Warioba: Mimi na Salim urais basi

Warioba: Mimi na Salim urais basi

Hapo kwenye nyekundu naona hujamtendea haki Dr. Salim na sisi wanajamvi, maana sijaona mahali mwandishi kamtuhumu kwa vile ni mwislamu. Kwangu hoja ingekuwa hivi akina Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Slaa, Lipumba, Cheo, nk waliogombea na wengine wakashinda kuwa maraisi walikuwa na CV kubwa kuliko ya Salim? Labda tumtoe Nyerere kwa kwenda UN na kueleza kuwa tunahitaji kujitawala nchi ikiwa na wenye degree wasiofika kumi labda huu ulikuwa ujasiri. Lakini wengine hawa, sijaona kilichowafanya wawe wagombea tofauti na yeye Salim. Sidhani kama kuwa karibu na wananchi ni kigezo cha kuwa kiongozi bora hata kama kuwa karibu nao kunamaanisha kuwaibia na kuwachomolea hata mia tano waliyoweka mifukoni mwao. Pia mimi mbona naona ana ukaribu sana na Nyerere Foundation kama mwenyekiti amekosaje kuwa karibu na wananchi?

Akigombea na kupitishwa na CCM au akihamia chama chochote mi binafsi nitampa kura yangu si kwa sababu ya dini yake, au sura yake (maana mambo ya sura za watu tunaona yalikotufikisha) bali kwa sababu ya weledi wake wa masuala ya kimataifa na kitaifa.

Ningefurahi kuwasaidia kupata uelewa wa hoja yako wachangiaji kama ungezipangua hoja zangu zote hapo juu kujenga utetezi wa kumpa Kura Salim Ahmed Salim. Sijaona hoja ulizojengea utetezi wako, mleta mada ameanika hoja na madhaifu ambayo anaona Salim si hastahili tu bali hafai kuwa rais wa Tanzania.
 
Mbona Kikwete alipewa,au naye si mwislam? BTW, Jemedali Mwislam Kikwete alimfanyia Zengwe na Fitna Mwislam mwingine Dr Salim A Salim. Hivyo MBWA KALA MBWA. The rest ni chuki na upungufu wa hekima kichwani.
UKWELIKITUGANI,Kikwete alipewa sababu Kanisa lilimtangaza kuwa ni chaguo la Mungu na kupata zaidi ya aslimia 85! angalia ni ngapi alipata uchaguzi wa pili baada ya kutemwa na Kanisa!
 
Tulieni pro lowassa,membe na chadema mbona mnaweweseka hagombei urais hajatangaza bado subiri akitangaza au akionyesha nia ndio muanze kelele zenu inaonekana mnamuogopa enhe coz naona wote mmeungana kumshambulia tehtehteh!!
 
Hayo yanayozungumzwa ni kweli? Au ndio stori za vijiweni

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Tulieni pro lowassa,membe na chadema mbona mnaweweseka hagombei urais hajatangaza bado subiri akitangaza au akionyesha nia ndio muanze kelele zenu inaonekana mnamuogopa enhe coz naona wote mmeungana kumshambulia tehtehteh!!

Wagombea nafasi hiyo nyeti si kwamba msukumo binafsi ndio unaowafikisha kutangaza dhamira ya kutaka kukalia kiti cha Magogoni, bali kuna watu, vikundi na taasisi mbalimbali zinazomzungumzia au kushauri mtu kutokana na kuonyesha uwezo wake kuwa anafaa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho. Tunachofanya hapa ni kusaidia zaidi Mwenyewe kujielewe, jamii kumwelewa, na kama atakuwa na malengo siku za usoni kugombea ajua kasoro alizo nazo ambazo anahitaji kuzifanyia kazi.
 
Hayo yanayozungumzwa ni kweli? Au ndio stori za vijiweni

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Kama hayana ukweli kwamba ni story za vijiweni, tunasubiri hoja zako zenye ukweli kupinga hizo zilizowekwa hapo juu vinginevyo ni utetezi usio na hoja za msingi.
 
hivi Candid Scope kila mpiga kelele na mwenda kwa wanyonge ndo mwenye uchungu na nchi?
 
Ndugu zangu Kusema Kweli, huyu Mzee Jaji Joseph Warioba ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Mpya, ametokea Kuwa Kiongozi wa tatu Baada ya Dr.Slaa na Mhe.Mbowe, Kunivutia sana hasa Kwa Misimamo yao ya Kiutendaji pale Wanaposimamia Kile Wanachokiamini Kwa niaba ya wengi. Jaji Warioba licha ya Kuwa Kada na Mwanachama wa CCM, ameuonyesha Dhahiri Ukomavu wake wa Kisiasa Katika Kujenga, Kutetea na Kusimamia hoja zake zenye Maslahi Kwa Taifa letu Kwa Ujumla bila Kuelemea Upande wowote.

Jaji Warioba pamoja na Kukumbana na Shinikizo Kubwa Kutoka Upande wa Chama Chake, tena Shinikizo linaloambatana na Matusi, Kebehi, Dharau, Udharirishwaji n.k, Lakini Jaji Warioba anaendelea Kuwa Jasiri Kila Kukicha Katika Kutetea hoja za Wanyonge wa Taifa hili na Kubeba Mzigo wa Lawama zote Inazotupiwa Tume anayoiongoza, Ilimradi Kile anachoamini Kimeelezwa na Watanzania, Kiwasilishwe Bungeni. Mzee Warioba ni Mtu wa Pili baada ya Dr.Slaa, anayeweza Kugombea Urais 2015 Kwa Sababu ya Hekima, na Busara zake Kama za Mwl.Nyerere.
 
Ndugu zangu Kusema Kweli, huyu Mzee Jaji Joseph Warioba ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Mpya, ametokea Kuwa Kiongozi wa tatu Baada ya Dr.Slaa na Mhe.Mbowe, Kunivutia sana hasa Kwa Misimamo yao ya Kiutendaji pale Wanaposimamia Kile Wanachokiamini Kwa niaba ya wengi. Jaji Warioba licha ya Kuwa Kada na Mwanachama wa CCM, ameuonyesha Dhahiri Ukomavu wake wa Kisiasa Katika Kujenga, Kutetea na Kusimamia hoja zake zenye Maslahi Kwa Taifa letu Kwa Ujumla bila Kuelemea Upande wowote. Jaji Warioba pamoja na Kukumbana na Shinikizo Kubwa Kutoka Upande wa Chama Chake, tena Shinikizo linaloambatana na Matusi, Kebehi, Dharau, Udharirishwaji n.k, Lakini Jaji Warioba anaendelea Kuwa Jasiri Kila Kukicha Katika Kutetea hoja za Wanyonge wa Taifa hili na Kubeba Mzigo wa Lawama zote Inazotupiwa Tume anayoiongoza, Ilimradi Kile anachoamini Kimeelezwa na Watanzania, Kiwasilishwe Bungeni. Mzee Warioba ni Mtu wa Pili baada ya Dr.Slaa, anayeweza Kugombea Urais 2015. Saaaaafi sana Kamanda Francis
 
Last edited by a moderator:
Du makala zingine sijui wanapata wapi?

Hiv sijui kama akili yangu inaakili
Hivyo vihabari sijui namii nianzishe kamtandao.
 
Wakuu, Jana Kwenye Kongamano la Vyama vya Siasa, Jaji Warioba alitoa Ufafanuzi wa Kitaalamu Kuhusu hoja ya Serikali tatu Inayoonekana Kuwa mwiba Kwa CCM na Serikali yao Baada ya Makamo wa Rais Dr.Gharib Bilal Kwa niaba ya Rais Kikwete, Kumrushia Makombora Mazito Jaji Warioba bila Kufafanua Umuhimu wa Serikali Mbili Kama Jaji Warioba anavyoonekana Kutoa Ufafanuzi wa Kitaalamu Unaoungwa Mkono na Idadi Kubwa ya Wasomi hapa Nchini, huku CCM wao Wakiupuuza Ufafanuzi huo Wakihofia Kukaa Bench baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 Endapo Kipengele hicho Cha Serikali tatu Kitapitishwa na Bunge la Katiba.
 
Wakuu, Jana Kwenye Kongamano la Vyama vya Siasa, Jaji Warioba alitoa Ufafanuzi wa Kitaalamu Kuhusu hoja ya Serikali tatu Inayoonekana Kuwa mwiba Kwa CCM na Serikali yao Baada ya Makamo wa Rais Dr.Gharib Bilal Kwa niaba ya Rais Kikwete, Kumrushia Makombora Mazito Jaji Warioba bila Kufafanua Umuhimu wa Serikali Mbili Kama Jaji Warioba anavyoonekana Kutoa Ufafanuzi wa Kitaalamu Unaoungwa Mkono na Idadi Kubwa ya Wasomi hapa Nchini, huku CCM wao Wakiupuuza Ufafanuzi huo Wakihofia Kukaa Bench baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 Endapo Kipengele hicho Cha Serikali tatu Kitapitishwa na Bunge la Katiba.

Kamanda Francis, Umetoa hoja za Msingi sana, ngoja nisubiri Comment za Wengine nipate taathmin Kamili kisha ntarudi niongee Jambo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom