenye degree wasiofika kumi labda huu ulikuwa ujasiri. Lakini wengine hawa, sijaona kilichowafanya wawe wagombea tofauti na yeye Salim. Sidhani kama kuwa karibu na wananchi ni kigezo cha kuwa kiongozi bora hata kama kuwa karibu nao kunamaanisha kuwaibia na kuwachomolea hata mia tano waliyoweka mifukoni mwao. Pia mimi mbona naona ana ukaribu sana na Nyerere Foundation kama mwenyekiti amekosaje kuwa karibu na wananchi?

Akigombea na kupitishwa na CCM au akihamia chama chochote mi binafsi nitampa kura yangu si kwa sababu ya dini yake, au sura yake (maana mambo ya sura za watu tunaona yalikotufikisha) bali kwa sababu ya weledi wake wa masuala ya kimataifa na kitaifa.
 
Kwani Dr Salim amekwambia anataka urais? Au ndoto zako tu?

Alipopata knock out toka kwa Kikwete kipindi kile na we ulikuwa wapi? Hali kadhalika hiyo ilikuwa knock out ya pili, ya kwanza ni pale Alhassan Mwingi alipitinga Magogoni na kumwacha Salim akigaagaa huku usanii wa CCM ukiendelea kumwimbia nyingi mwenye majukwaa na vyombo vya habari ati "SALIM MTU WA KIMATAIFA" wakati wamemfanyia mizengwe.

Anapenda sana kuwa Rais, tatizo hayuko karibu na wenzake, yuko juu mno, anafikiri jina lake pekee ndio kipenga cha kumpitisha kugombea urais.
 
Back
Top Bottom